Ni sahihi mwenye nyumba kumwekea mpangaji sharti la aina ya wageni wanaomtembelea?

Bull Bucka

Member
Oct 5, 2023
34
46
Jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini Tanzania, suala la makubaliano kati ya mwenye nyumba na mpangaji ni jambo la kawaida. Makubaliano haya hujumuisha mambo mengi kama vile kodi, malipo ya huduma za nyumba, na masuala mengine yanayohusiana na kukaa kwenye nyumba ya kupanga. Hata hivyo, kuna baadhi ya wenye nyumba ambao huenda zaidi kwa kumuwekea mpangaji sharti la aina ya wageni wa kumtembelea.

Njoja niwape stori kwanza. Mwaka 2017, niliamua kuishi kwenye nyumba moja maeneo fulani huko Goba, Dar es Salaam. Mwenye nyumba naye alikuwa anaishi hapo, na tukiwa tayari kwenye mkataba wa kupanga, hakunipa taarifa yoyote kuhusu sharti la kutoleta wageni wa jinsia tofauti.

Mwenye nyumba alianza kuonesha wasiwasi juu ya wageni wa kike waliokuwa wakija kunitembelea. Alifanya mambo kama kuniangalia kwa jicho la tatu kila wageni wa kike walipokuja. Yaani alikuwa hadi akisimamisha shughuli zake ili kujiridhisha kama walikuwa wageni aliowahi kuwaona awali au ni wageni wapya.

Siku moja, alinitolea uvivu na kuniambia kuwa wageni wa kike wamekuwa wengi sana kwenye nyumba. Nilimuuliza ikiwa kuna siku nilivunja amani au niliwahi kusababisha fujo na kelele zisizo za kistaarabu, na jibu lake lilikuwa "hapana." Tatizo lake na wageni wa kike eti ni kwamba nitawaharibu wanae kwa kushuhudia vitendo vya “kimalaya”. Cha! Nilichoka.

Hata hivyo sikukaa kimya. Nilimkumbusha mwenye nyumba kuwa watoto wake wanahitaji kufundishwa kuhusu ustaarabu na kuheshimu watu na wasiige mambo ya kipuuzi hata wakiwa huko shule. Nilimkumbusha kuwa ana jukumu hilo la kutekeleza kwa wanae na si kwa kumzuia mpangaji kuleta wageni.

Nilisisitiza pia kuwa si kila mwanaume au mwanamke anayekuja kumtembelea mpangaji anakuja kwa lengo la kufanya mambo ya kimapenzi. Baadhi ya wageni ni marafiki wa kawaida, ndugu, au jamaa ambao wanataka kutembelea na kufurahi pamoja. Nilimwambia kuwa si sahihi kuvunja ustaarabu na uhuru wa mpangaji kwa kisingizio cha kuwalinda watoto wake.

Lakini pia nilimwambia kuwa bado mimi ni kijana na nipo katika mchakato wa kutafuta mwenza wa maisha. Kwa hiyo, baadhi ya wageni wa kike, mbali na marafiki na familia, wanaweza kuwa wanawake ambao ninafikiria kuwa huenda nikaoa siku za usoni, kwahiyo hakupaswa kuninyima fursa ya kupenda na kupendwa. Sijui alitaka niishi vipi mzee yule. Sema alijitahidi kunielewa.

Wenye nyumba, kuweka mazingira ya kukodisha ambayo yanawapa wapangaji uhuru wa kufanya maamuzi kuhusu wageni wao ni muhimu sana. Hii inahitaji uelewa wa utofauti wa tamaduni, imani, na mienendo ya kijinsia.

Kuwapa wapangaji nafasi ya kuwa na wageni au marafiki bila kuwahukumu au kuwabagua ni ni jambo la msingi sana. Pia, ni muhimu kuondoa ubaguzi wa kijinsia na kuacha watu wa jinsia tofauti kuwa na mahusiano ya urafiki au kufanya shughuli pamoja bila kutafsiriwa kwa dhana za ngono. Cha!
 
Kwa kawaida sipendi kupanga nyumba pamoja na mwenye nyumba, namuona kama mshirikina na mchawi mkubwa. Wanye nyumba huchimbia uchawi kuzunguka nyumba zao. Dawa yao ni kushusha maombi ya nguvu ili uchawi wao ushindwe. Unaweza kugeuzwa chuma ulete ukaishia kupanga kwake tu hujengi kwako.
 
Kiwango cha pesa ndicho kinatuamulia mambo mengi sana ktk maisha.

Ukiwa na pesa fulani utaamua tu sitaki kuchangamana na wapangaji wengine, achia mbali mwenye nyumba.

Sasa wakati huu ambao mimi na wewe hatuna pesa, inabidi tu tuwe wapole, ndani ya nyumba na mwenye nyumba lazima kuwe na miongozo kwa usalama na ustawi wa familia yake.
 
Wengine wanasema kabisa hawataki kijana ambae hajaoa au mwanamke asieolewa sometimes wageni nyumba za watu sio vizuri linaweza kutokea tatizo wakhis wageni wako ndo sababu kama una mtu mmoja mlete huyohuyo marafiki nao wasizid sana waambie ukweli
 
Kwahiyo ulitaka mwenye nyumba akuchekee unavyokuwa unavusha?

Umepanga chumba cha kuishi au gesti?
Jamani, sasa nisipate huduma za msingi za kimwili? Lakini pia, kila mwanamke anayekutembelea lazima awe mshirika wako wa kingono? Na hata akiwa mpenzi wangu, kuna shida gani yeye kuja ninapoishi tukapika, tukackeki muvi na kufurahiana?

Itabidi tukutane gesti kila siku?
 
Kiwango cha pesa ndicho kinatuamulia mambo mengi sana ktk maisha.

Ukiwa na pesa fulani utaamua tu sitaki kuchangamana na wapangaji wengine, achia mbali mwenye nyumba.

Sasa wakati huu ambao mimi na wewe hatuna pesa, inabidi tu tuwe wapole, ndani ya nyumba na mwenye nyumba lazima kuwe na miongozo kwa usalama na ustawi wa familia yake.
Ni mapambano kinoma, ndugu yangu.
 
Kiwango cha pesa ndicho kinatuamulia mambo mengi sana ktk maisha.

Ukiwa na pesa fulani utaamua tu sitaki kuchangamana na wapangaji wengine, achia mbali mwenye nyumba.

Sasa wakati huu ambao mimi na wewe hatuna pesa, inabidi tu tuwe wapole, ndani ya nyumba na mwenye nyumba lazima kuwe na miongozo kwa usalama na ustawi wa familia yake.
wanajiamini sana kiasi cha kupangia wapangaji masharti ya kuishi. Unapangiwa namna ya kutumia choo na kujisafisha utumie material gani, muda wa kurudi usiku, aina ya vyakula vya kupikwa, muziki wa kuwekwa na aina ya wageni wa kuja
 
Back
Top Bottom