Miaka ya 90 pale uwanja wa ndege mzee Mwinyi aliwahi kunipa hela, fulana kwa mkono wake mwenyewe kisha akanambia maneno haya...

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Nikiwa na umri mdogo nilihudhuria pale katika uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Dar es salaam, kumuaga mzee wetu mzee Ally Hassan Mwinyi ambae alikuwa anaondoka kuelekea Zanzibar, baada ya utawala wake wa miaka 10 kuisha kikatiba.

Bibi yangu ambae alikuwa na umri sawa na marehemu mzee Mwinyi ila bibi alimzidi Mwinyi miezi miwili, alikuwa ni kiongozi wa kikundi fulan cha ngoma za kitamaduni zilizokuwa zinachaguliwa mara kwa mara kwenda kutumbuiza sehemu mbali mbali alizofika raisi Mwinyi enzi za utawala wake. Bibi yangu alikuwa na tatizo la ulemavu wa macho, hivyo mzee Mwinyi alitokea kumzoea na kumfahamu bibi yangu haraka sana (nahisi ni kutokana na ulemavu wake na pia kujituma hata pale alipokuwa mlemavu) mpaka kufikia kipindi mzee Mwinyi akawa anamwita bibi yangu "bi siti Mwinyi" kwa jina la utani.

Siku hiyo ya kumuaga mzee Mwinyi bibi na kikundi chake cha utamaduni walialikwa, hivyo wakati wakifanya maandalizi ya kujiandaa kwenda uwanja wa ndege mimi nikawa nang'ang'ania ili niende nao uwanja wa ndege kwa sababu usafiri ulikuwa wa bure tena basi la jeshi. Wakati huo nilikuwa bado kijana mdogo alafu ni mjukuu wa mwenye kikundi, hivyo hakuna aliepinga mimi kwenda hadi uwanja wa ndege kumuaga mzee Mwinyi.

Tulivyofika pale tukakuta vikundi vingine mbali mbali vya ngoma za kiutamaduni kutoka katika makabila na jamii mbali mbali, basi na sisi tukajumuika nao kumsubiri mgeni husika afike ili tumuage. Masaa mawili baada ya sisi kufika mzee Mwinyi alifika akiwa na familia yake akawa anapita katika kikundi kimoja kimoja ili kusikiliza nyimbo zao za kumuaga.

Alipofika pale katika kikundi cha bibi yangu alimsalimia bibi na kikundi chake chote kwa mkono, kisha akanisogelea na kuniuliza "mjukuu wangu wewe unaitwa nani?" Nikamjibu "naitwa M....", akaendelea "unasoma darasa la ngapi", nikamjibu ..., akauliza "umekuja na nani?" Nikamjibu "nimekuja na bibi yangu", bibi akaingilia kati na kumwambia "huyo ni mjukuu wangu", mzee Mwinyi akatabasamu akaingiza mkono mfukoni na kutoa kibunda cha pesa akanikabidhi nikakitia mfukoni.

Kulikuwa na jamaa pembeni (nahisi ni mlinzi au mpambe wake) akamwambia ampe tshirt 1 nyeupe iliyokuwa na picha yake akanikabidhi kama zawadi, kisha akanambia 👉 "Mjukuu wangu dunia ya leo ni elimu, hivyo pamoja na kupenda kuongozana na bibi yako katika mambo haya ya kitamaduni, lakini hakikisha elimu ndio kinakuwa kipaumbele chako cha kila siku katika maisha yako". Nikaitikia kwa kichwa huku nikitabasamu 😊 na yeye akatabasamu 😊

Kisha walinzi wake wakamwambia mzee muda wa ndege kuondoka unakaribia, akaendelea kuwaaga watu wengine mbali mbali waliokuwa pale uwanja wa ndege kumuaga, kisha akaingia ndani ya ndege huku akitupungia mkono.

Mzee Mwinyi alikuwa mtu mwenye moyo wa utu, wala hakuwahi kuwa na visasi na watu.
Aliwapenda watu na yeye alipendwa na watu. Taifa limepoteza mtu muhimu sana, ila ndo hivyo kazi ya Mungu haina makosa. Tulikuja kutoka udongoni, na tutarudia huko huko udongoni.

Bibi yangu yeye bado yupo hai ila ameshapoteza kumbukumbu, muda mwingine anamsahau mpaka mama yangu ambae ni mtoto wake mwenyewe wa kumzaa. Kidogo anamkumbuka mama yetu mdogo ambae ndio anaishi nae kwa sasa.

Pumzika kwa amani mzee Mwinyi, Mw/Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi ameena.
 
Daah ker elimu muhimu
 
Mkuu Mr Dudumizi, simulizi yako inaniliza. Hasa hapo alipoagwa na kuelekea Zanzibar. Na leo ataagwa tena na kuelekea Zanzibar tena. Ila leo ni tofauti na mwaka 1995. Mwaka 1995 aliondoka akiwa hai, leo atasafirishwa akiwa si hai. Ni maisha tu!

Mimi nami nilikutana na kupokea zawadi kutoka kwake mwaka 1992 alipotembelea Shule yetu ya Msingi akiwa Rais. Alianzia mahali alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi. Alinipa zawadi baada ya kufanya vyema kwenye kujieleza mbele yake.

Pumzika pema Mzee Mwinyi, Rais wetu wa awamu ya pili!
 
SIsi ni wanafiki sana, mtu akifa tunamsifia weee.

Mwinyi huyu aliyesababisha watumishi wa serikali waache kazi na kuingia kwenye biashara?

Mfumuko wa bei ulikuwa juu?

Nyerere kumlaumu kuwa aligeuza Ikuly kuwa nyumba ya walanguzi?

Akaiuza Loliondo?

Udini ukashamiri?

Mpeni mtu haki yake akiwa hai na akiwa mfu
 
Back
Top Bottom