Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Hii ndio CCM ya siku hizi, mjumbe wa NEC anaeneza ujumbe unaosema WAREMBO HUNUKA KIKWAPA

Kwani uongo? Mjumbe wa NEC lazima ajue kucheza na nahau za lugha eti! huo msemo si ni sawa tu na si vyote ving'aavyo ni dhahabu?
 
Guninita alinyweshwa chungu
Kabila fulani wanaita 'tindishubila'. Akome na kihelehele!
Na 'tindishubila aba naluga aha gombolola' yaani maana yake 'anayesema sirudii tena kufanya kosa huwa anatokea mahakamani'!
 
Well, pima mwenyewe uamue. Nilikuwa ndani ya kikao. Waandishi wanaoandika kuwa kaomba radhi wanasema "Chanzo chetu cha uhakika ndani ya kikao".

Ni kweli mambo yalikuwa mazito kweli kwa sababu wabaya wa Sitta walipoona hawaungwi mkono kama walivyotaka, na hasa baada ya kuona JK hashtuki na kuwaunga mkono, wakaja na kubwa zaidi: Wakadai Sitta anautaka Urais kupitia bungeni na wakataja matukio kadhaa kuunga mkono madai yao hayo.

Tunakoenda ni giza tupu ndugu zangu. Akina mama wengi wamelia sana ukumbini.

Hee........ sikujua kama kumbe 6 hatakuwi kuwa raisi.........
 
Kwani NEC walikaa kwaajili ya SItta?
Na kama ni hivyo kosa gani alifanya la kukaliwa kikao ili aombe radhi?
 
I really don't care kile CCM wanafanya kwenye mikutano yao na kwa wanachama wao! Hizo ni "party politics". Lakini wanapovuka mpaka wa kuanza kuhoji mambo yanayofanyika Bungeni kwenye vikao vyao vya chama wanavunja mpaka wa uelewa wa uhuru wa mihimili. Hivi ni kitu gani kitawazuia nec kujadili Mahakama Kuu siku Mahakama hiyo ikitoa hukumu ya kuiumiza CCM?

Kosa la Sitta katika hili ni kuentertain malalamiko yanayohusiana na Bunge kujadiliwa kwenye kikao cha CCM. Alitakiwa kuwakatalia pale pale kuwa kama kuna mtu ana issue na yeye kuhusu Bungeni ailete Bungeni; kama siyo Mbunge awasiliane na Mbunge wake wailete Bungeni; na kama ni wabunge wengi wa CCM basi wana kakasi zao kule Bungeni wangeweza kuzungumza na kuchukua msimamo kule. ASINGEKUBALI kabisa kujadili mambo ya Bunge au kuacha watu wamuweke kwenye kona kutokana na nafasi yake ambayo si ya chama.

Kwa kukubali ameshusha hadhi ya uhuruwa USPIKA ni lazima arudishe. Sitarajii Jaji Mkuu kuitwa na CCM na kwenda kuwatolea maelezo ya jinsi gani maamuzu fulani yamefikiwa, kwanini SPIKA akubali?

Mwanakijji,
Sita hakuwa mwenyekiti wa CC au NEC. Hivyo basi hakuwa kwenye nafasi ya kukubali au kukataa nafasi yake kama spika kutokujadiliwa ndani ya CC au NEC. Mwenye wajibu hapa wa kulizuia hilo alitakiwa kuwa JK ambaye naamini alikuwa anajua nini kinafanyika na kwa sababu gani.
 
Nimepima Mwenyewe ila nashindwa kukutofautisha wewe Baija na hao waliosema Chanzo chetu cha uhakika ndani ya kikao kwa sababu kama wewe umeshindwa kujitaja iweje uwalaumu walioshindwa kutaja Chanzo?

Acha u-bazazi na wewe, unang'ang'ania ajitaje wewe mbona hujajitaja? Amekwambia ukitaka amini yake ukitaka pia acha usiamini, kwa ni utavunjika mguu ukiamini au usipoamini??
 
CCM kwa sasa hawana UBAVU wa kumnyang'anya kadi Sitta. Wanajua walivyohangaika na Mrema 1995. Mtu kama Mwalimu hayupo ndani ya CCM kwa sasa. Ambacho watakifanya 2010 ni kutompa tiketi ya kugombea Uspika. Kwa sasa tuendelee kutia story tu humu jamvini.
 
Hii thread kali,naona sasa hivi kuna wageni 64 na wenye jamvi 27,MOD anzisha award ya 'thread of the year' mimi nitatoa zawadi ya dolari za kimarekani 500.- kwa atakaye ipost.
 
Shukrani za dhati Mkuu Baija Balobi (Mjumbe wa NEC-CCM Kama ulivyojiita mwenyewe) kwa ufafanuzi wako wa nini kilichojiri huko Dodoma,Lakini pamoja na maelezo yako yote,ni ukweli usiopingika kwamba Mh.Sitta amepoteza Imani/umaarufu kwa Wabunge walio wengi haswa Wabunge wa CCM.

Kwa kuwa Wana-NEC (Haswa Wabunge wa CCM) walipendekeza Spika apokonywe kadi yake ya chama ili wamvue Ubunge na baadaye Uspika ,kushindwa njama hiyo.Nafikiri Spika kwa hiyari yake mwenyewe ajiuzulu Uspika,kwa sababu katika mazingira yaliyopo sasa,hawezi kuongoza Chombo hicho ikiwa Idadi kubwa ya Wabunge hawamkubali.

Ni wazi kuwa atabaki na Ubunge wake wa Urambo,mpaka hapo mwakani katika Uchaguzi....Atakuwa ana nafasi kubwa ya kuwashitaki Wapinzani/Wabaya wake kwa wananchi kwa jinsi walivyomfanyia Fitina kwa kutetea haki ya watanzania.....Sitomuelewa Sitta ikiwa atang'ang'ania kubaki na Uspika wake!Kule kukubali suluhisho Dodoma ilikuwa kwa Mantiki ya kutaka Kubaki na Wadhifa wa Ubunge (Anawajali watu wa Urambo waliompigia kura),Maana kama angekubali kurudisha Kadi,ni wazi kwamba angejivua Ubunge na kujiondoa kwenye Uspika.Na moja kwa moja angekuwa hajawatendea haki waliomchagua.

Hata hivyo imefika Wakati sasa kumtafuta SPIKA nje ya Bunge...Wanazuoni tuangalie sheria za Bunge zinasema vipi...Kwa sababu kwa mtindo huu wa sasa,kila wakati Spika atakuwa anaendesha Bunge kwa matakwa ya Chama chake kwa kuhofia kuwa atashitakiwa kwenye Vikao vya chama.

Utabiri wangu unaniambia kuwa Mh.Sitta atajiuzulu Uspika wa Bunge la Jamuhuri,kutokufanya hivyo itakuwa ni kufilisika Kisiasa...Huwezi kuongoza watu wasiokuwa na imani nawe.
 
CCM kwa sasa hawana UBAVU wa kumnyang'anya kadi Sitta. Wanajua walivyohangaika na Mrema 1995. Mtu kama Mwalimu hayupo ndani ya CCM kwa sasa. Ambacho watakifanya 2010 ni kutompa tiketi ya kugombea Uspika. Kwa sasa tuendelee kutia story tu humu jamvini.

Mkuu Wildcard, umesema kweli kabisa. Pamoja na kuwa uwezo wa kumnyang'anya kadi Spika Sitta wanao, hawataweza kuthubutu kufanya hivyo, hasa wakati huu ambao chama kina misukosuko mingi na kuelekea kugawanyika. Ni wakati ambapo uongozi wa juu wa chama unatakiwa kuwa makini sana. Bahati mbaya wanasiasa ni very unpredictable. Huwezi kuwa na uhakika wa 100% wa support ya wanasiasa wengi katika mambo yanayohutaji uungwaji mkono.

Vile vile, wanaweza kupiga zengwe asirudi kwenye kiti cha u-Spika baada ya uchaguzi mwakani, lakini hilo pia linategemea sana kama watashinda vita hivi vilivyoanza. Wakishinda, azma zao nyingi pia zitafanikiwa. Wakishindwa, Sitta atarudi kwa kishindo kwenye kiti chake. Inategemea nani mwenye Karata ya dume na ataitupa wakati gani, tusubiri tuone, kindumbwendumbwe ndio kinaanza.
 
Ninashukuru kwa ufafanizi huu Baija, kwani niliposoma taarifa kuwa Sitta aliomba radhi baada ya yule mwizi ambae pia ni mwenyekiti wa CCm Shinyanga na mafisadi wenzie kuropoka hovyo mkutanoni, sikuelewa sababu ambayo ingemfanya Sitta aombe radhi!! Mtu huomba radhi baada ya kufanya kosa au makosa ,sasa Sitta alifanya kosa gani kuweka bayana baada ya ushahidi kuwa Makamba na Londa walihusika na ufisadi katika halmashauri ya Kinondoni? Je ni kuikosea CCM kuiambia serikali yake kuwa haikuwajibika vilivyo kutekeleza maagizo ya BUNGE kuhusu mafisadi wa RICHMOND?? Kama hivyo ndivyo basi Sitta hana budi kufanya uamuzi wa busara na wa kishujaa juu ya nchi yake kuhusiana na chama cha Mafisadi!!!

Mwache akae humo kwanza na awafundishe adabu wapuuzi hao.. akuondoka watamueka mtu wao pale bungeni sasa ndo tuburuzwa ipasavyo kama enzi ya MKAPA na yuel spika kabla ya 6 nimeshamsahau jina (kwajinsi asivokuwa ameacha positive impact @#$^%^&*)
 
Last edited:
Mimi nadhani hoja yako haina mshiko kwa maana unazungumzia jambo ambalo undani wake linahukumika kimazingira na siyo wewe kusema nilikuwa ndani ama nje ya kikao pia kuhusu Spika tusibiri tutaona bunge lijalo ukweli kama kakubaliana na uovu na hoja zitazimika na uhuru wa bunge tulioshuhudia utawakuwa umefikia kikomo

ila kwa watanzania wenzangu wote mabaliko ya siasa ya nchi yetu yanafanyika kwa sisi watanzania wote tuishio mijini na vijiji kuwa wapiga kura na kuweza kuelewa kwa nini unampa kura yako mtu fulani

kwa ujumla NEC ya ccm siyo idadi ya watanzania ila ni kundi la wachache waliojijengea ama waliokasimiwa dhamana ya kuongoza watanzania hivyo watu kama spika sita nao ni sehemu ya muundo uliopo kama muundo wao wenyewe wawayumbisha sidhani kama ni sahihi kuendelea kuwa nao eti kwa kuwa NEC ya watu wasiozidi 1000 kutuongoza watanzania milioni 40 kama sisi tukiwakataa kwenye ballot box siku ya uchaguzi

mimi nasema kataa uovu jiandikishe kupiga kura tunza shahada yako hakikisha umepiga kura kwa kiongozi wa unaeamini anaweza kukuongoza

Wazee na Waheshimiwa wana jamvi

Nikiwa mjumbe wa NEC nisiye na kundi lolote, nawajibika kuweka sawa rekodi moja katika mjadala unaoendelea kuhusu Spika Sitta na kilichotokea ndani ya ukumbi wa mkutano wa NEC.

Baada ya mjadala mrefu ulioshabikiwa sana na wajumbe wengi huku hoja zao zikijiwa bila jazba na wajumbe wachache lakini wanaoheshimika, Spika Sitta alikutana faragha na Mwenyekiti JK, Rais Mwinyi na Kinana. Baada ya faragha ile ambayo bado ni siri, Spika Sitta alipopata nafasi alisema maneno machache sana yenye pointi mbili. Kwanza, aliwashukuru wajumbe kwa kutumia uhuru wao kutoa maoni yao. Pili, alisema anaiachia meza kuu kutafakari yaliyosemwa na pande zote. Kisha alimaliza na kukaa.

Hata kama sikubaliani na baadhi ya misimamo yake, siwezi kusema kuwa aliomba radhi. Lakini pia siwezi sema alikosa watetezi kama inavyoripotiwa. Kulikuwa na hoja nzito, tena nyingine kutoka visiwani zilizomtetea.

Kiroja cha mjadala alikuwa Guninita, Mwenyekiti wa Mkoa wa DSM aliyechemka lakini JK akamzodoa kwa kumwambia "kama ana uchungu na chama mbona alikiacha na kwenda CHADEMA na kuitukana CCM kwa miaka miwili?"

Habari ni hiyo.

Baija
 
Kwa kuwa Wana-NEC (Haswa Wabunge wa CCM) walipendekeza Spika apokonywe kadi yake ya chama ili wamvue Ubunge na baadaye Uspika ,kushindwa njama hiyo.Nafikiri Spika kwa hiyari yake mwenyewe ajiuzulu Uspika,kwa sababu katika mazingira yaliyopo sasa,hawezi kuongoza Chombo hicho ikiwa Idadi kubwa ya Wabunge hawamkubali.

Utabiri wangu unaniambia kuwa Mh.Sitta atajiuzulu Uspika wa Bunge la Jamuhuri,kutokufanya hivyo itakuwa ni kufilisika Kisiasa...Huwezi kuongoza watu wasiokuwa na imani nawe.

Nani kukuambia kuwa wabunge wengi hawana imani na Sitta? au umefanya research lini? NEC siyo wabunge wa CCM, kwani bunge lina-members wangapi? na walioko NEC ni wangapi? hata huko NEC si wote wanaompinga.

Pia unapaswa kujua kuwa waananchi wengi wanachukia ufisadi hasa suala la Richmond na EPA. Sitta akiachia kiti, itakuwa hatari kubwa kwa CCM kwani itaonyesha wazi na rasmi kuwa CCM ni chama cha mafisadi.
 
Shukrani za dhati Mkuu Baija Balobi (Mjumbe wa NEC-CCM Kama ulivyojiita mwenyewe) kwa ufafanuzi wako wa nini kilichojiri huko Dodoma,Lakini pamoja na maelezo yako yote,ni ukweli usiopingika kwamba Mh.Sitta amepoteza Imani/umaarufu kwa Wabunge walio wengi haswa Wabunge wa CCM.

Kwa kuwa Wana-NEC (Haswa Wabunge wa CCM) walipendekeza Spika apokonywe kadi yake ya chama ili wamvue Ubunge na baadaye Uspika ,kushindwa njama hiyo.Nafikiri Spika kwa hiyari yake mwenyewe ajiuzulu Uspika,kwa sababu katika mazingira yaliyopo sasa,hawezi kuongoza Chombo hicho ikiwa Idadi kubwa ya Wabunge hawamkubali.

Ni wazi kuwa atabaki na Ubunge wake wa Urambo,mpaka hapo mwakani katika Uchaguzi....Atakuwa ana nafasi kubwa ya kuwashitaki Wapinzani/Wabaya wake kwa wananchi kwa jinsi walivyomfanyia Fitina kwa kutetea haki ya watanzania.....Sitomuelewa Sitta ikiwa atang'ang'ania kubaki na Uspika wake!Kule kukubali suluhisho Dodoma ilikuwa kwa Mantiki ya kutaka Kubaki na Wadhifa wa Ubunge (Anawajali watu wa Urambo waliompigia kura),Maana kama angekubali kurudisha Kadi,ni wazi kwamba angejivua Ubunge na kujiondoa kwenye Uspika.Na moja kwa moja angekuwa hajawatendea haki waliomchagua.

Hata hivyo imefika Wakati sasa kumtafuta SPIKA nje ya Bunge...Wanazuoni tuangalie sheria za Bunge zinasema vipi...Kwa sababu kwa mtindo huu wa sasa,kila wakati Spika atakuwa anaendesha Bunge kwa matakwa ya Chama chake kwa kuhofia kuwa atashitakiwa kwenye Vikao vya chama.

Utabiri wangu unaniambia kuwa Mh.Sitta atajiuzulu Uspika wa Bunge la Jamuhuri,kutokufanya hivyo itakuwa ni kufilisika Kisiasa...Huwezi kuongoza watu wasiokuwa na imani nawe.

Nafikiri na naamini u spika si lazima uwe mbunge , nakumbuka ktk kinyang'anyiro cha uspika wakati wa sitta kulikuwa na mwanafunzi kutoka udsm aliyejitupa ktk kinyang'anyiro hicho.
 
Mimi naona Sita arejeshe silaha zake Bungeni mpaka Watanzania wote waelewe anasimamia nini na hapo sasa ajiuzulu hasa hapo ambapo uchaguzi wa serikali za mtaa utakua unakaribia.CCM wataumia!
 
Shukrani za dhati Mkuu Baija Balobi (Mjumbe wa NEC-CCM Kama ulivyojiita mwenyewe) kwa ufafanuzi wako wa nini kilichojiri huko Dodoma,Lakini pamoja na maelezo yako yote,ni ukweli usiopingika kwamba Mh.Sitta amepoteza Imani/umaarufu kwa Wabunge walio wengi haswa Wabunge wa CCM.

Kwa kuwa Wana-NEC (Haswa Wabunge wa CCM) walipendekeza Spika apokonywe kadi yake ya chama ili wamvue Ubunge na baadaye Uspika ,kushindwa njama hiyo.Nafikiri Spika kwa hiyari yake mwenyewe ajiuzulu Uspika,kwa sababu katika mazingira yaliyopo sasa,hawezi kuongoza Chombo hicho ikiwa Idadi kubwa ya Wabunge hawamkubali.

Ni wazi kuwa atabaki na Ubunge wake wa Urambo,mpaka hapo mwakani katika Uchaguzi....Atakuwa ana nafasi kubwa ya kuwashitaki Wapinzani/Wabaya wake kwa wananchi kwa jinsi walivyomfanyia Fitina kwa kutetea haki ya watanzania.....Sitomuelewa Sitta ikiwa atang'ang'ania kubaki na Uspika wake!Kule kukubali suluhisho Dodoma ilikuwa kwa Mantiki ya kutaka Kubaki na Wadhifa wa Ubunge (Anawajali watu wa Urambo waliompigia kura),Maana kama angekubali kurudisha Kadi,ni wazi kwamba angejivua Ubunge na kujiondoa kwenye Uspika.Na moja kwa moja angekuwa hajawatendea haki waliomchagua.

Hata hivyo imefika Wakati sasa kumtafuta SPIKA nje ya Bunge...Wanazuoni tuangalie sheria za Bunge zinasema vipi...Kwa sababu kwa mtindo huu wa sasa,kila wakati Spika atakuwa anaendesha Bunge kwa matakwa ya Chama chake kwa kuhofia kuwa atashitakiwa kwenye Vikao vya chama.

Utabiri wangu unaniambia kuwa Mh.Sitta atajiuzulu Uspika wa Bunge la Jamuhuri,kutokufanya hivyo itakuwa ni kufilisika Kisiasa...Huwezi kuongoza watu wasiokuwa na imani nawe.

Hii ni vita hakuna ku surrender

Isitoshe si wabunge wote ni wajumbe wa NEC
 
haya mambo yeu ya kuegemea kundi fulani ndo yanatuchanganya hapa..mambo ya rostam yanatoka wapi..au na wewe ulikuwa dodoma.mara ngapi CCM wanakaa dodoma na vyomba vya habari vinakwenda kuripoti habari..acha ubabaishaji hapa

Du!!!! Ngoma inogile sasa. Mtu keshaeleza kuwa alikuwa Dodoma na alihudhuria kikao. Na ameeleza undani wa anayoyajua. Jazba ya nini tena.

Haya!! NEC iya CCM imemaliza kikao chake sasa NEC ya JF inaanza. Tutaona na kusikia mengi.
 
Shukrani za dhati Mkuu Baija Balobi (Mjumbe wa NEC-CCM Kama ulivyojiita mwenyewe) kwa ufafanuzi wako wa nini kilichojiri huko Dodoma,Lakini pamoja na maelezo yako yote,ni ukweli usiopingika kwamba Mh.Sitta amepoteza Imani/umaarufu kwa Wabunge walio wengi haswa Wabunge wa CCM.

Kwa kuwa Wana-NEC (Haswa Wabunge wa CCM) walipendekeza Spika apokonywe kadi yake ya chama ili wamvue Ubunge na baadaye Uspika ,kushindwa njama hiyo.Nafikiri Spika kwa hiyari yake mwenyewe ajiuzulu Uspika,kwa sababu katika mazingira yaliyopo sasa,hawezi kuongoza Chombo hicho ikiwa Idadi kubwa ya Wabunge hawamkubali.

Ni wazi kuwa atabaki na Ubunge wake wa Urambo,mpaka hapo mwakani katika Uchaguzi....Atakuwa ana nafasi kubwa ya kuwashitaki Wapinzani/Wabaya wake kwa wananchi kwa jinsi walivyomfanyia Fitina kwa kutetea haki ya watanzania.....Sitomuelewa Sitta ikiwa atang'ang'ania kubaki na Uspika wake!Kule kukubali suluhisho Dodoma ilikuwa kwa Mantiki ya kutaka Kubaki na Wadhifa wa Ubunge (Anawajali watu wa Urambo waliompigia kura),Maana kama angekubali kurudisha Kadi,ni wazi kwamba angejivua Ubunge na kujiondoa kwenye Uspika.Na moja kwa moja angekuwa hajawatendea haki waliomchagua.

Hata hivyo imefika Wakati sasa kumtafuta SPIKA nje ya Bunge...Wanazuoni tuangalie sheria za Bunge zinasema vipi...Kwa sababu kwa mtindo huu wa sasa,kila wakati Spika atakuwa anaendesha Bunge kwa matakwa ya Chama chake kwa kuhofia kuwa atashitakiwa kwenye Vikao vya chama.

Utabiri wangu unaniambia kuwa Mh.Sitta atajiuzulu Uspika wa Bunge la Jamuhuri,kutokufanya hivyo itakuwa ni kufilisika Kisiasa...Huwezi kuongoza watu wasiokuwa na imani nawe.

Mkuu Mwawado, naheshimu sana mawazo yako. Ila napingana na hayo hapo juu, sana. Nilipokuwa nasoma ulichokiandika hapo juu, sikuweza kuelewa nia yako halisi, kwa maana sikuamini na bado siamini kuwa ushauri wako kwa Spika ni wa nia njema na wa dhati kabisa.

Mkuu kwanza naomba utambue kuwa Bunge silo lililoonyesha kutokuwa na imani na Spika. Walioonyesha hivyo ni baadhi tu ya wajumbe wa NEC-CCM ambao pia nia yao ilipingwa kwa hoja ndani ya kikao hicho na Wajumbe wengine. Kama kweli Spika haungwi mkono na Wabunge wengi, basi hilo lingejidhihirisha ndani ya Bunge na si kwenye vikao vyovyote vya CCM. Inawezekana kuwa kuungwa kwake mkono na Wabunge wengi ndiko chimbuko la hasira za wajumbe hao wa NEC na hofu yao kuhusiana na uimara wa Spika.

Kumbuka pia Mkuu, kwamba baada ya kushindwa kwa hoja, wajumbe hao walijaribu kupitisha fitina kuwa Spika ana nia ya kugombea uRais kwa kupitia support ya Wabunge (kwa mujibu wa M-NEC; Baija). Kama angekuwa hana support ya Wabunge, hili lisingeweza kuanzishwa, na harakati za kumchomoa zingekuwa zimeanzia Bungeni.

Mkuu, katika vita/mapambano au mashindano yoyote, kususia mashindano hayo hakuweza hata mara moja kukupa ushindi. Spika anatakiwa kuendelea kutumikia Bunge kama alivyochaguliwa na Wabunge wenzake kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu za Bunge hilo bila hofu, haya, uonevu wala upendeleo. Anatakiwa kufanya hivyo hivyo katika kuhudimia wapiga kura wake wa Urambo. Akiamua kujiuzuru U-Spika, si tu kwamba atadhihirisha udhaifu wa kiuongozi kwa kiwango cha juu kabisa, bali pia atakuwa ame-surrender kwa wale wote wenye nia ya kuliteka nyara Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa faida wanazozijua wao. Hilo ndilo la kuomba asifanye asilani.

Ajitolee muanga kuitetea nchi yake, Katiba na haki kama alivyoapa. Hata ikibidi kupoteza rasilimali zake zote katika kufanya hivyo. Na kwa kufanya hivyo, atakuwa shujaa wa Taifa hili hata baada ya kuondoka duniani.
 
I really don't care kile CCM wanafanya kwenye mikutano yao na kwa wanachama wao! Hizo ni "party politics". Lakini wanapovuka mpaka wa kuanza kuhoji mambo yanayofanyika Bungeni kwenye vikao vyao vya chama wanavunja mpaka wa uelewa wa uhuru wa mihimili. Hivi ni kitu gani kitawazuia nec kujadili Mahakama Kuu siku Mahakama hiyo ikitoa hukumu ya kuiumiza CCM?

Kosa la Sitta katika hili ni kuentertain malalamiko yanayohusiana na Bunge kujadiliwa kwenye kikao cha CCM. Alitakiwa kuwakatalia pale pale kuwa kama kuna mtu ana issue na yeye kuhusu Bungeni ailete Bungeni; kama siyo Mbunge awasiliane na Mbunge wake wailete Bungeni; na kama ni wabunge wengi wa CCM basi wana kakasi zao kule Bungeni wangeweza kuzungumza na kuchukua msimamo kule. ASINGEKUBALI kabisa kujadili mambo ya Bunge au kuacha watu wamuweke kwenye kona kutokana na nafasi yake ambayo si ya chama.

Kwa kukubali ameshusha hadhi ya uhuruwa USPIKA ni lazima arudishe. Sitarajii Jaji Mkuu kuitwa na CCM na kwenda kuwatolea maelezo ya jinsi gani maamuzu fulani yamefikiwa, kwanini SPIKA akubali?
Mwanakijiji, ni vigumu mno kutenganisha BUNGE, SERIKALI na CCM angalau kwa sasa. Sitta anaingia CC ya CCM kwa wadhifa wake kama Spika. Serikali kwa asilimia zaidi ya 98 inaundwa na WABUNGE, Wabunge wote wa CCM ni wajumbe wa mkutano mkuu wa Taifa wa CCM. Kwa mchanganyiko huu na hasa ikizingatiwa kwamba hata tiketi ya kugombea USPIKA kapewa na vikao hivyohivyo vya CCM kumjadili kama Spika hakuepukiki. Kuna UJINGA mwingi sana kwenye KATIBA yetu.
 
Yaliojiri katika mkutano wa CCM Dodoma yameniacha njia panda hasa kuhusiana na ile dhana ya Separation of Powers. Mahakama ni chombo huru chenye mamlaka yake ambacho hakitakiwi kuingiliwa, vivyo hivyo na Bunge na Serikali (Executive). Ila yaliyotokea Dodoma kwa ndugu yetu Sitta (Spika=Bunge) kuwekwa kiti moto inanipa tabu kuelewa hii dhana ya sep of powers imekaaje. Msaada tafadhali.
 
Back
Top Bottom