Mtoa mada hongera kwa kujikubali na Ahsante kwa kutia moyo wengine.
Mwaka flan nilitelekezwa na ujauzito , siku ya kwanza kuanza clinic ndiyo siku niligundulika na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Niliumia sana ila nilijipa moyo kuwa mfariji wangu pekee ni mtoto nitakayemzaa hivyo sikuwa na budi kujikubali maisha yaendelee.
Hata hivyo haikuwa rizki, ujauzito uliharibika ikiwa zimebakia wiki mbili mtoto aanze kucheza tumboni.
Nilijifunza kumshukuru Mungu kwa kila jambo na sasa hivi maisha yanakwenda.
Kuugua sio kufa. Nafurahia kila chance ninayoipata katika maisha. Najipenda haswa, na nilivyo karembo sasa[emoji23] (joke).........