Live Kutoka Karimjee Hall: Kumuaga Bob Makani

Live Kutoka Karimjee Hall: Kumuaga Bob Makani



Huu ushamba wa kuwacha lebo ya suti mkonini nimeuona sana Tanzania, jamani hizo hun'golewa kabla ya suti kuvaliwa, hebu wacheni ushamba.

Inawezekana amekodisha kwa hiyo hawezi kuondoa lebo..
 
JK ndie sio tuu anaongoza umati wa Watanzania katika heshima za mwisho za Bob Makani, pali pia ni JK ndiye aliyetoa PA inayotumika hapa!.

Kitendo cha heshima za mwisho za Kiongozi na muasisi wa Chadema kuagwa kwa kutumia PA ya Mwenyekiti wa CCM ni kitendo cha uthibitisho wa baadhi ya mazuri ya Kikwete!. Nilisema JK ni mtu wa watu!.

Matumizi haya ya PA ya JK pia ni uthibitisho wa political tolerance kuwa upinzani wa vyama sio uadui, Watanzani ni wamoja kwenye shida na raha.

Nawaombeni wapenzi wa Chadema wenye nia njema, lazima mtamshukuru JK hata kimoyomoyo tuu!.

RIP Bob Makani!.

Saa hii Freeman Mbowe anaongea atafuatiwa na JK!.

JK si mtu wa watu, ni mwepesi na ni mshiriki na mtoa pole mzuri kwenye misiba, na aliingilia uhuru wa Mahakama kwenye kesi ya Lema, atakumbukwa kwa hilo
 
Hiyo ni flash ya camera, siyo lebo.

mpaka sasa bado sijafanikiwa kuiona hiyo lebo, ngoja niizoom zaidi huwenda nikafanikiwa

SAM_2469.JPG


bado sijafanikiwa
 
Bodygurd wa Mbowe siku zote anapenda kusimama nyuma ya Mbowe pamoja kuwa ana kitambi lakini ni mwepesi kama Chadema wenyewe wanavyosema.

leo umeni furahisha
 
Mkuu Pasco, sikutegemea kama utaandika hivyo. Mimi hapa mtaani suala la ufuasi wa wa mtu wa chama fulani cha siasa huwa nalijua kipindi cha uchaguzi tu, na mtu akifiwa huwa hatuna hata chembe ya mawazo kwamba yeye ni chama gani. Nimeshtuka kuona ukiandika kwamba Public Addressing System (PA) inayotumika kwenye msiba huo (wa CDM) ni mali ya mwenyekiti wa CCM! Kuna ajabu gani hapo hadi uandike? Mbona mimi huwa natoa maturubai yangu au umeme wangu kwenye misiba ya wasio na vitu hivyo bila kujali vyama vyao vya siasa? Sijawahi kufikiria kama kuna mtu atakuja kutokea na hoja ya kisiasa kwenye msiba wa jirani! Pole sana Pasco, maybe JK alikushinda tender mliyo.bid wote katika kutoa huduma ya PA, lakini naona kama vile unamchafua JK hapa!

fikra zake naza mkama hazina tofauti.
 
Sikufanikiwa kuwepo karimjee. Nimesikitika sana kukosa kumuaga mzee mwenzangu, Comrade mwenzangu.
 
Kaka wachaga wamekukosea nini? Mbona unaonekana unawachukia sana. Au ni siasa za maji taka zinakusababisha uongee haya. Pole mkuu ila badilika,

bora umuulize vizuri,hana hoja kabisa, bado ni mtoto, we angalia hoja yake eti PA ya jk.
Adhabu yake ni kumpuuza akili zake na za mukama hazina utofauti.
 


Huu ushamba wa kuwacha lebo ya suti mkonini nimeuona sana Tanzania, jamani hizo hun'golewa kabla ya suti kuvaliwa, hebu wacheni ushamba.

Thubutu hawezi kuitoa hiyo lebo wanakodi hizo suti 10,
000 kwa saa halafu ni marufuku hata kukaa.
 
Thubutu hawezi kuitoa hiyo lebo wanakodi hizo suti 10,
000 kwa saa halafu ni marufuku hata kukaa.

Mkuu ritz mimi huwa najua kwamba wanamuziki ndio huwa wanaazima nguo na kwenda nazo majukwaani zikiwa na lebo kumbe hata hawa wenzetu? Mimi ni mpenzi wa Wazee wa NGwasuma kuna siku nilimuuliza Jesus kwa nini huwa hawaondoi lebo kwenye mijinzi wanayipanda nayo jukwaani akaniambia MUKUBWA HIZI NGUO HUWA TUNAAZIMA KWENYE MA BOUTIQUE tunalipia kwa siku na kesho yake zinarudi na kutundikwa kwa mauzo. ritz umeniongezea lingine kwamba huwa hata kukaa hawaruhusiwi! Kumbe ndio maana unaweza kuta mtu kalamba suti jasho linamtoka kijana akimpisha apumzike anasema aaah endelea tu kukaa mimi nimekaa sana sasa nafanya mazoezi. Kumbe kuna marufuku nyuma yake!
 
Last edited by a moderator:
mpaka sasa bado sijafanikiwa kuiona hiyo lebo, ngoja niizoom zaidi huwenda nikafanikiwa

SAM_2469.JPG


bado sijafanikiwa
Mkuu nimeiangalia kwa karibu siyo lebel. ritz iangalie kwa karibu siyo lebel ni kitu kingime kabisa!
 
Last edited by a moderator:
Binadamu wema na walitumika kwa manufaa ya wengine hufa kimwili bali huishi kwa kukumbukwa kwa mema yao. Tutakukumbuka Daima Bob Makani
 
mkuu pasco kati ya watu niliowaona hawana misimamo ni wewe,mara kikwete hamtaki lowassa,mara kiwete hafai kuongoza,mara kikwete ni mtu wa watu,sasa unasimamia wapi mbona hueleweki????au ulisharudi kambi ya mkweree????ukipewa uongozi nchi hii utatusumbuwa sana wee jamaa
episodes, humu jf tuna tatizo na watu wenye kambi zao, hivyo mnataka kila mtu humu ama awe ni CCM au Chadema!.

Kwa hiyo ukisifia jema lolote la JK basi wewe ndio CCM?!. Kama unanidhania mimi ni mtu wa kujikomba komba kwa JK, tafuta uzi wangu wa mapungufu ya JK!. Siku zote nasisitiza mimi Pasco wa jf sina chama. Nikipewa uongozi nitawasumbua sana!. Very unfortunatelly, mimi sio mtu wa kusubiri kupewa!. Huo uongozi nipewe na nani ili iweje?. Sio kila mtu ana ambition ya uongozi!, mimi ni mmoja wao!.
 
JK ndie sio tuu anaongoza umati wa Watanzania katika heshima za mwisho za Bob Makani, pali pia ni JK ndiye aliyetoa PA inayotumika hapa!.

Kitendo cha heshima za mwisho za Kiongozi na muasisi wa Chadema kuagwa kwa kutumia PA ya Mwenyekiti wa CCM ni kitendo cha uthibitisho wa baadhi ya mazuri ya Kikwete!. Nilisema JK ni mtu wa watu!.

Matumizi haya ya PA ya JK pia ni uthibitisho wa political tolerance kuwa upinzani wa vyama sio uadui, Watanzani ni wamoja kwenye shida na raha.

Nawaombeni wapenzi wa Chadema wenye nia njema, lazima mtamshukuru JK hata kimoyomoyo tuu!.

RIP Bob Makani!.

Saa hii Freeman Mbowe anaongea atafuatiwa na JK!.
Siyo kwa hapa tu yatupasa watanzania kuelewa ya kuwa JK ni muungwana na tena siyo dikiteta kwani anayo nafasi kubwa sana ya kuukandamiza upinzani kama angependa lakini amewaacha tu waendeshe siasa bila kuwawekee mizengwe kama wafanyiwavyo wenzetu ktk nchi zinazotuzunguka,hata zinapofanyika chaguzi mbalimbali pale ccm inaposhindwa hatumii mabavu kulazimisha ushindi na hata kwenye mazishi ya kiongozi wa chama cha upinzani anashiriki kwa dhati,na hii ni ishara nyingine anatuonyesha ya kuwa hata ktk uchaguzi mkuu wa urais upinzani ukishinda hawezi kulazimisha ushindi kwa chama anachokiongoza atakubaliana na matokeo japo kibinadamu atakuwa anaumia
 
b3.jpg

Viongozi mbali mbali wa kitaifa na vyama vya siasa wakisubiri kuuaga mwili wa marehemu Bob Nyanga Makani huko viwanja vya Kareem Jee jijini Dar es Salaam (tarehe 11/06/2012). Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti wa Tume ya marekebisho ya katiba Tanzania Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba
 
Mbona wengi mawazo yao kama vile hayapo hapo? wanawaza tu kusafiri kwenda misibani? hasa huyo wa pili toka kulia, sijui ni nani huyu hata nimemsahau jamani, oooh kumbe kuna msiba kwa Jirani hapo Kenya
 
Back
Top Bottom