Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Pakacha tusiwalaumu sana waandishi manake ni jadi yao maana hata kwenye Biblia wameandikwa kwamba ni wanafiki na wamelaaniwa. Nao wanaangalia maslahi yao binafsi na wenginee majuzi wamenunuliwa magari na mheshimiwa mmoja
Du! Shangazi inaeleka unajua siri nyingi sana, ebu tupakulie basi
 
Huu ni uedelezaji wa ukabaila na ukoloni mambo leo ,Spika si kwa ajili ya CCM wala wabunge wanapokuwa ndani ya bunge hawaiwakilishi CCM,inakuwaje kuwaje CC na NEC za CCM ziwe zinawashambulia na kuiwatisha ?

Hivi hawa wabunge wanaotishwa wafanye nini ? Ndio wameshatishwa kwa maana mashahara uliojaa vikolombwezo vya posho wataukosa na ikibidi kufuatiliwa na vyombo vya usalama wa CCM.

Nchi sasa inaendeshwa kidikteta ,hili halina ubishi na kitakachopatikana hapo itakuwa ni matumizi ya nguvu kuipindisha haki ya raia kumchagua anemtaka,WaTanganyika kaeni tayari maana kinachokuja safari hii sio washawasha tena bali ni risasi za moto hili halina ubishi kabisa.Mugabe style au Mwai style au yote kwa pamoja ,ila waTanzania walio wengi wakae tayari kwa kujibu kwa aina ya Odinga style ili paeleweke na hio ndio dawa peke yake haina mbadala kwa utawala huu wa kifashisti.

CCM imeshang'amua kuwa hawawezi kukubalika tena ,hivyo kwa kuanza ndio wameunda tume ili kuwajua na kuwabana wasiokuwa na wao katika kuwaunga mkono kuizamisha nchi hii.
Suali waliloulizwa wabunge ambao wapo mstari wa mbele kupinga utawala mbovu wa CCM wakiwa ndani ya CCM"...Are You with us ? If not you will see the consiquency(If correct)" Hivyo ni vitisho ,ambavyo nadhani vimekusudiwa kuwatenga wale ambao wamekusudia kujitokeza kupambana na Kikwete katika uchaguzi ujao kwa kutumia karata ya CCM ,kitu kimoja ili kuwajua waovu wa Nchi hii ni kuwatanzama wale walioitwa chemba na kummuonya spika ,hao ni watu hatari na inafaa kuepukwa wengine ni wale waliopewa jukumu la lusimamia ambao wamepewa idara maalum itanayojulikana kama Kamati ,hii si kamati ya kuiletea wala kuitetea heri hapa Tanzania bali ni kamati ya maangamizi ambayo imewekwa kuikandamiza haki pale inapotetewa kwa kuwabana na kuwadhoofisha wale watakaojitokeza kukemea na kupinga maovi yanayoonekana kufanywa na utawala wa CCM ,kwamba sasa imefika wakati kuwa litakalosemwa na CCM ndio hilo hilo hakuna wa kulipinga ,natumai waTanzania mmepata uelewa kwa hali ya mambo inavyoendeshwa na CCM ,sio jambo la mchezo hawa watu wamekusudia shari kabisa na sio kwa wabunge wao tu bali kwa wabunge waote na yeyote yule atakayeonekana analeta vya kuleta.
Hongera Wapemba kwa msimamo wenu wa kuilinda haki kwa bei yeyote ile karibu waTanganyika watawaelewa.
 
tunao wazalendo wa kutosha hata mafisadi wakinywa damu ya mr six, watatokea mr mseven na mr. eigth
 
Kama kweli JK akiwa mwenyekiti wa Chama, akiwa Rais wa nchi na akiwa mtu mzima, sitegemei kama anaweza kutoa maneno ya kejeli kwa Guninita, tena ndani ya kikao kikubwa cha Chama. Sijui ni kwanini viongozi wetu wasiwe na manners za kuongea.

Inazidu kuonesha kuwa heshima ya vikao vya juu inazidi kupungua. Kama lugha ya kistaarabu haitumiki, inawezekana hata maamuzi yasiwe ya kistaarabu.

Bongolander ninawasiwasi humjui jk wewe otherwise usingeshangaa hilo mbona dogo sana?!! Hivi tukisema hii nchi inaongozwa na wahuni mbona hamtuelewi au mnahisi tunatania nini? Ndio hivyo tumeliwa tusubiri 2015 labda tutakuwa tumejifunza.
 
Nakushukuru kwa kubaini kuwa spika hakuomba radhi kwa wabunge na hta hivyo sioni sababu ya yeye kuomba radhi kwani ayafanyao bungeni ni uhuru wa ki demokrasia. Hivi mtu kuwasakama Mafisadi ndio liwe kusa la kumtaka yeye aombe radhi kwa wabunge wasikuwa na uchungu na nchi yetu?
 
Kuna wadau hapo juu wameshauri Spika abwage manyanga,that will be a very wrong move. Kumbuka matakwa ya wabaya wake hayakuwa yeye kunyang'anywa kadi ya CCM,matakwa ya wabaya wake yalikuwa ni Sitta ku cease kuwa Spika wa Bunge,hiyo ndiyo nia na lengo hasa la move yote,those men do'nt care kama Sitta ni mbunge au la,all they care about asiwe Spika and they believe they are awash with enough cash to attain that aim. Sasa aki resign hiyo si ni sawa na kufurahia kubakwa? Kumbuka when the going get tough the tough get going,Sitta ang'ang'anie hapo hapo mpaka wabaya wake wamwage manyanga au wapepewe na khanga!
 
Other delegates from Zanzibar not at the meetings include immediate past Zanzibar President Salmin Amour Juma and Isles’ Water, Construction, Energy and Lands minister Mansour Yussuf Himid. The minister is the one who recently tabled in the Isles’ House of Representatives the decision by the Karume government to withdraw oil and natural gas from the list of Union affairs. His only response when contacted by this paper yesterday by phone on why he was not in Dodoma was a snappy ‘No comment’.au kwa maana ingine mtajiju. Kaazi kweli kweli 😀
 
Kwa muda mrefu namefuatilia baadhi ya mijadala ndani ya forum na kwa maoni yangu baadhi ya wachangiaji wanawakilisha makundi tofauti ndani ya siasa za chama tawala. naamini kuwa kama tunataka kuwa impartial and independent we need to state the source of the information if someone is not the source or we must verify the veracity of what is stated lest we may be called gossipers.
 
Tunakoenda ni giza tupu ndugu zangu. Akina mama wengi wamelia sana ukumbini.

wamelizwa na nini mkuu...kwamba tuendako ni giza tupu kwa hiyo hawaoni nani atawaongoza...kwamba sitta anaonewa....kwamba mafisadi wanaonewa....nini kilichowaliza.

Unaweza kutusaidia majina ya waliolia maana mara nyingi kilio huwa ni dalili ya kushindwa kufanya lolote na hivyo kuiachia fate ifanye kazi yake na kama huo ndiyo mtazamo wa viongozi wetu wa kike basi tunahitaji kufikiria mara mbili ikiwa tunahitaji viongozi ambao wanaposhindwa na jambo badili ya kulirudisha kwa wananchi wasaidie mawazo wao wanaangua kilio.
 
Mbona sijaona mahali panasea Karume akachia ama mie kizungu kinanizingua?
 
Baraza la wawakilishi ni kiboko kabisa hawataki ujinga kabisa sio kama hawa wazandidu wa bara wanawakumbatia...na kuwachekelea mafisadi nawapongeza sana ............wazalendo wa zbar haki tena wale ni wazalendo na wanapiga sana ufisadi.....
 
wamelizwa na nini mkuu...kwamba tuendako ni giza tupu kwa hiyo hawaoni nani atawaongoza...kwamba sitta anaonewa....kwamba mafisadi wanaonewa....nini kilichowaliza.

Unaweza kutusaidia majina ya waliolia maana mara nyingi kilio huwa ni dalili ya kushindwa kufanya lolote na hivyo kuiachia fate ifanye kazi yake na kama huo ndiyo mtazamo wa viongozi wetu wa kike basi tunahitaji kufikiria mara mbili ikiwa tunahitaji viongozi ambao wanaposhindwa na jambo badili ya kulirudisha kwa wananchi wasaidie mawazo wao wanaangua kilio.

Pinda, sitta wote waliwahi kulia sasa sidhani kama wanatofauti na hao wanawake waliolia.
 
Mbona sijaona mahali panasea Karume akachia ama mie kizungu kinanizingua?
Wacha kikuzungue ,hivi ulimuona hapo au ulisikia kuwepo ? Inatakiwe ujiulize mbona hukumuona ,sijui anakuwa makamo mwenyekiti au mwenye meza ,mradi ndio hivyo ,sasa sijui kama watamfukuza ?
 
Pinda, sitta wote waliwahi kulia sasa sidhani kama wanatofauti na hao wanawake waliolia.
Kulia ni utamaduni wa kiafrika. Ni ishara inayonyesha -uchungu- kukereketwa kulikopita kiasi, kuumizwa na jambo fulani. Kulia siyo ubwege- ni ishara ya ufahari.
 
CCM kumbuka kuwa u Mavumbi weeeeweeee, na mavumbini utaruuuudi.
 
Wacha kikuzungue ,hivi ulimuona hapo au ulisikia kuwepo ? Inatakiwe ujiulize mbona hukumuona ,sijui anakuwa makamo mwenyekiti au mwenye meza ,mradi ndio hivyo ,sasa sijui kama watamfukuza ?

Hilo la kumfukuza hawasubutu hata siku moja .
 
Back
Top Bottom