Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,811
4,533
Dkt. Gwajima apiga marufuku kuwauzia akina mama kadi za kliniki

PICHA: Dkt. Dorothy Gwajima

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amesema serikali haitatumia nguvu katika kukabilia wimbi la tatu la virusi vya corona, na badala yake watajikita katika utoaji elimu zaidi.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari jana Dar es Salaam lililoulizwa kuwa ni kwa nini mikusanyiko katika vyombo vya usafiri na matukio mbalimbali yanaendelea huku kukiwa na tishio la wimbi hilo, Dk Gwajima alisema bado wananchi wanatakiwa kuendelea kuelimishwa ili wajue jinsi ya kujikinga na kuepuka misongamano.

“Tumesema serikali haitatumia nguvu nyingi kuanza kukimbizana na watu tunachokilenga kwa sasa ni elimu kwanza itolewe iwafikie watabadilika,” alisema Dk Gwajima.

Aliongeza, “Tunahitaji vyombo vya habari visaidie kuelimisha na visaidiane na wakuu wa mikoa na wilaya kwani watu wengi wanakuwa hawajasikia kwa sababu tuna redio za kijamii sambazeni elimu watu wasikie watu wakishasikia watachukua tahadhari na wataacha wenyewe.”

Dk Gwajima alisema wapo watu walioelimika sasa wanavaa barakoa hivyo ni muhimu waandishi kufikisha elimu. “Baada ya kutoa elimu hatua zitachukuliwa kwa watu ambazo wanapuuzia kwa sababu nao wanasababisha maambukizi yaendelee halafu tunachukua hela ambazo zingeweza kumtibu mtoto mchanga na mama mjamzito tunakwenda kununua mitungi ya oksijeni kuwaletea watu,” alisema Dk Gwajima.

“Lakini kwanza tuwaelimishe Watanzania serikali ina uwezo wa kuchukua hatua nyingi lakini hatua iliyoamua kuchukua kwanza na muhimu ni elimu,” aliongeza.

Julai 10, mwaka huu akiwa Dodoma, Dk Gwajima alibainisha kuwa hadi kufikia Julai 8, mwaka huu jumla ya wagonjwa 408 walikutwa na virusi vya corona huku wagonjwa 284 wakipumua kwa msaada wa mashine za oksijeni.
 
Mtu ukienda kutafuta mahitaji yako ya siku kwa siku, uende ukijua, huko kuna simba, dubu, chui na vitu vingi vya hatari, kwa hiyo ni mhimu kujilinda uwapo mawindoni, usipojilinda, utaliwa nyama na wanyama wakali,

Nimemwelewa Doctor! Ila inatofautiana msemo tu, lakini kila kitu na matamko hayo, ni mtindo wa kiJPM
 
Magufuli alikuwa anajulikana msimamo wake ni ipi ila Mama Samia haeleweki bado anaishi kwenye misimamo ya Magufuli ila ananena tofauti na Magufuli.
 
E1753ACF-AF37-4B9B-AC46-E73DBB88B7C2.jpeg


Vijana pale Airport wakipatiwa mafunzi ya kazi, kuhudumia wageni/arrivals kwa ujumla, ikiwemo umakini juu ya kupambana na COVID-19.

sasa unapomwambia mfanyakazi kua njia moja wapo ni kupeana nafasi (6ft) kati ya mtu na mtu ataelewa umuhim wake!?

kwa ukaaji huu wa “ZERO DISTANCE!!!”
 
Kwenu wenye mamlaka, naomba kutoa ushauri kwa kutoa takwimu kila siku kuhusu ugonjwa huu wa Covid 19.

Mosi itasaidia watu kuchukua tahadhari kwa woga. Pia ni sehemu ya elimu, watu bado hawaamini huku minong'ono ikiwa mingi kuwa kuna wagonjwa na vifo vingi vinavyotokana na Covid 19.

Taarifa za kila kona ya Nchi zitasaidia kumfanya mwananchi ajithamini kufuata Kanuni za ugonjwa huu.
 
Tukipeana hiyo distance sijui kuna jambo lolote litafanyika, hata watoto hawatazaliwa tena.......take easy hofu ndo korona yenyewe.
 
Corona ni upumbavu mtupu, mafua yapo, yalikuwepo na yataendelea kuwepo miaka elfu na elfu hadi mwisho wa dunia

 
View attachment 1852945Vijana pale Airport wakipatiwa mafunzi ya kazi, kuhudumia wageni/arrivals kwa ujumla, ikiwemo umakini juu ya kupambana na COVID-19.

sasa unapomwambia mfanyakazi kua njia moja wapo ni kupeana nafasi (6ft) (mita 1) kati ya mtu na mtu ataelewa umuhim wake!?

kwa ukaaji huu wa “ZERO DISTANCE!!!”
6ft ni mita 1??!!!
 
Kwani tuna mpango wa kuimaliza corona ?

Si tumekubaliana tutaishi nayo kama magonjwa mengine !
 
Kushughulika na C19 imekuwa maneno mengi sana kuliko matendo hadi inachosha sasa kuzisikia hizi habari
 
Kwenu wenye mamlaka, naomba kutoa ushauri kwa kutoa takwimu kila siku kuhusu ugonjwa huu wa Covid 19.

Mosi itasaidia watu kuchukua tahadhari kwa woga. Pia ni sehemu ya elimu, watu bado hawaamini huku minong'ono ikiwa mingi kuwa kuna wagonjwa na vifo vingi vinavyotokana na Covid 19.

Taarifa za kila kona ya Nchi zitasaidia kumfanya mwananchi ajithamini kufuata Kanuni za ugonjwa huu.
Huo uwoga nao una madhara yake tutapata vifo kutokana na huo uwoga hata visivyohusika na corona,kama unakumbuka mwaka jana kuna kipindi wagonjwa wa moyo presha .n.k walikuwa hawaendi kwenye clinic zao kwa kuogopa corona, magonjwa mengine uangalizi sasa kama hali ile ingeendelea hadi leo unafikiri hali ingekuaje?
 
Back
Top Bottom