Siku ,saa zinapita,kila mja wa Mwenyezi Mungu anazidi kukisogelea kifo chake.Hatujui siku wala saa ila yatupasa tujiandae kwani wakati unataradadi.Wengi tumeshistushwa na msiba wa mzee wetu Bob Nyanaga Makani,japo tulikuwa tunajua ni mgonjwa,lakini hatukutarajia itakuwa mapema mno kiasi hiki. Bob Makani,mwanafunzi wa Makerere University akisoma pamoja na Mkapa aliyekuwa rais wa Tanzania ameondoka lakini atakumbukwa kwa wengi na makubwa aliyoyafanya ndani ya nchi yetu.
Mchango wake hautasaulika katika medania za kisiasa,kwa hoja zake madhubuti.Ni pigo kubwa kwa wakazi wa manispaa ya Shinyanaga kwa jinsi alivyoshirikiana bega kwa bega katika kuleta mageuzi makubwa mkoani humo. Kila mwana wa Shinyanga analia akikumbuka harakati zake za kuleta mageuzi nchini akipambana na mabavu ya watawala wasiopenda kuambiwa ukweli.
Umakini wake na kutokujali kwake kutokana na kejeli za watawala leo hii kimeifikisha CDM hapa ilipo.Tunakumbuka sana hotuba yake aliyoitoa viwanja vya shule ya msingi Jomu iliyoko manispaa ya Shinyanga mjini,alisema"Nimeamua kupumzika,napumzika kwa kukifikisha chama hapa kilipo.Huko tulikotoka na sasa CDM kimekuwa ni chama makini,ila sitawacha hivi hivi,nina waletea kijana mwenzenu tuliyempika akapikika na hakika hatotuangusha.Pia ni utaratibu wetu ndani ya chama kuachiana nafasi za uongozi kama mimi nilivyoachiwa na mzee Mtei".
Maneno haya ni mazito,tena mno,ni changamoto ambayo CDM wanatakiwa kuifanyia kazi.Ikiwa msingi wake mkubwa kukiimarisha chama.Changamoto aliyoiacha mzee Makani iwe dira na muuongozo kwa wale wote wenye tabia ya kung'ang'ania madaraka si ndani ya CDM pekee bali na taifa kwa ujumla. Ilikumuenzi mzee wetu huyu,ni lazima tutekeleze kwa vitendo na kutembea ndani ya meneno yetu bila kujali msimamo wa kimakundi ambao hupelekea kuyumbishwa kwa maslahi ya taifa na watu wake.
Tukienda kinyume na kuanza kurumbana,madhila ya kumuenzi hayatakuwa na maana.Alikubali kukiendesha chama bila kujali nafasi ya urais.Umakini huo ndiyo uliopelekea CDM kuwa chama makini tofauti na vyama vingine huku akiamini,ule ulikuwa muda wa kujifunza na kujiweka sawa.Migogoro ya mbio za urais inayo sababisha vyama vingi kupoteza umakini wake kwa kujikita zaidi katika mbio za urais kuliko kutatua matatizo ya wananchi,ndizo changamoto ambazo tunapaswa kuzizingatia katika kumuenzi Bob Makani.