Field Marshall Es,
Mkuu wangu huwezi kuwajua wabaya wako bila kuwapa nafasi wakajikaanga wenyewe.. maneno mazito yaliyosemwa against Sitta ni ushahidi tosha wa watu waliopo nyuma ya Lowassa na RO..this is what JK alikuwa akihitaji siku zote.. names!..Tena basi wamepatikana na wengine waliokuwa wamejificha kwa sababu tu walifikiria JK yuko nao pamoja..
FMES, kwa lugha yetu ya kizamani unaitwa borntown,hivi kweli unaamini JK angetaka Sitta atolewe nje angekuwa na mazungumzo naye baadaye!.. Mbona asimshauri Lowassa kuomba msamaha bungeni..JK anamhitaji Sitta na kazi yake kaifanya hasa ktk mkutano huu mkuu kwani prediction za mzee Malecela zilihusiana zaidi na watu wanaotakiwa kusimama Ubunge mwaka 2010. By now wameisha jua wataanzia wapi kufanya usafi kisha mtaambiwa wananchi kuwa wachafu wote wameondolewa!..Na wananchi wasipokaa macho mshindi CCM kwa goli la kilaini utadhani Droba dakika ya 90 kuleta ushindi.
nashawishika kuamini kwamba MAFISADI WATASHINDA!
- Very strong analysis Bob, lakini the damage was done mkuu, kama sio hoja ya kumng'oa Makamba kuchomekewa na wapiganaji mle ndani ya kikao, saa hizi Six angekua njiani kurudi Urambo tayari mazee! maana Muungwana ni mazishi bro, halafu umesikia mafisadi walivyomchokonoa Mengi tena! Inasikitisha sana! Bob Muungwana hatabiriki, muulize Mkulu Saeed.
Respect.
FMEs!
Naomba Mungu hadithi zako ziwe za uwongo kwani hakuna mtu anayenikatisha tamaa kama wewe. JM anayepanga mikakati ya kuiba kura (busanda) ni hatari sana. Tunapoongea kung'oa mafisadi nadhani na yeye yumo!
Mkuu unaweza tutajia waliokuwa upande wa six na walio upande wa Muungwana?? muungwana atabirike kivipi wakati group lake linaeleweka ni mtandao halisi yani Lowasa,Ra,Nchimbi nk
Wacheni ushamba huo. Sisi hatubabaiki na vijipesa kama hivyo. Na kwa taarifa yako wajumbe wa Visiwani(sema Zanzibar mara nyengine) are not cheap as you are. Lakini huyo Spika wenu haizungumzii Zanzibar -uzuri- ndiyo anakandiwa hivyo. Tafuta kumbu kumbu kuna wakati fulani Spika aliepita (Msekwa ) alikandiwa hivyo hivyo na wajumbe wa Zanzibar kwa sababu ya hulka yake ya kuisema vibaya Zanzibar. Ni jambo zuri kuwa alijirekebisha. This is food for thoughtdu kembe mil 50 inaweza kufanya mambo mengi kiasi hicho
siamini!!!!!
kweli wajumbe wa nec ccm ni very cheap?????
ndio maana kila siku wanarudi kuwa omba omba, sasa hiyo mil 50 wakigawana itawapeleka wapi
halafu wenzao wanakamua bil 50
- Muungwana ana kundi moja tu sasa hivi nalo ni yeye na Membe, that is it! the rest anacheza tu mchezo wa kuigiza!
Respect.
FMEs!
Yote hii ilipangwa babuuu, kama JK angetaka Sitta awe nje hakuna mtu yeyote angepinga lakini kwa ujinga wao walifikiria JK yuko nao na huu ndio mwisho wa makelele ya Sitta bungeni.- Very strong analysis Bob, lakini the damage was done mkuu, kama sio hoja ya kumng'oa Makamba kuchomekewa na wapiganaji mle ndani ya kikao, saa hizi Six angekua njiani kurudi Urambo tayari mazee! maana Muungwana ni mazishi bro, halafu umesikia mafisadi walivyomchokonoa Mengi tena! Inasikitisha sana! Bob Muungwana hatabiriki, muulize Mkulu Saeed.
Respect.
FMEs!
Duh, kama ni kweli basi anatakiwa kufikiria kwa mapana kauli kama hiyo!Kiroja cha mjadala alikuwa Guninita, Mwenyekiti wa Mkoa wa DSM aliyechemka lakini JK akamzodoa kwa kumwambia "kama ana uchungu na chama mbona alikiacha na kwenda CHADEMA na kuitukana CCM kwa miaka miwili?"
Nidhamu hairejeshwi kwa kukumbatia ufisadi. CCM imepoteza mwelekeo, chama kilichodaiwa kuwa cha wakulima na wafanyakazi sasa kimetekwa na mafisadi na ndiyo ambao wanaongoza nchi. Ninawashangaa ambao sio mafisadi kuendelea kung'ang'ania chama ambacho kimeishaonyesha wazi kwamba mwelekeo wake ni upi.
Hao mafisadi wanaomwaga hela ili kupata support kwenye NEC na CC, hawaendi kuzomewa wakati wa kampeni na chaguzi, wala hawapazi sauti kwenye majukwaa kujitetea kwamba wao siyo mafisadi.
Tusibiri 2010 inakuja na by then wananchi watakuwa walishajua fisadi ni nani na nani achaguliwe kuwa kiongozi. CCM itakapoteza majimbo ya kutosha ndipo watakapojifunza kwamba walifanya kosa kukumbatia ufisadi.
mi mbona sielewi haya mambo jamani
Ukweli ndo huo. Habari za kuwa Sitta ameomba radhi zinaenezwa na akina Rostam ambao wamehangaika usiku kucha kutugongea vyumbani wakitubembeleza tumtose Sitta. Ndio wameita magazeti mbalimbali kueneza uvumi kuwa Sitta ameomba radhi kwa NEC.
mhh nimechoka kabisa...Nani wa kumwamini sasa....kazi kweli kweli
haya mambo yeu ya kuegemea kundi fulani ndo yanatuchanganya hapa..mambo ya rostam yanatoka wapi..au na wewe ulikuwa dodoma.mara ngapi CCM wanakaa dodoma na vyomba vya habari vinakwenda kuripoti habari..acha ubabaishaji hapa