Waziri wa fedha alipaswa kumshauri Rais kukata matumizi kwa muda ya vitu kama mbio za Mwenge na sikukuu wakati huu ambao tunapambana na covid, kusambaza umeme na maji, kujenga bwawa la umeme, reli, barabara na makao makuu badala ya kupandisha mafuta na tozo za miamala. Wananchi hawawezi kuoni nia nzuri kwenye mboni za macho ya serikali badala yake watu wanaona viongozi wa serikali wasiojali watu wake wanalimaje, wanauzaje, wanavuaje, kufugaje, wanakulaje, wanajengaje na kusomeshaje. Takwimu zinatuambia kuwa 90% ya watanzania ni tegemezi, hivyo vurugu zote hizi za miamala, mafuta, PAYE, VAT, nk zinawalenga hawa 10% ya watanzania. Hawa 10% kumudu kuhudumia 90% itawalazimu watafute ujanjaujanja wa mbio za mwenye, sherehe za uhuru na muungano, semina nyingi, kufanya tafiti za kufoji, kusifia viongozi hata kama hawapendi, kukwepa kodi, kuiba vitu au muda wa mwajili wao, kula rushwa na ujambazi. Kila mtumishi na mfanyabiashara ni mwizi wa mali, muda, ama fedha za mwajili au umma.