Kwanza niseme wazi kuwa leo timu imecheza hovyo hovyo balaa, yaani it was extremely poor performance.
Pili niseme wazi kuwa Klopp leo maamuzi yake hayakuwa sahihi hata kidogo, especially baada ya kipindi cha pili kuanza. Mtu kama Salah hakutakiwa kurudi kipindi cha pili, ilitakiwa nafasi yake ichukuliwe na Shaqiri. Pia Firmino ndiyo angetoka nafasi yake aingie Sturridge. Kitendo cha kusubiria mpaka dakika ya 88 ndiyo unamuingiza Sturridge ni upuuzi. Mimi siyo kocha lakini niliona mapungufu ya wazi kabisa, nashangaa yeye Klopp kwa nini hakuyaona hayo.
Tatu niseme wazi kuwa mchezaji kama James Milner kwa umri wake na mechi zote anacheza siyo sahihi, ni wakati sasa wa Fabinho kuanza kucheza. Last season hatukuwa na depth kwenye squad yetu kwahiyo it was understandable wachezaji hao hao kucheza daily, this season Klopp afanye rotation ya akili.
Nne niseme wazi kuwa kwenye timu yetu kuna wachezaji washajua wao ni a must first eleven players, kwahiyo wameanza kubweteka...kocha afanye kazi yake hapo.
Mwisho niwapongeze Napoli although walitakiwa watupige kama nne hivi, maana leo tulikuwa hovyo sana!
Tukiendelea kucheza hivi tumekwisha, tutakuwa tunapigwa za kutosha.