Kabla Allison hajaanza kutoa maboko kuna game kadhaa yeye ndiye alikuwa Man of The Match.
Tukatoa tahadhari kwamba inapofikia Man Of The Match anakuwa golikipa, tena mara nyingi basi ujue yajayo hayafurahishi.
Mkuu Don Clericuzio haya ya leo tumeyasema mno kikosi hakina depth ya maana yaani game changers hawapo kabisa...
Hua muda mwingi nawatazama Manchester City maana ndio timu bora kwa hii misimu ya hivi karibuni na sasa.. Anachojivunia Pep sio tu kuwa kocha bora mbali ana kikosi kipana kila idara na angalau hawa wachezaji wake wanaridhika na dakika wanazopata.. Tulisema sana humu kuhusu sub za Liverpool unamtoa Firmino anaingia Origi ambaye hata goli lake la mwisho haijulikani ni lini alifunga.. Sasa tazama kwa Pep unamtoa Sterling anaingia Mahrez, unamtoa Dias anaingia Laporte, unamtoa Gudo anaingia Jesus na kadhalika... Yaani ni unatoa moto unaingiza moto sasa kwanini wasiwe bora zaidi ya wengine..
Hii dhana ya Klopp kua muumini eti wa kikosi kidogo kwa kweli ni janga na kama anafanya hivyo kwa kua FSG hawampi sapoti sokoni basi tusubirii kutembelea nyota ya Klopp na ramli kwa timu pinzani kumstopisha Manchester City.
Huwezi kua ni kikosi ambacho benchi ipo hoi na utegemee ushindi hapana...
Zipo taarifa Klopp na FSG ni ugomvi mpaka sasa kwa vile alihitaji sapoti ya kuletewa wachezaji wapya mapema January 2021 lakini FSG kama kawaida yao wakaingia mitini kwamba hakuna ela na mpaka sasa Edwards ndio anatumika kama mtu wa kati kujaribu kuwarudisha pamoja ili kuwe na harmony kama zamani... Klopp hakufurahia kwanza kuletewa hawa mabeki maana wapo aliochagua yeye lakini kwa vile wale ilitakiwa ela cash basi FSG hao mitini wakimuacha Klopp kwenye mataa huku wakihitaji ushindi uwanjani lol like serious..
Allison ki ukweli ni binadamu hivyo makosa kufanya hakwepi.. Hata hii nafasi tulipo aliyechangia zaidi ni huyu huyu Allison...
Klopp pamoja na kukosa bench la uhaika lazima tulipofikia akumbali anajiangusha mwenyewe na sub zake nadhani hii ni gemu ya 3 anamtoa Jones na hapo hapo tunasambaratika kwa vipigo sijui kama ni sadfa ama niaje, sasa cha kujiuliza kwa nini huyu dogo asimuache akipige dakika 90+...
Leo tena anasingizia goli lao la kwanza ni offside bla bla... Sababu zimekua nyingi na ukweli ni kwamba wenzetu wanacheza bora zaidi yetu wakati sahihi, tazama Manchester City tulipoteana kipindi cha pili na leo ndio vile vile ina maana half time kocha anachosema kinatekelezwa lakini sisi lol ni janga tupu..
Kwa hali hii sasa ni rasmi tunaelekea nafasi ya 6 au 7 tukibahatisha...
Ni muda pia awaamini mabeki waliopo kikosini wafanye kazi yao na kuwarudisha MFs kwenye nafasi zao, kwa hio gemu zijazo tuwaone Kabak, Davis ama Kabak Nats angalua wao wana instinct za kibeki sio kubahatisha na hawa MFS...
Yajayo yanatisha.
YNWA