Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 28,394
- 81,877
Kwa wale wasio ufahamu huo Mji; kwa ufupi tu uko ndani ya Mkoa wa Iringa (Kilomita chache kutoka Iringa mjini kama unaelekea Mbeya, Njombe au Ruvuma), uko ndani ya Wilaya ya Mufindi, na ni mji maarufu kwa biashara ya mbao na pia nguzo! Maana uko jirani na kiwanda maarufu cha Sao Hill.
Kwa kweli huu Mji ni mdogo tu lakini uko busy sana kibiashara, na ikumbukwe maeneo ya pembezoni mfano Madibira, Sadani, Mgololo, na pia Mufindi yote kwa ujumla; huutegemea huu mji kwenye suala zima la mahitaji yao muhimu ya kila siku.
Ingawa huu Mji umekuwa ukipokea wageni wa kila aina kila siku kwa ajili ya kununua mbao, nguzo, na mahitaji mengine, umekuwa na upungufu wa nyumba za wageni zenye hadhi. Kiukweli nyumba nyingi za kulala wageni (Lodges + Guest Houses) zilizopo Mafinga ni chafu!
Kwanza mablanketi yao huwa hawafui (ifahamike hili eneo lina baridi mwaka mzima, hivyo lazima ujifunike blanketi). Mara kadhaa nimelazimika kulala Iringa mjini, kwa sababu tu ya huu udhaifu wa nyumba za wageni pale Mafinga.
Hivi shida ni nini kwa wamiliki wa nyumba za wageniza Mafinga? Au ni kwa sababu mnapata faida kubwa kupitia short time? Maana hizo bar zenu maarufu, pamoja na night clubs chache zilizopo; si haba!
Kwa kweli nawashauri mbadilike. Kama vipi pandisheni hata bei za vyumba, huku mkiboresha pia huduma. Kwa kweli mablanketi yeni ni machafu sana. Mtakuja kuwasababishia wateja wenu magonjwa ya ngozi kwa sababu zinazoweza kuzuilika.