Wakuu tunaendelea kuchambua yaliyojiri kwenye kikao cha juzi NEC, Dodoma:-
- The More dataz ni kwamba Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Bwana Wilson Kusila, ambaye huko nyuma kuliwahi kuwa na ripoti kwamba alipewa jumla ya shillingi Millioni 10 na Rostam, ili kuweza kumshinda Bwana Masima, aliyegombea naye nafasi hiyo ya mkoa wa Dodoma, alitaka wapiganaji wote kufunguliwa kesi ya uhaini.
- Alipopewa nafasi ya kuzungumza na Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri, alienda mbali zaidi na kutaka mashitaka ya uhaini yafunguliwe mara moja kwa Spika na wapiganaji wote, kwa sababu wanachokifanya bungeni kwa kushikiriana na Spika, ni Uhaini period!
- Huku wajumbe karibu wote wa mkutano huo wakiwa wamepigwa na mshangao, Kusila aliendelea ku-charge kwamba Uhaini huu unaanzishwa na kuendeshwa na waliokosa Urais kwenye uchaguzi wa Mwaka 2005, hawa wakamatwe mara moja na kufikishwa kwenye mkono wa sheria za jamhuri na hasa Spika Sitta, wakati wote huu Mwenyekiti wa CCM hakuficha kabisa furaha yake akimsikiliza kwa makini sana Kusila na huku akimuashiria kuendelea na hoja zake!
- Kusila aliendelea kwa kumuomba radhi Rais Mkapa, akisema kwamba "..unashambuliwa na hawa wahaini kwa sababu moja tu, nayo ni kwamba ulimchagua Kikwete kwenye urais wa 2005 na ukawaacha wengine...", hapa Mkapa akasimama juu na kupiga makofi huku akicheka sana, huku pembeni Mwenyekiti wa CCM akiendelea kucheka kwa sauti ya juu sana,
- Kusila alimalizia kwa kudai "..hata hawa wanaosema bungeni hapatatosha wote ni wahaini wakubwa na wakamtwe na kufikishwa kwenye mkono wa sheria maramoja!..."
Respect.
Field Marshall Es!
NB: Wajumbe wengi wa kikao hicho wanajiuliza swali moja muhimu, kwamba kwa nini Rais aliruhusu kutokea kwa yote yaliyojiri kwenye hiki kikao?