Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Tatizo kubwa ni ripoti kuja kwa namna ambavyo wahusika wanaegemea kwenye makundi yao. Siku hizi hakuna hata chombo cha habari kinaaminika kwa kuripoti unbiased information. Hawa jamaa wameiteka nchi nzima? Hata hapa JF watu wanaleta taarifa zenye mwelekeo wanaoutaka badala ya kuripoti ukweli uliojiri.
 
Kigogo, ni kweli niko Dodoma hata sasa. Ukipenda niweke upande wowote, maana hali ilivyo kwa sasa, kubaki katikati ni hatari zaidi.

Unaogopa nini ndio gharama ya kukumbatia uovu. Upo ndani ya CCM na NEC kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi au unalinda maslahi? Hao akinamama walie tu hao ndio waliokuwa wanaimba wanamtaka Rais handsome aarghhhhh!!
 
Jamani mtaniwia radhi kwani kuna vitu bado sijavielewa, kwa hiyo kosa la Sitta haswa ni nini ?

Kosa lake ni kushupalia ufisadi. Wanataka atimize 'collective responsibility.' Hii inajadilika kama ifuatavyo: Ni kweli katika misingi ya utawala ukiwa ndani ya kikundi, kama chama au baraza fulani, tuseme mfano ukiwa ndani ya CCM au ukiwa katika Baraza la Mawaziri unatakiwa kukubali na kusimamia yote yanayokubalika huko hata kama mengine binafsi huyaelewi au huyapendi. Katika msingi huu ikiwa hautakuabaliana na jambo fulani kubwa, mfano Ufisadi, inabidi utoke kwenye kikundi hiki ndipo ulaani au kupinga hicho kinachokuuzi.

Yanajitokeza mambo kadhaa ndani ya hili. Mosi, kwa kweli huwa ni hatari kupinga kikundi ukiwa bado uko ndani. Yanaweza kukuta ya Mrema. Unaweza pia kuKolimb'wa! Pili, utagundua kwamba CCM hasa leo hii wanatangazia Watanzania kwamba mtu yeyote anayefanya yanayofaa na hataki ufisadi ni hana hiyo collective resposibility. Ni sawa na kutangazia dunia kwamba ufisadi ni suala ambalo kila aliyemo anatakiwa alilinde! Tatu, wanachanganya kabisa nafasi ya Spika wa Bunge ambayo ni nafasi kubwa, tena sana, ndani ya Katiba ya Jamhuri. Wanataka yeye na waTanzania wakubali kwamba bungeni anafanya kazi ya CCM! Hii mimi naona ni hatari, tena sana.

Kwa kifupi, Sitta hana kosa ila CCM kwani bunge sio CCM na hivyo hategemewi kuilinda. Kiongozi wa CCM (Serikali) bungeni ni Waziri Mkuu na wakati wote Spika hawajibiki kwa CCM wala kwa Serikali yake.

Inatakiwa vijana wachache tuandamane kumuunga mkono na jitihada zake. Pia kumpa moyo. Tanzania inahitaji watu wengi wanaoweza kuthubutu kama Sitta. Ninaomba Mungu kabla sijafa nione nchi inaendeshwa tofauti na naahidi pia kufanya lolote, hata kufa kwenyewe, kufikia ndoto yangu.
 
Mimi nafikiri huyu bwana alipewa nchi watu wakamwita msanii akakubali, sasa hii imeleta taabu tuna rais wa nchi lakini Msanii na hata katika chama chake anaendeleza usanii na ukosefu wa analytical capacity, hivi wangechukua kadi ya spika naye akaamua kuzunguka na kuwashitaki kwa wananchi ccm ingekuwa wapi? Lowasa is hopeles na nafikiri reasoning capacity yake is zero na is morally sick hana hata chembe ya kumfikia Sitta, chamsingi hapa ni wana ccm ambao wako bado nadhamira safi kumshauri M/kiti wao kuchukua hatua dhidi ya mafisadi. Duniani kote inajulikana kuwa Haki itaishida dhuluma Kikwete should know that!! kwa hivi ukimsurubu mtu mtetea haki maana yake wewe ni mpenda dhuluma fisadi hakuna jina lingine na kwa wakati huu sijui!!! you must be blind or a fool for you not to see that,
Mungu Ibariki Tanzania
 
Chama Cha Mapinduzi ni chama cha wananchi. Kiongozi yeyote aliye madarakani kwa tiketi ya CCM aelewe kuwa nafasi hiyo aliyonayo ni dhamana aliyopewa kwa ridhaa ya wanachama wa CCM. Haitavumilika wala kukubalika kwa kiongozi yeyote yule anayetokea CCM kutumia nafasi hiyo kwa ajili ya kujijenga binafsi kwa gharama ya kuharibu maadili na maslahi ya chama. Pia ieleweke kuwa Chama cha Mapinduzi kina utaratibu na, viongozi na wanachama waliomakini katika kukabiliana na matatizo yanayoweza kujitokeza ndani na nje ya Chama.
Endapo kiongozi yeyote yule amekwenda kinyume na maadili au maslahi ya Chama basi hana budi kuwa muungwana na kuomba radhi na ajisahihishe. Vinginevyo, arudishe kadi!

Pundamilia maneno yako mazuri sana. Yananikiumbusha "Zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti wa CCM.".... Unaposema Chama cha wananchi (CUF???!) halafu unarudi kusema "Kiongozi yeyote aliye madarakani kwa tiketi ya CCM aelewe kuwa nafasi hiyo aliyonayo ni dhamana aliyopewa kwa ridhaa ya wanachama wa CCM" inakuwa vigumu kueleweka maana "Wananchi" wote si "wanachama wa CCM"... Kuna wenye vyama tofauti na wengine wasio na vyama kabisa. Lakini pia, zile zama za kusema, "kuna utaratibu" zimepitwa na wakati na ndio maana Sitta alijifunza kwa "Zitto vs Buzwagi" ambako mawaziri walizomewa na Zitto kupokewa kama shujaa Jangwani na nchini kote. Kwa hesabu za haraka haraka, Sitta na wenzake wakaikomboa CCM kwa kuteka ajenda ya kina Dr. Slaa na Zitto na kuibeba kwamba ni ajenda yao. Ikumbukwe hoja ya vita ya ufisadi ilipata kasi Mwembe Yanga kwenye List of Shame. Sasa yapi ni "maadili na Maslahi ya chama" unayoyazungumzia? Huu upofu utawaisha lini? Hata hizo 'ajira za ngoma' kutoa burudani kwa kupigwa magumi zitawaumiza baadaye maana mwisho wa ngoma kunoga ni kupasuka na mpiga ngoma ataunda nyingine kwa kutumia maiti za ng'ombe wengine kama yule wa mwanzo. Kama maadili na maslahi ya chama ni kumsafisha Lowassa na wenzake, basi mujue mumeamua kwa makusudi kukiondoa chama chenu (CCM) kutoka kwa wananchi na kukiacha solemba. Itakua vugumu sana kuwanunua (kama ilivyokua Dodoma) Watanzania wote na kama nilivyowahi kusema, :NCHI HAITATAWALIKA JAMANI:
 
Bhaghosha,
Kwakweli nilipata tetesi toka Dom,Dar, Rock City, A town zilikuwa nyingi sana kuhusu ilo swala la Spika sitta kuomba radhi NEC,
Ivi niwaulizeni kati ya mafiga haya 3 Mahakama, Bunge, Serikali, ni mali ya chama Fulani wanao miliki hiyo mihimili 3? Au ni ya watanzania bila kuangalia huyu ni chama Fulani au hana chama?? Kwanza Sidhani kwenye katiba ya nchi kumendikwa kuwa chama Fulani hili ndilo bunge lake na chama Fulani hii ndio mahakama au serikali yake plz fungueni upeo wa kuona mbali wana CCM & wananchi siku hizi hata ile elimu ya kufuta ujinga wanaijua fika na wantambua yote.
Jamani hapa me najua fika kuna mizimu 2 inawasumbua wana CCM wanaojitia wao ni vigogo wa chama,kwanza mzimu wa mwalimu JK nyerere kuna baadhi ya viongozi walikuwa wakipigwa vita wazi wazi na mwalimu aka mr. white hair, M JK na wafuasi wao kile kipindi cha uchaguzi wa Ben Mkapa sasa walirudi na mtindo wao mpya wa wanamtandao na walijipanga kweli kuwatumia matajiri kuingia Ikulu na walifanikiwa ila walisahau kitu Je ni jinsi gani ya kuliongoza Taifa huko ndiko wallah toba hawakujipanga na wameparaganyika sasa na hawajui wapi waanzie kujiweka sawa, kila kukicha shtuma fulu esp UFISADA ukichunguza sana wana ukaribu sana na Ikulu.
Mzimu mwiungine unao kikabli CCM ni Ule wa Horce Kolimba (CCM HAINA DIRA) hapa waliguswa mbaya wakaja na hasira na wakiongozwa na Jemedari wao mkuu Ben na kumpoteza mwezao Mungu ailaze Roho yake mahali pema peponi, Jamani , Ili swala la Dira ndilo lililopo sasa na kweli wamepoteza mwelekeo na ALAMA ZA NYAKATI kila kukicha kila mtu analake hakuna mwenye nchi, wale walioko madarakani ndio wale wale walikuwepo ndani ya chama wakati Kolimba akisema chama kimekosa Dira je leo wao wanaya yafanya nini na yapi? Leo wana taka kulifanya Bunge ni lao? au la wananchi? CCM inakwenda wapi? kwakweli ilo swala linatuchanganya sana wananchi, nchi inatawaliwa na kundi Fulani la watu wachache kweli hii ni haki?? Leo Sitta anasimama nakujaribu kuirekebisha CCM wajumbe kumbe wao kinawauma sasa wanataka nini hawajui tofauti ya Chama na Bunge??Hao si ndio wanafiki???? Ushauri kwangu kwao CCM Kuna haja ya kurudi nyuma na kuitazama irani ya CCM upya kama kweli kunahitajika mapinduzi ya Kisiasa, Kiuchumi na Kimaendeleo na siasa bora na safi na kuwepo na utawala bora wa sheria,Haiwezekani Irani ya CCM inayatimiza yote iliyo yasema itawatendea wananchi jamin sisi ni binadamu twapaswa wekana wazi ktk democrasia hii jamani mapungufu huwa yapo na yakubaliwe na ndio tutakwenda.

UV-CCM nanyi siwaaachi nyuma kwani nyie ndio ngao kuu ya CCM kushinda je nyie hili hamlioni au nanyi mafisadi walisha wapa kidogo??UV-CCM ni damu changa sana kwani mpaka leo hamuoni viongozi walioko madarakani ndio wale wale tokea enzi mkiwa mashuleni mpaka leo mwisha ingia ndani ya chama?? M'meshindwa simama kwa kauli mbiu moja na kusema iliyo kweli? UV-CCM ndio ngao ya CCM hilo liko wazi ila hatuji ni jinamizi gani nanyi limeisha wakumba? Ila twasikia na vingine tunavyo vielelezo mna vijembe vya hapa na pale na unafiki ni mwingi sana na mpaka sasa nyie kwa nyie UV-CCM hata kuongea au kukosoana mnashindwa na ndipo hapo wazee wa CCM wamewakamatia mnabishaaaa?? ushauri kwenu UV-CCM " TUSIMAME NA KUSEMA LUGHA MOJA, MUDA NA WAKATI NDIO HUU" nimewapa msemo huo 2010 mwapaswa chukua viti vingi vya ubunge kwaitajika Fikra mpya na mwendokasi mpya kulijenga Taifa TANZANIA
Tafakarini sana kwanini Spika sitta hakusema chochote CCM- JE NI KWELI CCM DIRA BADO IMEPOTEA AU HAWASOMI ALAMA ZA NYAKATI
 
JK hana sasa hivi na hakuwa na kabla sifa wala uwezo wa kuingoza Tanzania .Mtabisha laini ukweli ni huo.
 
Kigogo, ni kweli niko Dodoma hata sasa. Ukipenda niweke upande wowote, maana hali ilivyo kwa sasa, kubaki katikati ni hatari zaidi.

mihao wakina mama waliolia ukumbini ndo walionipa raha zaidi..hvi TOT band haikuwepo tutumbuiza
 
JK hana sasa hivi na hakuwa na kabla sifa wala uwezo wa kuingoza Tanzania .Mtabisha laini ukweli ni huo.

Nani atabisha? labda Salma pekee, hii ilijulikana na inajulikana, wenye akili wamemweka na kumfanya kama Robot, some guys outthere are controling him, either manually or automatic, Haiingii akilini kashfa zote hizo, hajafanya any remarkable move, bado yupo na anatabasamu , mtasema yuko sawasawa kweli?
 
lakini ilikuwaje akina mama kulia? walimuonea huruma Mzee Cx?
 
Mr.Baija Balobi,

Vipi wana UV-CCM wapo huko na wanamsimamo gani au tetesi zao zikoje??me hao ndio napenda kujua wana hali gani na mtazamo upi maana najua wapo huko, maana wao ndio wapiga debe full kwenye makampeni??
 
Mr.Baija Balobi,

Vipi wana UV-CCM wapo huko na wanamsimamo gani au tetesi zao zikoje??me hao ndio napenda kujua wana hali gani na mtazamo upi maana najua wapo huko, maana wao ndio wapiga debe full kwenye makampeni??

Mkuu mtazamo gani tena wakati wakubwa wao walishawakilisha? Kama Sitta alikuwa na supporter mmoja ambaye ni mke wake then hali hiyo inajieleza wazi.
 
Lunyungu,
Swala la kuongoza hiyo ni issue nyingine lakini ktk majungu na kuweka migonzo, JK yupo ktk wajanja..Na ndio maana alichukua Ikulu bila kuwa na sifa zinazotakiwa.

Waboreya,
Mkuu wangu ni lini scandal hazikuwepo Tanzania?..sema JK kaweza kuruhusu zianikwe ndio maana zinazungumziwa zaidi lakini toka Mwinyi hadi Mkapa wote hawa walifunika kombe wanaharamu (wananchi) wapite kapa..na ukiwa mjanja sana wanakumaliza..list unaijua vizuri.
Kumbuka Mrema hakupata sifa kwa sababu yeye ni kiongozi mzuri. Lipumba Au Mtikila wote hawa walitumia sababu za mafisadi kupata kura za wananchi.
 
Yote hii ilipangwa babuuu, kama JK angetaka Sitta awe nje hakuna mtu yeyote angepinga lakini kwa ujinga wao walifikiria JK yuko nao na huu ndio mwisho wa makelele ya Sitta bungeni.

"Sitta amefika mahala ameligeuza Bunge kuwa sehemu ya kuibua mashitaka, kuendesha kesi na kutoa hukumu, badala ya kuwa chombo cha kutunga sheria," alisema mmoja wa wajumbe wa NEC

Kumbuka mkuu Sitta wa leo sii yule aliyenza na Lowassa au wakati sakata la Richmond linapingwa na Lowassa kuzungumziwa.. Sitta alikuwa mklai hata Zitto kutolewa nje ya kikao lakini baada ya kupata baraka za JK unajua yaliyofuata.

"Huyu jamaa (Sitta) na wapambe wake wamekuwa wakikivuruga chama na serikali ndani na nje ya Bunge kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, kwa kisingizio cha ufisadi. Leo hii wamejionea wenyewe namna damu ya watu waliowaonea kama Edward Lowassa na wenzake inavyowalilia," alisema mjumbe mwingine.

Ilibidi ionekane kuwa JK hayupo na Sitta ili kujaza kokoro..kisha ajabu kutoka kwa Sitta kulikuwa rahisi sana kwani waamuzi hawakuwa tena wajumbe wapinzani ila wazee wa CC kina Mwinyi ambao tayari wanajua kinachofuatia..

"Bunge limeanza kuwa kama mchezo wa (kikundi cha televisheni cha vichekesho) The Comedy. Yaani kila mtu anafanya mambo yake mwenyewe, hali ambayo inaweza kusababisha watu kurushiana hata viatu ndani ya Ukumbi wa Bunge, sasa hali hii maana yake nini?," alisema katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, John Chiligati

Mkuu wangu wazee wote wa CCM wanataka JK akawajibishe Mafisadi kukisafisha chama -How na ukubwa wa kundi hilo ndio ilikuwa shida kwani uchaguizi mkuu wa 2010 adui wa kwanza wa CCM ni Mtandao.. wakiwaondoa hao, kazi iliyobakia ndogo sana..

"Kwa hiyo tumesema inatosha, hapo tulipofikia tusiendelee mbele. Wanaoropoka ovyo ni walevi na tumeona kuna kundi dogo ambalo limejiona kama ni wateule wa kuzungumzia sakata hilo (la ufisadi) bila ya kujua wabunge wote wana haki ya kuzungumzia suala hilo, lakini kwa utaratibu tena kwa kupitia katika vikao vya kamati za wabunge." aliongezea John Chiligati.

"Mkapa anastahili pongezi sio kejeli; anastahili heshima sio dharau na pia anastahili kuenziwa sio matusi," alimalizia.

Mkuu Mkandara, Mwenyekiti wa CCM na Raisi wa JMT, Mrisho Jakaya Kikwete unadai aliruhusu haya yote yasemwe kwenye kikao rasmi cha NEC ili awajue wabaya wake ! Sasa hapa atakuwa na mpango wa kumtosa nani - mafisadi au wapinga ufisadi ? Kwa maana nyingine unasema hakuwa na tatizo na Bunge kudhalilishwa maadam sasa kazi ya kuisafisha CCM inakuwa rahisi baada ya hiki kikao.
Duh, JMK ni kiboko - ana akili ya ziada ati !
 
“Sitta amefika mahala ameligeuza Bunge kuwa sehemu ya kuibua mashitaka, kuendesha kesi na kutoa hukumu, badala ya kuwa chombo cha kutunga sheria,” alisema mmoja wa wajumbe wa NEC



“Huyu jamaa (Sitta) na wapambe wake wamekuwa wakikivuruga chama na serikali ndani na nje ya Bunge kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, kwa kisingizio cha ufisadi. Leo hii wamejionea wenyewe namna damu ya watu waliowaonea kama Edward Lowassa na wenzake inavyowalilia,” alisema mjumbe mwingine.



“Bunge limeanza kuwa kama mchezo wa (kikundi cha televisheni cha vichekesho) The Comedy. Yaani kila mtu anafanya mambo yake mwenyewe, hali ambayo inaweza kusababisha watu kurushiana hata viatu ndani ya Ukumbi wa Bunge, sasa hali hii maana yake nini?," alisema katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, John Chiligati



“Kwa hiyo tumesema inatosha, hapo tulipofikia tusiendelee mbele. Wanaoropoka ovyo ni walevi na tumeona kuna kundi dogo ambalo limejiona kama ni wateule wa kuzungumzia sakata hilo (la ufisadi) bila ya kujua wabunge wote wana haki ya kuzungumzia suala hilo, lakini kwa utaratibu tena kwa kupitia katika vikao vya kamati za wabunge.”
aliongezea John Chiligati.

"Mkapa anastahili pongezi sio kejeli; anastahili heshima sio dharau na pia anastahili kuenziwa sio matusi," alimalizia.

Mkuu Mkandara, Mwenyekiti wa CCM na Raisi wa JMT, Mrisho Jakaya Kikwete unadai aliruhusu haya yote yasemwe kwenye kikao rasmi cha NEC ili awajue wabaya wake ! Sasa hapa atakuwa na mpango wa kumtosa nani - mafisadi au wapinga ufisadi ? Kwa maana nyingine unasema hakuwa na tatizo na Bunge kudhalilishwa maadam sasa kazi ya kuisafisha CCM inakuwa rahisi baada ya hiki kikao.
Duh, JMK ni kiboko - ana akili ya ziada ati
!

- Mkulu Mag3, haya yako ni mawazo ya a Great Thinker period!

Respect.


FMEs!
 
Indume Yene,
hapo wang'wise sasa mambo,kama kweli unachokisema ni kweli duh ivikweli kura yako unaambiwa nyamaza na ukweli unauona hao UV-CCM wanjengwa kuwa watu gani sasa?? Na kama kweli mke wake ndie alie kuwa ana m' support na hao watu ya kanda ya ziwa nao walikuwa kimya kweli? na wakati wao rasilimali nyingi za madini zatokea kwao?? kasoro yule mbunge sijui ni Mk wa ccm mkoa wa shy ndio najua hayuko karibu na sitta wa hamuungi mkono sitta. ivi jamani kweli kama hali ndio hio kanda ya ziwa hata kama nchi ikigawnywa kimajimbo huko tutamalizana wenyewe kwa wenyewe,

Nipagumu hapo ngoja tujesikia tamko lao hata la kujificha na kusema mitaani
 
Mag3,
Jibu lako rahisi sana.. Alichofanya JK ktk kikao hicho ndicho alichofanya Sitta Bungeni. Sasa kama Sitta analaaniwa kwa kulifanya Bunge kuwa sehemu ya kuibua mashitaka, kuendesha kesi na kutoa hukumu, badala ya kuwa chombo cha kutunga sheria," Unafikiri JK kafanya nini pale mkutano mkuu wa chama ambacho ni tofauti na Sitta?..

JK kaachia vurugu lipambe ktk mkutano muhimu wa chama... tumeona mashtaka, kuendeshwa kwa kesi, na hukumu zikitolewa badala ya kupanga mikakati endelevu ya chama..lengo lake ni ktk kutaka mafisadi wajitokeze kama Sitta alivyowakoroga Mafisadi bungeni.

Unless unataka kunambia Sitta hakujua alichokuwa akifanya Bungeni hivyo yawezekana kabisa hata JK hakufahamu jinsi ya ku deal na swala hilo ktk kikao hicho. Na hata kama hakujua kumbuka agenda hizi hupitiwa na baraza klabla hawakubali ziwekwe mbele.. pale mchezo ulishapangwa mkuu wangu.. ruksa haikutoka bure!

JK kama mwenyekiti angeweza kabisa kuiondoa mada hiyo ktk agenda za mkutano lakini aliachia wazi kama alivyokuwa akiachia Sitta habari za mafisadi..Jmimi nadhani JK kawavuruga CCM kuliko hata Sitta bungeni kwani sasa hivi uhasama wao uko nje nje..wanajua nani yuko upande gani.
Umenipata mkuu wangu...
 
Back
Top Bottom