KARATU: Mji wenye vumbi kali na fursa nyingi za kiuchumi

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,223
22,300
Majuzi nilileta uzi wa miji yenye vumbi jingi ambapo Karatu ilikuwa namba moja na hakuna aliyepinga. Baadhi ya comments zilizonekana kugusiagusia kuhusu huu mji ambao hauna mpinzani kwa kiwango cha vumbi jekundu kusini mwa jangwa la sahara. Lakini pamoja na vumbi bado Karatu ni mji mmoja uliokaa kimkakati sana kwa wale wapambanaji kama ilivyo Tunduma mpakani.

Karatu iko mkoani Arusha, mwendo kama masaa mawili toka jijini Arusha. Ni mji ulio kwenye mwinuko kama Iringa. Baridi la kutosha. Shughuli kubwa wilayani Karatu ni kilimo. Mahindi, Maharage, Ngano, Bale, Vitunguu, Mpunga na Kahawa ni mazao maarufu yanayolimwa Karatu. Ardhi ya Karatu ni mojawapo ya ardhi zenye rutuba ya kipekee.

Kilimo cha huko sehemu kubwa haihitaji hata mbolea ili kupata mavuno mengi. Kata ya Eyasi ndo maarufu kwa kilimo cha Mpunga na Vitunguu. Hilo eneo utakutana na watu kutoka karibu kila pembe ya Tanzania wakitafuta utajiri kupitia kilimo cha vitunguu na mpunga. Na kweli huko kuna wakulima matajiri kwelikweli. Mbunge wa sasa wa Karatu ni mkulima maarufu wa vitunguu.

Utalii ni shughuli nyingine kubwa inayofanyika Karatu. Tukiachana na Arusha na Zanzibar, naweza sema Karatu ni mji mwingine unaotembelewa na watalii wengi zaidi. Idadi ya watalii wanaopita Karatu kwa siku ni kubwa.

Ikumbukwe huwezi kufika Serengeti na Ngorongoro kwa kutokea Arusha bila kupita Karatu. Huu ni mji wenye baadhi ya hoteli na maduka ya kitalii yenye hadhi ya nyota tano. Hotel kama Bougaiville, Manyara, Crater Rim, Eilleen tree, Kudu na zingine nyingi zinafanya huo mji kuwa wa gharama sana. Kiburi cha wafanyabiashara wa Karatu ni kama wenzao wa Arusha kutokana na pesa za utalii.

Kimsingi ukiwa Karatu fungua macho yako yaone fursa zote zinazotokana na utalii. Hata baadhi ya vijana wengi wa hovyo kutoka Karatu nao waliona fursa ya kuchakata mbususu za kitasha ili kusaka fedha. Kuna baadhi ya matajiri wa sasa wa Arusha & Karatu walipitia njia hiyo ya vijana wa hovyo na kuishia kupata mitaji kutoka kwa vibibi vya kizungu.

Binafsi namjua tajiri mmoja ambaye alikutana na fursa ya mbususu ya mama wa kizungu huku akiwa kaoa. Ikabidi amkalishe mke wake mchaga kuhusu huo mchongo. Mke akatoa ruhusa mumewe akachakate mbususu ya kizungu wapate hela za kubadili maisha yao. Na kweli ikawa hivyo.

Siku za karibuni kumegunduliwa madini huko kata ya Endabash. Hii ni fursa mpya sana kwa Karatu. Wale wanaopenda hizi ishu za madini nadhani Karatu pia kutawafaa. Kwa ujumla Karatu ni mji unaofaa kibiashara kwasababu ni njiapanda ya kwenda Ngorongoro, Serengeti hadi wilaya zingine za Mara. Pia ni njiapanda ya kwenda Mbulu na wilaya za mkoa wa Shinyanga kama Meatu.

Kasoro waliyo nayo watu wa Karatu ni kupenda siasa za upinzani. Enzi za Mwalimu waligoma kumchagua mgombea wa TANU na kumchagua mgombea binafsi wa ubunge. Ndo ikawa chanzo cha kufutwa mgombea binafsi.

Ni miongoni mwa wilaya chache za Tanzania ambazo tangu 1995 zimekuwa ngome za upinzani hadi uchaguzi wa 2020 ambao haukuwa wa haki. Mbunge wa sasa yupo tu kwa hisani ya Polepole. CCM tutaweka mgombea mwenye vigezo 2025 vinginevyo hawa CHADEMA watarudi tena kwenye ubunge.
 
Kuna sifa moja kubwa sana ya karatu hujaisema

Kuna mabinti wazuri balaa kabila lao wambulu na wafiomi

Hawa mababu zao walihamia mkoa wa manyara kutoka Somalia na Ethiopia miaka kama 200 iliyopita

Ikitoka kondoa mkoa wa manyara ni wapili kwa wanawake wazuri


Mkoa wa tatu Kilimanjaro
 
Kuna sifa moja kubwa sana ya karatu hujaisema

Kuna mabinti wazuri balaa kabila lao wambulu na wafiomi

Hawa mababu zao walihamia mkoa wa manyara kutoka Somalia na Ethiopia miaka kama 200 iliyopita

Ikitoka kondoa mkoa wa manyara ni wapili kwa wanawake wazuri


Mkoa wa tatu Kilimanjaro
Hawana uzuri wowote hao wambulu
 
KARATU NDIO MAKAO MAKUU YA UPINZANI TANGIA ENZI YA NYERERE WALIKUWA WANAPIGIA KIVULI KURA BADALA YA NYERERE
20230521_192807.jpg
 
Back
Top Bottom