Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Asante sana kwa taarifa hiyo fupi lakini inayoeleweka vizuri.
Nimefuatilia na maoni ya wengine kujua hisia zao nimeona. Ukweli hatuwezi kujua yote yaliyotokea kule mkutanoni, ila hostility ya environment naamini Sitta aliitarajia na ndiyo maana hakuwa na sababu ya kuwapa faida opponents wake kwa kusema mambo mengi. kweli aliyosema kila mtu alitumia haki yake ya kuongea mambo yake, na kilichosalia ni meza kuu kuamua kwa kupima hoja zilizopo mezani na kutumia silaha walizo nazo kuchunguza ukweli zaidi wa hoja hizo kisha kuongeza na busara zao kama kiungo murua cha mapishi hayo na kutuletea maamuzi yao.

Sitta hapotezi heshima kwa wananchi hapo. Of course naye anayo mapungufu yake kama binadamu mwingine, lakini hata wanaomponda sana nao sio malaika, huenda wao ndio pumba zaidi. Wanachokiona kibaya wao ni mazoea ya CCM na serikali kubebwa tu bungeni hata bila mantiki, kulikofanywa spika zilizotangulia. Wakati huo bunge liliendeshwa kiCCM kweli, maana wapinzani walibezwa kila sentensi hata kama ina maana na faida ya kiasi gani.

Ilifikia hata upinzani kuambiwa bayana kwamba hawana kizuri kinachoweza kutokea kwao, kikianza kutokea kilidakwa na CCM na kuwekwa hati miliki, upinzani ukapigwa stop kuendeleza hoja. Aliyejitia kugangamala alipata misukosuko mingi enzi za spika aliyeishia. Sasa huyu wa sasa yuko so balanced kiasi kwamba wakati mwingine unaweza kushindwa kujua kama na CCM huyu au la. Wapinzani this time wamepata hadhi yao sawasawa, walipofulia wameambiwa na walipofanya kweli wamepongezwa na kuelekezwa vizuri zaidi na spika huyu wa sasa. Sidhani kama hata katika wapinzani wapo wengi wabubge wanaompinga sana Sitta. He is an exceptionally genuine guy when it comes to kukalia kiti kile.

Sasa angeomba radhi kwa ajili ya kuwa neutral? CCM na serikali yake wamejikuta hawana pa kujificha tena, wnaambiwa wazi leteni majibu ya uhakika na sio kubabaisha bunge. Mawaziri hawaonewi, wanaambiwa ukweli. Daima msema kweli hakosi maadui. Mungu naye siku zote yuko upande wa msema kweli, wataumbuka wenyewe.

Angalia sasa mafisadi wanatetewa na CCM na serikali yake, wauaji kwa vyeo vyao (Zombe) wanapeta. Maana yake nini? ..... kwamba masikini hana haki milele. Mwenye nguvu apishwe daima. Ataua na hakuna kitakachotokea. Angalia dereva wa Shinyanga aliyeokoa watu kibao kwenye bus lake na kujikuta anaua mpanda baiskeli bila hata kujua, anafungwa miaka 30. Lakini Zombe anayeamuru kuua masikini watafuta maisha na kuwapora mali zao eti sio kosa, tena vyombo heshimika kabisa vinatumika kulinda uozo huo.

Jambo moja liko wazi, kwamba Mungu humlipa kila mtu stahili yake. Huwezi kuua na ukakata viuno barabarani for free. Kumbuka Dito, kumbuka aliyesababisha kifo cha Sokoine ..... Tatizo la CCM ni kwamba siku zote wanaccm wamekuwa wakiogopa kuwa wakweli wasije wakafa masikini au wakapoteza maisha kabisa. Kumbuka Katibu Mkuu wa zamani mbunge wa Ludewa, yuko wapi yule mdada wa majuzi, nani nani nani yule mrembo wa kimakonde Chifupa ati?

Lakini bora kufa mwenye haki kuliko kufa fisadi. Historia itakukumbuka, hata hao wabaya wako watasutwa na ukweli huo. DSM sasa hivi inapendeza pavements mjini, vivuli vya miti kila mahali, nyumba zina rangi safi, nani huyo kama sio Lyatonga? Leo hii haonekani kwa maneno lakini historia inamkumbuka sana Lyatonga. Siku saba bado zinatumika na wat wa serikalini hata leo.

Leka
 
nchi hadi ilipo haina mwenyewe, watu wanakaa na kuanza kutunga sentesi za uzushi ili kuwaaminisha watu kuwa hiki ni hiki, hii sio sawa, sasa napata picha kuwa kama kweli aliomba radhi hao wajumbe naona wasinge kuwa na haja ya kuunda tume ila kwa kuwa amewaambia waamue cha kufanya imewastua na kuamua kumuundia tume ili kumchunguza wajue amepataje huo ujasiri
 
Nani kukuambia kuwa wabunge wengi hawana imani na Sitta? au umefanya research lini? NEC siyo wabunge wa CCM, kwani bunge lina-members wangapi? na walioko NEC ni wangapi? hata huko NEC si wote wanaompinga.

Pia unapaswa kujua kuwa waananchi wengi wanachukia ufisadi hasa suala la Richmond na EPA. Sitta akiachia kiti, itakuwa hatari kubwa kwa CCM kwani itaonyesha wazi na rasmi kuwa CCM ni chama cha mafisadi.

Hili suala la Mh.Sitta sio dogo kama hivyo unavyofikiri,kabla ya kufika kwenye NEC ya CCM lilijadiliwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Chama kabla ya kupelekwa kwenye CC baada ya kuwa na Mshike mshike huko ndio likapelekwa kwenye NEC ambako pia Wabunge wengi wa CCM wapo huko.

Kwa Utaratibu wa maamuzi ya CCM mpaka jambo hilo limepita katika Vikao vitatu vya Chama ujue kuwa ni jambo kubwa na zito,hata hao Viongozi wakuu wa chama wana mawazo tofauti katika hukumu ya Jambo hilo....Hatuwanyoshei Vidole ,lakini katibu Mkuu wa Chama anaungana na wanaomtakia mabaya Mh.Sitta,Makamu wa Mwenyekiti yupo Upande wa Mh.Sitta,waasisi wengi wa Chama wapo na Sitta, kwa maana hiyo Mwenyekiti anavutwa kila Upande,Kwa sababu nae anaingia kwa namna fulani kwenye upande wa Mafisadi .........Na amini maneno ya watu hapa ....Bado Upande unaompiga Vita Mh.Sitta una nguvu za ajabu....Una pesa na upo karibu na Watendaji wengi wa Serikali.

Bunge letu lina Wabunge karibu 320.Ukiacha Wabunge wa Upinzani,Wabunge wa kuteuliwa na wale wa Majimbo wana ukaribu zaidi na Wabunge Magwiji wanaompiga Vita Mh.Sitta...kumbuka kuwa Wabunge wengi wameingia kwa kupewa na kukopeshwa pesa za kutafuta huo Ubunge!......waliowasaidia kutafuta Ubunge huo ndio hao leo hawamtaki Mh.Sitta.

Mkuu Nemesis fumbua macho vita hii ni kubwa....Na nakwambia kweli...Mh.Sitta awe na jeuri na kusimamia anachoamini vinginevyo kipindi cha kumalizia Bunge hili Uspika wake utakuwa Mgumu.
 
Wazee na Waheshimiwa wana jamvi

Nikiwa mjumbe wa NEC nisiye na kundi lolote, nawajibika kuweka sawa rekodi moja katika mjadala unaoendelea kuhusu Spika Sitta na kilichotokea ndani ya ukumbi wa mkutano wa NEC.

Baada ya mjadala mrefu ulioshabikiwa sana na wajumbe wengi huku hoja zao zikijiwa bila jazba na wajumbe wachache lakini wanaoheshimika, Spika Sitta alikutana faragha na Mwenyekiti JK, Rais Mwinyi na Kinana. Baada ya faragha ile ambayo bado ni siri, Spika Sitta alipopata nafasi alisema maneno machache sana yenye pointi mbili. Kwanza, aliwashukuru wajumbe kwa kutumia uhuru wao kutoa maoni yao. Pili, alisema anaiachia meza kuu kutafakari yaliyosemwa na pande zote. Kisha alimaliza na kukaa.

Hata kama sikubaliani na baadhi ya misimamo yake, siwezi kusema kuwa aliomba radhi. Lakini pia siwezi sema alikosa watetezi kama inavyoripotiwa. Kulikuwa na hoja nzito, tena nyingine kutoka visiwani zilizomtetea.

Kiroja cha mjadala alikuwa Guninita, Mwenyekiti wa Mkoa wa DSM aliyechemka lakini JK akamzodoa kwa kumwambia "kama ana uchungu na chama mbona alikiacha na kwenda CHADEMA na kuitukana CCM kwa miaka miwili?"

Habari ni hiyo.

Baija

Hii ndio raha ya kuwa JF, tunapata kitu roho inapenda siyo kulishwa makapi ya ujinga wa Waandishi wajinga na vikaragosi. Ahsante sana mkuu angalau hata sisi akina Tomaso tunaweza kuanza kuamini ulichokisema bila ya kuhitaji kushuhudia kwa macho.
 
Wazee na Waheshimiwa wana jamvi

Nikiwa mjumbe wa NEC nisiye na kundi lolote, nawajibika kuweka sawa rekodi moja katika mjadala unaoendelea kuhusu Spika Sitta na kilichotokea ndani ya ukumbi wa mkutano wa NEC.

Baada ya mjadala mrefu ulioshabikiwa sana na wajumbe wengi huku hoja zao zikijiwa bila jazba na wajumbe wachache lakini wanaoheshimika, Spika Sitta alikutana faragha na Mwenyekiti JK, Rais Mwinyi na Kinana. Baada ya faragha ile ambayo bado ni siri, Spika Sitta alipopata nafasi alisema maneno machache sana yenye pointi mbili. Kwanza, aliwashukuru wajumbe kwa kutumia uhuru wao kutoa maoni yao. Pili, alisema anaiachia meza kuu kutafakari yaliyosemwa na pande zote. Kisha alimaliza na kukaa.

Hata kama sikubaliani na baadhi ya misimamo yake, siwezi kusema kuwa aliomba radhi. Lakini pia siwezi sema alikosa watetezi kama inavyoripotiwa. Kulikuwa na hoja nzito, tena nyingine kutoka visiwani zilizomtetea.

Kiroja cha mjadala alikuwa Guninita, Mwenyekiti wa Mkoa wa DSM aliyechemka lakini JK akamzodoa kwa kumwambia "kama ana uchungu na chama mbona alikiacha na kwenda CHADEMA na kuitukana CCM kwa miaka miwili?"

Habari ni hiyo.

Baija

Hodi hodi hodi wananzengo. Heshima kwenu.
 
Shukrani za dhati Mkuu Baija Balobi (Mjumbe wa NEC-CCM Kama ulivyojiita mwenyewe) kwa ufafanuzi wako wa nini kilichojiri huko Dodoma,Lakini pamoja na maelezo yako yote,ni ukweli usiopingika kwamba Mh.Sitta amepoteza Imani/umaarufu kwa Wabunge walio wengi haswa Wabunge wa CCM.

Kwa kuwa Wana-NEC (Haswa Wabunge wa CCM) walipendekeza Spika apokonywe kadi yake ya chama ili wamvue Ubunge na baadaye Uspika ,kushindwa njama hiyo.Nafikiri Spika kwa hiyari yake mwenyewe ajiuzulu Uspika,kwa sababu katika mazingira yaliyopo sasa,hawezi kuongoza Chombo hicho ikiwa Idadi kubwa ya Wabunge hawamkubali.

Ni wazi kuwa atabaki na Ubunge wake wa Urambo,mpaka hapo mwakani katika Uchaguzi....Atakuwa ana nafasi kubwa ya kuwashitaki Wapinzani/Wabaya wake kwa wananchi kwa jinsi walivyomfanyia Fitina kwa kutetea haki ya watanzania.....Sitomuelewa Sitta ikiwa atang'ang'ania kubaki na Uspika wake!Kule kukubali suluhisho Dodoma ilikuwa kwa Mantiki ya kutaka Kubaki na Wadhifa wa Ubunge (Anawajali watu wa Urambo waliompigia kura),Maana kama angekubali kurudisha Kadi,ni wazi kwamba angejivua Ubunge na kujiondoa kwenye Uspika.Na moja kwa moja angekuwa hajawatendea haki waliomchagua.

Hata hivyo imefika Wakati sasa kumtafuta SPIKA nje ya Bunge...Wanazuoni tuangalie sheria za Bunge zinasema vipi...Kwa sababu kwa mtindo huu wa sasa,kila wakati Spika atakuwa anaendesha Bunge kwa matakwa ya Chama chake kwa kuhofia kuwa atashitakiwa kwenye Vikao vya chama.

Utabiri wangu unaniambia kuwa Mh.Sitta atajiuzulu Uspika wa Bunge la Jamuhuri,kutokufanya hivyo itakuwa ni kufilisika Kisiasa...Huwezi kuongoza watu wasiokuwa na imani nawe.

Naheshimu Mawazo yako ila naomba kupinga baadhi ya vipengele. (font red).

Nitaendelea kuamini alichokisema MMM juu ya spika

Na. M. M. Mwanakijiji
Alichofanya Spika Sitta ni kile vitani kinaitwa "strategic retreat" yaani kurudi nyuma kimkakati ili kujipanga upya. Kama nilivyoandika wiki iliyopita hii ni vita na siyo mapambano. Unaweza ukapoteza pambano moja au mawili lakini mwisho wa siku utashinda vita.

So kwa hali inavyokwenda, ukisema 6 aachie ngazi tutakua tumekosa mpambanaji. Well, sita anaweza asiwe that effective and perfect lakini hapa alipotufikisha napo si haba. What if 6 anaresign then anakuja mtu kama Msekwa...si Bunge litazimika kabisa. At least now there is something to talk about since Sitta's presence.
 
Yaliojiri katika mkutano wa CCM Dodoma yameniacha njia panda hasa kuhusiana na ile dhana ya Separation of Powers. Mahakama ni chombo huru chenye mamlaka yake ambacho hakitakiwi kuingiliwa, vivyo hivyo na Bunge na Serikali (Executive). Ila yaliyotokea Dodoma kwa ndugu yetu Sitta (Spika=Bunge) kuwekwa kiti moto inanipa tabu kuelewa hii dhana ya sep of powers imekaaje. Msaada tafadhali.

Magehema

Umeshawahi kuona separation of powers inakuwa practised hapa kwetu?

Hapa kwetu chama kinashika hatamu, iwe kwenye Bunge, Serikali au

Mahakama, ndo maana umeyaona hayo yaliyojiri Dodoma!

Unadhani Spika angekuwa wa chama kingine hayo yangetokea?

Jibu unalo.
 
Hili suala la Mh.Sitta sio dogo kama hivyo unavyofikiri,kabla ya kufika kwenye NEC ya CCM lilijadiliwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Chama kabla ya kupelekwa kwenye CC baada ya kuwa na Mshike mshike huko ndio likapelekwa kwenye NEC ambako pia Wabunge wengi wa CCM wapo huko.

Kwa Utaratibu wa maamuzi ya CCM mpaka jambo hilo limepita katika Vikao vitatu vya Chama ujue kuwa ni jambo kubwa na zito,hata hao Viongozi wakuu wa chama wana mawazo tofauti katika hukumu ya Jambo hilo....
Ningekubaliana na wewe kuwa hili jambo si dogo kama lingekuwa limejadiliwa na CCM ile iliyokuwa inajadili mambo bila ya kuwa na macho ya makengeza, bila ya kuangalia maslahi ya mtu au kikundi. lakini mwa mwendo huu wa sasa, ambao mtu mmoja anawezxa ku-influence kikao chochote cha CCM, siungani na mawazo yako
 
Mkuu, wala si peke yako. Mambo yanayofanywa na kusemwa na CCM yanaekleweka kwa mtu mwenye akili kama za mwendawazimu

na CCM ndo wakitakacho..muwadharauuuuuuu... muone kuwafatilia ni akili za kiuenda wazimu .. huku wao wakifany avitu vyao... bila maovu haya ya sisiemu hungekuwa nahali nasikini hivi wakati tunautajiri wa kutupa???
 
Hili suala la Mh.Sitta sio dogo kama hivyo unavyofikiri,kabla ya kufika kwenye NEC ya CCM lilijadiliwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Chama kabla ya kupelekwa kwenye CC baada ya kuwa na Mshike mshike huko ndio likapelekwa kwenye NEC ambako pia Wabunge wengi wa CCM wapo huko.

Kwa Utaratibu wa maamuzi ya CCM mpaka jambo hilo limepita katika Vikao vitatu vya Chama ujue kuwa ni jambo kubwa na zito,hata hao Viongozi wakuu wa chama wana mawazo tofauti katika hukumu ya Jambo hilo....Hatuwanyoshei Vidole ,lakini katibu Mkuu wa Chama anaungana na wanaomtakia mabaya Mh.Sitta,Makamu wa Mwenyekiti yupo Upande wa Mh.Sitta,waasisi wengi wa Chama wapo na Sitta, kwa maana hiyo Mwenyekiti anavutwa kila Upande,Kwa sababu nae anaingia kwa namna fulani kwenye upande wa Mafisadi .........Na amini maneno ya watu hapa ....Bado Upande unaompiga Vita Mh.Sitta una nguvu za ajabu....Una pesa na upo karibu na Watendaji wengi wa Serikali.

Bunge letu lina Wabunge karibu 320.Ukiacha Wabunge wa Upinzani,Wabunge wa kuteuliwa na wale wa Majimbo wana ukaribu zaidi na Wabunge Magwiji wanaompiga Vita Mh.Sitta...kumbuka kuwa Wabunge wengi wameingia kwa kupewa na kukopeshwa pesa za kutafuta huo Ubunge!......waliowasaidia kutafuta Ubunge huo ndio hao leo hawamtaki Mh.Sitta.

Mkuu Nemesis fumbua macho vita hii ni kubwa....Na nakwambia kweli...Mh.Sitta awe na jeuri na kusimamia anachoamini vinginevyo kipindi cha kumalizia Bunge hili Uspika wake utakuwa Mgumu.

Mkuu, ninachopingana na wewe ni hoja yako kwamba Spika haungwi mkono na wabunge wengi kiasi cha kushindwa kuliongoza bunge ktk kipindi kilichobakia. natambua kuwa vita ni kubwa, hata Mzee Sitta anajua vizuri ndo maana siku za karibuni alimuomba Mhe. waziri Mkuu amuongezee ulinzi.

Si kweli kwamba idadi kubwa ya wabunge wanampinga Sitta (vinginevyo thibitisha). Hoja ya kwamba wabunge wengi walipewa fedha za kampeni toka kwa mafisadi bado ni hear say pia kupewa pesa za kampeni hakumfanyi mtu awe follower of everything, is it'n?

Sitta hawezi kujiuzuru otherwise, tunatangaza uhuru mapema dhidi ya sultan CCM.
 
na CCM ndo wakitakacho..muwadharauuuuuuu... muone kuwafatilia ni akili za kiuenda wazimu .. huku wao wakifany avitu vyao... bila maovu haya ya sisiemu hungekuwa nahali nasikini hivi wakati tunautajiri wa kutupa???
Na wasichokijua wao ni kuwa wanaua ule mfumo wa chama endelevu. Hivyo, mafanikio yao yatakuwa ya muda na yatafika mwisho, na mwisho huo, kwa kutokujua kwao, waja upesi kuliko wanavyofikiria
 
- Nilisema toka siku ya kwanza ya huu mkutano kwamba habari za Spika kuomba radhi hazikuwa na ukweli wowote, ahsante mkuu kwa kuthibitisha hilo.

Respect.

FMEs!
 
Ukweli ndo huo. Habari za kuwa Sitta ameomba radhi zinaenezwa na akina Rostam ambao wamehangaika usiku kucha kutugongea vyumbani wakitubembeleza tumtose Sitta. Ndio wameita magazeti mbalimbali kueneza uvumi kuwa Sitta ameomba radhi kwa NEC.

Hebu tudokeze wakati akina Rostam wanawagongea milango waliwalipa shilingi ngapi? Hivi inakuwaje watu tunaowategemea kutuongoza mnakuwa cheap namna hiyo? Ili kuiweka nchi sawa wakati umefika sasa wa kuachana na CCM.
 
- Hela zote walizi-invest kwa wajumbe wa visiwani knowing kwamba huwa wanaweza kumtishia Muungwana, lakini wakachemsha Spika ana support kubwa sana ya wabunge aliowapa marupu rupu mengi ya ajabu, lakini the damage is done na ninaamini kwamba Spika hatarudi bungeni kwani anahitaji miracle kushinda tena jimbo!

Respect.

FMES!
 
- Nilisema toka siku ya kwanza ya huu mkutano kwamba habari za Spika kuomba radhi hazikuwa na ukweli wowote, ahsante mkuu kwa kuthibitisha hilo.

Respect.

FMEs!
FMES,
Ndio uzuri wa kujenga INSTITUTIONS zenye nguvu kama anavyofanya yeye sasa kwenye Bunge letu. Bunge letu sasa linaelekea kuwa na nguvu sana kuliko hiyo NEC ya CCM.
Akirudi Bungeni atafakari jinsi ya kuondoa wadhifa wa SPIKA kwenye vikao vya juu vya CCM.
 
- Hela zote walizi-invest kwa wajumbe wa visiwani knowing kwamba huwa wanaweza kumtishia Muungwana, lakini wakachemsha Spika ana support kubwa sana ya wabunge aliowapa marupu rupu mengi ya ajabu, lakini the damage is done na ninaamini kwamba Spika hatarudi bungeni kwani anahitaji miracle kushinda tena jimbo!

Respect.

FMES!

Hii nchi sijui inaenda wapi, yani watu hawalali wameshatangulia jimboni kumzibia 6.. nisaidieni.. kwani spika lazma awe mbunge wa kuchaguliwa ndo awe spika???
 
Hii nchi sijui inaenda wapi, yani watu hawalali wameshatangulia jimboni kumzibia 6.. nisaidieni.. kwani spika lazma awe mbunge wa kuchaguliwa ndo awe spika???
Mtanzania yeyote mwenye sifa ya kuwa MBUNGE anaweza kugombea nafasi ya SPIKA.. Shida ni KURA utazipataje bila kuungwa mkono na Wabunge wa Chama chako.
 
Baija Bolobi said:
Wakadai Sitta anautaka Urais kupitia bungeni na wakataja matukio kadhaa kuunga mkono madai yao hayo.

Kauli hii haina tofauti kabisa na ile iliyotolewa na wadhambi wa wakati ule wakiharalisha mashtaka ya Yesu mbele ya Pilato. Baada ya kushindwa katika hoja zoote wakamwambia Pilato "Huyu anajiita mfalme" wakijua kabisa Pilato iwapo bado atagoma kumsulubisha basi atakuwa amemuudhi Mfalme na hivyo atapoteza cheo. Yaliyofuatia Wakritu wanayajua...

Baija Bolobile, Bagaluka Bateirwe
 
Back
Top Bottom