Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,754
Poleni watanzania mlioguswa na msiba huu mzito wa Bernard Kamilius Membe.
Ninaangalia live capture ya sherehe ya kumuaga Marehemu Membe hapo Karimjee. Naona kuna itifaki imeandaliwa kwa namna ambayo inanipa dukuduku kufahamu undani wake.
Protokali za Mkuu wa Nchi kushiriki msiba wa mtumishi ama mstaafu zinafahamika. Na ikumbukwe marehemu Membe alikuwa amestaafu na sheo chake cha juu cha mwisho kilikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nje.
Nimeona Serikali nzima imejaa pale Karimjee, na hata wakuu wa mihimili ya dola nao wameshiriki kupata mimbari ya kutoa salaam kwa protokali za serikali.
Nafahamu humu JF kuna wataalam wengi, naomba tuelimishane inakuwaje huu msiba kuwa na protokali za juu kuliko misiba hata ya mawaziri waliowahi kufariki wakiwa madarakani.
Tunamkumbuka aliyekuwa Waziri wa Ulinzi alipofariki hatukuona ukuu wa protokali namna hii.
R.I.P. Membe