Mungu amesahau dhambi zenu

Mungu amesahau dhambi zenu

MIHAYO1710

Member
Joined
Apr 7, 2018
Posts
22
Reaction score
50
MUNGU AMESAHAU DHAMBI ZETU!!!

"A KINGDOM FORGIVENESS STANDARD: A PRAGMATIC APPROACH"

Amani na Salama 🙏🙏🙏

Ninayo FURAHA na ujasiri mkubwa kukupasha habari hii njema Sana! "Mungu AMESAHAU DHAMBI ZETU 🔥🔥

KIVIPI? Fuatana nami . ....!!!

Ni ndoto ya Kila binadamu mwovu kumsahaulisha mdeni wake😁 Na akishajua aliyekuwa anamdai kasahau, basi huyu binadamu mwovu hufurahi! Lakini ghafla akigundua kuwa mdeni wake hajasahau, Bali kaamua tu kumsaheme na yeye kujisahaulisha, (Kumpotezea) basi mlengwa (kama ana akili) huogopa sana na kuona aibu! Lakini akielezwa bila UNAFIKI kwamba kusamehe na kusahau Ndiyo ulikuwa mpango mzima na adhima ya huyo anayemdai, basi, hujaa shukrani, fuhana na ujasiri!!

MUNGU KASAHAU DHAMBI KWELI?

Jibu la kweli na la haraka ni Ndiyo!!

Kwa kigezo Gani?

Twende taratibu.. ...!

Zamani za agano la kale, Mungu, kupitia kinywa Cha nabii Yeremia, alitangaza ujio wa agano jipya. Pamoja na mambo mengine, agano Hilo litakuwa tofauti sana na lile za zamani! Na kipengele/Ibara Mojawalo katika agano jipya ni Mungu kusamehe uovu wa mwanadamu pamoja na kusahau kabisa maovu Yao!

Yeremia 31:31-34

Tunukuu mstari wa 34!

Yeremia 31:34

[34]Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao SITAIKUMBUKA tena.

☝️☝️Huo Ndiyo unabii wa kweli uliotangazwa na nabii Yeremia!

👉Swali ni je, unabii huo ulitimia??

Ndiyo! Unabii huo wa ujio wa agano jipya ulitimia, baada ya mwana wa MUNGU, Yesu Kristo kuzaliwa, kuteswa na kufa msalabani! Kifo chake msalabani Ndiyo kilikuwa kilele Cha kuashiria mwanzo wa nyakati Mpya, katika historia ya mwanadamu! "Maisha bila dhambi!!"

Kwa Nini maisha bila dhambi? Kwa sababu Mungu kasamehe na Kusahau🙌🙌🙌

Kanisa la kwanza lilitambua wazi kutimia kwa unabii huo, na Ndiyo maana mtume akasisitiza sana suala hilo "La Mungu kusahau dhambi" katika waraka kwa waebrania.

Waebrania 8:12
[12]Kwa sababu nitawasamehe maovu yao,
Na dhambi zao sitazikumbuka tena.

Mtume alifundisha jambo Hilo akiwakumbusha watu kuwa zile nyakati zilizotabiriwa hapo zamani, Sasa nimefika, zipo!

👉☝️ Unaweza kusoma pote kuanzia mstari wa 7-13.

KIGEZO CHA MUNGU KUSAHAU DHAMBI ZAKO.

Mungu kwa hakika amezisahau kabisa dhambi za watoto wake! Kwa sababu ni ahadi yake kuwa katika majira ya agano jipya, atasamehe na Kusahau maovu ya watoto wake.

SWALI. JE, umefanyika kuwa mtoto wa MUNGU?

👉Siyo Kila binadamu ni mtoto wa MUNGU!

Watoto wa MUNGU ni wale tu waliompokea Yesu na kuliamini jina lake!

Yohana 1:12

[12]Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;

👉Kwa hiyo, watoto Hawa wa MUNGU siyo wale wanaozaliwa kimwili! Ni wale tu waliokubali mwaliko wa kugeuza fikira, kumwamini Bwana Yesu na kuzaliwa upya kwa Roho.

Yohana 3:3-5

[3]Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
[4]Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

[5]Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

Watoto wa MUNGU ni wale tu wanaoongozwa na Roho Mtakatifu!

Warumi 8:14

[14]Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.

🔥Kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu Moja kwa moja huyatenda mapenzi yake!

Ezekieli 36:27

[27]Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu na kuzitenda.

👉Kwa hiyo watoto wa MUNGU hupatikana kwa mchakato huo ☝️

Kumwamini Bwana Yesu na kubatizwa katika Roho Mtakatifu na baada ya hapo, kukubali kuongozwa na huyo Roho Mtakatifu.

(Siyo Kumwagiwa Wala kuzamishwa Kwenye maji Kwa maana ya H²O)

👉Kwa Nini MUNGU asahau maovu Ya watoto wake?

Mungu amesamehe na Kusahau maovu ya watoto wake kwa sababu daima Mungu haangalii mapito ya zamani, Bali huangalia Hali ya Sasa!

Na ndiposa mtume Paulo anasisitiza👇👇

2 Wakorintho 5:17

[17]Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama yamekuwa mapya!

🥰Kwa Hiyo kama wewe una historia mbaya ya mtu kabla ya Wokovu, hiyo ni ya kwako tu kwa sababu amefunguliwa faili jipya! Ni KIUMBE kipya kabisa, Hana dhambi!

👉Kwa upande mwingine, mtoto wa MUNGU Huwa hatendi dhambi. Na hii Ndiyo hasa sababu inayomfanya Mungu kusahau kabisa, kwa sababu anajua na Hana hofu kuwa watoto wake ni watakatifu na hawawezi kutenda dhambi.👇👇

1 Yohana 3:6,9

[6]Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.

[9]Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.

👉Kwa Hiyo watoto kamili wa MUNGU Huwa hawatendi dhambi.

Kinginee, Mungu ni UPENDO, UPENDO wa Kweli hauhesabu MABAYA!👇👇👇

MUNGU NI UPENDO 🥰🥰

Na tabia ya UPENDO ni hii Hapa 👇👇👇

1 Wakorintho 13:1-5

[1]Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu.
[2]Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.

[3]Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

[4]Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

[5]haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; HAUHESABU MABAYA

👉Umeona hapo☝️☝️

UPENDO wa Kweli huww hauhesabu MABAYA na Mungu Ndiyo UPENDO WENYEWE 🔥

👉MFALME Daudi, kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu aliwahi kugundua na kuweka wazi kuwa tabia ya Mungu siyo kama ya binadamu mwovu aliyeharibika akili. Tabia ya binadamu mwovu ni kuweka kumbukumbu ya mabaya tu. Mme/mke mwovu hujipa Kazi ya kuhesabu makosa ya mwenzi wake😢 Tabia ya kuhesabu makosa ya mwenzi imedhoofisha mahusiano mengi ya wanandoa.

👉Ikiwa tabia ya mwenzi kuweka kumbukumbu ya mabaya ya Mme/mke wake inakera na kuleta majeraha ndani ya ndoa, JE, Mungu aliye mwingi wa rehema na huruma aweza kujipa Kazi ya kutunza kumbukumbu ya MATENDO Yako ya kijinga na kipumbavu?

Hapa Daudi alisema hivi, namimi namnukuu👇👇👇

Zaburi 130:3

[3]BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu,
Ee Bwana, nani angesimama?

Ikiwa dini Yako inakukatisha tamaa kwa kukuambia kwamba "Mungu ana malaika wenye jukumu la kuhesabu makosa yako"

Tambua wazi kuwa Huyo Mungu wao, siyo Mungu wa mbinguni ambaye habari zake zimeandikwa Kwenye biblia.

NI KWELI KATUSAMEHE NA MADHAMBI YETU HAYA???

Ndiyo! Baada ya kufanyika kuwa watoto wake, kwa kumwamini Bwana Yesu na kuzaliwa upya kwa ubatizo katika Roho Mtakatifu, tumesamehewa na dhambi zetu zimesahaulika kabisa!

👉Tumesamehewa kwa sababu tulikuwa na dhambi!

👉 Tumesamehewa si kwa sababu tumetenda MATENDO ya kiungwana! Lahasha, Tumesamehewa na dhambi zetu zimesahaulika kabisa kwa sababu tumemwamini Bwana Yesu!

👇👇👇

Warumi 3:23-25

[23]kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;

[24]wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.

[25]ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho
kwa njia ya imani katika damu yake, ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa;

🤭Umeelewa???

Kwa Hiyo, unapaswa ubadiri fikira na kumwamini Bwana Yesu, ili uingie katika UFALME wa MUNGU na Mungu akusamehe MADHAMBI Yako na kuyasahau.

👇👇👇

Matendo ya Mitume 2:37-39

[37]Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

[38]Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39]Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wetu!

👉Kwa Hiyo ahadi hii ya Mungu kukusamehe dhambi zako na kuzisahau, si kwa ajili ya wanaoitwa Wakristo tu, ni ahadi ya jumla kwa ajili ya Kila mtu anayeitikia wito huu wa tumaini la neema ya Mungu, iliyoletwa kwa mkono wa Bwana wetu Yesu Kristo!

Hata nabii Isaya aliwahi kusema kuwa, ukiitikia mwaliko na kusemezana na Mungu, basi dhambi zako hata kama zingekuwa nyekundu kama damu, zingesafishwa!

Isaya 1:18

[18]Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji, zijapokuwa nyekundu kama benders, zitakuwa kama sufu.

Kwa Hiyo ni uamuzi wako, kumfanya Mungu akusamehe na Kusahau maovu Yako. Kwa kugeuza fikira, akili, maoni na kuungia Ufalme wa MUNGU!

🤣😂 Mfano wa mwana mpotevu ni uhalisia wa namna na jinsi Mungu anavyoweza kumchukulia mtoto wake hata baada ya kujichanganya.

👉Pamoja na kujisheua kuomba msamaha na kupanga kuishi kama mtumwa Kwenye nyumba ya baba yake, kama sehemu ya Toba na kuonesha kujutia, lakini Baba anaonesha Hana kabisa habari na maigizo ya yule mtoto. Anamkaribisha, kumvika mavazi ya HESHIMA na kumfanyia kalamu kubwa🔥

Halafu, maisha yanaendelea......!

Ukisoma kwa uangalifu, utagundua kuwa kijana wake tu ndo alikuwa anateseka na kujutishwa na dhambi zake za kijinga! Baba yake hakuwa na habari naye, Tena anapokekelewa kwa FURAHA, bila kukanywa Wala kukumbushwa dhambi zake. Baba ni kama alikuwa amesamehe na Kusahau 🙌

😳😳 Mwisho kabisa nimalize kwa kutoa angalizo!

JE, kwa kuwa Mungu kasahau dhambi zetu, kwa njia hii ya neema, JE tuendelee kupeta tu na maisha ya anasa, zinaa na uasi?

Hapana! Sisi watoto wa MUNGU, tunayafahamu vyema kabisa mapenzi ya baba yetu! Kwa sababu hiyo tunampenda kwa moyo, akili na NGUVU zetu, hivyo hatuwezi kukusudia kutenda dhambi 😍

Kwa Nini? Mtume Paulo anatoa Majibu Hapa 👇👇

Warumi 6:1-14

[1]Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?

[2]Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?
[3]Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?

[4]Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.

[5]Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;

[6]mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;
[7]kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.

[8]Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye;

[9]tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena.

[10]Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu.

[11]Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.

[12]Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;

[13]wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.
[14]Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.

#Umebarikiwa milele.

Kama hujampa Yesu Kristo maisha yako basi nakushauri Ufanye hivyo mapema iwezekanavyo!

#shetanianaogopamtuanayejuakitu
 
Back
Top Bottom