Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,603
- 29,747
1. Rais wa awamu ya 5 Hayati JPM mpaka umauti unamkumba hakubadilisha msimamo wa serikali yake kuhusu chanjo ya UVIKO 19. Alisema wazi kila mahala alipoenda kwamba huu ugonjwa ni hofu inayoenezwa makusudikally kuwatisha watu na kuyumbisha mataifa duniani.
Alienda mbele zaidi kwa kusema Chanjo ya UVIKO imeandaliwa mahususi kututhuru waafrika na inawezekana kuna maradhi yamepandikizwa humo.
2. Tangu mazishi ya kitaifa ya Hayati JPM kamilike, serikali ya awamu ta 6 ikitumia maafisa walewale ambao walisimama kidete kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa tiba na kinga za asili dhidi ya COVID-19, ilianza kugeuza wimbo huo kwa kuanza kuigeukia sayansi ambayo waliipa kisogo kipindi cha awamu ya 5.
3. Kabla hata ya miezi 6 tangu kipenzi chetu JPM atutoke, serikali ya awamu ya 6 ilishapeleka maombi ya kupata mkopo wa UVIKO Relief Fund kutoka mashirika makubwa ya fedha duniani ambapo inaonesha walipewa masharti muhimu kabla haijapewa fedha hizo.
Pamoja na serikali nzima ngazi za juu kuamua kuvaa barakoa kila wanapokiwa kwenye public, lakini walianza kueneza hofu ya uwepo wa wagonjwa mahututi wa UVIKO. Lakini wananchi hawakuhamasika na hizo hoja kwani Awamu ya 5 ilishafanyakazi kubwa kuwatoa hofu wananchi dhidi ya hili gonjwa.
Kinachofurahisha zaidi ni kwamba Waziri wa Afya ambaye pia ni mtaaluma wa Udaktari aligeuka kuwa COMICAL ALI kwenye awamu ya Tano, leo ndiye anayeongoza jahazi la kuyabugia matapishi yake yote bila kusaza kuhusu stigma dhidi ya UVIKO.
4. Serikali imepokea msaada wa chanjo 1M za UVIKO 19. Amiri Jeshi Mkuu alichanjwa hadharani kuonesha imani na usalama wa CHANJO hiyo kwa watu wake. Viongozi mbalimbali walijitokeza kuchanja wakiwemo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Serikali imetoa maelekezo wananchi waanze kupokea chanjo kwa utaratibu uliowekwa ambapo makundi maalumu yataanza na kupewa kipaumbele.
==========
Kwa namna matukio yalivyokwenda kwa kasi kubwa, ni wazi Serikali ilipaswa kutafakari na kufanya maandalizi ya hatua hizi zote zilizofanyika kabla usiku wa msiba kumalizika.
A. ELIMU
Serikali ilipaswa kuanza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu CORONA na kutoa muda mzuri wa elimu hiyo kuenea na kueleweka kwa wananchi. Ikumbukwe kwamba kwenye Hotuba za Hayati JPM aliweka quotations za Uzalendo na mahaba kwa wananchi wa hali ya chini (target ya Serikali) na ikichukuliwa taaluma yake ya UFAMASIA ilimpa nafasi nzuri kueleweka na wananchi na kumuamini.
Elimu dhidi ya magonjwa ya mlipuko haitolewi kupitia matamko. Ni muhimu sana kushirikisha kada mbalimbali. Kwanza unawajengea uelewa kisha wanaenda kuwaelimisha wengine. Leo tunashuhudia tafsiri za jumbe mbalimbali kwa Kiswahili zikisambazwa kwa kasi kubwa kupitia mitandao ya kijamii na makundi ya WhatsApp dhidi ya agenda hasi zilizo nyuma ya huu ugonjwa wa UVIKO 19 na chanjo zake. Kuna taarifa mbali mbali zinazohusu athari za chanjo zenye ushahidi.
Elimu ya kuikataa chanjo ilifanyika tangu awamu ya 5. Leo tunawaona watu kama Gwajima wakisimama hadharani kuhamasisha wananchi kuikataa chanjo hiyo. Serikali imeshikwa na kigugumizi
B. WAZIRI na NAIBU WAKE
Serikali kuendelea kuwatumia Waziri na Naibu walewale waliotuaminisha kuwa huu ugonjwa ni kituko cha kimataifa, ni wazi wananchi wanaona kuwa kinachoendelea ni Pwagu na Pwaguzi.
Kisiasa, walipaswa kuondolewa hapo na kuketwa sura mpya.
Kisayansi walipaswa kutolewa kwenye nafasi zao kwani wakiwa kwenye awamu ya 5 waliisaliti sayansi kwa viwango vya juu vya heshima (Hons)
Kama CCM iliweza kuwaweka pembeni wasaidizi wakuu wa Hayati JPM ili iweze kumpa mwanzo mpya Mwenyekiti mpya wa CCM Taifa, basi Ikulu inapaswa kupiga hesabu kwenye eneo la wizara ya Afya na maeneo mengine
C. DHAMANA kwa WANAOCHANJWA
Serikali kupitia Msemaji wake Mkuu, imeweka utaratibu kwamba kabla mtu hajachanjwa (kwa hiyari), analazimika kujaza na kusaini fomu inayoitoa lawamani serikali endapo chanjo italeta changamoto kwa mchanjwaji.
Hii fomu inapingana na ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ijayotoa haki ya kuishi na hifadhi ya jamii. Serikali ilipaswa kuwalinda wananchi wake kwa any possible attack iwe ya kivita au kibaolojia kwani inapojiweka pembeni kitowajibika na athari za chanjo ni kukwepa jukumu la Kikatiba. Serikali ilipaswa basi kuwawajibisha watengemezaji ww chanjo hiyo ili kuondoa dhana inayoenea kuwa imekuja kwa majaribio na kabla haijathibitishwa nje ya mipaka ya dharura.
All in All Serikali ingeandaa mikakati na mpangokazi wa kutoa elimu inayoenda kufuta taswira hasi (kama zipo) zinazoweza kuzuia mafanikio ya kufikia malengo ya utoaji chanjo.
JamiiForums kama kisima cha thinkers, tujadili hili suala kwa lengo la kuisaidia nchi kwani tayari chanjo imefika na conspiracy imekuwa kubwa sana against.