Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Tumeshuhudia mengi tangu Ndugu Samuel Sitta awe Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kiasi kikubwa amekuwa na tofauti na maspika waliomtangulia kwa jinsi anavyoendesha shughuli zake kama kiongozi wa mmojawapo ya mihimili ya dola. Kuna wanaomsifu kwa utendaji wake na kuna wanaodai kuwa ana 'nguvu ya soda' hivyo tusitarajie lolote jipya zaidi ya 'longolongo' huku akijificha nyuma ya kivuli cha chama chake.

Mtu upimwa uwezo wake pale afikwapo na misukosuko inayohitaji busara na uwezo wa kutetea kile unachoamini kwa masilahi ya wanyonge amabo wameweka imani kwako kama kiongozi wao.

Yaliyojiri katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM yanabainisha kuwa ile slogan ya Ndugu Sitta ya 'kasi na viwango' inawezekana ikagonga mwamba hasa ukizingatia kuwa ikija kwenye suala la 'ulaji' CCM inabakia kuwa CCM bila kujali una wadhifa gani. Kitendo cha Ndugu Sitta kunywea wakati wa kikao cha NEC kinanipa picha kuwa Spika ana hali ya uvuguvugu...ana chembe chembe za uzalendo na pia ana chembe chembe za masilahi binafsi na ya chama....aidha ana chembe chembe za masilahi ya taifa lakini nashawishika kuamini kuwa kiasilimia chembe chembe za utaifa alizonazo ni kidogo mno. Sitashangaa Spika Sitta akigeuka nyuma na kuwa nguzo ya chumvi katika vikao vijavyo vya bunge.

Hayo ni mawazo yangu......wewe unadhani tutarajie lipi kwa Spika Sitta kwa kipindi kilichobakia cha uspika wake hasa ukizingatia "wenye chama" wameshamwonyesha kadi ya manjano?
 
magazeti ya rostam ndio yaliripoti kuwa sitta ameomba radhi na mhariri wao kibaraka muhingo rweyemamau yule jamaa mwembamba mwenye pua ndefu na sura ya ajabu kibaraka wa rostam na lowassa alikuwapo dodoma na ndio alitunga uongo huo kwa kusaidiana na kibaraka balile mtoto wa mkulima anaye futa viatu vya mafisadi ili apate ugali.kimsingi ni vijigazeti vilevile vya udaku yaani mtanzania na tanzania daima ndio vili exagarate habari hiyo ionekane sitta ameomba radhi ila kimsingi mafisadi wamekwama tena,..

Kweli kabisa PhD! Taarifa zilizoripotiwa na magazeti hayo mawili ya mafisadi yalipotosha suala zima kwa makusudi ili ionekane kwamba Spika Sitta aliumbuka kwenye hicho kikao. Huyo Muhingo na kibaraka mwenzake Balile walienda Dodoma wakiamini walichoambiwa na mabwana zao ROSTAM na LOWASSA kwamba Sitta atafukuzwa CCM. Bila shaka walishaandaa hata vichwa vya habari kwenye magazeti yao yaliyopoteza hadhi (kwa ujinga wao). Mafisadi hawa walitumia muda mwingi kabla ya kikao cha Dodoma kuweka mikakati ya kumng'oa Spika ambaye wanamuona kuwa kikwazo kikubwa katika harakati zao za kutaka kujisafisha na hatimaye eti washike dola. Mavi yao... Sio nchi hii! Tumeshawashtukia na tutapita kila kijiji kuwaeleza Watanzania jinsi walivyo watu hatari na wa kuogopwa kama ukoma!
 
Tumeshuhudia mengi tangu Ndugu Samuel Sitta awe Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kiasi kikubwa amekuwa na tofauti na maspika waliomtangulia kwa jinsi anavyoendesha shughuli zake kama kiongozi wa mmojawapo ya mihimili ya dola. Kuna wanaomsifu kwa utendaji wake na kuna wanaodai kuwa ana 'nguvu ya soda' hivyo tusitarajie lolote jipya zaidi ya 'longolongo' huku akijificha nyuma ya kivuli cha chama chake.

Mtu upimwa uwezo wake pale afikwapo na misukosuko inayohitaji busara na uwezo wa kutetea kile unachoamini kwa masilahi ya wanyonge amabo wameweka imani kwako kama kiongozi wao.

Yaliyojiri katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM yanabainisha kuwa ile slogan ya Ndugu Sitta ya 'kasi na viwango' inawezekana ikagonga mwamba hasa ukizingatia kuwa ikija kwenye suala la 'ulaji' CCM inabakia kuwa CCM bila kujali una wadhifa gani. Kitendo cha Ndugu Sitta kunywea wakati wa kikao cha NEC kinanipa picha kuwa Spika ana hali ya uvuguvugu...ana chembe chembe za uzalendo na pia ana chembe chembe za masilahi binafsi na ya chama....aidha ana chembe chembe za masilahi ya taifa lakini nashawishika kuamini kuwa kiasilimia chembe chembe za utaifa alizonazo ni kidogo mno. Sitashangaa Spika Sitta akigeuka nyuma na kuwa nguzo ya chumvi katika vikao vijavyo vya bunge.

Hayo ni mawazo yangu......wewe unadhani tutarajie lipi kwa Spika Sitta kwa kipindi kilichobakia cha uspika wake hasa ukizingatia "wenye chama" wameshamwonyesha kadi ya manjano?

Kuwabana wapinzani kwa kutumia kanuni za Bunge na kufanay delaying tactics katika issues
 
Ninachoamini ni kwamba siasa za Tanganyika hazitabiriki hata kidogo na kumbuka Politicians have no permanent friends but permanent interests, inategemeana Bwana Spika alikuwa anafanya hayo aliyokuwa anayafanywa kwa maslahi ya nani. kama kweli amedhamiria kupinga vita ufisadi hatatishwa na chama na ataendelea. Akiendelea mwisho wake utakuwa kama wa Lyatonga, yeye binafsi anajua hilo. Naamini walionyuma yake hawataweza kumshawishi aendelee na nguvu aliyo nayo sasa. Tutarajie uliberali mkubwa katika mapambano haya
 
vyovyote vile nadhani tuangalie kama Spika ataendelea na mambo ambayo amekuwa akiyafanya na kuonekana kero kwa upande mmoja au atabadilika! swala la kuwa yupi ni mkweli itajulikana baadae ikiwa ni pamoja na mikutano ambayo imeandaliwa kabla kabla ya kikao cha NEC ya akina Sita na wenzake hususani wilaya ya NZega. tupunguze munkari ukweli u njiani waja
 
Ccm acheni kuipeleka nchi kubaya. Watanzania tuna macho na masikio.
 
- Hela zote walizi-invest kwa wajumbe wa visiwani knowing kwamba huwa wanaweza kumtishia Muungwana, lakini wakachemsha Spika ana support kubwa sana ya wabunge aliowapa marupu rupu mengi ya ajabu, lakini the damage is done na ninaamini kwamba Spika hatarudi bungeni kwani anahitaji miracle kushinda tena jimbo!

Respect.

FMES!

haa haa haa ee jamani watu wanafatilia mshiko mpaka kujua umeishia ZNZ kazi kweli kweli
 
haa haa haa ee jamani watu wanafatilia mshiko mpaka kujua umeishia ZNZ kazi kweli kweli

Of course! kama chanzo cha hizo pesa kinajulikana (EPA=Milambo street) then ni rahisi kutabiri au kujua mwisho wake (kuziba midomo wazalendo na kununua busara za vikao vya CC na NEC).
 
ccm na sitta wenu na watanganyika nyote upeo wenu kisiasa ni mdogo sana,
msitubabaishe nyote ni vilaza tu.
mnakwenda kwa emotion sio hoja.
sisi hapa ukumbini tungependa hoja zaidi mtu akitoa hoja ajibiwe kwa hoja sio upumbavu na kurukia mada kujihami kwa kutaja watu wengine sitta na ristam ni sawa tuu wote mafisadi papa,nyangumi utavota.
 
Kulia ni utamaduni wa kiafrika. Ni ishara inayonyesha -uchungu- kukereketwa kulikopita kiasi, kuumizwa na jambo fulani. Kulia siyo ubwege- ni ishara ya ufahari.

Hapana mkuu kulia sio utamaduni ni tukio amablo linafanywa na kiumbe yoyote aina ya mnyama.
 
Tuache haya mambo ya kujifanya kuwa eti miongoni mwa wachangiaji wa forum hii walikuwepo kwenye kikao cha nec hicho cha kihistoria. Huo ni uongo. aliyesema kuwa alikuwemo kwenye kikao hicho ni mwongo mkubwa. Tujadili issues zilizojitokeza katika nec bila jazba wala kudanganyana. Ilikuwa ni lazima Sitta aonekane kuwa ameomba radhi. Ilibidi atumie maneno ya kidiplomasia katika kuizima hoja ya kumvua uanachama, kupoteza uspika na kwa kufanya hivyo kuisambaratisha CCM.

Wako wanaodhani kuwa yaliyotokea Dodoma ni madogo, hapana, ni makubwa. Wabaya wa Sitta walijipanga kwelikweli kumng'oa. Swali kubwa ambalo hatuna budi kujiuliza ni kuwa je, kama wangefanikiwa kumng'oa Sitta hali ingekuwaje? Siyo rahisi kutabiri lakini inawezekana kuwa huo ungekuwa ndiyo mwisho wa mshikamano ndani ya CCM.

Unapochambua kilichotokea Dodoma ni lazima uende mbali zaidi. Je, wajkumbe wa Nec ni akina nani na wako wangapi? Je, misimamo yao ikoje? Je, wajumbe hao wa nec misimamo yao inawakilisha wanachama wengine wa CCM nchi nzima? Je, wanec hao waliingiaje katika nec? je, inawezekana lile wanec hawa wengi wao waliingia katika nec kama kundi na ndiyo maana kilichotokea Dodoma kinadhihirika?

Je, misimamo ya nec na ile ya bunge inashabihiana? je, ni idadi ya wabunge wa ccm walioko nec inazidiwa na wanec wengine?

Haya ni maswali magumu ambayo ni lazima tuyatafutie majibu kwa uchambuzi yakinifu kama kweli tunaitakia mema nchi hii.

Ni maoni yangu kuwa ilibidi Sitta aombe radhi au aonekane kuwa ameomba radhi ili kukinusuru chama. Nina hakika wabaya wa Sitta hawajafurahi kuona Sitta amepona. Baadhi yao walisema wazi kuwa akiachiwa atakuwa sawa na nyati aliyejeruhiwa na kuwadhuru baadaye. Tusubiri tuone kitakachotokea muda siyo mrefu ujao.

Mimi binafsi jambo ambalo sijalielewa mpaka sasa ni kuwa ilikuwaje Sitta asuigundue kuwa wabaya wake wanajipanga kwenye kika hicho cha nec na hivyo naye ajiandae? Kwani ni ukweli usiopingika kuwa wote waliomshambulia sitta walikuwa wamejipanga vizuri nani azungmze na afuatiwe na nani na nani amalizie katika "kumyonga' Sitta.Je, Sitta hakuliona hilo? Au ni kweli hawana wafuasi wa kumuunga mkono?

Swali kubwa jingine la kujiuliza ni kuwa je, umma uko upande upi kati ya misimamo ya sitta na wabaya wake? Je, inawezekana kuwa kama sitta angetoswa angeonekana shujaa miongoni mwa wananchi na wanachama wa kawaida wa CCM?

Jamani nchi yetu inayumba. ' Bila CCM imara nchi itayumba'.

Kwa hakika tuko katika kipindi kigumu mno. Watanzania tuna mtihani mzito.

Idumu Tanzania, Wadumu wale wote wanaoipenda nchi hii kwa dhati.
 
wewe 1954 mawazo yako ni finyu sana sana unaongea pumba tupu.
nani kakwambia bila ccm nchi itayumba acha upumbumbavu wa miaka ya nyerere mpaka leo unamawazo ya kinyerere nyerere.

ama kweliiii watanzaniaa tuko nyuma kweliiiii DUHHHHHHHHHHHHHH!
 
We ulikuwepo? ua unabisha tu? maana sentensi zimejaa "Kwa maoni yangu"
 
Tujifunze kwa chadema.
Hoja ikigonga mwamba mujengoni, ipelekwe kwa wananchi bila woga na hapo ndipo kifo cha waliokunywa maji ya kijani kilipo.
Sita akiogopa aogope kivyake; akitaka kuwabana wapinzani bungeni hawezi kuwabana kwenda kwa wapiga kura na kuwambia ili uamuzi uwe wao.
 
Unafikiri wakishika nchi watawaleteeni tena hoja wananchi!!!! thubutuu! muwachape tena kama Tarime..hahahaha
 
Chama Cha Mapinduzi ni chama cha wananchi. Kiongozi yeyote aliye madarakani kwa tiketi ya CCM aelewe kuwa nafasi hiyo aliyonayo ni dhamana aliyopewa kwa ridhaa ya wanachama wa CCM. Haitavumilika wala kukubalika kwa kiongozi yeyote yule anayetokea CCM kutumia nafasi hiyo kwa ajili ya kujijenga binafsi kwa gharama ya kuharibu maadili na maslahi ya chama. Pia ieleweke kuwa Chama cha Mapinduzi kina utaratibu na, viongozi na wanachama waliomakini katika kukabiliana na matatizo yanayoweza kujitokeza ndani na nje ya Chama.
Endapo kiongozi yeyote yule amekwenda kinyume na maadili au maslahi ya Chama basi hana budi kuwa muungwana na kuomba radhi na ajisahihishe. Vinginevyo, arudishe kadi!

Safi sana, Ndio maana mmemuacha Chenge hadi leo kwenye kamati ya maadili asimamie maadili/maslahi yenu ya kifisadi!
 
Unapochambua kilichotokea Dodoma ni lazima uende mbali zaidi. Je, wajkumbe wa Nec ni akina nani na wako wangapi? Je, misimamo yao ikoje? Je, wajumbe hao wa nec misimamo yao inawakilisha wanachama wengine wa CCM nchi nzima? Je, wanec hao waliingiaje katika nec? je, inawezekana lile wanec hawa wengi wao waliingia katika nec kama kundi na ndiyo maana kilichotokea Dodoma kinadhihirika?
Sawa Ndugu yangu tuyaangalie hayo kwa undani. Lakini na wewe muangalie Sitta na Uspika wake- Huo ubabe wake na hizo jeuri zake - Si afahamu tu kuwa kuna na CCM na ndiyo inayodhamini huo Uspika wake. Ikiwa kama ameomba radhi - yamekwisha hayo. Siiratta-l- mustakina.
 
Tehe tehe tehe heeee kwi kwi kwi😀

Amekaangwa kweli kweli "kikaangoni' akitoka atabakia nchele bila pumba! tehe thee😀😀

Ngoja nipumzike manake kawimbo haka sasa...'sitta' sitta' 'sitta' 'sitta' ebo!😱

Bado mie CCM.
 
Wakuu tunaendelea kuchambua yaliyojiri kwenye kikao cha juzi NEC, Dodoma:-

- The More dataz ni kwamba Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Bwana Wilson Kusila, ambaye huko nyuma kuliwahi kuwa na ripoti kwamba alipewa jumla ya shillingi Millioni 10 na Rostam, ili kuweza kumshinda Bwana Masima, aliyegombea naye nafasi hiyo ya mkoa wa Dodoma, alitaka wapiganaji wote kufunguliwa kesi ya uhaini.

- Alipopewa nafasi ya kuzungumza na Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri, alienda mbali zaidi na kutaka mashitaka ya uhaini yafunguliwe mara moja kwa Spika na wapiganaji wote, kwa sababu wanachokifanya bungeni kwa kushikiriana na Spika, ni Uhaini period!

- Huku wajumbe karibu wote wa mkutano huo wakiwa wamepigwa na mshangao, Kusila aliendelea ku-charge kwamba Uhaini huu unaanzishwa na kuendeshwa na waliokosa Urais kwenye uchaguzi wa Mwaka 2005, hawa wakamatwe mara moja na kufikishwa kwenye mkono wa sheria za jamhuri na hasa Spika Sitta, wakati wote huu Mwenyekiti wa CCM hakuficha kabisa furaha yake akimsikiliza kwa makini sana Kusila na huku akimuashiria kuendelea na hoja zake!

- Kusila aliendelea kwa kumuomba radhi Rais Mkapa, akisema kwamba "..unashambuliwa na hawa wahaini kwa sababu moja tu, nayo ni kwamba ulimchagua Kikwete kwenye urais wa 2005 na ukawaacha wengine...", hapa Mkapa akasimama juu na kupiga makofi huku akicheka sana, huku pembeni Mwenyekiti wa CCM akiendelea kucheka kwa sauti ya juu sana,

- Kusila alimalizia kwa kudai "..hata hawa wanaosema bungeni hapatatosha wote ni wahaini wakubwa na wakamtwe na kufikishwa kwenye mkono wa sheria maramoja!..."

Respect.

Field Marshall Es!

NB: Wajumbe wengi wa kikao hicho wanajiuliza swali moja muhimu, kwamba kwa nini Rais aliruhusu kutokea kwa yote yaliyojiri kwenye hiki kikao?
 
Back
Top Bottom