Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Huyo guninita afikirie kauli ya kikwete kumwambia maneno makali hayo bila kupindiisha..asijiweke mbele kuongelea mabaya ya wenzake.
 
Ukweli ndo huo. Habari za kuwa Sitta ameomba radhi zinaenezwa na akina Rostam ambao wamehangaika usiku kucha kutugongea vyumbani wakitubembeleza tumtose Sitta. Ndio wameita magazeti mbalimbali kueneza uvumi kuwa Sitta ameomba radhi kwa NEC.
Sitta ni mwanamume. Wenye uchungu na nchi yetu, tumtie moyo, na kumwombea. Kama NEC ingemtaka kuomba radhi kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari basi kila mwananchi wa Tanzania labda mpumbafu angeelewa kuwa CCM ni ya mafisadi. Na kama ingekuwa kweli basi kundi la akina Kilango tungepaswa kuwashangaa kama wangeendelea kubaki CCM.
J.R
 
Hata mimi ninaweza kujitambulisha kama Mjumbe wa NEC, na nikasema Six aliungama, je utaniamini?

Suala sio kuamini. Suala ni ku-verify source. Hivyo ukisema wewe ni mjumbe wa NEC, itabidi nipime uzito wa kile unachosema na vilevile kulinganisha na source zingine.

Watu wengi wanataka kusikia kuwa mafisadi walimlazimisha spika kuomba radhi na wakisikia kuwa hakuomba radhi wanaenda bazooka.
 
Magazeti jana yalituchanganya ndo maana nikapost matatu humu kwenye JF kusudi tupime.

NEC ya juzi ilikuwa imeongwa pesa tokea Zanzibar hadi Mtwara mpaka Bukoba. Ndo maana wanawake wale unasikia walilia ile ni usanii. Na ebu jiulize Rostam hakuhudhuria vikao vya Bunge kwenye bajeti lakini kwenye NEC na CC alikuwa msemaji mkubwa na kuhamasisha kusudi apate pa kutokea!!! Hawa watu nikama wachawi ukijumlisha na JK ambaye hana msimamo basi nchi haina mwenyewe. Wacha tusubiri kwani haya ni mapito.

Ila kinachoniogopesha zaidi ni CHADEMA wamekaa kimyaa sijui kuna nini manake hii ndo advantage yao.

Watu makini hawakurupuki.Chadema ni Chama makini na kina namna ya kuendesha mambo yake .KUna mkanganyiko mkubwa wa habari za hasa Speaker .So one must sit and wait kabla haja anza kusema kwa kufuata mkumbo.Habari za spika za kuomba msamaha zina ukweli natakla kujua wana CCM hapa wanakuja na hoja ipi jamvini .
 
Nukuu kutoka Raia Mwema

"Karibu wajumbe 40 walizungumza dhidi ya Sitta. Walikuwa wakitoa wito afukuzwe kwa jinsi alivyoliendesha bunge ambalo katika siku za hivi karibuni limekuwa likiibana sana Serikali. Aliomba sana msamaha lakini dhahiri hakuna hata mmoja aliyekuwa akimsikiliza hata wachache waliomuunga mkono walizomewa wasiweze kuendelea kusema lolote"

Asante
 
Duh...ivi Sitta kweli ni tishia kwa mafisadi namna hii? mbona na yeye kakaa kifisadi tu? Au hapa tunatakiwa tuchague 'the better of the two evil'?
 
Suala sio kuamini. Suala ni ku-verify source. Hivyo ukisema wewe ni mjumbe wa NEC, itabidi nipime uzito wa kile unachosema na vilevile kulinganisha na source zingine.

Watu wengi wanataka kusikia kuwa mafisadi walimlazimisha spika kuomba radhi na wakisikia kuwa hakuomba radhi wanaenda bazooka.

Sasa ipi ni credible source? Baija ( Anayejiita mNEC ) au magazeti yaliyodai kupata habari kutoka kwa fellow Baijas NEC Members?

Mimi siendeshwi kwa Hisia mpaka sasa niko katikati yawezekana aliomba Msamha au Hakuomba je waweza kunipa Source?

Sasa huamini kama mimi ni mNEC?
 
Duh...ivi Sitta kweli ni tishia kwa mafisadi namna hii? mbona na yeye kakaa kifisadi tu? Au hapa tunatakiwa tuchague 'the better of the two evil'?

Na ukiangalia kwa umakini zaidi hata wewe mwenyewe unaweza kuitwa fisadi, suala hapa ni tafsiri ya hilo neno, nani analitumia kwa minajili gani. Sina tatizo ukimwita Sita fisadi, lakini kwa kigezo gani?
 
Naombeni namba ya Simu ya Mh Samwel Sita (Mb) nimalize utata hapa.....

Mwuulize Shalom akuambie kama kuna mtu zaidi ya Mwakalinga anayeweza kuwa sehemu tofauti katika muda huo huo. Shalom anafahamu watu gani wana uwezo huo wa KIROHO.

Sasa Ndugu yangu Masa, si muulizeni George Mwakalinga awaambie nini kilikuwa huko ndani? Inawezekana moja ya UTANO (hapa si UTATU TENA) wake Mwakalinga, mmoja ulikuwa kwenye kikao hicho......

This was BREAK, HAVE TIME...... Tuendelee na zile story za uko jela JKT na mkisikia sauti ya buti mwaulizana " huyo atakuwa afande Magwega..."
 
Ndio tujadili yaliyojiri ndani ya vikao vya CCM na Mh. Spika, lakini tuwe waangalifu katika maeneo fulani. Hivi huyu Baija Bolobi ni kweli M-NEC na habari aliyoitoa ni ya kweli? Je, hakuna chanzo (source) kingine cha kutuhabarisha tukalinganisha taarifa hii?
Nje ya mh. Spika ni yapi mengine yameongelewa? Makamba je?

soma nipashe ya jana 18/8/09 Spika hakuomba msamaha na alikuwa na wajumbe wengi wanamuunga mkono.
 
Kaazi kweli kweli,Kwanza si kweli ulichoandika,na kauli inayomuhusu Guninita anayodai kuwa ilitamkwa na JK ni aina mpya kabisa ya uongo uliopo katika medani za kisiasa katika Nchii hii,JK hakutoa kauli kama hiyo.

Pia ni aina mpya ya Uzandiki na uongo uliotumia hapa unataka kutuaminisha kwa hoja kuwa wewe i mjumbe wa Nec ulikuwepo na wengi wetu inaonyeha tumeamini,tusihukumu vyomo vya habari eti vimeshabikia tujifunze ukubali kuona na kusikia tusivovipenda, na nina shangaa watu humu ktk Jamvi kuwa mashabiki na kuunga mkono kauli na post yako ambao haihitaji nguvu kubwa kujua kuwa ni ushabiki.

Hebu jiulize swali dogo,kama kweli sita hakuomba Radhi MWANAHALISI lisingekuwa ripoti hiyo?wakati Ripota mkubwa wa Mwanahalisi ndani ya Vikao vya NEC bwana Ndhi,NAPE alikuwepo asingetoa taarifa hiyo?

It is True kuwa Sita ameomba Radhi na kwa Mara ya kwanza Naungana na Mwanakijiji ktk moja ya Post yake niliosoma leo sikumbuki ni wapi akisema kuwa alichofanya SITTA ni (Strategic Retreat) nakubaliana na mtazamo huu na sitta kwa wanaomfahmu tusubiri bunge la NOV na Feb,tunaweza kuona kitu kipya na jambo kubwa.

But hakuna faida kujidanganya na kujipa False hopes haina Doubt yaliyotokea ndo yaliyoripotiwa na Vyombo vya habari na hakuna upotoshaji wa aina yoyote

Pamoja na kukanusha habari ya mNEC nafikiri itakuwa vigumu kwetu kukubaliana na wewe. nNEC alikuwa ndani ya NEC na ametupa upande wake wa story. Sasa kama na wewe ungetuelezea walau kwa ufupi tu what really happened in there may be tungejaribu kuona kama mNEC ametumwa na Bwana Six kuja kupotosha mambo. Otherwise you do not have a case here!!!!
 
haya mambo yeu ya kuegemea kundi fulani ndo yanatuchanganya hapa..mambo ya rostam yanatoka wapi..au na wewe ulikuwa dodoma.mara ngapi CCM wanakaa dodoma na vyomba vya habari vinakwenda kuripoti habari..acha ubabaishaji hapa

Hutaki kusikia Rostam akitajwa kiasi kwamba sasa hukuona hata maelezo ya mjumbe kwamba ni memba wa kikao hicho.

Kama Rostam alipita-pita na kama anachangia ktk habari zisizo sahihi, kwa nini mjumbe asimtaje?

hakuna mtu awezaye kuwa neutral, ila sifa huwaendea wale walioko upande wenye substance.
 
Sasa ipi ni credible source? Baija ( Anayejiita mNEC ) au magazeti yaliyodai kupata habari kutoka kwa fellow Baijas NEC Members?

Mimi siendeshwi kwa Hisia mpaka sasa niko katikati yawezekana aliomba Msamha au Hakuomba je waweza kunipa Source?

Sasa huamini kama mimi ni mNEC?

Hisia sina-run high kwenye thread hii. Kwikwikwi. Credible source zitapatikana baada ya watu kutulia. Watu kurudi makwao na kuanza kusimulia.

Sasa hivi hii ni breaking news, kila gazeti linataka kuuza na kila mwanaJF anataka kuwa news analyst.
 
Mkuu Halisi,

Naona upo online, ebu tupe maoni yako

FP

Kwani Halisi naye ni mNEC???

I cannot Iimagine mpaka sasa tumeshindwa kupata story halisi na ukweli wa mkutano ambao una watu zaidi ya 200.

Nafikiri kwa ujumla wana wana CCM hawaangalii maslahi ya taifa ila wanaangalia maslahi yao. No wonder Six hawezi kutoka huko!!!
 
Hisia sina-run high kwenye thread hii. Kwikwikwi. Credible source zitapatikana baada ya watu kutulia. Watu kurudi makwao na kuanza kusimulia.

Sasa hivi hii ni breaking news, kila gazeti linataka kuuza na kila mwanaJF anataka kuwa news analyst.

I think you are 100 % correct!!!

Kwa sasa inabidi tusubiri uoga uwatoke ndiyo tuanze kupata story. Si umesikia kuwa hata RO iliitwa kule. May be kuwatia wajumbe uoga wadhani kuwa wanafuatiliwa.
 
Mwuulize Shalom akuambie kama kuna mtu zaidi ya Mwakalinga anayeweza kuwa sehemu tofauti katika muda huo huo. Shalom anafahamu watu gani wana uwezo huo wa KIROHO.

Sasa Ndugu yangu Masa, si muulizeni George Mwakalinga awaambie nini kilikuwa huko ndani? Inawezekana moja ya UTANO (hapa si UTATU TENA) wake Mwakalinga, mmoja ulikuwa kwenye kikao hicho......

This was BREAK, HAVE TIME...... Tuendelee na zile story za uko jela JKT na mkisikia sauti ya buti mwaulizana " huyo atakuwa afande Magwega..."

mbavu zangu jamani... I like that... "UTANO"
 
Kaazi kweli kweli,Kwanza si kweli ulichoandika,na kauli inayomuhusu Guninita anayodai kuwa ilitamkwa na JK ni aina mpya kabisa ya uongo uliopo katika medani za kisiasa katika Nchii hii,JK hakutoa kauli kama hiyo.

Pia ni aina mpya ya Uzandiki na uongo uliotumia hapa unataka kutuaminisha kwa hoja kuwa wewe i mjumbe wa Nec ulikuwepo na wengi wetu inaonyeha tumeamini,tusihukumu vyomo vya habari eti vimeshabikia tujifunze ukubali kuona na kusikia tusivovipenda, na nina shangaa watu humu ktk Jamvi kuwa mashabiki na kuunga mkono kauli na post yako ambao haihitaji nguvu kubwa kujua kuwa ni ushabiki.

Hebu jiulize swali dogo,kama kweli sita hakuomba Radhi MWANAHALISI lisingekuwa ripoti hiyo?wakati Ripota mkubwa wa Mwanahalisi ndani ya Vikao vya NEC bwana Ndhi,NAPE alikuwepo asingetoa taarifa hiyo?

It is True kuwa Sita ameomba Radhi na kwa Mara ya kwanza Naungana na Mwanakijiji ktk moja ya Post yake niliosoma leo sikumbuki ni wapi akisema kuwa alichofanya SITTA ni (Strategic Retreat) nakubaliana na mtazamo huu na sitta kwa wanaomfahmu tusubiri bunge la NOV na Feb,tunaweza kuona kitu kipya na jambo kubwa.

But hakuna faida kujidanganya na kujipa False hopes haina Doubt yaliyotokea ndo yaliyoripotiwa na Vyombo vya habari na hakuna upotoshaji wa aina yoyote

Soma vizuri MWANAHALISI Spika hakuomba radhi wanaelezea kuwa alisema "kufanya kosa si kosa; kosa ni kurudia kosa"
 
Acha kuharibu post wewe, nitakuita Kibwengo bure! Msalimie Samweli

Back
Top Bottom