Maisha baada ya kubainika kuwa upo HIV+

Maisha baada ya kubainika kuwa upo HIV+

Kupima ukimwi naisee mtihan nlienda na wife kipnd mjamzto nkamkimbia clinik Duuh bahat alikutwa neg acheni kabisa ukikutwa nao unahesabu umebakisha makombe ya dunia mawili tuu
 
Ni kweli ukuzingatia unazitumia kwa muda mrefu. Ukiwa kwenye kitengo wana angalia kila kitu kuanzia mapigo ya moyo mpaka ufanyaji kazi wa figo. Kukiwa na matatizo unabadilishiwa Dawa.

Fikiria na athari zote hizo za ARV kuna wengine wanazipiga na bia au methadone.
Nilisikai bia haina athari kwa ARV cha msingi ni usisahau kuzimeza maana ukisahau ukiharibu dozi wale virusi wanapata nguvu ingine na ile dawa ya awali inakua haiwezi kufanya kazi inabaidi ibadilishwe
 
Kupima sio issue,issue kuchukua majibu.maana muweka bandiko kakili siku za mwanzo n tatizo kuizoea hiyo shida.
 
Afadhali wewe umeshajua status yako, kuna waathirika kibao hawajijui na wanaogopa kupimwa.
[emoji276] [emoji276] [emoji276] Wewe umepima lkn ? usisemee mwenzio check afya yako kwanza na kupima co jambo la mchezo ww
 
Kupima sio issue,issue kuchukua majibu.maana muweka bandiko kakili siku za mwanzo n tatizo kuizoea hiyo shida.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Daaah vipimo siyo kbs kikikukataa jua umeisha.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Daaah vipimo siyo kbs kikikukataa jua umeisha.
Mambo ya kuanza kushinda kwa akina gwajima ya nn..!!!ntakomaa hivi hivi.mbona hata kaburini hatujui kunani,tunahadithiwa tyu na bado tunakomaa na cake za happy birthday
 
Habari wana JamiiForums,

Nina muda kidogo sijaingia humu, ila leo nilipopata nafasi ya kupitia nyuzi tofauti tofauti nimejisikia kushare na nyinyi ili.

Siku kadhaa zilizopita ilikuwa ni siku ya UIMWI Duniani, kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp iliiongelea tofauti sana siku iyo kutokana na kubeba kitu UKIMWI ndani yake kulingana na fikra na imani za wengi ambazo tunaziita ni hafifu.

Kuna watu mpaka leo wanaogopa HIV/AIDS kuliko hata wanavyoogopa Cancer, Blood Pressure, Visukari Na magonjwa mengine makubwa kulingana na imani mbaya walionayo juu ya HIV.

Watanzania HIV/AIDS sio mbaya wala ya hatari kama mnavyoidhania, iwapo tu utafata masharti na maelekezo ya daktari wako, na kufanya peace nayo from the very start point.

Binafsi nakumbuka siku ya kwanza naambiwa kua Nimeathirika, Honestly nilichanganyikiwa sana, nililia sana, nilihisi pengine ndo nakufa, picha zilizokuwa zinajitengeneza kichwani kwangu juu ya HIV ni tofauti kabisa na navyoishi leo, imeshapita miaka miwili sasa na sijawahi kuumwa chochote cha kunilaza kitandani, ukisikia naumwa labda mafua mafua, au zaidi malaria kama wengine, ila yote hii ni kwa sababu nililia sana ila ikafika hatua nikasema basi, imeshatokea na hakuna nachoweza kubadilisha, nikachukulia kama malaria tu and since then am good and have never being this good in my 16 nor 18.

Watu wengi hatuna tabia ya kucheck afya zetu, sababu ya woga au mapicha picha yaliojaa vichwani mwetu lakini leo hii tukichukua watu 50, tukawapima kwa nguvu kuna 10 au zaidi kati yao wapo positive lakini hawajui, hata mimi siku niliopima sikuwa na mpango wa kupima, nilikuwa tu nimekaa mahali nikimsubiri rafiki yangu atoke ndani kwake tuondoke ndipo kuona gari limepaki pembeni wanatangaza, ndio nikasema acha nipime fasta majibu yaliyotoka, Ah ile siku sijaisahau.

Maisha yangu baada ya HIV yapo poa, sioni kilichobadilika kwangu labda tu being on ARV's mwanzoni ilikuwa ngumu ila now we good, sioni cha kunitisha, sioni ambacho kinaweza kikanifanya niamini HIV ni kitu cha kutisha kwa kiasi kinachoongelewa na watu ambao hawajapitia hili. Tusiogope kupima afya zetu kwa manufaa yetu wenyewe.

Ushauri wangu kwa ambao ndio mmeambiwa mpo positive na mnasoma hapa, take it easy, hii sio death statement, unauwezo wa kuishi hata zaidi ya alie negative, na hata kama imepangwa ufe kesho unaweza ukaondoka kwa sababu zingine ila sio HIV, inaweza ikawa ajali au mengine, ivo wewe tengeneza amani nayo, ujikubali afu usijiwekee tofauti na wengine kwamba wewe sio binadamu tena hapana, ukiwa na amani, usiwe na mawazo, kula vizuri, fata maelekezo, nenda clinic kwa wakati, basi kila kitu kitakua sawa.
[emoji117]Kama upo kwenye wakati mgumu unaoona ni mgumu sana with this, just PM Me, And we can have a very friendly talk.

Don't say that will never happen to you, life got so many ways to prove us wrong. Remember! A lot of us tested positive, and so many people out there test the same.

[emoji117][emoji117]I once tested Negative! This means wote hatuijui kesho Yetu. Never say this will never happen to me, Life and time got so many ways to prove us wrong.
And Yes I was never a Hoe! This means being Positive haimaanishi it was just through sex! Zipo njia nyingi mtu anaweza Kua affected, au lah! Mtu huyohuyo mmoja anaweza kukuchange status yako.
And Yes! I never believed that I will ever test positive...tusijiamini kupitiliza
And Yeah! Siku niliopima, sikuwa na mpango, na hata nilipojiambia acha nipime tu sikuwa na chembe ya woga! This means tusiwe na uhakika sana na afya zetu kabla ya vipimo.
And Today! I and HIV We made peace, we good, we OK, that means sijaona kitu cha kunitisha in it.
Hapana mwili ukishaingia maradhi kiukweli unapoteza ubora na si kitu cha kuzoeleka kirahisi.


Ushauri mzuri maana maji ya kimwagika hayazoleki
 
Nilisikai bia haina athari kwa ARV cha msingi ni usisahau kuzimeza maana ukisahau ukiharibu dozi wale virusi wanapata nguvu ingine na ile dawa ya awali inakua haiwezi kufanya kazi inabaidi ibadilishwe
Ni kweli kabisa mkuu
 
Kupima ngoma sio jambo rahisi na pia kuishi maisha ya kunywa dawa unadhani ni masihara? Unakunywa dawa tu miaka yote sio rahisi wazee.
 
Hongera sana kwa ushujaa wako .Umesema mtu akitaka mawasiliano na aku pm mbona mie sijui jinsi ya kukupata in box tuongee zaidi niko serius .
 
Furaha pekee waliyonayo wagonjwa wa ukimwi wanaojijua ni kusex pasipo stress na hiyo ukimwi utazidi sana
 
Mimi kusema ukweli naogopa sana HIV, niko makini sana kwa kweli, MUNGU nisaidie katika hili, ukiupata upate kwa njia nyingine ila sio Ngono.

NAUHAKIKA UKIMWI SINA ILA NAOGOPA KUPIMA
 
Back
Top Bottom