Live Kutoka Karimjee Hall: Kumuaga Bob Makani

Live Kutoka Karimjee Hall: Kumuaga Bob Makani

R.I.P. Bob Nyanga Makani,you were a true role model!
 
R.i.i bob makani harakati zako hazitasahaulika
 
Timu nzima ya Chadema iko ndani ya nyumba!. Dr. Slaa ndiye wa kwanza kuzungumza!.

Mhe. Mbowe anapiga siasa ya kufa mtu hapa msibani!.

Sasa siasa za nini msibani anatakiwa kujikita zaidi kwenye maombelezo!
 
Samahani, hivi marehemu alikua muumini wa dini gani!???


Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 
R.I.P Mzee Nyanga Bob Makani nakumbuka mbali mwaka 1992 tulipokuwa tunaitambulisha Chadema pale Mnazi mmoja... du nimetokwa na machozi .... nilitamani uione siku ya ahadi... lakini mungu amekupenda zaidi....
 
Namuona Slaa, kakaa karibu na Rais Kikwete inatia moyo mpaka wamepeana mkono wa majonzi.
 
Huyo Zitto kutuvalia jeans tena tight msibani imehusu na nini?
 
Wadau sijajua ni protokal ama la ila bodigadi wa mbowe ameondolewa karibu na mwenyekiti wetu hapa! Tutawajua zaidi
 
Mukama alitaka kupotosha umma, kwa data zake za majitaka msibani!
 
JK ndie sio tuu anaongoza umati wa Watanzania katika heshima za mwisho za Bob Makani, pali pia ni JK ndiye aliyetoa PA inayotumika hapa!.

Kitendo cha heshima za mwisho za Kiongozi na muasisi wa Chadema kuagwa kwa kutumia PA ya Mwenyekiti wa CCM ni kitendo cha uthibitisho wa baadhi ya mazuri ya Kikwete!. Nilisema JK ni mtu wa watu!.

Matumizi haya ya PA ya JK pia ni uthibitisho wa political tolerance kuwa upinzani wa vyama sio uadui, Watanzani ni wamoja kwenye shida na raha.

Nawaombeni wapenzi wa Chadema wenye nia njema, lazima mtamshukuru JK hata kimoyomoyo tuu!.

RIP Bob Makani!.

Saa hii Freeman Mbowe anaongea atafuatiwa na JK!.

Kwenye red unaomba halafu lazima!?!?!?!? Pasco Pasco???
 
Kweli rais ni rais hata viti walivyokalia ni tofauti Rais JK kwa nini kiti chake tofauti na cha Mbowe na Slaa?
 
Wakati tunahuzunika kwa kumpoteza mzee makani pia ni wakati wa kufurahia yale aliyotufanyia enzi ya uhai wake.
R.i.p bob makani
 
Siku ,saa zinapita,kila mja wa Mwenyezi Mungu anazidi kukisogelea kifo chake.Hatujui siku wala saa ila yatupasa tujiandae kwani wakati unataradadi.Wengi tumeshistushwa na msiba wa mzee wetu Bob Nyanaga Makani,japo tulikuwa tunajua ni mgonjwa,lakini hatukutarajia itakuwa mapema mno kiasi hiki. Bob Makani,mwanafunzi wa Makerere University akisoma pamoja na Mkapa aliyekuwa rais wa Tanzania ameondoka lakini atakumbukwa kwa wengi na makubwa aliyoyafanya ndani ya nchi yetu.

Mchango wake hautasaulika katika medania za kisiasa,kwa hoja zake madhubuti.Ni pigo kubwa kwa wakazi wa manispaa ya Shinyanaga kwa jinsi alivyoshirikiana bega kwa bega katika kuleta mageuzi makubwa mkoani humo. Kila mwana wa Shinyanga analia akikumbuka harakati zake za kuleta mageuzi nchini akipambana na mabavu ya watawala wasiopenda kuambiwa ukweli.

Umakini wake na kutokujali kwake kutokana na kejeli za watawala leo hii kimeifikisha CDM hapa ilipo.Tunakumbuka sana hotuba yake aliyoitoa viwanja vya shule ya msingi Jomu iliyoko manispaa ya Shinyanga mjini,alisema"Nimeamua kupumzika,napumzika kwa kukifikisha chama hapa kilipo.Huko tulikotoka na sasa CDM kimekuwa ni chama makini,ila sitawacha hivi hivi,nina waletea kijana mwenzenu tuliyempika akapikika na hakika hatotuangusha.Pia ni utaratibu wetu ndani ya chama kuachiana nafasi za uongozi kama mimi nilivyoachiwa na mzee Mtei".

Maneno haya ni mazito,tena mno,ni changamoto ambayo CDM wanatakiwa kuifanyia kazi.Ikiwa msingi wake mkubwa kukiimarisha chama.Changamoto aliyoiacha mzee Makani iwe dira na muuongozo kwa wale wote wenye tabia ya kung'ang'ania madaraka si ndani ya CDM pekee bali na taifa kwa ujumla. Ilikumuenzi mzee wetu huyu,ni lazima tutekeleze kwa vitendo na kutembea ndani ya meneno yetu bila kujali msimamo wa kimakundi ambao hupelekea kuyumbishwa kwa maslahi ya taifa na watu wake.

Tukienda kinyume na kuanza kurumbana,madhila ya kumuenzi hayatakuwa na maana.Alikubali kukiendesha chama bila kujali nafasi ya urais.Umakini huo ndiyo uliopelekea CDM kuwa chama makini tofauti na vyama vingine huku akiamini,ule ulikuwa muda wa kujifunza na kujiweka sawa.Migogoro ya mbio za urais inayo sababisha vyama vingi kupoteza umakini wake kwa kujikita zaidi katika mbio za urais kuliko kutatua matatizo ya wananchi,ndizo changamoto ambazo tunapaswa kuzizingatia katika kumuenzi Bob Makani.

Huu ndio unafiki unaonipa kichefu chefu.
Jana nilianzisha sredi jinsi CDM ilivomsahau mzee Makani kiasi hata cha kulitelekeza gari lake pale nyumbani kwake likiwa na pancha.
JF Mods wameitoa sredi hiyo.
Leo mnamsifia na kumuenzi kwa maneno matupu, huu ni ulaghai mkubwa usio na kifani.
 
Back
Top Bottom