Maisha baada ya kubainika kuwa upo HIV+

Maisha baada ya kubainika kuwa upo HIV+

Hata December 1 siku ya UKIMWI nilipima.
Nakumbuka iyo siku nilikuwa na kaka yangu nikamtania "Kaka leo si unajua siku ya UKIMWI duniani, nenda kapime '

Akanijibu kwa msisitizo kabisa..." Nani mimi?! Weeh nitapima vyote ila sio iyo kitu yaan, yaan waniambie nakufa kesho mimi? Ahna siwezi tena nakushauri na wewe na ilo limwili lako ukijipeleka kupima sijui nani atakubeba"

Ilinibidi nicheke tu, Maana usilolijua ni sawa na usiku mnene wa giza.
Baadae nilijitahidi kumuelewesha juu ya umuhimu wa kujua afya yake lkn wapi hakuna lugha alielewa.
 
Hili ndo neno mkuu....nikiwazaga iko siku ntakufa natetemekaa!

Naogopa kifo asee
Wala usiogope, it's our fate. Kufa ni hakika, iwe kwa mafua, kisukari, ajali, saratani au ukimwi. Ni ukweli unaouma ila tutakufa lazima.
 
Nasikia Uganda ipo sindano unapiga Kila baada ya miezi Minne,huna haja ya kunywa ARV kila siku
Hiyo sindano ipo hata ulaya tena ni ya miezi 18. Wanapewa wenye matatizo kama ya akili, alcoholic na drug users wale ambao hawatakumbuka kunywa dawa kila siku.
 
Ikifika huku itatuokoa wengi maana itaondoa usumbufu na pia kuonekana kwenye vituo Kila mwezi
Wanaifanyia research bado wanasema kama inaweza kudhibiti wadudu kwa miezi 18 basi kuna uwezekano ikaongezewa mpaka miaka 5 au kufikia tiba kamili.
 
Wanaifanyia research bado wanasema kama inaweza kudhibiti wadudu kwa miezi 18 basi kuna uwezekano ikaongezewa mpaka miaka 5 au kufikia tiba kamili.
Yaani miaka 5 si utajisahau Kama we ni mgonjwa?
Sasa naona kwanini elimu ni muhimu, pressure, Sukari, malaria ni hatari zaidi ya ukimwi
 
Hongera mkuu kwa ujasiri wa kuweka mambo hadharani, mm nataka unipe elimu hii, hivi ni kweli ukifanya mapenzi na mtu aliye + anayetumia ARV wewe negative haupati maambukizo?
 
dah kwa mbinde...mi napima tu vyote including HIV ila sio niende specificaly for HIV...napima malari awingi wa damu typhoid, kilo zangu..minyoo HIV infections bacteriala any etc
 
Back
Top Bottom