Maisha baada ya kubainika kuwa upo HIV+

Maisha baada ya kubainika kuwa upo HIV+

Kuambukiza?! No! Pengine Yes, Maana pengine sindano ilionichoma mimi ikamchoma na mwenzangu bahati mbaya bila kujua.... Hapo ni kwakua akili ya wengi inapokuja swala la HIV wanafikiria ngono tu, kuhusu tishio, best! Tishio as in how?! Maana kwanza hadi tunapitiana kabisa clinic au tunachukuliana, au unatukuta tunacheka nje ya clinic wala habari hatuna.... Tishio as in how?....
Tuukubali ukweli na kuukiri kwamba hizo njia nyingine apart from "ngono isiyo salama" zinachangia maambukizi kwa asilimia chini ya 5.

Maambukizi kwa asilimia kubwa ni kupitia "ngono zisizo salama".

Hongera kwa kupima na kuikubali Hali yako.

HIV no ugonjwa Kama yalivyo magonjwa mengine na kimsingi haupaswi kuogopwa Sana na kuijengea hofu jamii tuliyomo.
 
Upo vizur mkuu na utaishi maika mingi kwanza umeanza dozi ukiwa cd4 hazijashuka tofauti na hawa waoga kupima alafu cd4 zinashuka mpaka 100 yupo hoi kitandani tb ishamtandika,kashadhohofuu sasa hapa akiambiwa ana ngoma kwa mawazo anadhohofika zaidi,na kukata tamaa hapa mpaka cd4 zipande si mchezo anaeza ishia njiani maana magonjwa nyemelezi yanamshambulia ...ila kiukweli kujua afya yako ni muhimu
Hivi HIV Na TB kuna nini mahusiano yake maana wengi nakuta akiwa na HIV utakuta ana TB pia why?
 
The Stigma Must Fall..... Life Must Go On Sweetheart..... Watu waliowengi hawana elimu ya kutosha juu ya HIV/AIDS, afu wanaogopa sana, hapo ndo unakuta mtu akiambiwa yupo positive, anajiua, mwingine anakata tamaa.. Lakini ukifatilia kwa karibu sana hakuna tofauti kubwa zaidi ya zile dawa tu na kufata taratibu za wataalamu.
Ni kweli aiseee Nina ndugu yangu wa damu kabisa,hapa juzi juzi kapima kakutwa Na HIV pia TB.Baada ya kugundulika hayo kama kusingekuwa na uangalizi wa karibu angejiua.Kwa sababu alitaka kumeza dawa Za TB Na ARV vidonge vyote alivyopewa.
Pia baada ya kuanza kutumia ni kama alipata uchizi Fulani.Sasa hivi kaanza kurecover Na mnaweza ongea mkaelewana.Lakini kila ikifika siku ya Clinic nikimpeleka hospital Huwa anawehuka tena anakuwa kama chizi mpaka zipite siku mbili ndio anarudi kuwa normal.Nahisi ile Hali Bado hajaikubali
 
Daah huu ujasiri wa kupima huu ugonjwa kwa kweli sina. Labda nikishafika level fulani ya maisha ila kwa sasa hapana kabisa sitakwepa kuwaza na kibaya bado nipo kwenye hatua za mwanzo kutafuta maisha. Ngoja hiyo energy na ujasiri wa kupima ni vi reserve kwenye kutafuta pesa kwanza. Kupima baadae sana..

Ila hongera sana mtoa mada kwa ujasiri. One love
 
Ni kweli aiseee Nina ndugu yangu wa damu kabisa,hapa juzi juzi kapima kakutwa Na HIV pia TB.Baada ya kugundulika hayo kama kusingekuwa na uangalizi wa karibu angejiua.Kwa sababu alitaka kumeza dawa Za TB Na ARV vidonge vyote alivyopewa.
Pia baada ya kuanza kutumia ni kama alipata uchizi Fulani.Sasa hivi kaanza kurecover Na mnaweza ongea mkaelewana.Lakini kila ikifika siku ya Clinic nikimpeleka hospital Huwa anawehuka tena anakuwa kama chizi mpaka zipite siku mbili ndio anarudi kuwa normal.Nahisi ile Hali Bado hajaikubali
Mh uyo itakua alikuwa na iyo issue zamani ila alikuwa hajui, na pengine kajua pindi cd4 zimeshashuka sana magonjwa kama hayo TB na mengine ndo yanashambulia sana, ila ukiwahi unadunda tu, ukajikubali hupati shida kabisa. Ila daah taking all of the ARV's at once mmh, zilivyokubwa vile dah'[emoji47][emoji47] atakua poa uyo
 
Kuna MTU aliniuliza swali nilishindwa kumjibu maana sikuwa na uhakika,

Aliuliza hivi, " hivi kama mbu akumung%ata MTU kwenye HIV na akaning'ata mm ambae sina HIV je anaweza kuniambukiza?

Nilimjibu hapana ila sina uakika, kama kuna kwenye jibu naomba
Kitalaam hilo haliwezekeni,na wanasema kirusi kinapendelea kuishi kwenye damu sana sana na laiti ingelikuwa ni kwel huo ugonjwa ungesambaa kwa kas zaid
 
Ni kweli aiseee Nina ndugu yangu wa damu kabisa,hapa juzi juzi kapima kakutwa Na HIV pia TB.Baada ya kugundulika hayo kama kusingekuwa na uangalizi wa karibu angejiua.Kwa sababu alitaka kumeza dawa Za TB Na ARV vidonge vyote alivyopewa.
Pia baada ya kuanza kutumia ni kama alipata uchizi Fulani.Sasa hivi kaanza kurecover Na mnaweza ongea mkaelewana.Lakini kila ikifika siku ya Clinic nikimpeleka hospital Huwa anawehuka tena anakuwa kama chizi mpaka zipite siku mbili ndio anarudi kuwa normal.Nahisi ile Hali Bado hajaikubali
Kwel mkuu na huyo anahitaji uangalizi wa karibu zaid na ushauri pia,muanganishe na mkuu naye ajaribu kumshauri japo inahitaji muda kuikubali hiyo hali
 
Ni kweli ukuzingatia unazitumia kwa muda mrefu. Ukiwa kwenye kitengo wana angalia kila kitu kuanzia mapigo ya moyo mpaka ufanyaji kazi wa figo. Kukiwa na matatizo unabadilishiwa Dawa.

Fikiria na athari zote hizo za ARV kuna wengine wanazipiga na bia au methadone.
Bia ukinywa mbili tatu hazina shida mradi usiwe mlevi sana ukasahau muda wa dawa pia kwenye side efect kila kitu kina madhara hata vyakula pia unaweza ukawa hutumii hizo arvs ukawa mlaji mbovu wa mavyakula na unywaji pombe kali kali pia ukapata ugonjwa wa moyo ,na figo kufel pia kuna ambao hawatumii pombe na figo zinafeli na ini xo hapa ni kuacha tuu woga arvs unakunywa na unakunywa pombe ila isizidishe ....
 
54359e8cd3e89ae4aa256022862ca178.jpg
 
Hivi HIV Na TB kuna nini mahusiano yake maana wengi nakuta akiwa na HIV utakuta ana TB pia why?
HIV ina stage tatu,,
1. acute stage
2.latency stage
3.AIDS

stage ya kwanza huanza week 2 au tatu baada ya kupata maambukizi ambapo dalili kubwa katika kipind hiki mtu hupata mafua, sore throat(madonda koo) , homa, kuvimba tezi(lymphadenopathy) nk. japo asilimia kubwa hua hawaonyeshi dalili zozote katika kipindi hiki na pia dalili hizi hupotea baada ya mda mfupi allmost 2weeks na mtu kupona kabisa na kuishi bila dalili zozote

stage ya pili ni latency stage ambapo kirusi cha HIV kinakua latent mwilini yani namaanisha kirusi kinakuepo na kinakua kina haribu kinga ya mwili kidogo kidogo (stage hii huchukua zaidi ya miaka kumi )na zaidi kulingana na kinga yako ya mwili..

stage ya tatu ni AIDS (acquired immuno deficiency syndrome) baada ya HIV kuharibu sana kinga ya mwili yani kua na CD4 counts chini ya 200 ndipo magonjwa nyemelezi huanza kumshambulia mtu (syndrome -meaning muunganiko wa Magonjwa) ambapo magonjwa kama TB, mkanda wa jeshi( herpes zoster) ,karposi sarcoma( cancer) ,oral candidiasis, n.k
ambapo dalili kubwa katika stage hii ni homa kali(39-42 degrees) , kutokwa na jasho kali usiku, kuharisha, kukonda sana ( unintentional weight loss- loosing more than 10-20percent weight) kutapika n.k

so kuchelewa kupima na kuanza kutumia dawa ndo husababisha watu wengi kupata TB na HIV kwa pamoja kwan TB mostly ni opportunistic infection kama kinga ya mwili imeharibiwa vibaya na virusi vya ukimwi
.
but ukipima mapema na kuanza kutumia antiretrovirals unaweza kuishi normal life with normal life expectancy kwasababu utapunguza viral loads na kufanya kirusi kisionekane kabisa na usiweze kuambukiza wengine ( being on ARVs for more than two years makes the viral load to be very low to undetected level and its more protecting than using condom )

current studies shows people who got HIV On there twenties they have lived to 65yrs which is mostly like normal normal life..

na kwa sasa ukianza kutumia anti retrovirals mapema unaweza kuishi to 70years ambayo ni almost like normal health life..

@dr Masesa. KCMC university
 
Kuna MTU aliniuliza swali nilishindwa kumjibu maana sikuwa na uhakika,

Aliuliza hivi, " hivi kama mbu akumung%ata MTU kwenye HIV na akaning'ata mm ambae sina HIV je anaweza kuniambukiza?

Nilimjibu hapana ila sina uakika, kama kuna kwenye jibu naomba
Mbu ni vector mkuu hawezi kusambaza.
 
Back
Top Bottom