Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Natamani MWALIMU arudi japo sikumoja awacharaze bakora zaidi ya wale walimu wa kule Kagera then aondoke tena labda watakuwa na nidhamu. Kweli inatia uchungu sana wanavyotaka kutumbukiza kweli sijui Mungu atusaidia maana tusije fikia Zimbabwe.
 
jamani hivi akina Rostam hawezi kusoma alama za nyakati? wanafikiri wenyewe ni akina nani nasikia hata kichefuchefu nikiona au kusikia jina lake na hao wanaomlamba. CCM wawe makini na hao mafisadi hata maamuzi yaliyotolewa mi naona ni kizungu mkuti tu. Guninita kibarakatu hana jipya
 
Mwawando unanitia wasi wasi na uwezo wako wa kufikiri na kujenga hoja. Ni wabunge wangapi ambao ni wajumbe wa NEC? Una facts gani kwamba wabunge hawana imani na spika? manake naelewa hili lingeonekana bungeni kwenyewe. Niambie ni nini ulikiona bungeni kilichoonyesha hawana imani nae. Wasiwe na imani nae wakati kawaboreshea maslahi mara dufu?

Naomba nisiendelee kukuhiji manake sifanyagi mjadala na mafisadi kama wewe na usijisumbue kusema nikuombe radhi manake sitafanya hivyo wala sitatubu


Asante aunt baeleze baelewe!
 
Nikupongeze Shangazi kwa bandiko hili. nafikiri jamaa zangu nao (Waandishi) wana matatizo. Wanashabikia rumours na siyo facts. Sasa huo ni uandishi gani. Wapi Professionalism.


Pakacha tusiwalaumu sana waandishi manake ni jadi yao maana hata kwenye Biblia wameandikwa kwamba ni wanafiki na wamelaaniwa. Nao wanaangalia maslahi yao binafsi na wenginee majuzi wamenunuliwa magari na mheshimiwa mmoja
 
Tatizo kubwa ni ripoti kuja kwa namna ambavyo wahusika wanaegemea kwenye makundi yao. Siku hizi hakuna hata chombo cha habari kinaaminika kwa kuripoti unbiased information. Hawa jamaa wameiteka nchi nzima? Hata hapa JF watu wanaleta taarifa zenye mwelekeo wanaoutaka badala ya kuripoti ukweli uliojiri.

Mimi bado na imani na Saed Kubenea; nasubiri kwa hamu gazeti la wiki hii. Lazima atatupa mawili matatu kwa UHAKIKA kama yalivyojiri ndani ya kikao.
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 160 (54 members and 106 guests)

Jamani nyie 106 guests jiungeni na JF inawezekana mna majibu ya baadhi ya maswali tunayojiuliza hapa. Please Joine the forum of Great Thinkers pse pse.

Shapu!!

Wengine ni membaz ila hawaja log-in; usitie shaka, hapa ni mtakuja!!!
 
=Rev. Kishoka;556382]Je ina maana CCM si tena Chama cha Wakulima na Wafanyakazi?
Kwa walio na akili jibu ni "ndiyo" na wale vilaza jibu ni "hapana"

Je ina maana Maslahi ya CCM ni ya muhimu na yapewe kipaumbele kuliko maslahi ya Taifa na Wananchi wa Tanzania?
Kwa wanaCCM, jibu ni "ndiyo". Chama kwanza na Tanzania baadaye!

Je Maadili na Maslahi ya CCM ni yapi?
Kukubali kwamba na kuhakikisha kuwa wote waliomo ndani lao ni moja. Hata mimi binafsi nakubaliana nao. You are either with them or against them. You can't be neutral and remain with them!

Kama CCM ina nguvu na uwezo wa kuijtegemea kivyakevyake, kwa nini inang'ang'ania Katiba ya Tanzania na kulazimisha kila mtu afuate na kusika inachokisema?
Wanahitaji katiba kuendelea kutuzuga. Mfano kutueleza kuwa Tz ni nchi ya ujamaa na kujitegemea (wakati tufisadiwa na pia watoza ushuru, na wapambe wanakomba zaidi ya 18m), kutumia tume ya uchaguzi ambayo ni kiini macho kuingia ikulu na kukwepa wajibu wao wakuwatukimia wananchi kama ambayo wangefanya iwapo wangekubali kuandikwa kwa katiba mpya. Lakini katika utendaji wao wa kazi za kila siku, katiba si lolote si chochote. Kinachobaki kuwa cha maana ni mwenyekiti wa CCM (anayesimamia nani ateuliwe kuwa mbunge n.k) na vikao vyao vya kimangimeza!
 
Huyo mmiliki Hila Soud aangalie yasije kumpata yale ya mwekezaji kule Kenya. Wananchi walichoshwa wakamvaa...alipoteza maisha.
 
Kwa mtazamo wangu, JK aliamua kuwapa uwanja akina EL na wenzake ili watoe madukuduku yao yote kama ambavyo wamekuwa wakimuomba asaidie kuweka sawa misimamo ya Spika na wenzake. hiyo haimaanishi kuwa JK yuko upande wowote. Nadhani anatamani sana makundi haya yaishe ili mambo yaweze kuwa sawa na chama kiweze kujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao.

Mkuu Recta,

Napata taabu kukubaliana na wewe, kwa sababu hiyo philosophy itakuwa ndiyo kwanza inabuniwa na JK au ni utabiri wa shekh Yahaya Hussein. Akili yangu inashindwa kupata picha ya kiongozi (hata awe weak kiasi gani) anayeweza kuruhusu mjadala ambao hauna tija na hawezi kuumudu hadi kufikia hatima yake. Kwa lolote lile JK yuko na hao waliotaka kumsulubu Sitta labda ameshindwa kumudu kazi hiyo kwa sababu ya kutokuwa na msimamo. Sipati picha ya hilo unalolijadili hata kidogo!
 
- Hela zote walizi-invest kwa wajumbe wa visiwani knowing kwamba huwa wanaweza kumtishia Muungwana, lakini wakachemsha Spika ana support kubwa sana ya wabunge aliowapa marupu rupu mengi ya ajabu, lakini the damage is done na ninaamini kwamba Spika hatarudi bungeni kwani anahitaji miracle kushinda tena jimbo!
Respect.

FMES!

Mkuu FMES,
Uwezekano wa Six kurudi bungeni ni mkubwa kuliko wa kutorudi. Sina hakika kama JK anaweza kuridhia NEC kutorudisha jina la Six kwa ajili ya uchaguzi na hasa baada ya kura za maoni.
Msingi wa hoja yangu hapa ni kuwa, iwapo Six hatapata nafasi ya kugombea ubunge kwa jina lake kutorudishwa, ni dhahiri kuwa atasimama kugombea uspika wa Bunge bila kupitia CCM, hapa hatari yake ni kubwa kwa Chama na JK mwenyewe, kuliko kumhakikishia ubunge kwa CCM na kumnyima tiketi ya kugombea uspika kwenye uchaguzi wa spika.
 
waache waendelee kuharibu ili uchaguzi ujao uwe mgumu kwao.
naomba vyama vya upinzania tujiimarishe jamani wakati ndio huu. wakati ccm-mafisadi wanakaangana sisi tujiweke sawa wakati ni ukuta. Mheshimiwa sita Komaa nao na usibadili msimamo wakikutema njoo huku.
 
Mkuu FMES,
.....
Msingi wa hoja yangu hapa ni kuwa, iwapo Six hatapata nafasi ya kugombea ubunge kwa jina lake kutorudishwa, ni dhahiri kuwa atasimama kugombea uspika wa Bunge bila kupitia CCM, hapa hatari yake ni kubwa kwa Chama na JK mwenyewe, kuliko kumhakikishia ubunge kwa CCM na kumnyima tiketi ya kugombea uspika kwenye uchaguzi wa spika.

Sure!
Ila kwa sisiemu hii chafu lolote linaweza kutokea kwa Sita, kwani hata yeye bila pesa za RA asingemshinda Msekwa kwa kura nyingi kiasi kile!
 
Tunakoenda ni giza tupu ndugu zangu. Akina mama wengi wamelia sana ukumbini.

Hawa akina mama walikuwa wanalia nini? Kwa nini akina mama tu! Wao wao wanalia wakiwa upande gani? Msaada hapo. Mambo haya ni makubwa mno
 
Hawa akina mama walikuwa wanalia nini? Kwa nini akina mama tu! Wao wao wanalia wakiwa upande gani? Msaada hapo. Mambo haya ni makubwa mno
Akina mama kulia ni jadi yao. Nenda kwenye makanisa haya mapya ushuhudie wanavyolizwa.
 
Mkuu MTM,
kwa sisiemu tunayoiongelea hapa na kwa hatua iliyofikia, suala hili la kuwa na kauli moja na kwenda nayo kwa wananchi ni ngumu sana. Hio ilikuwa ni sisiemu ya Mwalimu na aliondoka nayo.
Kwa sasa kuna:-
Sisiemu Mtandao
Sisiemu Maslahi
Sisiemu matumaini
Sisiemu Bara
Sisiemu Visiwani
Sisiemu Nyanda za juu Kusini
Sisiemu Kaskazini
Sisiemu wapinga Ufisadi
Sisiemu pro-mafisadi
Sisiemu neutral (akina Balobi)
Sisiemu.........
[/QUOTE]

Mkuu hapo umeyapatia vya kutosha baadhi ya makundi ya hawa jamaa. Ulichokosea ni kuyaita ya Sisi 'M'. Hiyo sio kweli. Kwa matendo yao hawa ni "Fisi Wenu". Ni fisi kwa vile wamekula kila cha Watanzania. Sifa ya pili ni kuwa mmekuwa mkiwachagua kila mara kwa hiyo ninyi ndio mnaowaweka na kwa mantiki hiyo wanakuwa wenu. Mie simo.

Dawa ya mjinga ni kuumia
 
Baada ya spika sitta kuonyesha ukakamavu kuhusu suala la mafisadi na pia kutotoa upendeleo kwa chama chochote,serikali ya ccm imekuja juu na kusema kuwa spika sitta ndio chanzo cha kuvurugika kwa ccm.Na sasa nimesikia eti ndani ya halmashauri kuu ya ccm (NEC) kuna mipango ya kumng`oa spika sitta kwa sababu anafanya bunge liwe moto kwa serikali.Lakini ukweli ni kwamba spika sitta anafanya kazi anayotakiwa kufanya akiwa kama spika wa jamhuri ya muungano ya Tanzania(he`s doing the right things..) na sio kama kamati ya CCM inavyotaka.sasa swali linakuja je aliyekuwa spika wa zamani alikuwa anaficha maovu ya serikali na alikuwa anafanya kama ccm inavyotaka?
 
Una maana Pius Msekwa......edit heading yako yasomeka Msweka
 
Duh jamani.... Hatima ya watz ni nini? Kwa nini jambo jema hupingwa?. Ushetwani, au? Hivi huwezi mtu kufanya mema kwa ajili ya watu wako?

Tunahitaji kuziba mapengo yanayoruhusu wezi wa mali ya umma. Tunahitaji kuhakikisha mafisadi hayapati nguvu. Tunahitaji kuhakikisha mianya yote ya ufisadi inazibwa kwa chuma kigumu sana.
 
Back
Top Bottom