Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,276
125
Nyepesi nyepesi zinazojiri kutoka NEC ya CCM Dodoma jana Spika Samwel Sitta kawekwa mtu kati kwa namna anavyolipeleka Bunge mpera mpera.

Miongoni mwa wachangiaji waliomshambulia wazi wazi ni Mwenyekiti wa CCM Shinyanga ambae bila kumung'unya maneno alimwambia Sitta alirudishe kadi ya CCM. Kwa ujumla wachangiaji wengi wameonyeshwa kutoridhiswa na utendaji wa Sitta isipokuwa wawili tu Eng Stellah Manyanya na Mh John Shibuda.

Chungu kimefunikwa na kikao kinaendelea leo ambapo tusishangae kusikia Sitta kasitishwa U-Spika.

Stay tuned...
 
Last edited by a moderator:
huyo mwenyekiti wa mkoa wa Shinyanga ni nani? Mbona anakuwa Mjinga hivyo, wakati watu waliopata maafa ya Ufisadi ni wa Mkoa wa Shinyanga, maana madini yamechukuliwa, wakati miundo mbinu ya mkoa ni duni, elimu duni, umeme kimeo etc
 
Mara nyingi namna yetu ya kuangalia tatizo ndo tatizo lenyewe
 
Unajua Tanzania huwa tunawapa madaraka watu wazembe sana,hivi hoja ya huyo kiongozi ni nini hasa?
 
huyo mwenyekiti wa mkoa wa Shinyanga ni nani? Mbona anakuwa Mjinga hivyo, wakati watu waliopata maafa ya Ufisadi ni wa Mkoa wa Shinyanga, maana madini yamechukuliwa, wakati miundo mbinu ya mkoa ni duni, elimu duni, umeme kimeo etc

Mh!!!!! Kwani mmemsahau Hamisi Mgeja? Kipi tutakachoshangaa kusikia kuwa Mgeja anamshambulia Sita. Kama mtakumbuka Huyo Mgeja akiongozana na Mabina, ndiye aliyeongoza maandamano ya kumlaki Chenge baada ya kashfa ya vijisenti.

Should we expect anything different?
 
Mh sitta pamoja na wewe una matatizo lakini wakitaka kadi yao wape ukaungane na Slaa upande wa pili. Tunahitaji nguvu upande wa pili
 
Jamani!!! waachani wafu wawazike wafu wenzao, huu ndio mwishon wa CCM maamuzi wanayotoa ni ya yarabi nafsi yangu. dawa ni mgombea binafsi hakuna mwenye busara atakayegombea kwa tiketi ya hicho chama. wanawafagilia njia wapinzani hivihivi! nicheke mie tusubiri. KIDUMU CHAMA CHA WENYEWE
 
Sasa huyu anayejitahidi kuweka sawa mambo anashambuliwa kwa sababu chama kimeshika hatamu! Manyang'au wengi wanajificha kwenye mwamvuli wa hatamu za chama. Argh!!
 
Kwenye mabadiliko ya kweli, kusigishana ni jambo la kawaida maana kuna wanaoona wanapoteza kutokana na faida wanayopata na system iliyopo. Lakini kama ilivyo ngumu kuzuia thumani isipite, mabadiliko yatakuja tu hata kama CC, NEC na CCM wataamua kugoma. Hii inatokana na ukweli kwamba muda unabadilika, elimu imebadilika na juu ya yote na pasipo shaka, watu nao wanatamaa ya kuona mabadiliko. Kazi kwenu..mkimalizana na Sitta sijui atafuatia nani
 
8D6U1287.JPG

Tumwombee Spika amefanya mabadiliko kwenye bunge letu mpaka mawe yanaongea.
 
Nyepesi nyepesi zinazojiri kutoka NEC ya CCM Dodoma jana Spika Samwel Sitta kawekwa mtu kati kwa namna anavyolipeleka Bunge mpera mpera.

Miongoni mwa wachangiaji waliomshambulia wazi wazi ni Mwenyekiti wa CCM Shinyanga ambae bila kumung'unya maneno alimwambia Sitta alirudishe kadi ya CCM. Kwa ujumla wachangiaji wengi wameonyeshwa kutoridhiswa na utendaji wa Sitta isipokuwa wawili tu Eng Stellah Manyanya na Mh John Shibuda.

Chungu kimefunikwa na kikao kinaendelea leo ambapo tusishangae kusikia Sitta kasitishwa U-Spika.

Stay tuned...

Hamis Mgeja Mwenyekiti wa CCM Shinyanga,.....

Aliyemuandalia mapokezi ya kufa mtu mzee wa vijisenti baada ya kujiuzulu uwaziri kufuatia kashfa ya vijisenti.

Ana kashfa ya kujitafunia vijisenti vya halmashauri ya wilya ya Kahama kiasi cha zaidi ya milioni 70 alipokuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo.

Haishangazi kwa yeye kumshambulia Sitta,(hata kama spika ana matatizo), kwa namna anavyoliongoza bunge, mafisadi na uzao wao lazima wachukie, wanune, na watafute mbinu za kupunguza mashambulizi.
 
naama, nilivyo ona katika mikoa mingi viongozi wengi wa mikoa wa ccm, ni watu walio na kashfa aidha ya kula hela za halmashauri au za ushrika, na ninafikiri ccm makao makuu/ mwenyekiti hasa wakati wa mkapa aliruhusu hali hiyo ili nae akiiba, hakuna wakumsema, maana alikuwa anawaambia Fulani naona kuna faili lako huku takukuru, lakini nitakusaidia, wazee wa watu bila kuelewa kitu wakaachia madini yote yameenda. maana wakimbishia jamaa, anawafunguliwa 100% PCB, na mahakama wafanye kazi yao.
 
Mh sitta pamoja na wewe una matatizo lakini wakitaka kadi yao wape ukaungane na Slaa upande wa pili. Tunahitaji nguvu upande wa pili

Arurishee!! Tangu lini mambo haya yakatokea CCM. Huko ni kubanana mbele kwa mbele. Hatoki mtu pale hata kama maji yako shingoni. TZ hakuna ambitious politician wa ukweli wote ni waganga jaa tu na bendela fuata upepo.
 
Hivi huyo kiongozi ana akili timamu.Huyo naona amehongwa na akina Lowassa . nionavyo mimi hana tofauti na kingunge .akili zao zina uchafu . wanahitaji msasa ili kuzisugua. Naona afadhali baba wa taifa alijifia mapema .Na hawa ndio waliompa presha. Hawa ni afadhali kuongoza watoto wadogo . Hivi wanafikili watanzania wamelala tu kama zamani? Nahayo mayebo yebo yenu mmnayoyajenga si kwamba wanaambulia hata kidogo? mwisho wa maneno majukwaani umeisha sasa ,ahadi na vitendo au nje. Hakuna malefu yasiyo na icha.
YOU CAN LIQUIDATE PEOPLE, YOU CAN BAN ORGANIZATIONS,BUT REVOLUTIONIALLY IDEAS NEVER DIE>......................................................
 
Wana Jf taarifa zilizonifikia sashivi ni kwamba JK amemuita Sita na kumwambia kuwa hali ya ukumbi umeina nitakupa DK kumi ujiteteee ukizitumia vizuri utapona ukishindwa kuzitumia sitazuia wazo la wewe kutakiwa kurudisha kadi ya ccm.

Taarifa zaidi ni kuwa babu sita wapambe wote wamemkimbia hakuna anesimama kumtetea na anaonekana mpweke amebaki na mama sita ambae inaaminika anatiiza wajibu wa mke kwa mumewe.
 
Natamani airudishe hiyo kadi ili kupambazuke, na Giza na Mwanga vijitenge.
Mama Sitta nae naamini atarudisha hiyo kadi yao.

Je kina Rostam, Chenge na Lowassa pia hawajatakiwa kurudisha. Najaribu kuimagine ikiwa hatarudisha na December Bunge.
 
Back
Top Bottom