Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Tatizo watu mnasahau sana. Liverpool pool ya zamani isingepata matokeo kwenye game ya Sheffield united na hii ya Salzburg .
kabisa ndugu, japo King Ngwaba si muumini wa haya yanayotokea ya winning ugly weekd na jana mi naona tuangalie pointi 3 mambo ya clean sheet na kadhalika kwa sasa tuyaache...
 
Sijawahi kumkubali huyo magwaya , ukiacha World cup alivyopambana , maana hata pale Leicester yule Soyuchu kaziba pengo lake vzr ,utadhan hakukuwahi kuwepo MTU anaitwa magwaya ,
Mkuu kumbe umemuona Soyuchu duh ndogo ni kama yupo pale siku nyingi nadhani uwepo wa Toure pale Foxes unawasaidia kuwapa mbinu za kuboresha defence...

Soyuchu japo hajafika levo za juu lakini kwa kazi yake aisee namkumbali..

Maguire aanze kutudhibitishia ile bei akina Honestty, Mc Cain hawajapigwa...

nasubiri na yule ndogo uliemtoa Celtic apone nione kazi yake...
 
Tumepata matokeo timu ipo vizuri, kikubwa beki line hasa full beki zetu ziwe zinagawa Muda wa kupandisha mashambulizi kuliko kushambulia muda Wote

Hii inawafanya wachoke hivyo kuwapa tabu CB mfano jana Robb na TAA walikuwa wanachelewa kurudi matokeo yake VVD akawa anafanya Kazi za watu watatu ukizingatia Gomez ametoka majeruhi hana fitness ya kutosha

Pia wachezaji wanaonekana wana uchovu sana lazima tuwape nafasi wengine
mkuu hao wengine ndio akina nani kwa mfano Salah atoke awekwe nani, Robbo atoke awekwe nani, Fabi nae hivyo hivyo, TAA nae hivyo n.k ukweli tuna benchi dhaifu mno yaani Klopp hana namna zaidi ya afanyayo...tuna watoto ambao ni trials kwenye big stage, tuna ma brexit wenye impact ndogo mno..kidogo Chamberlin na ambae kwa 4 3 3 ameonekana kupwaya

hatuna like for like subs zaidi ya Gomez, Matip nayo pia sio like for like 100%...

hao wengine ni tuzidi kuomba dua zote majeraha yatupite mbali...

vijana mpaka sasa wamepambana sana tunaongoza ligi, tuna supercup sealed sweetly and sweatly, UCL bado tupo na nafasi nzuri
 
Rabiot Ramsey na Fekir wote walitaka kuja bureee kawakataa alaumiwe nani ikiwa anabenchi dogo? Alionao ndo kawaona wazuri hivyo kila sifa ni zake yeye za ubovu au mafanikio zote ni zake tusubiri mwisho wa msimu.

Kuna mechi nne matata sana hapa mbele.
 
Klopp mechi ya pili kàmpeteni anatolewa hii imenifanya nipate tumaini flani kama la mtu aliyepo jangwani ila kwa mbaaali anayaona makazi ya watu.,

Hii ni wazi klopp mwenyewe ndani ya nafsi yake anaukiri ukweli juu ya kapten sisi tunaendelea kuangalia tu kati ya stelingi mkuu na stelingi makamu.
Ila hii imenifurahisha sababu ikiwa moja italeta umakini kuliko tukishinda kiwepesi wepesi tu.
 
Mkuu kumbe umemuona Soyuchu duh ndogo ni kama yupo pale siku nyingi nadhani uwepo wa Toure pale Foxes unawasaidia kuwapa mbinu za kuboresha defence...

Soyuchu japo hajafika levo za juu lakini kwa kazi yake aisee namkumbali..

Maguire aanze kutudhibitishia ile bei akina Honestty, Mc Cain hawajapigwa...

nasubiri na yule ndogo uliemtoa Celtic apone nione kazi yake...
Soyuch ni mzuri sana , tulimuhitaji , kwa hela ndogo tu, mwisho wa siku tukamuacha ,

Yule dogo wa Celtic ameshapona , Balaa alilofanya sio la kitoto .....
 
Erling Braut Haland na Hwang hee chan wapo form kali sana gotta be so good to be in our Squad kabisa

Hwang hee umri miaka 23 game 7 za ligi katupia manne msimu huu huyo dogo Haland ndio moto zaidi yaani umri miaka 19 ila anafunga magoli mengi kuliko idadi ya mechi zake

Hwang hee tukimchukua itasaidia kutengeneza far east Asian fan base
 
Rabiot Ramsey na Fekir wote walitaka kuja bureee kawakataa alaumiwe nani ikiwa anabenchi dogo? Alionao ndo kawaona wazuri hivyo kila sifa ni zake yeye za ubovu au mafanikio zote ni zake tusubiri mwisho wa msimu.

Kuna mechi nne matata sana hapa mbele.
Mkuu unaamini fekir kweli alikataliwa !? ..mpaka iliripotiwa na vipimo alifanya kabisa ..sawa Rabiot alitaka kuja ni mzuri labda kocha mwenyewe maamuzi yake (ya kimfumo)..mi nadhani January tunavunja kibubu ..atashushwa mtu/watu pale ..tuko kwa mapambano bado uzuri tumewapiga watu waliokuwa na records ya kutofungwa game 8 away na ni wakali wale watoto ..pamoja na majeruhi tumepata point ..tuombe yasitokee majeruhi mwngine first xi..akipona Alison .. Nathaniel ..Matip tuwe full naamini tutatoboa..
 
alaumiwe Klopp kwa kubaki na hii benchi na si mwingine, hii falsafa yake ya kutaka kufanya kazi na kikosi kindogo ilishamgharimu na pengine itamgharimu tena...

wapo wachezaji ambao naamini wasingefosi kua serial starters kama Timo,Hakim, Neres, Fernades, Iranian Messi,Thorgan nk hao angalau wangempa dimension mpya ya kua na mfumo tofauti na huu 4 3 3 ambao ki ukweli wachezaji wanatumika sana tu...

tangu gemu ya the Blades dalili zipo wazi kinachotusukuma kwa sasa ni uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na pongezi pia kwa Adrian jamaa anatuokoa sana tu pamoja na wasiwasi mwingi alionao kwa back pass lakini mpaka sasa tulipo amechangia...

tuendako kunaogopesha ndugu hatuna namna ni ku chill tu...
 
Soyuch ni mzuri sana , tulimuhitaji , kwa hela ndogo tu, mwisho wa siku tukamuacha ,

Yule dogo wa Celtic ameshapona , Balaa alilofanya sio la kitoto .....
hapo sawa kabisa maana defence mlipwaya na pale mbele mlikamilika ishu ilikua pale nyuma sasa akipona na manywele mspanish naaamini Big Four mtamchomoa angalau Spurs aafu mjipange kusonga mbele zaidi...
 
Erling Braut Haland na Hwang hee chan wapo form kali sana gotta be so good to be in our Squad kabisa

Hwang hee umri miaka 23 game 7 za ligi katupia manne msimu huu huyo dogo Haland ndio moto zaidi yaani umri miaka 19 ila anafunga magoli mengi kuliko idadi ya mechi zake

Hwang hee tukimchukua itasaidia kutengeneza far east Asian fan base
wazo poa kabisaa...na vizuri hao hawaji kukomaa waanzishwe kila mechi pia inakua maandalizi ya maisha bila mmoja au wote wa ma front three wetu pindi wakiamua kutafuta challenge mpya kwingineko...
 
Tunapozungumzia usajili na tukasema tuna kikosi chembamba, kuna watu (Washabiki wenzetu wa Liverpool) wanatuambia kuwa hakuna Mchezaji mzuri ambaye yupo tayari kuja Liverpool kukaa Benchi kwasababu kuna Salah, Mane na Firmino.

Hivi hawa watu wanatumia hoja gani? Jamani hebu nifahamisheni kwa hili!

Kwa kigezo gani Kuwa wachezaji wetu (Mane, Bobby na Salah) hawawezi kuekwa Bench?

Kwa mfano tungemsajili Joao Felix ndiyo angekaa bench mbele ya hawa Mane, Bobby na Salah?

Tuwe wakweli bhana hao wachezaji ni wa Kawaida sana na wachezaji wa Kiwaeka Bench wapo wengi!

Hata Coutinho tuliamini hakuna mchezaji wa kumueka Benchi kumbe nje ya Liverpool ni wa kawaida sana tu.

Kwahiyo ni kwamba wachezaji wanaonekana wakali kwasababu wanafaidika na Mfumo wa Klopp tu!

Inamaana hata hao kina Timo Werner wakija Liverpool nawao watafaidika na Mfumo wa Klopp na watakuwa wakali kuwaweka benchi hao Front 3.

Klopp asajili tusilete visingizio kuwa wachezaji hawatotaka kwasababu kuna Mane, Bobby na Salah.

PSG kuna Neymar, Mbappe, Di Maria na Cavani lakini kina Icardi wameenda kujichomeka palepale.

Idriss Gana Gueye hakusema kuwa haendi PSG kwasababu kuna kina Verrati, ameenda na ameweza kutoboa.

Kwahiyo tuwe positive jamani.
 
Hapa umeongea
 
Hats uvunje kibubu huezi pata viwango vya kina Rabiot huo mfumo ni kudanganyana tu mbona anafosi Hendo acheze akijua wazi ni mzigo kwa team.
Mkuu unaamini fekir kweli alikataliwa !? ..mpaka iliripotiwa na vipimo alifanya kabisa ..sawa Rabiot alitaka kuja ni mzuri labda kocha mwenyewe maamuzi yake (ya kimfumo)..mi nadhani January tunavunja kibubu ..atashushwa mtu/watu pale ..tuko kwa mapambano bado uzuri tumewapiga watu waliokuwa na records ya kutofungwa game 8 away na ni wakali wale watoto ..pamoja na majeruhi tumepata point ..tuombe yasitokee majeruhi mwngine first xi..akipona Alison .. Nathaniel ..Matip tuwe full naamini tutatoboa..
 
Tunapozungumzia usajili na tukasema tuna kikosi chembamba, kuna watu (Washabiki wenzetu wa Liverpool) wanatuambia kuwa hakuna Mchezaji mzuri ambaye yupo tayari kuja Liverpool kukaa Benchi kwasababu kuna Salah, Mane na Firmino.

Hivi hawa watu wanatumia hoja gani? Jamani hebu nifahamisheni kwa hili!

Kwa kigezo gani Kuwa wachezaji wetu (Mane, Bobby na Salah) hawawezi kuekwa Bench?

Kwa mfano tungemsajili Joao Felix ndiyo angekaa bench mbele ya hawa Mane, Bobby na Salah?

Tuwe wakweli bhana hao wachezaji ni wa Kawaida sana na wachezaji wa Kiwaeka Bench wapo wengi!

Hata Coutinho tuliamini hakuna mchezaji wa kumueka Benchi kumbe nje ya Liverpool ni wa kawaida sana tu.

Kwahiyo ni kwamba wachezaji wanaonekana wakali kwasababu wanafaidika na Mfumo wa Klopp tu!

Inamaana hata hao kina Timo Werner wakija Liverpool nawao watafaidika na Mfumo wa Klopp na watakuwa wakali kuwaweka benchi hao Front 3.

Klopp asajili tusilete visingizio kuwa wachezaji hawatotaka kwasababu kuna Mane, Bobby na Salah.

PSG kuna Neymar, Mbappe, Di Maria na Cavani lakini kina Icardi wameenda kujichomeka palepale.

Idriss Gana Gueye hakusema kuwa haendi PSG kwasababu kuna kina Verrati, ameenda na ameweza kutoboa.

Kwahiyo tuwe positive jamani.
Umewaacha Juve pale zile mido mwenye hakika ya namba ni yule anaevaa jezi namba 5 prujin sina hakika jina.waliobaki wote inategemea na mechi.sasa sie tuna gandisha kina Shaqil benchi hafu tunatangaza hatuna benchi bora.kuna mcheji gani anaekua bora akiwa benchi?
Hata Ronaldo ukimueka bench mech kadhaa siku utakayo mpanga atakua na mapungufu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom