Shughuli ya kuaga mwili wa Hayati Edward Lowassa Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kwenye shughuli kuaga mwili wa Edward Lowassa inayofanyika leo tarehe 2/23/2024 katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam.


Salamu kutoka kwa viongozi mbalimbali

Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye
: Tunayo mengi ya kumkumbuka Lowassa

Rais Mstaafu Ali Mohamed Shein: Lowassa alikuwa akinivutia kwenye utendaji wake.

Jaji Joseph Warioba

1995 Lowassa alinitafuta akiwa na uchungu sana baada ya kuambiwa Nyerere ndio aliyetia ugumu kuwania Urais. Nilimtia moyo, hakukata tamaa.

2008 Lowassa alinitafuta baada ya kujiuzulu, alisema hakutendewa haki, wamemuhukumu bila kumsikiliza, alinitafuta tukazungumza, nilimwambia haya ni mambo ya kisiasa, asikate tamaa.

Alikuwa alipenda elimu, ni mtu mwenye imani kuwa ana wajibu wa kutumikia taifa, hakuwa mangimeza, alikuwa mtu wa vitendo, pamoja na mapungufu yake hakuwa mtu anayependa kugombana na watu, alikuwa kiongozi mvumilivu, alikuwa ni kiongozi mwenye sifa ya kuwa kiongozi, mwenye maono.

Jakaya Kikwete: Lowassa ametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi yetu, na ameacha alama zitakazokumbukwa daima.

Rais Hussein Mwinyi: Nimejifunza kutoka kwa Lowassa Uzalendo, uwajibikaji, ushirikiano na makundi mbalimbali na pamoja na kuweka mbele maslahi ya nchi.

Makamu wa Rais Philip Mpango: Alikuwa mtetezi wa maslahi wa wananchi wake wa Monduli, nasi tunapaswa kumuiga katika utumishi wetu
 
Mzee wa MADILIKO

Mzee alipenda vijana wafanikiwe

Mzee aliyechukia Umaskini yaani UNYONGE

Kanda ya Ziwa uliipambania MAJI jana leo kesho HATUTAKUSAHAU

Sasa hivi UNYONGE ni mtaji wa MABWANYENYE

Shetani apigwe mawe.....Taifa lingekuwa mbali sana

Rip Laigwanan wa Losimingor Mountain's
 
FB_IMG_1707813166963.jpg
 
Mnafiki wa Taifa anaongea sasa, na hotuba yake imekuwa fupi kwa aibu.
Hakuna mnafiki, kama umemsikiliza Warioba vizuri amesema Lowasa aliwekewa vikwazo na mowamo wa kuwa rais hata na baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mungu hakutaka Lowasa awe rais, hivyo hawa akina Nyerere na Kikwete walitumika tu.

Ni ujinga kumlaumu Yuda kwa kumsaliti Yesu wakati ilikuwa ni mpango wa Mungu.
 
Back
Top Bottom