Shukrani za dhati Mkuu Baija Balobi (Mjumbe wa NEC-CCM Kama ulivyojiita mwenyewe) kwa ufafanuzi wako wa nini kilichojiri huko Dodoma,Lakini pamoja na maelezo yako yote,ni ukweli usiopingika kwamba Mh.Sitta amepoteza Imani/umaarufu kwa Wabunge walio wengi haswa Wabunge wa CCM.
Kwa kuwa Wana-NEC (Haswa Wabunge wa CCM) walipendekeza Spika apokonywe kadi yake ya chama ili wamvue Ubunge na baadaye Uspika ,kushindwa njama hiyo.Nafikiri Spika kwa hiyari yake mwenyewe ajiuzulu Uspika,kwa sababu katika mazingira yaliyopo sasa,hawezi kuongoza Chombo hicho ikiwa Idadi kubwa ya Wabunge hawamkubali.
Ni wazi kuwa atabaki na Ubunge wake wa Urambo,mpaka hapo mwakani katika Uchaguzi....Atakuwa ana nafasi kubwa ya kuwashitaki Wapinzani/Wabaya wake kwa wananchi kwa jinsi walivyomfanyia Fitina kwa kutetea haki ya watanzania.....Sitomuelewa Sitta ikiwa atang'ang'ania kubaki na Uspika wake!Kule kukubali suluhisho Dodoma ilikuwa kwa Mantiki ya kutaka Kubaki na Wadhifa wa Ubunge (Anawajali watu wa Urambo waliompigia kura),Maana kama angekubali kurudisha Kadi,ni wazi kwamba angejivua Ubunge na kujiondoa kwenye Uspika.Na moja kwa moja angekuwa hajawatendea haki waliomchagua.
Hata hivyo imefika Wakati sasa kumtafuta SPIKA nje ya Bunge...Wanazuoni tuangalie sheria za Bunge zinasema vipi...Kwa sababu kwa mtindo huu wa sasa,kila wakati Spika atakuwa anaendesha Bunge kwa matakwa ya Chama chake kwa kuhofia kuwa atashitakiwa kwenye Vikao vya chama.
Utabiri wangu unaniambia kuwa Mh.Sitta atajiuzulu Uspika wa Bunge la Jamuhuri,kutokufanya hivyo itakuwa ni kufilisika Kisiasa...Huwezi kuongoza watu wasiokuwa na imani nawe.