#COVID19 Zanzibar: Kila Mzanzibar anayetaka Chanjo ya COVID-19 atapata, hakuna mgeni ataingia bila cheti cha Vipimo vya Corona

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,343
217,371
Hii ndio Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya wa serikali ya Mapinduzi , Mh Nassoro Mazrui , lengo ni kudhibiti maambukizi ya wimbi la tatu

Bado haijafahamika kama wageni kutoka Tanganyika nao watahusishwa au la .

Chanzo : ITV

FB_IMG_1624393489384.jpg


====

WANAOINGIA ZANZIBAR SHURTI CHETI CHANJO YA COVID-19

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeanza kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Covid-19 awamu ya tatu na kutangaza wageni wote watakaoingia nchini kuhakikisha wanakuwa na vyeti vya chanjo vya ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto, Nassor Ahmed Mazrui wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tahadhari ya ugonjwa huo kutokana na taarifa za kuingia kwa wimbi la tatu.

Mazrui alisema zipo baadhi ya nchi jirani zenye mahusiano makubwa na Tanzania ikiwemo Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) pamoja na Rwanda tayari wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid-19 limeingia na serikali za nchi hizo zimetangaza karantini kudhibiti athari zaidi.

Aidha alisema kwa upande wa wizara tayari imejipanga kukabiliana na janga hilo kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huo huku vituo vyote vya afya vikiwekwa tahadhari za ziada.

‘’Wizara ya Afya inatoa tahadhari kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Covid-19 awamu ya tatu ambapo baadhi ya nchi za Ulaya na Asia umeanza kusababisha maafa makubwa na nchi jirani ya Tanzania...kuanzia sasa wageni wote watakaoingia nchini watalazimika kuonesha cheti cha chanjo kwa ugonjwa huo,’’alisema.

Aidha aliitaja mikakati mingine inayotarajiwa kuchukuliwa kukabiliana na janga hilo ikiwemo wananchi kuvaa barakoa pamoja na kuepuka mikusanyiko ya watu wengi isiyokuwa na sababu za lazima.

Kuhusu suala la chanjo ya corona kwa wananchi wa Zanzibar, alisema suala hilo linasubiri tangazo rasmi la Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi mmoja Dk Abdallah Suleiman alisema wamejipanga kuhakikisha wafanyakazi wote kuanzia vituo vya afya hadi hospitali kuu wapo tayari kutoa huduma za dharura kwa wagonjwa watakaojitokeza wa Covid-19.

Alisema hadi sasa hakuna mgonjwa aliyetambuliwa kuambukizwa na ugonjwa huo huku akisisitiza hakuna taarifa za kuficha matukio ya ugonjwa huo.
CamScanner 06-23-2021 11.12.41_1.jpg

CamScanner 06-23-2021 11.12.41_2.jpg
CamScanner 06-23-2021 11.12.41_3.jpg
 
Hii haijakaa vizuri, ninavyofahamu mimi Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Tanzania hivyo anayepaswa kutoa kauli hiyo ni Serikali ya Jamuhuri ya Muungano.

Ila kwa kuwa humu Jf tunawanasheria wazuri, nina imani tutapata elimu juu ya hili
Katika huu muungano kuna mambo ya muungano na yasiyo ya muungano. Masuala ya afya si Jambo la muungano.

Kuna haja mashuleni kuanzia shule ya msingi kuwepo mada rasmi juu ya huu muungano.
 
Pole ndugu. Basi pata nafasi u google katiba ya Zanzibar kwa jibu la uhakika.
Sidhani kama kuna haja hiyo, kama Katiba ya Jamuhuri haitambui Zanzibar kama nchi bali ni sehemu ya muungano hiyo inatosha.
Yani ni kama vile tuseme Palestina ijiite nchi huru yenye mipaka, rais na bendera yake na huku UN haiitambui Palestina kama nchi, basi ujue Palestine sio nchi.

Hivyo basi katiba ya Zanzibar ata iandike Mara 100 kuwa Zanzibar ni nchi huku katiba ya Jamuuri ya muungano haitambui hilo basi ujue Zanzibar sio nchi.
 
Katika huu muungano kuna mambo ya muungano na yasiyo ya muungano. Masuala ya afya si Jambo la muungano.

Kuna haja mashuleni kuanzia shule ya msingi kuwepo mada rasmi juu ya huu muungano.
Aiseeee !!
 
Hii haijakaa vizuri, ninavyofahamu mimi Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Tanzania hivyo anayepaswa kutoa kauli hiyo ni Serikali ya Jamuhuri ya Muungano.

Ila kwa kuwa humu Jf tunawanasheria wazuri, nina imani tutapata elimu juu ya hili
Zanzibar ni nchi mkuu.

Laa kama ndio tunataka kuanzisha mijadala basi na tuendelee, ila huku tunajadiliana kule wenzetu wanatenda kama nchi. Tayari tamko limetoka hilo kutoka kwenye SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.

kazi iendelee
 
Back
Top Bottom