Hichi kitita kipya cha NHIF kina nini ndani yake? Kwanini kipigiwe debe na kupingwa vikali? Tujadiliane

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,129
35,152
Kama ulidhani hilo jambo halikuhusu basi anza sasa kufikiri tofauti. Yanayoendelea baina ya NHIF na watoa huduma za afya binafsi ndio mwanzo wa picha itayokuja kwenye suala la bima ya afya kwa wote, ambayo itapaswa kuwa ya lazima kwa watu wote. Kwa kifupi sana Yatakayofuata yatakuwa marudio tu.

Kwa kuufungua mjadala, nitaweka baadhi ya hoja zinazojadiliwa na pande zote. Kwa mfano:

1. DAWA

NHIF wanasema wameongeza orodha ya dawa kwenye kitita hivyo wagonjwa watafaidika, wamiliki wa vituo vya afya binafsi wanasema bei ya dawa kwa NHIF imepunguzwa na kuwa chini zaidi ya bei ya soko hivyo ni hasara kwao, hawataweza kutoa baadhi ya dawa kwa wagonjwa wa NHIF.

2. VIPIMO
NHIF inasema vipimo vingi zaidi vimeongezwa katika kitita kipya hivyo wagonjwa watafaidika. Watoa huduma binafsi wanasema, malipo ya vipimo vingi yamepunguzwa sana kiasi cha wao kushindwa kuzifidia gharama za kuendelea kuvifanya kwa wagonjwa wa NHIF.

3. HUDUMA ZINGINE (Procedure)
Mfuko wa NHIF unasema umeongeza huduma ambazo hapo awali hazikuwepo kwenye mfuko wa NHIF. Wamiliki wa vituo binafsi wanasema malipo ya kufidia kuzitoa hizo huduma yako chini na hayakidhi gharama ambazo wao huziingia hapo kabla ili kuwezesha utoaji wa hizo huduma.

4. HUDUMA YA KUMUONA DAKTARI (Medical consultation)
NHIF wanasema pesa kwa ajili ya consultation ni hisani (motisha) kwa watoa huduma lakini sio jambo la lazima kuwepo kama mshahara au posho na kwa sasa wigo umepanuliwa kwa ngazi zote za utoaji huduma kulipwa malipo hayo. Wamiliki wa vituo vya afya wanalisema, msingi wa kutoa huduma za afya huanzia na kuishia kwenye medical consultation, hivyo wataalamu wa afya ni haki yao kulipwa kikamiliki medical consultation fee kulingana na soko la utoaji huduma za afya na siku zote inapaswa kuwa ni malipo ya lazima na sio hisani kutoka NHIF. Viwango vipya vimepunguzwa na vimeshindwa kuendana na soko lilivyo.

MAONI YANGU
NHIF imepanua wigo wa kutoa huduma kwa wanufaika wa mfuko lakini kwa gharama ya kuwabebesha mzigo wamiliki wa vituo binafsi vya afya.
 
Binafsi naona serikali inazingua. Kwanza NHIF wana tozo hadi basi. Wanapiga sana hela kupitia hizo tozo. Pili. Kuna changamoto moja ambayo inachelewesha sana matibabu. Baadhi ya vipimo huwa hospitali wanawasiliana kwanza na bima. Inaweza kuchukua saa zima hadi siku.

Serikali itambue kuna ufujaji mkubwa wa hela za serikali. Wapambane kuzima huo ufujaji na kiasi kilichookolewa kiwe ruzuku, na mojawapo wa wafaidika ni hao bima ili wananchi wakapate matibabu kwenye hospitali wanazotamani kwenda
 
Hao NHIF wameisha zingua, sasa wanataka kuwatwisha mzigo hospitali binafsi.
Kama hayo malipo yanatosha basi waende hospitali za serikali
 
Hapa Dawa kila taasisi ianzishe tu Bima zake, tumechoka haya malalamiko aaaagh
 
Binafsi naona serikali inazingua. Kwanza NHIF wana tozo hadi basi. Wanapiga sana hela kupitia hizo tozo. Pili. Kuna changamoto moja ambayo inachelewesha sana matibabu. Baadhi ya vipimo huwa hospitali wanawasiliana kwanza na bima. Inaweza kuchukua saa zima hadi siku. Serikali itambue kuna ufujaji mkubwa wa hela za serikali. Wapambane kuzima huo ufujaji na kiasi kilichookolewa kiwe ruzuku, na mojawapo wa wafaidika ni hao bima ili wananchi wakapate matibabu kwenye hospitali wanazotamani kwenda
Sijawahi kuzinguliwa na kadi yangu ya NHIF hospital zote nilizowahi kwenda kutibiwa,
 
The best ni serikali kuhakikisha inajenga hospitali angalau kila kata (kama ilivyokuwa innovation ya hayati Lowasa sekondari kila kata) tuachane na Hao wahuni.

Suala la afya sio la Kufanyia mzaha; iwe kipaumbele kwenye sera za 2025.
 
Kama ulidhani hilo jambo halikuhusu basi anza sasa kufikiri tofauti. Yanayoendelea baina ya NHIF na watoa huduma za afya binafsi ndio mwanzo wa picha itayokuja kwenye suala la bima ya afya kwa wote, ambayo itapaswa kuwa ya lazima kwa watu wote. Kwa kifupi sana Yatakayofuata yatakuwa marudio tu.

Kwa kuufungua mjadala, nitaweka baadhi ya hoja zinazojadiliwa na pande zote. Kwa mfano:

1. DAWA
NHIF wanasema wameongeza orodha ya dawa kwenye kitita hivyo wagonjwa watafaidika, wamiliki wa vituo vya afya binafsi wanasema bei ya dawa kwa NHIF imepunguzwa na kuwa chini zaidi ya bei ya soko hivyo ni hasara kwao, hawataweza kutoa baadhi ya dawa kwa wagonjwa wa NHIF.

2. VIPIMO
NHIF inasema vipimo vingi zaidi vimeongezwa katika kitita kipya hivyo wagonjwa watafaidika. Watoa huduma binafsi wanasema, malipo ya vipimo vingi yamepunguzwa sana kiasi cha wao kushindwa kuzifidia gharama za kuendelea kuvifanya kwa wagonjwa wa NHIF.

3. HUDUMA ZINGINE (Procedure)
Mfuko wa NHIF unasema umeongeza huduma ambazo hapo awali hazikuwepo kwenye mfuko wa NHIF. Wamiliki wa vituo binafsi wanasema malipo ya kufidia kuzitoa hizo huduma yako chini na hayakidhi gharama ambazo wao huziingia hapo kabla ili kuwezesha utoaji wa hizo huduma.

4. HUDUMA YA KUMUONA DAKTARI (Medical consultation)
NHIF wanasema pesa kwa ajili ya consultation ni hisani (motisha) kwa watoa huduma lakini sio jambo la lazima kuwepo kama mshahara au posho na kwa sasa wigo umepanuliwa kwa ngazi zote za utoaji huduma kulipwa malipo hayo. Wamiliki wa vituo vya afya wanalisema, msingi wa kutoa huduma za afya huanzia na kuishia kwenye medical consultation, hivyo wataalamu wa afya ni haki yao kulipwa kikamiliki medical consultation fee kulingana na soko la utoaji huduma za afya na siku zote inapaswa kuwa ni malipo ya lazima na sio hisani kutoka NHIF. Viwango vipya vimepunguzwa na vimeshindwa kuendana na soko lilivyo.

MAONI YANGU
NHIF imepanua wigo wa kutoa huduma kwa wanufaika wa mfuko lakini kwa gharama ya kuwabebesha mzigo wamiliki wa vituo binafsi vya afya.
Kiufupu serikali imwtuhadaa wananchi na kuwakandamiza watoa huduma za afya binafsi.
 
Sijawahi kuzinguliwa na kadi yangu ya NHIF hospital zote nilizowahi kwenda kutibiwa,
Hujahitaji vipimo vya juu labda. Pia ukitaka kujua usumbufu wao ni uwe na changamoto kwenye kadi au kwa wategemezi wako. Nenda pale makao makuu
 
The best ni serikali kuhakikisha inajenga hospitali angalau kila kata (kama ilivyokuwa innovation ya hayati Lowasa sekondari kila kata) tuachane na Hao wahuni.

Suala la afya sio la Kufanyia mzaha; iwe kipaumbele kwenye sera za 2025.
Kwenye dunia ya sasa huwezi kufanya jambo kubwa kama hilo bila kushirikisha private sekta.
 
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu uendeshaji wa NHIF. Serikali inabidi kuiangalia NHIF kwa jicho la karibu zaidi kujua changamoto zilizopo na kuangalia namna bora ya kuzitatua. Kinachoendelea kuhusu benefit package iliyotolewa inawaathiri wananchi zaidi kuliko NHIF na vituo binafsi.
Mapendekezo yangu ni kama ifuatavyo;
1. Wizara ya Afya irudishe kitita cha zamani kiendelee kutumika wakati wanaendelea kujadiliana na vituo binafsi ili kufikia muafaka wa kitita kipya cha NHIF.

2. Mh Rais aude kamati itakayojumuisha makundi yote kujadili na kufikia muafaka wa swala hili. Kamati iliyoundwa na Mh Waziri Ummy imeshindwa kuleta matokeo na akipewa nafasi aunde kamati nyingine sidhani kama tutapata matokeo chanya. Kamati hiyo nina hakika itakua neutral na itakuja na mapendekezo yatakayosaidia pande zote mbili.

3. Kuwepo na benefit package ya hospitali za serikali na hospitali binafsi. Ukiangalia benefit package iliyoandaliwa na NHIF imetoa bei kwa kuziangalia zaidi hospitali za serikali ambazo zinapata zuruku kutoka serikalini, hospitali binafsi hazina ruzuku,zinajiendesha zenyewe. Kuwepo kwa benefit package tofautitofauti itasaidi kupunguza mzigo kwenye mfuko kwa kiasi fulani.

4. Kama kuna madeni ambayo NHIF inaidai serikali, basi serikali iyalipe ili kurudisha ustahimilivu wa mfuko.

5. CAG afanye special audit ili kujua nini hasa kinaendelea kuhusu michango ya wanachama wa NHIF. Ripoti ya CAG ya mwaka 2022 ilionyesha kuwa kuna takribani 41 bilioni za mfuko zilizotumika kuwakopesha wafanyakazi wa NHIF. Inawezekana kuna mengi yataibuka ikifanyika special audit yatakayosaidia kuiweka NHIF iwe imara zaidi.

Kwa haya yanayoendelea, naona kuna kazi kubwa ya kufanya kabla hatujaenda kwenye bima ya afya kwa wote. NHIF imesajili wananchi takribani 15% tu. Sasa wananchi wote wakiwa na bima watawezaje kuendesha bima ya afya kwa wote?
Nashauri kuwepo na mfuko wa NHIF utakojuhusisha na wafanyakazi tu na mfuko mwingine utakaosaidia wananchi ambao hawapo kwenye sekta rasmi ambao ni wengi zaidi. Hiyo itasaidia usimamizi wa mifuko hiyo miwili.

Ninaamini Rais wetu ni msikivu na atatatua hizi changamoto zilizopo.
 
Kitu pekee nachoweza kuwaunga mkono NHIF ni hiyo consultation fee.

Lakini mambo mnegine yote NHIF wamepuyanga. Kama hizo dawa waseme basi ziwe zinapatikana huko MSD kwa bei nafuu zaidi.

Pia viwe pamoja na vitendea kazi katika hizo procedures.

Vinginevyo tutazika sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom