Kwanini Mwl Nyerere hakuweka ukweli hadharani juu ya kifo cha Kassim Hanga? Mbona CCM huwa hawataki ukweli kuhusu mauaji ya Kassim Hanga kuwa wazi?

FORTALEZA Mwalimu alimfahamu Hanga kabla ya Mapinduzi vile vile aliwahi kumpa msaada wa kifedha Hanga.Hanga alisoma London pamoja na Kambona na wakawa marafiki.Baadaye Hanga na Kambona wakatuhumiwa kutaka kumpindua Mwalimu na Karume.Kambona akakimbilia UK na Hanga akakimbilia Guinea.
Hanga hakukumbulia Guinea bali alikuwa Balozi kule hivyo akarudishwa nyumbani
 
Wewe bwege, kachero hatakiwi kuchukua story kijiweni?
Ww ndio bwege tena mshamba. Kazi ya uchunguzi ina require ku chakata kuchunguza information zinazopatikana. Sio kuhamisha umbea kutoka sehem moja kwenda nyingine bila kufanyia kazi

Ww hujafanya chochote, umechukua zima zima na kurusha public, ni sawa kuchukua taarifa mtaa A na kupeleka mtaa B bila ku consider effect ya hiyo taarifa.
 
Hanga hakukumbulia Guinea bali alikuwa Balozi kule hivyo akarudishwa nyumbani
Baada ya kwenda Guinea, Hanga alihakikishiwa na Rais wa nchi hiyo, Ahmed Sekou Toure, na Nyerere wa Tanzania, kwamba angekuwa huru na salama akirejea nchini. Hanga alirejeshwa Tanzania kutoka Guinea.

Hanga hakuuona uhuru alioahidiwa na, badala yake, Desemba 1967 alikamatwa kwa tuhuma za uhaini. Alipohoji sababu ya kukamatwa alijibiwa kuwa alikula njama za kuwarubuni maofisa wa jeshi ili aweze kuiangusha serikali ya Sheikh Abeid Karume. Katika mahojiano aliyoruhusiwa kufanyiwa akiwa rumande, kwa mujibu wa jarida Africa Confidential, Hanga alikana kuhusika kwa vyovyote katika kula njama na maofisa wa jeshi na akasisitiza kwamba siku zote jitihada zake zilikuwa ni katika kutaka kuwapatanisha Kambona na Nyerere.

Courtesy: EMT
 
Nipo mahala hapa kijiweni nafuatilia story kibao juu ya masuala yanayohusu matukio kibao yaliyotokea baada ya mapinduzi ya Zanzibar.

Kuna mzee anasimulia hapa juu ya watu kibao kuuliwa baada ya mapinduzi kutokea. Anadai kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Zanzibar Kassim Hanga aliuliwa na mpaka leo haijulikani aliyemuua ni nani na aliuawa wapi.

Je, ni kwanini CCM tokea wakati wa hayati Nyerere hawataki kuweka wazi ukweli juu ya hili suala?
Si umuulize Karume?
 
Rais wa JMT hana mamlaka Zanzibar?
Karume alimtaka Hanga Zanzibar baada ya Nyerere kumficha huku bara. Alipompata akamtosa baharini. Mauaji yalifanywa siri lakini duniani hakuna siri.

Ingawa zipo habari za Nyerere kumzodoa Hanga hadharani pale mnazi mmoja uwanjani mbele ya Arnatoglo hall miaka hiyo ya sitini.
 
Karume alimtaka Hanga Zanzibar baada ya Nyerere kumficha huku bara. Alipompata akamtosa baharini. Mauaji yalifanywa siri lakini duniani hakuna siri.

Ingawa zipo habari za Nyerere kumzodoa Hanga hadharani pale mnazi mmoja uwanjani mbele ya Arnatoglo hall miaka hiyo ya sitini.
Karume alikuwa kiongozi kama viongozi wa jadi. Lilikuwa bonge la katili
 
FORTALEZA Mwalimu alimfahamu Hanga kabla ya Mapinduzi vile vile aliwahi kumpa msaada wa kifedha Hanga.Hanga alisoma London pamoja na Kambona na wakawa marafiki.Baadaye Hanga na Kambona wakatuhumiwa kutaka kumpindua Mwalimu na Karume.Kambona akakimbilia UK na Hanga akakimbilia Guinea.
Malizia mkuu, wala wali tu juu mpishi kaweka nyama nyingi chini.

Elezea kwanini Hanga ilibidi arudi TZ kutokea Guinea na yakamkuta yalomkuta.
 
Jibu rahisi tu,system iliyomuua na iliyofsidika na kifo chake,Bado ipo Madarakani.
Mauaji ya kisiasa hufanyika sana,pale Kenya,Robert ouko,Tom mboya,waliuliwa na Idara ya ujasusi ya Kenya,special branch kipindi Cha Raisi Kenyata,huo ukweli hauwezi kuwekwa wazi kabisa,kwa sababu madhara yake yanaweza kuwa makubwa sana,Inahitaji,umakini sana kuweka wazi madhira na mauaji ya kisiasa yaliyofanywa na tawala zilizopita,wakati mwingine,kwa usalama wa nchi,na nchi ibaki moja,mambo mengine Bora yafichwe tu,
Hata yule msimamizi wa tume ya uchaguzi ya Kenya nae kifo chake kilikuwa kibaya sana.

Ilikuwa baada ya yeye (amesoma nje) kuja na mfumo mpya wa kupiga kura ambao ungetoa matokeo ya kihistoria.
 
Kwenye mapinduzi teacher konde alifanya mambo ya ajabu mengi saana, ila historia inapindishwa.
 
Malizia mkuu, wala wali tu juu mpishi kaweka nyama nyingi chini.

Elezea kwanini Hanga ilibidi arudi TZ kutokea Guinea na yakamkuta yalomkuta.
Tunao wanahistoria wengi makini wanaoweza kueleza mambo haya kinagaubaga kuliko tunavyofanya katika makala za magazetini, lakini ama hawajapata jukwaa au hawako tayari kufanya hivyo. Namuunga mkono Issa bin Nasser kwa aliyosema katika kitabu chake, Zanzibar: Kinyanganyiro na Utumwa. Aliandika: Mwenyezi Mungu ndiye mjuaji wa yote. Sentensi inayotangulia maneno hayo, ambayo ndiyo imenikopesha maneno ya kichwa cha habari ya mada hii, inatia uchungu hata zaidi inaposomeka hivi: Mwenyezi Mungu mwenyewe anaelewa namna ya kuihukumu dhuluma hii iliyotendeka

Naiandika mada hii kwa ufupi sana kutokana na ufinyu wa nafasi. Kassim Hanga alikuwa rafiki mkubwa wa kisiasa wa Oscar Kambona. Kama Kambona alivyopoteza nyadhifa zake katika siasa, ndivyo Hanga naye alipoteza nyadhifa zake katika Serikali ya Muungano wakati yalipofanyika mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri. Hanga hakujua mambo mengi kuhusu Tanzania kama Kambona alivyojua. Baada ya kwenda Guinea, Hanga alihakikishiwa na Rais wa nchi hiyo, Ahmed Sekou Toure, na Nyerere wa Tanzania, kwamba angekuwa huru na salama akirejea nchini. Hanga alirejeshwa Tanzania kutoka Guinea.

Hanga hakuuona uhuru alioahidiwa na, badala yake, Desemba 1967 alikamatwa kwa tuhuma za uhaini. Alipohoji sababu ya kukamatwa alijibiwa kuwa alikula njama za kuwarubuni maofisa wa jeshi ili aweze kuiangusha serikali ya Sheikh Abeid Karume. Katika mahojiano aliyoruhusiwa kufanyiwa akiwa rumande, kwa mujibu wa jarida Africa Confidential, Hanga alikana kuhusika kwa vyovyote katika kula njama na maofisa wa jeshi na akasisitiza kwamba siku zote jitihada zake zilikuwa ni katika kutaka kuwapatanisha Kambona na Nyerere.

Mapema mwaka 1969, Kassim Hanga aliachiwa huru kutoka rumande. Badala ya kurejea Zanzibar, aliondoka na kwenda kuishi katika mojawapo ya nyumba zilizomilikiwa na Kambona mjini Dar es Salaam ambayo ilikuwa bado kutaifishwa. Lakini matatizo yake na serikali za Tanganyika na Zanzibar hayakuwa yamemalizika. Kuna Watanzania ambao hawakuridhishwa na hali ya kisiasa nchini. Miongoni mwa mengi waliyohoji ni suala la Kassim Hanga na udikteta wa Zanzibar wakidai kuwa Karume hakutaka uchaguzi kufanyika Zanzibar.

Baada ya kupinga sana sera za serikali, Oktoba 1968, wabunge kadhaa walitimuliwa Bungeni na baadhi ya watu wengine wakakamatwa na kutiwa kizuizini. Hawa walikuwa ni pamoja na Eli Anangisye, Joseph Kasella-Bantu, Christopher Kassanga Tumbo, Ndugu Choga, Ndugu Bakampenja na Ndugu Kaneno. Taarifa za watu kutiwa kizuizini zilipochapishwa katika gazeti Daily Nation (Okt. 2, 1968) la Kenya, serikali ya Tanzania iliamuru kukamatwa kwa mwandishi wa Kitanzania aliyevujisha habari hizo, Melek Mzirai Kangero.

Baadaye ikajulikana kuwa Hanga na Othman Sharif walikamatwa mjini Dar es Salaam kutokana na shinikizo la Karume aliyewataka watu hao kwa gharama zozotehata kama ni kwa kuuvunja Muungano. Othman Sharif, msomi kutoka Chuo cha Makerere, alikuwa mmoja wa waasisi wa Afro-Shirazi na kiongozi wa chama Bungeni wakati Karume akishikilia Urais wa chama. Mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kudhani kuwa Othman alikuwa na tamaa ya mamlaka ya kisiasa na uwezekano wake wa kula njama za kuiangusha serikali yake, akisaidiwa na Nyerere, Karume alimwondosha Othman Unguja na kufanywa kuwa Balozi.

Kwanza alikuwa Balozi wa Tanzania mjini London, Uigereza, kisha akapelekwa Washington, Marekani. Wakati mmoja, inadaiwa, Othman Sharif aliporudi Zanzibar kwa matembezi aliponyoka kuingia katika kucha za Abeid Karume. Karume alianza kumwandama kama simba anavyoandama windo lake. Kuona hivyo, Nyerere aliingilia kati mara hiyo hiyo akidai kwamba Othman Sharif alikuwa Balozi wa Muungano wa Tanzania, na si Balozi wa Zanzibar. Karume alipotambua kuwa hakuwa na mamlaka kisheria ya kumdhibiti Othman, alibadili mbinu ya kumtafuta. Nyerere alipogundua hilo alijaribu kufanya kila mbinu aliyoweza ili Othman asirudi Zanzibar.

Baada ya kupoteza wadhifa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mwalimu Nyerere alimpatia Othman kazi nyingine kwa kumteua kuwa afisa uganga wa mifugo mkoani Iringa. Lakini hiyo haikumzuia Karume kumwandama hadi mkoani Iringa na, kwa mujibu wa kitabu Conflict and Harmony in Zanzibar, Karume aliwashawishi Wazanzibari watatu waliokuwa marafiki wa karibu sana wa Othman ili wamsaliti.

Watu hao walikubali. Wakafikishwa mbele ya Baraza la Mapinduzi, wakatoa ushahidi kwa kiapo na kudai kwamba ni kweli Othman Sharif alikula njama za kutaka kuiangusha serikali ya Karume. Watu hao walipelekwa kwa Nyerere na kurudia madai hayo hayo. Wakati Nyerere anaelekea kuuamini huo mchezo wa kuigiza, tayari uhusiano kati yake na Karume ulianza kuingiwa na dosari nyingine. Muungano wa Tanganyika-Zanzibar ulikuwa majaribuni.

Hatimaye Nyerere akasema watu hao watapokea hukumu ya haki Zanzibar. Gazeti Ulimwengu (Nov. 19, 1967) katika tahariri yake liliandika kuwa lazima hukumu ya haki itolewe. Kisha likaonyesha kupinga suala la watu kuwekwa kizuizini. Kama matokeo, mhariri wa gazeti hilo, Otini Kambona, alikamatwa. Hata ndugu yake Otini, aliyeitwa Mathias, naye alikamatwa kwa sababu nyingine tofauti kwa madai ya kushiriki katika njama za kuiangusha Serikali.

Kikundi cha viongozi kutoka mkoani Iringa, ambako Sheikh Sharrif alikuwa akifanya kazi, walimsihi sana Nyerere asiruhusu watu hao wapelekwe Zanzibar kwani walijua hatima yao. Jawabu la Nyerere lilikuwa hivi: Hili si jambo la ubishi kwa sababu halina uzito wa kubishaniwa. Lakini kama kutakuwa salama, ni vizuri tukajua watu hawa watakuwa salama kiasi gani. Lakini historia ni shahidi. Hakukuwa na usalama wa kiasi chochote. Wanadamu hawa walinyanganywa haki yao ya kuishi.

Baada ya kuona kuwa mambo yameshindikana, na kwa kuwa Muungano wa Tanzania ndilo lililokuwa suala kuu katika akili yake, Mwalimu alibwaga manyanga. Septemba 1969 Nyerere akajikuta akiwapa idhini maofisa wake kuwatoa Kassim Hanga na Othman Sharif wakabidhiwe SMZ kama Abeid Karume alivyotaka. Walipelekwa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Dar es Salaam (DIA), wakipewa maneno ya kuwafariji, na kisha wakasafirishwa kwenda Zanzibar. Hiyo ikawa ndiyo safari yao ya mwishoangalau safari ya mwisho kutoka Dar es Salaamtena, inadaiwa, wakiwa na wamefungwa pingu.

Huko ndiko walikokutana na mauti yao, pengine kwa kupigwa risasiingawa taarifa nyingine zilisema kuwa waliuawa kwa kuzamishwa katika maji. Lakini, kinasema kitabu Conflict and Harmony in Zanzibar, hata wale waliomsaliti Othman Sharif nao waliuawa mmoja baada ya mwingine. Machapisho mengine ya kihistoria yanaunga mkono madai hayo. Katika hotuba aliyoitoa Oktoba 1969, ukiwa ni mwezi mmoja baada ya kufanyika kwa mauaji hayo, Abeid Karume alitangaza kuwa watu wanne waliokuwa wakila njama za kuiangusha serikali yake wameuawa kwa kupigwa risasi. Hili alilikiri mwenyewe.

Vyanzo kadhaa vinasema kuwa Kassim Hanga, na aliyekuwa Waziri wa Elimu na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Sheikh Othman Sharrif, waliuawa Zanzibar na utawala wa Karume. Hata hivyo mauaji hayo hayakuwa mwisho wa mambo. Inaelekea kuanzia hapo, au kabla ya hapo, kulijengeka utamaduni wa kuwakamata watu, kuwaweka kizuizini na hatimaye wengine kuuawa.

Zaidi ya watu kuwekwa kizuizini bila kufunguliwa mashitaka, kulikuwa na madai ya kuweko kwa zile kambi za mateso. Kwa mfano katika miaka ya 1960 na mwanzoni mwa 1970, inasemwa, Zanzibar kulikuwa na ile kambi iliyoitwa Kwa Bamkwe au Kwa Mandera. Mkoani Mwanza kaskazini mwa Tanzania kulikuwa na (kambi ya) Kigoto. Hiyo ni moja ya kambi zilizokuwa mbaya. Baada ya kuwakamata watu kwa tuhuma za uchawi mwaka 1977 katika maeneo ya Mwanza na Shinyanga, ikijumlishwa na matendo waliyofanyiwa watu hao, ilitosha kumfanya Alhaj Ali Hassan Mwinyi kujiuzulu kwa kuwajibika.

Ingawa wengi walitarajia kuwa kuwajibika huko kungekuwa ndio mwisho wa Mwinyi katika siasa, Nyerere alimpigia debe kuwa Rais wa Zanzibar (Jan. 30, 1984Okt. 24, 1985) na hatimaye Rais wa Tanzania (Nov. 5, 1985Nov. 23, 1995) kwa kura za NDIYO. Kwa mujibu wa kitabu Zanzibar: Kinyanganyiro na Utumwa, mwanasiasa aliyekuwa Unguja wakati mambo yote hayo yakitokea, Issa bin Nasser Al-Ismaily, anaandika kuwa mwaka 1970 Wazanzibari tisa walitiwa nguvuni na Serikali ya ASP kwa kisingizio cha kutaka kuipindua serikali hiyo. Wazanzibari hao ni Salim Ahmed Busaidi, Abdallah Suleiman Riyami, Othman Soud, Aziz Bualy, Hemed Said, Muhammed Juma, Muhammed Hamza, Musa Ali na Said Hamoud.

Bila ya kufikishwa mahakamani, Karume aliwahukumu kutupwa gerezani na kupewa kazi ya kuchunga ngombe katika uwanda wa Hanyagwa-Mchana. Baada ya kifo cha Karume Aprili 1972, wananchi hao waliuawa wakati wa utawala wa mrithi wa Karume, Aboud Jumbe. Kitabu hicho kinaomboleza hivi: Mwenyezi Mungu mwenyewe anaelewa namna ya kuihukumu dhuluma hii iliyotendeka; kwani Mwenyezi Mungu ndiye mjuaji wa yote. Ni kweli kwamba Mwenyezi Mungu ndiye mjuaji wa yote kwa sababu hakuna mwanadamu atakayejua yote yaliyotendeka, hasa yale ambayo hayatajulikana kamwe.

Courtesy: EMT
 
Back
Top Bottom