JK ndie sio tuu anaongoza umati wa Watanzania katika heshima za mwisho za Bob Makani, pali pia ni JK ndiye aliyetoa PA inayotumika hapa!.
Kitendo cha heshima za mwisho za Kiongozi na muasisi wa Chadema kuagwa kwa kutumia PA ya Mwenyekiti wa CCM ni kitendo cha uthibitisho wa baadhi ya mazuri ya Kikwete!. Nilisema JK ni mtu wa watu!.
Matumizi haya ya PA ya JK pia ni uthibitisho wa political tolerance kuwa upinzani wa vyama sio uadui, Watanzani ni wamoja kwenye shida na raha.
Nawaombeni wapenzi wa Chadema wenye nia njema, lazima mtamshukuru JK hata kimoyomoyo tuu!.
RIP Bob Makani!.
Saa hii Freeman Mbowe anaongea atafuatiwa na JK!.