MAISHA YANGU YA SOCCER VS NEEMA YA MUNGU

MAISHA YANGU YA SOCCER VS NEEMA YA MUNGU

MIHAYO1710

Member
Joined
Apr 7, 2018
Posts
22
Reaction score
59
Wakuu ningependa kuelezea kwa kifupi zaidi maana ya neema ya Mungu, kupitia maisha yangu halisi ya soccer.

👉Mimi niliupenda sana mpira wa miguu, lakini mpira wenyewe haukuwahi kunipenda! Ukoo wangu (Upande wa baba na mama) hakuna historia inayoonesha kwamba aliwahi kuwepo mcheza soccer machachari😅

👉Kila nilipobahatika kupewa namba, Kwenye mazoezi au mechi za kirafiki, niligeuka kichekesho, kivutio na burudani Kwa watazamaji, Kwa namna nilivyokuwa nabutua na kupigwa chenga mpaka naanguka mwenyewe bila kugusa mpira au kuguswa na mtu yeyote!

👉Nikiwa darasa la tano au la sita hivi, (Shule ya msingi Kawekunelela) tulienda kucheza mchezo wa kirafiki katika Shule jirani ya kisuke!! Kahama au Ushetu kwa Sasa.

👉Siku hiyo ikawa bahati kwangu😅😅

Pamoja na ubovu wangu, kocha akanipanga Kwenye kikosi Cha kwanza🤸🤸🤸

😅Pamoja na ubovu wangu, mashabiki wangu nje ya uwanja hawakuwa haba(Nyomi)

(mchezaji mbovu kisawasawa Huwa burudani na kivutio KAMILI uwanjani, kama mashindano siyo serious)

😂 Hadi dakika ya 45 ya mchezo kipindi Cha kwanza kinakamilika kama sikosei nilifanikiwa kuugusa mpira si zaidi ya mara tatu na Kila nilipopata mpira mchezaji wa timu pinzani alinipokonya kabla sijampasia mwenzangu!

👉 ng'we ya kwanza ilikamilika huku hakuna timu iliyokuwa imefanikiwa kuona lango la mwenzake (0 - 0)

👉 Katika kipindi Cha mapumziko, baadhi ya wachezaji walimshauri kocha wetu afanye sub, nitolewe🙌 Lakini katika Hali isiyokuwa ya kawaida ulitokea upinzani mkali kutoka Kwa kocha, baadhi ya wachezaji na mashabiki wakisisitiza nimalizie ng'we ya pili, hivyohivyo! Sijui walitaka nife? Nadhani Ile burudani ya Mimi kupigwa chenga mpaka naweweseka hawakutaka kabisa iwapite Wala kuikosa😂🤣

👉Kwa Upande wangu, ukweli Sikuamini kabisa kinachoendelea. Kwanza Nilikuwa nimechoka kabisa kukimbia kimbia bila tija na kuonekana kioja na kituko uwanjani!

👉Nilitamani sana wafanye hiyo sub, ili nikapumzike na kukwepa fedheha na hiyo aibu, yaan mbumbumbu wa soka promax!, lakini nilikaa kimyaa Nikawa nawachora tu!

👉Muda wa mapumziko ukakata, Refa alipuliza kipenga, kuashiria kuanza Kwa ng'we ya pili.

👉 Kwa kweli kipindi Cha pili nilivunja rekodi Kwa sababu sikufanikiwa kabisa kugusa mpira hata mara Moja mpaka dakika ya 85 ya mchezo!

👉 Ghafla bin vuu, tukapata Kona! Nikiwa Sina Ari Wala nguvu ya kufanya lolote, nilijisogeza Kwenye lango la timu pinzani na kusimama wima bila kujali Wala kujishughulisha kabisa na kilichokuwa kinaendelea pale! Muda wote nilitamani kusikia kipenga Cha mwisho, ili tuondoke niwahi Nyumbani nikapumzike!

👉Jamaa yangu mmoja akaichonga Ile Kona Kwa weledi, ikaja Moja kwa moja na kunigonga (Mimi) kichwani bila juhudi Wala ridhaa yangu na kutikisa nyavu 🙌🙌🤸🤸

(Nikiwa sijui kinachoendelea kabisa na maumivu ya kichwa kutokana na kugongwa na mpira Kwenye komwe )

👇👇
Ghafla, nikaona nabebelewa juu Kwa juu na wachezaji pamoja na mashabiki!

🤣😂😅Kumbe nimefunga bila kujua🙌🤸🤸 Shangwe zile ziliendelea Kwa muda kidogo, na shamra shamra zilipoisha Refa alipuliza kipenga kuashiria kukamilika Kwa dakika 90 za mchezo, huku nikiiandikia timu yangu goli la USHINDI katika dakika ya 89 ya mchezo!,😅😅

(1 - 0)

👉Nikawa "man of the match" nikapongezwa na Kila mtu, zawadi kama zote, Kila mtu alitamani kunishika mkono! Ghafla nikawa wa thamani, na wengine wakadhani nilikuwa natania tu uwanjani yawezekana ni msakata kabumbu machachari mithili ya Ronaldo de Lima aliyekuwa akiwika na kutamba Kwa kipindi Kile😅

👉Nilibaki na Ile Siri kwamba, Pamoja na mizawadi na pongezi nyingi kibao, lakini ni Mimi yule yule mbumbumbu wa soka. Sikufunga Kwa jitihada zangu, ila ni mpira tu ulipotea njia ukanigonga na kutikisa nyavu!

Ninapotafakari Habari ya Neema ya Mungu na kuhesabiwa haki Bure, naikumbuka siku Ile jinsi ya shindano "Nilivyoheahimishwa na mpira bila Nguvu Wala juhudi"

👉Kwa Hiyo?

👇👇👇

Warumi 11:6

[6]Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema.

Warumi 3:23-24

[23]kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;

[24]wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
 

Attachments

  • 1782500445830.jpg
    1782500445830.jpg
    44.1 KB · Views: 8
🤣😂😅Kumbe nimefunga bila kujua🙌🤸🤸 Shangwe zile ziliendelea Kwa muda kidogo, na shamra shamra zilipoisha Refa alipuliza kipenga kuashiria kukamilika Kwa dakika 90 za mchezo, huku nikiiandikia timu yangu goli la USHINDI katika dakika ya 89 ya mchezo!,😅😅
We jamaa ni Charlie chaplin
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom