Wazee na Waheshimiwa wana jamvi
Nikiwa mjumbe wa NEC nisiye na kundi lolote, nawajibika kuweka sawa rekodi moja katika mjadala unaoendelea kuhusu Spika Sitta na kilichotokea ndani ya ukumbi wa mkutano wa NEC.
Baada ya mjadala mrefu ulioshabikiwa sana na wajumbe wengi huku hoja zao zikijiwa bila jazba na wajumbe wachache lakini wanaoheshimika, Spika Sitta alikutana faragha na Mwenyekiti JK, Rais Mwinyi na Kinana. Baada ya faragha ile ambayo bado ni siri, Spika Sitta alipopata nafasi alisema maneno machache sana yenye pointi mbili. Kwanza, aliwashukuru wajumbe kwa kutumia uhuru wao kutoa maoni yao. Pili, alisema anaiachia meza kuu kutafakari yaliyosemwa na pande zote. Kisha alimaliza na kukaa.
Hata kama sikubaliani na baadhi ya misimamo yake, siwezi kusema kuwa aliomba radhi. Lakini pia siwezi sema alikosa watetezi kama inavyoripotiwa. Kulikuwa na hoja nzito, tena nyingine kutoka visiwani zilizomtetea.
Kiroja cha mjadala alikuwa Guninita, Mwenyekiti wa Mkoa wa DSM aliyechemka lakini JK akamzodoa kwa kumwambia "kama ana uchungu na chama mbona alikiacha na kwenda CHADEMA na kuitukana CCM kwa miaka miwili?"
Habari ni hiyo.
Baija