Mtatiro: Hatua za Bunge, Lipumba na msimamo wangu! Na maajabu ya Bunge na serikali ya CCM

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,571
2,000
HATUA ZA BUNGE, LIPUMBA NA MSIMAMO WANGU!

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J,
[HASHTAG]#NewYork[/HASHTAG].

1. Juzi Jumatatu Lipumba na Sakaya walimuandikia Spika wa Bunge kumjulisha kuwa "Baraza Kuu la CUF" (feki) limewafukuza uanachama Wabunge 8 wa Viti Maalum wa CUF. (Spika alishaandikiwa na Katibu Mkuu kumjulisha kuwa Baraza Kuu halali la CUF ni lile lililochaguliwa mwaka 2014 na muda wake utaisha mwaka 2019 na Baraza hilo halali ndilo lililomfukuza Lipumba).

2. Jana, Jumanne, Ofisi ya Bunge ilitoa taarifa kwa umma kuujulisha kuwa imepokea maelekezo kutoka kwa Sakaya na Lipumba kuwa wabunge hao 8 si wanachama na Ofisi hiyo ikaeleza kuwa bado inatafakari hatua za mwisho za kuchukua.

3. Leo Jumatano, Ofisi ya Bunge imetangaza uamuzi wake, kwamba inakubaliana na maelekezo ya Lipumba na Sakaya na kuwa imewavua wabunge hao 8 ubunge wao wa Viti Maalum, na kuwa imeiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuijulisha kujaza nafasi hizo zilizo wazi.

_________________________________________
Nataka kuwaeleza wanachama na watanzania wote, kwamba viongozi wa chama wanakutana kuendelea kuchukua hatua.

Tunajua kuwa Vyombo vya Serikali hivi sasa vinafanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa aidha CUF inamkubali "MSALITI" Lipumba kuwa Mwenyekiti wake, au CUF isambaratike. Na suluhisho la hali hii haliwezi kuwa kukaa chini na MSALITI.

Mnapopambana na WASALITI WALIOKUBUHU na wako ndani ya nyumba yenu, vita yake siyo ndogo. Lakini mimi binafsi ni muumini mkubwa wa HAKI na UKWELI. Naamini kuwa CUF itavuka misukosuko hii.

Kwa jicho moja wapo watu wanachekelea na kudhani kadhia hii ni ya CUF tu, mimi natizama hali hii kama Mapambano ya Dola ya kuhakikisha vyama mbadala vinaongozwa na wasaliti ili Dola iendelee kuwatumia kuzamisha demokrasia na ushindani wa kisiasa nchini.

Dola ikifanikiwa kuisambaratisha CUF, vyama vingine vya upinzani havitakuwa salama, taasisi zingine za kiraia hazitakuwa salama pia. Anayeyatizama mapambano haya kama vita ya ndani ya CUF hajaisoma dunia - haya ni mapambano makubwa, dhidi ya demokrasia ya Tanzania.

Mimi ni mwanademokrasia imara na sitayumbishwa na WASALITI. Kumkubali Lipumba na genge lake itakuwa na maana ya kuiua CUF moja kwa moja Tanzania Bara, maana alipojaribu kukimbia mwaka 2015, ndipo CUF iliibuka na kuwa chama imara mara 10 Tanzania bara. Na kurudishwa kwake kwa nguvu kunakofanywa na dola ni mkakati wa kuimaliza CUF na suluhisho lake haliwezi kuwa CUF kumtambua Lipumba.

Hata DOLA ikifanya nini, LIPUMBA ameshadharaulika na hawezi kuisaidia tena dola hii yenye upofu. Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. Seif Sharif Hamad na viongozi wa chama wanaendelea na hatua mbalimbali muhimu na mtajulishwa

Vita imeshapanuka, sasa ni LIPUMBA, OFISI YA MSAJILI WA VYAMA, RITA, BUNGE, NEC, IKULU, USALAMA WA TAIFA na CCM. Kundi lote hilo linaamini kuwa bila kumrudisha Lipumba halitaweza kuidhibiti CUF. Sisi viongozi tuko imara sana na tunaamini kuwa HAKI huweza kucheleweshwa tu!

We shall OVERCOME this! More Stable! And more Vibrant!

[HASHTAG]#JSM[/HASHTAG], 26 Julai 2017.

----------UPDATES 27 July, 2017---------

MWENDOKASI WA VI-WONDER TANZANIA!

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J,
#NYC_USA.

[HASHTAG]#Jumapili[/HASHTAG], Tarehe 23/07/2017, Saa 4 asubuhi - Kikao (Feki) cha Kamati ya Maadili ya Lipumba.

[HASHTAG]#Jumapili[/HASHTAG], Tarehe 23/07/2017 (siku hiyo hiyo), Saa 8. Mchana - Baraza Kuu (Feki) la Lipumba.

[HASHTAG]#Jumatatu[/HASHTAG], Tarehe 24/07/2017 asubuhi -
Barua ya Msaliti Lipumba kwenda kwa Spika wa Bunge.

[HASHTAG]#Jumanne[/HASHTAG], Tarehe 25/07/2017 - Ofisi ya Spika yakiri kupokea Barua ya Lipumba na Sakaya, yaujulisha umma na kueleza itafanya uamuzi baadaye.

[HASHTAG]#Jumanne[/HASHTAG], Tarehe 25/07/2017 jioni - Katibu Mkuu wa CUF (Seif Sharif) amuandikia Spika wa Bunge kumjulisha kuwa Barua za Lipumba na Sakaya ni Feki kwa sababu Lipumba si mwanachama, na kubwa kuliko yote hakuna kikao cha Baraza Kuu HALISI na HALALI kilichofanyika, maana vikao vyote vya chama havimuungi mkono Lipumba.

[HASHTAG]#Jumatano[/HASHTAG], Tarehe 26/07/2017 mchana - Spika aridhia kufukuzwa wabunge 8 na apeleka taarifa NEC. Adharau na kukiuka hata taarifa halisi aliyopewa na Katibu Mkuu kuwa barua alizopelekewa na Sakaya na Lipumba hazitoki kwenye mamlaka ya Baraza.

[HASHTAG]#Jumatano[/HASHTAG], Tarehe 26/07/2017 Jioni - Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaridhia na kutoa agizo kuandaliwa wa Wabunge wapya ikishawasiliana na Lipumba

Tarehe 27/07/2017 Asubuhi - NEC yatangaza Wabunge wapya wa Lipumba.
_________________##_####____________
[HASHTAG]#Najaribu[/HASHTAG] kujiuliza, Kasi hii ingetumika kuleta viwanda tangu John Magufuli aingie madarakani, hivi sasa si Tanzania ingekuwa na kiwanda cha ndege? Yaani Bombardier zingetengenezewa hapo nchini!

[HASHTAG]#Kasi[/HASHTAG] hii ingetumiwa na Serikali kutoa huduma hospitalini, shuleni, ofisini n.k. wagonjwa wasingekufa kwa Maradhi ya kijinga kwenye foleni za Upasuaji na huduma nyepesi.

[HASHTAG]#Kasi[/HASHTAG] hii ingetumiwa na serikali kusambaza umeme na maji safi na salama, kusingekuwa na familia inapoteza wapendwa wao kwa sababu ya maradhi ya maji.

[HASHTAG]#Kasi[/HASHTAG] hii ingetumika kupambana na mafisadi, wale wote waliongia mikataba ya kipuuzi ya madini, na walioisababishia nchi hasara kubwa kwenye sekta ya ujenzi, taifa letu lingekuwa la haki kweli kweli.

[HASHTAG]#Kasi[/HASHTAG] hii ingetumika kujenga viwanda vya nguo alivyoahidi JPM wiki iliyopita, hivi sasa (leo, kutokea wiki iliyopita) tungekuwa tunapandisha marobota ya mitumba kuwapelea wazungu wakavae Ulaya!

KASI! SPIDI! MBIO! MFUKUZANO.... call it any name!

@Nilikuwa naangalia uzinduzi wa Treni ya Risasi (Bullet Train) inayotembea Kilomita 350 kwa saa iliyozinduliwa nchini China jana. Post hii haihusu yanayoendelea huko nchini.

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J

HAKIKA KWA MWENDO KASI HUU TANZANIA YA VIWANDA NI SIKU CHACHE TU ZIJAZO.
 

vicdala55

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
986
1,000
Ni mpumbavu pekee anayeweza kushangilia ujinga huu!
Na ni Kiongozi asie makini pekee ndiye anayeweza kubariki unajisi huu wa haki!
Duniani kote na sehemu zote zilizopoteza Amani, watu wake hasa viongozi walitenda matendo haya.
Natabiri Amani ya Nchi hii itavurugika si muda mrefu. Ni vigumu kupora haki za watu kila kukicha kisha mtarajie utulivu.
Na kwa kuwa tumejawa unafiki, sitashangaa wapinzani wakipewa lawama baada ya Amani kutoweka!
Ifikie wakati wenye magonjwa mazito wazuie kuendelea na nyadhifa nyeti kwa usalama wa Nchi hii!
Uwezo wao wa kufanya maamuzi sahihi umeyumba!
 

mumburya

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
318
500
Wakuu mnakumbuka mahakama ilichukua juma moja kuondoa utata wa amri ya TRUMP Kwamba ni halali au sio halali. Jibu likawa ni HALALI na watu wakaendelea kuingia USA.

Sasa huku TZ, kuna utata, na kesi ipo mahakamani: LIPUMBA ni mwanachama/mwenyekiti halali au sio halali?

Sasa umekatika mwaka na nionavyo mimi uamuzi utatolewa 2021. Sababu ni nini?
je, athari za kuchelewesha kuondolewa utata ni zipi? je, mahakama zetu zipo huru kweli?
 

izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,814
2,000
Samahani waiter ongeza glass eee muhudumu ongeza glass ×2
Acha nilewe……nilewe tu.
Ee nilewe…. nilewe tu. aiwezekani umeingia Bungeni kwa tiket ya CUF ambae mwenyekiti wake ni Lipumba then maagizo unayapokea kutoka kwa Mbowe na Lissu
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,147
2,000
Mtatiro endelea kula bata huko uliko...mmewadanganya wabunge sasa washapigwa chini.


Nidhamu nidhamu
 

Mr.Junior

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
10,531
2,000
Ni mpumbavu pekee anayeweza kushangilia ujinga huu!
Na ni Kiongozi asie makini pekee ndiye anayeweza kubariki unajisi huu wa haki!
Duniani kote na sehemu zote zilizopoteza Amani, watu wake hasa viongozi walitenda matendo haya.
Natabiri Amani ya Nchi hii itavurugika si muda mrefu. Ni vigumu kupora haki za watu kila kukicha kisha mtarajie utulivu.
Na kwa kuwa tumejawa unafiki, sitashangaa wapinzani wakipewa lawama baada ya Amani kutoweka!
Ifikie wakati wenye magonjwa mazito wazuie kuendelea na nyadhifa nyeti kwa usalama wa Nchi hii!
Uwezo wao wa kufanya maamuzi sahihi umeyumba!

Wa kuharibu amani ni Watanzania hawa wa siku zote au kuna wengine?

Kama uchaguzi Zanzibar ulifutwa ukarudiwa na maisha yanaendelea hakuna jipya Watanzania tutafanya labda kizazi cha vitukuu vya wajukuu zetu.
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
26,073
2,000
Watu kama kina mtatiro ndio wanaoangusha chama.
Hatua zimechukuliwa yeye analeta kebehi,hivi Mtatiro kusoma hajui hata picha haoni.
Ruzuku hawana.
Bodi ya wadhamini yao imevunjwa,inayotambulika ni ya Lipumba
Halafu bado anaandika gazeti kama vile wamekidhibiti chama
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom