Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Wakuu tunaendelea kuchambua yaliyojiri kwenye kikao cha juzi NEC, Dodoma:-

- The More dataz ni kwamba Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Bwana Wilson Kusila, ambaye huko nyuma kuliwahi kuwa na ripoti kwamba alipewa jumla ya shillingi Millioni 10 na Rostam, ili kuweza kumshinda Bwana Masima, aliyegombea naye nafasi hiyo ya mkoa wa Dodoma, alitaka wapiganaji wote kufunguliwa kesi ya uhaini.

- Alipopewa nafasi ya kuzungumza na Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri, alienda mbali zaidi na kutaka mashitaka ya uhaini yafunguliwe mara moja kwa Spika na wapiganaji wote, kwa sababu wanachokifanya bungeni kwa kushikiriana na Spika, ni Uhaini period!

- Huku wajumbe karibu wote wa mkutano huo wakiwa wamepigwa na mshangao, Kusila aliendelea ku-charge kwamba Uhaini huu unaanzishwa na kuendeshwa na waliokosa Urais kwenye uchaguzi wa Mwaka 2005, hawa wakamatwe mara moja na kufikishwa kwenye mkono wa sheria za jamhuri na hasa Spika Sitta, wakati wote huu Mwenyekiti wa CCM hakuficha kabisa furaha yake akimsikiliza kwa makini sana Kusila na huku akimuashiria kuendelea na hoja zake!

- Kusila aliendelea kwa kumuomba radhi Rais Mkapa, akisema kwamba "..unashambuliwa na hawa wahaini kwa sababu moja tu, nayo ni kwamba ulimchagua Kikwete kwenye urais wa 2005 na ukawaacha wengine...", hapa Mkapa akasimama juu na kupiga makofi huku akicheka sana, huku pembeni Mwenyekiti wa CCM akiendelea kucheka kwa sauti ya juu sana,

- Kusila alimalizia kwa kudai "..hata hawa wanaosema bungeni hapatatosha wote ni wahaini wakubwa na wakamtwe na kufikishwa kwenye mkono wa sheria maramoja!..."

Respect.

Field Marshall Es!

NB: Wajumbe wengi wa kikao hicho wanajiuliza swali moja muhimu, kwamba kwa nini Rais aliruhusu kutokea kwa yote yaliyojiri kwenye hiki kikao?

Mkuu:

Hapa JF mpaka sasa inaonyesha kuwa wenyeviti wa CCM wa mikoa ya DSM, Shinyanga na Dodoma walichemsha. Na hawa wanaingia NEC kwa mujibu wa vyeo vyao.

Vikao vya CCM vinaendeshwa kwa agenda na sio mwenyekiti anayeandaa agenda. Na kama agenda ilikuwa ni kumweka Sitta kwenye kiti moto, basi JK hana lawama zozote hapa. Yeye ni mwenyekiti tu.
 
Jamani sisi wengine sio wazuri kwenye sheria, kuna mtu anaweza kutufafanulia katiba na sheria za nchi zinaweka bayana kesi ya uhaini inafunguliwa ukifanya makosa gani?? Halafu hiyo NEC ina power gani za kufungua mashtaka makubwa kama hayo??

Najaribu kufikiria hapa kosa la spika na wabunge wenye mapenzi ya kuzuia wizi wa rasilimali za wananchi wa jamhuri, wamefikia vipi kwenye hili janga la uhaini??

Je, mwenyekiti hakuweza kutoa mwongozo kufuatana na katiba ya nchi, hizi allegation za uhaini zilipotolewa??

Sisi wengine huku kuna kakosa ka TREASON ambakouwa tunakasikia tu kwenye malumbano kwenye FOXNEWS, lakini ni vigumu kukumbuka nani amewahi kupewa hiyo case ya treason!!

Je Treason ndio uhaini?? Kama ni ndio, du si level ya kufikia hii threshold iko very high kiasi ambacho hata sijui huyu KUSILA kama ni mzima au vipi!!

Viongozi wengi wa Tanzania hawasomi katiba ya vyama vyao au ya nchi na kuelewa yale wanayozungumza. Wanaendesha mamlaka yao kwa hisia na midadi tu.

Nakumbuka kwenye mkutano mmoja Padri Supa alimlalamikia Nyerere kuwa anawalundikia wakuu wa mikoa na wilaya madaraka. Kwa sababu wakuu hao walikuwa ni makatibu wa chama katika maeneo yao.

Ilibidi Nyerere asome katiba na kuwaambia wajumbe kuwa ni wao waliotunga. Na wakitaka ateue vingine, basi waitishe mkutano mwingine na kubadili katiba.
 
Bado napata shida sana kuona ni nini Kigoda, Salim, Shibuda na Mwandosya wamefanya hadi kustahili kufunguliwa kesi ya uhaini. Na sijui kama ni kweli hawa jamaa wanakinyongo na JK kuchaguliwa kuwa rais.

Kwa mara nyingine sasa naanza kuwa na wasiwasi mkubwa na uwezo wa NEC, kama wajumbe wake wanaonesha uelewa mdogo.

Kama si uelewa mdogo, na kama yeye ni mtu mwenye akili timamu basi inawezekana kuwa Bw Kusila anatuambia kuwa walioshindwa kwenye kura za maoni wakati wa kumchagua mgombea kwa tikiti ya CCM, ndio mafisadi ambao lengo lao ni kumpidua rais. Lakini so far hatujaaona hayo, labda Bw Kusila akitupa ushahidi tutaelewa zaidi nini kinaendelea. Huenda ana genuine allegations za treason. I hope soon tutaanza kuwasikia kina Kigoda, Salim, Shibuda na Mwandosya.
 
Nashindwa kuushawishi ubongo wangu kwamba Kusila ni mjinga kiasi hiki! labda anajua anachokiongea ambacho sisi hatukijui..! kuna zile habari ziliwahi kuandikwa na Mwanahalisi kua kuna mpango wa kumfanya kikwete kua rais wa muhura mmoja labda ndo hao alikua akiwasema Kusila
 
....The More dataz ni kwamba Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Bwana Wilson Kusila, ambaye huko nyuma kuliwahi kuwa na ripoti kwamba alipewa jumla ya shillingi Millioni 10 na Rostam, ili kuweza kumshinda Bwana Masima, aliyegombea naye nafasi hiyo ya mkoa wa Dodoma, alitaka wapiganaji wote kufunguliwa kesi ya uhaini.

WanaJF;

Yaani tunajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe kwa kutumia kuni zetu. Angalia hapa;

Rostam kwa kushirikiana na jamaa mmoja anaitwa Habib ndo wamiliki wa Caspian. Caspian ni mining contractor kule Nzega golden pride na Williamson Diamond Shinyanga. Habib ndo CEO na i hope sio mtz.

Hii ndo miradi mikubwa yao pamoja na Vodacom. Anapata pesa ambayo Kusila na wenzake wanamegewa na baada ya hapo wanafanya ujinga na us..nge kama huu.

Mungu utuepushe na dhahama hii.
 
Nashindwa kuushawishi ubongo wangu kwamba Kusila ni mjinga kiasi hiki! labda anajua anachokiongea ambacho sisi hatukijui..! kuna zile habari ziliwahi kuandikwa na Mwanahalisi kua kuna mpango wa kumfanya kikwete kua rais wa muhura mmoja labda ndo hao alikua akiwasema Kusila

Sio mjinga hii ni pesa. Tanzania tuna adui mmoja tu na tukimshinda basi hapo ndo tutajitawala ni RA, ametawala Vyombo vya usalama, Habari,Serikali, Chama kinachoongoza bado tu Bunge ndo kunaupinzani ila anatikisa. Lakini tuwaunge mkono wapambanaji TUTASHINDA!
 
Mimi nadhani katika swala hili mambo yanaanza kufumka wazi..
Nimesoma maelezo ya mbunge huyu wa Shinyanga kwa makini sana na kujaribu kutafakari nje ya mgogoro huu uliopo nikaona picha mpya ikiibuka..hasa pale alipomtaja Mkapa kuwa ndiye alimchagua JK!

Kama mnakumbuka uchaguzi mkuu wa CCM kupata mgombea wake ktk kiti cha Urais, hatua moja muhimu sana ilipinduliwa...Wazee wa CC waliondoa utaratibu wa kupiga kura mara tatu kumpata mshindi yaani ilitakiwa JK na Salim wapigiwe kura badala ya kuwa na wagombea watatu...

Sasa yawezekana baada ya Lowassa na kundi lake kuondolewa, zile siri za ushindi wa JK zinaanza kutoka na hakika kisheria hiyo ilikuwa treason...Kitendo kile kilikuwa cha Uhaini kabisa lakini nashindwa kuelewa Mkapa, Mwinyi, Kawawa na hawa kina Lowassa na RO watajiondoa vipi ktk sakata hili kwani decision ya kutopiga kura mara tatu waliifanya wazee wa chama na sii JK. dhahiri ushahidi utakao patikana utakuwa mikononi mwa watajwa..
 
Ni kipengele gani cha katiba yetu kitatumika kwa mashitaka hayo ya uhaini?

sijui!! labda kwa mtindo wa kizombe-zombe... letejambajamba na ukifika wakati wa hukumu, not guilty... kwisha kazi..

Huyo mzungumzaji alikuwa anachafua tu hali ya hewa na sidhani kama alikuwa anajua kwa makini jambo alilokuwa analizungumzia hasa juu ya uhaini...Full stop..
 
Last edited:
Upumbavu wa wajumbe wa NEC, CC ya CCM ndio ushindi wetu. Maneno yao ya ajabu na kipuuzi pamoja na utashi mdogo, ushabiki wao kwa mafisadi ndio ushindi wetu.

Huu ni mwanzo wa uelewa na kuhakikishiwa fedha zote za ufisadi zilitoka kwa baraka zote za serikali ya CCM kwa matumizi ya chama cha mapinduzi.

Kama kweli Sita na wenzake ni wateteaji wa kweli wa haki na wanachukia vitendo vya ufisadi, wizi, rushwa na utawala zobe warudishe kadi au wajiuzulu nyazifa zao kwani hawaruhusiwi tena kupambana na mafisadi ndani ya CCM , kwani CCM fisadi ni mtakatifu.
 
Niliyaona haya kwa macho yangu. Ama kweli vikao vyetu sasa havina siri tena!

Ukisikia unafiki ndio huu!

Umekuja na ngonjera kwenye thread yako ya Sitta kuomba radhi, wenye data wanakuja na za uhakika kwa majina na kilichosemwa.

Huyu ES hajawahi kusema ni mjumbe wa NEC au CC ya CCM zaidi ya kutegemea vyanzo vyake vya uhakika. Kisha wengine mnadandia hoja na kudai mliyaona!

Acheni hizo!
 
Niliyaona haya kwa macho yangu. Ama kweli vikao vyetu sasa havina siri tena!

FMES
Thanks so much mkubwa kwa hii.Taifa langu lina angamia kisa CCM kwanza .Watu sasa naomba mseme na hasa nyie wana CCM hapa forum .Hii ndiyo Tanzania mnayoitaka ?

Baija nadhani wewe unyamaze tu bwana acha wenye data wazimwage tafadhali .
 
- Alipopewa nafasi ya kuzungumza na Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri, alienda mbali zaidi na kutaka mashitaka ya uhaini yafunguliwe mara moja kwa Spika na wapiganaji wote, kwa sababu wanachokifanya bungeni kwa kushikiriana na Spika, ni Uhaini period!

- Huku wajumbe karibu wote wa mkutano huo wakiwa wamepigwa na mshangao, Kusila aliendelea ku-charge kwamba Uhaini huu unaanzishwa na kuendeshwa na waliokosa Urais kwenye uchaguzi wa Mwaka 2005, hawa wakamatwe mara moja na kufikishwa kwenye mkono wa sheria za jamhuri na hasa Spika Sitta, wakati wote huu Mwenyekiti wa CCM hakuficha kabisa furaha yake akimsikiliza kwa makini sana Kusila na huku akimuashiria kuendelea na hoja zake!

- Kusila aliendelea kwa kumuomba radhi Rais Mkapa, akisema kwamba "..unashambuliwa na hawa wahaini kwa sababu moja tu, nayo ni kwamba ulimchagua Kikwete kwenye urais wa 2005 na ukawaacha wengine...", hapa Mkapa akasimama juu na kupiga makofi huku akicheka sana, huku pembeni Mwenyekiti wa CCM akiendelea kucheka kwa sauti ya juu sana,

- Kusila alimalizia kwa kudai "..hata hawa wanaosema bungeni hapatatosha wote ni wahaini wakubwa na wakamtwe na kufikishwa kwenye mkono wa sheria maramoja!..."

Respect.

Field Marshall Es!

NB: Wajumbe wengi wa kikao hicho wanajiuliza swali moja muhimu, kwamba kwa nini Rais aliruhusu kutokea kwa yote yaliyojiri kwenye hiki kikao?

Ingepatika video yake hii kitu ingekuwa bonge la movie
Mitanzania bana kweli tutabaki maskini hadi mwisho wa karne
 
Wakuu tunaendelea kuchambua yaliyojiri kwenye kikao cha juzi NEC, Dodoma:-

- . [Snip}....................................................................
NB: Wajumbe wengi wa kikao hicho wanajiuliza swali moja muhimu, kwamba kwa nini Rais aliruhusu kutokea kwa yote yaliyojiri kwenye hiki kikao?

Usisema Rais, sema mwenyekiti wa CCM

Jibu ni Rahisi. Wanasiasa wetu wanapenda kusingiziwa sifa nzuri, za kuwapamba. Lakini hawapendi kabisa useme ukweli wa maovu yao.

Lakini kwa maelezo yako, inasikitisha kwamba kwa umri wa CCM na kiasi cha elimu tuliyokwisha fikia hapa tulipo, hawakustahili kuwa na mwenyekiti wa mkoa wa aina hiyo.

Kwa nini bado kuna wenyeviti kama hao, ni jambo la kushangaza.
 
Kitendo cha NEC ya CCM kumshambulia Sitta na kuwatisha wabunge wa CCM wanaopambana na ufisadi ni vita ya CCM dhidi ya wananchi wote wa Tanzania waliochangua.

Wabunge ambao wanachanguliwa na wananchi ambao ni wanachama wa vyama na wasio wanachama huwakilisha matakwa ya wanachi wote ili kusaidia katika kuwaletea maendeleo. Ufisadi umechangia sana katika kudidimiza maisha ya watanzania. Mifano ya ufisadi ni mingi mno. Kwa mfano hivi karibuni tumeona picha za wananchi wa Tarime ambao wameathirika na kemikali kwenye machimbo ya madini ambayo ni matokeo ya mikataba ya kifisadi. Utajiri wa nchi yetu ambao ungeleta maendeleo ya watanzania unaliwa kupitia ufisadi. Sasa NEC inawafunga mdomo wabunge ambao kwa msingi ni wawakilishi, midomo na watetezi wa wananchi wote na siyo vyama vya siasa. Maamuzi haya ya kutishia kuwafukuza uanachama wabunge ni hatari kwa nchi yetu na ni wajibu wa watanzania wote kupigana vita vikali dhidi ya CCM inayopinga maslahi ya watanzania.

Natoa changamoto kwa wabunge wote wa CCM na vyama vya upinzani kuendelea kutetea wananchi wote siyo ufisadi kama CCM inavyofanya. Na ninatoa changamoto kwa vyama vya siasa vifanye kampeni nchi nzima kupinga maamuzi ya kidikteta ya CCM ambayo yanaingilia mhimili wa Bunge ambao ndio wananchi wenyewe. Na Mh. Sitta, Kilango Malecela, Kimaro, Mwakyembe na wapambanaji wote wa CCM songeni mbele msiteteleke, wananchi tuko nanyi katika vita hii ya CCM dhidi ya wananchi wa Tanzania.
 
Mkuu:

Hapa JF mpaka sasa inaonyesha kuwa wenyeviti wa CCM wa mikoa ya DSM, Shinyanga na Dodoma walichemsha. Na hawa wanaingia NEC kwa mujibu wa vyeo vyao.

Vikao vya CCM vinaendeshwa kwa agenda na sio mwenyekiti anayeandaa agenda. Na kama agenda ilikuwa ni kumweka Sitta kwenye kiti moto, basi JK hana lawama zozote hapa. Yeye ni mwenyekiti tu.

Wazo langu ni kwamba, hata kama agenda ni mbovu kama kutafuta ngazi ya kufika mbinguni, bado ufahamu wa mwenyekiti ni kitu muhimu sana! Kama Mwenyekiti ni hoi kikao kitaamua yasiyoeleweka na watu watazungumza kama vichaa na kushangiliwa.

JK ana lawama ZOOTE.
 
huyu ni pumbaza wa fikra na bora akalime kwani anadhani kuwa hizi ni enzi za ujima naomba akampeleke mkeo na wannae kwani hao ndio wahaini na hajui asemacho. ila chama kinaelekea pabaya
 
Hapo alikuwa anamlenga Anne Kilango (aliwahi kusema Bungeni hapatatosha) nadhani pia anamlenga huyuhuyu kupitia mumewe (John Malecela) kujaribu kugombe uraisi 2005 na Mkapa kumpiga chini. Na hasa kauli za wote wawili za hivi karibuni kuwa nchi imetekwa na matajiri.
 
[Ukifuatilia utaona kuwa hawa wanapinga ufisadi ni wale ambao hawasomi nyakati. Huyo Kusila tunajua alishakuwa waziri wakati wa Mkapa hivyo lazima amtetee.Ila wasidhani KANU ya Kenya na UNIP ya Zambia waliangukaje.Ni kufikri kila kitu kiko OK lakini inafika mahali watashindwa kusave situation na Sababukubwa ni kufikiri watu wako mwaka 47 wakati tuko karne ya sayansi na Teknolojia. Hivyo kikao kijacho cha bunge ndio ukweli wote utakuwa wazi na tutamwona Mh. Sita kama amebadilika au vip
 
Back
Top Bottom