Baada ya uteuzi wa Paul Makonda Katibu mwenezi wa Taifa wa CCM: Fahamu hoja zake tano zinazopaswa kujibiwa badala ya kumshambulia mleta hoja

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,025
2,519

Tangu Paul Makonda alipoanza kazi baada ya kuteuliwa kuwa Katibu mwenezi wa Taifa wa CCM mitandao ya kijamii imesema mengi juu yake na ofisi aliyoteuliwa kuitumikia.

Maoni mengi yana sura hasi, baadhi wakiwa wanamtazama kwa kutumia miwani ya itikadi ya ujenitalia (genitalism), na hivyo kushindwa kuona picha kubwa iliyobebwa ba kauli zake. Kwa mfano kuna watu wanaongelea habari ya utowashi wa Makonda na kupiga kisogo kabisa masuala ya kiitikadi, kisera na kiutawala anayoyaongeleai.

Lakini, kwenye kauli zake kuna masuala yanayohusu misingi ya utu (personalism) ambayo hayapaswi kufunikwa na kejeli zinazia kwenye itikadi ya ujenitalia na ambayo nimeamua kuyaweka bayana hapa kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa.

Hivyo, katika aya ziafuatazo nitajadili mambo yafuatayo: (1) Hoja tano za Paul Makonda, (2) Umuhimu wa siasa zinazoongozwa na uchambuzi makini wa kisera, (3) Umuhumu wa kutofautisha tuhuma pasipo hatia na tuhuma zenye uthibitisho wa hatia, na (4) Umuhimu wa siasa zinazoongozwa na itikadi ya utu (personalism) badala ya itikadi ya ujenitalia (genitalism).

I. Hoja tano za Paul Makonda

Saa 03:00 asubuhi ya Alhamisi 26 Oktoba 2023 , Katibu mwenezi wa Taifa wa CCM Ndugu Paul C. Makonda alipokelewa Rasmi katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu Lumumba, Mkoani Dar es Salaam.

Siku hiyo, Makonda aliongea mengi, lakini kuna kauli tano zenye mtazamo chanya na zinazopaswa kufanyiwa kazi na wajasiriadola makini ndani na nje ya CCM. Kauli hizo nazifupisha hapa chini:

1. Utayari wa Makonda kukubaliana na kanuni kwamba kazi ya chama cha siasa ni kuisimamia serikali kwa kuwa sikio na ulimi wa kuwasemea wananchi. Kuhusu jambo hili Makonda alisema:

"Kazi ya chama ni kuwa sikio na kuwasemea wananchi... Tutachukua hatua bila kusubiri, kwa kiongozi yeyote atayerudisha nyuma jitihada za chama kuendelea kuaminiwa na wananchi."

2. Utayari wa Makonda kupinga taarifa zilizofitiniwa kimakusudi (disinformation), kukataa taarifa zilizofitinika kwa bahati mbaya (malinformation), na kupiga kisogo taarifa zilizomegwa kwa makusudi ili kupotosha hadhira (censorship). Kuhusu jambo hili Makonda alisema:

“Duniani kote watu wanaishi kwa taarifa na taarifa zinafanya uamuzi, ukiwa na chanzo kibovu utafanya uamuzi mbovu, lakini ukiwa na chanzo kizuri utafanya uamuzi sahihi wakati wote.”

3. Utayari wa Makonda kujitenga na tabia ya kusema uwongo kama mbinu ya kuwabeba watendaji wazembe serikalini. Kuhusu jambo hili Makonda alisema:

“Sitakuwa tayari kuwa msemaji wa chama ambacho kimepewa dhamana na wananchi, na wanaomsaidia mheshimiwa mwenyekiti wanashindwa kutekeleza nisimame hadharani kusema uongo, hapana. Kila kiongozi wa serikali atabeba msalaba wake mwenyewe.”

4. Utayari wa Makonda kuachana na siasa za jino kwa jino, kisasi kwa kisasi. Kuhusu jambo hili Makonda alisema:

“Wengi wanahamaki, wana bashasha na wengi wao wanawaza kwamba Makonda ataenda kulipa kisasi, wanawaza makonda atakwenda kufanya nini, wengine wanasema Usiyemtaka kaja na alikuwa haonekani alienda kujificha wapi? Nasema mbele ya watanzania na Mbele ya Mwenyenzi Mungu mimi sina kisasi kwa mtu yeyote."

5. Utayari wa Makonda kujumuika kwenye mashindano ya hoja zinazosimama au kuanguka kutokana na ushahidi uliowekwa mezani. Kuhusu jambo hili Makonda alisema:

"Mbowe akiruka [kwa hoja za] angani tutamfuata, akienda [kwa hoja za] nchi kavu tutamfuata, akiingia kwenye [hoja za] boti tutamfuata, atapigwa [kwa hoja] kila kona kwa sababu moja tu. Hoja, na uwezo na utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi hauna shaka."

Kwa maoni yangu, kauli tano za Makonda nilizonukuu hapo juu ni chachu katika ujenzi wa mwavuli wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini Tanzania.

Sasa Chadema, ACT na vyama vingine, ambavyo Makonda amevitaja kuwa ni "vyama vya watoa taarifa" wamepewa nafasi ya kumjibu Makonda kwa hoja kwa kufanya kazi ya "watoa taarifa" za kweli, hasa zile "taarifa" zitakazomnyima usingizi Makonda.

Kwa njia hiyo spoku za mwavuli wa siasa za vyama vingi zitaimarika na na kuuwezesha mwavuli kuzuia jua kali la utapiamaendeleo kuwachoma wananchi utosini.

II. Umuhimu wa siasa zinazoongozwa na uchambuzi makini wa kisera

Demokrasia ya vyama vingi ni kamamwavuli wenye spoku nyingi, kila spoku ikiwakilisha chama kimajawapo, wakati ile nguo ya juu ya mwavuli inawakilisha maslahi ya pamoja katika Taifa bila kujali tofauti za umri, dini, jinsia, itikadi, rangi wala ukanda.

Kusudi mwavuli huu uweze kuzalisha kivuli kinacholinda maslahi ya pamoja ni lazima spoku zote zifanye kazi kwa "mtindo wa vuta nikuvute."

Katika mtindo huu vyama vya upinzani hutafiti, kufanya uchambuzi wa kisera na kutoa taarifa za ukosoaji kwa umma kuhusu mapungufu ya serikali na chama tawala. Nachi chama tawala kikijibu mapiga ama kwa kukanusha au kuchukua hatua za marekebisho stahili.

Hivyo, katika hatua ya sasa, ambapo Ilani ya CCM (2020-2025) imekuwa inatekelezwa kwa mwaka wa tatu, kuna maswali mengi kuhusu utekelezwaji wake yanayopaswa kuibuliwa na vyama vya upinzania na yanayohitaji majibu kutoka kwa Makonda.

Kwa ujumla, napendekeza kwamba, sera zote zilizo katika ilani za vyama vyote vya siasa, zinaweza kugawanywa, bila kubaki, katika makundi matano. Makundi hayo ni: Afya tele, Elimu bora, Ikolojia rafiki, Ofisi zenye utawala bora, na Uchumi unaojali utu. Nakumbuka maeneo haya matano kwa msaada wa vokali tano za Kiswahili, yaani “A, E, I, O, U.”

Kwa kuzingatia maeneo haya matano, katika aya zifuatazo napendekeza kufupisha ahadi 90 nilizoziona kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ili kuweka rejea murua itakayotusaidia kufanya ufuatiliaji na tathmini ya kazi za serikali kuanzia 01 Januari 2021.

AFYA TELE: Afya ni hali ya binadamu kuwa na mwili na akili vyenye kutenda kazi zake barabara. Hali hii ni matokeo ya kuwa na kinga dhidi maradhi yanayoambukiza na yasiyoambukiza, mkamilishano thabiti kati ya nafsi na mwili, na masikilizano kati ya mwili na mazingira yake, ambapo mazingira yanahusisha makazi, malazi, chakula na jamii ya watu wanaomzunguka mhusika. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu afya ziko katika ibara za 81-100. Baada ya kuipitia Ilani hii, nimejiridhisha kwamba, kuna sera 16 ambazo zinapaswa kutekelezwa na serikali yake ili kukuza na kuhami afya ya kila raia.

 1. Kuna ahadi kuhusu ujenzi na ukarabati wa vituo vya huduma za afya, ushirikishwaji wa sekta binafsi katika huduma za afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, upatikanaji wa watumishi na mabingwa wa kada ya afya, na sera ya mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
 2. Pia, kuna ahadi kuhusu mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza, mapambano dhidi ya magonjwa yanayotokana na virusi kama vile VVU, upatikanaji wa mlo kamili na bora, na sera ya uduma za ustawi wa wazee.
 3. Aidha, kuna ahadi kuhusu huduma za ustawi wa watoto na familia, huduma za watu wenye ulemavu, kusimamia upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira, kusimamia mipango miji na mipango vijiji, sera ya ujenzi wa nyumba na makazi bora, sera ya bima ya afya kwa wote, na sera ya afya ya mama na mtoto. Lakini, katika ilani hii, haikutajwa ahadi ya “bima ya afya kwa watu wote.” Hii ni ahadi ya jukwaani.
ELIMU BORA: Elimu ni mchakato wa kupata taarifa, maarifa na ufundi wa kufanya utafiti na kubuni tekinolojia za kumsaidia mwanafunzi aliyefuzu kuyamudu mazingira yake ya kimaumbile, kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiutamaduni. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu elimu ziko katika ibara za 78-80, na ahadi kuhusu sayansi na tekinolojia ziko katika ibara za 101-103. Baada ya kupitia ilani hii, nimeona kuwa sekta hii itaboreshwa kwa kupitia utekelezaji wa mikakati ya kisera 10.
 1. Kuna ahadi kuhusu elimu ya msingi, elimu ya sekondari , elimu ya ufundi stadi, na sera ya elimu ya Juu.
 2. Pia kuna sera za kuanzisha makampuni ya katika sekta mbalimbali ili kuendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu; kujenga mfumo wa Taifa wa ubunifu (national innovation system); na sera ya kuendeleza vituo atamizi kwa ajili ya kukuza na kuendeleza ubunifu wa kisayansi na kitejinolojia.
 3. Kadhalika, kuna ahadi kuhusu kuhamasisha matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika uzalishaji, usambazaji, na utawala kwa kutumia tekinolojia ya kidijitali; kuanzisha vituo vya umahiri wa sayansi na teknolojia (centres of excellence) katika taasisi za elimu ya juu; na sera ya kuimarisha mafunzo ya walimu wa sayansi, teknolojia na ufundi katika ngazi za shule za msingi, shule za sekondari, vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi na vyuo vikuu.
IKOLOJIA RAFIKI: Neno "ikolojia" linamaanisha mazingira. Mazingira ya binadamu yanajumuisha wanyama, mimea, wadudu, hewa, maji na vitu vyote vilivyo baki vilivyoko ardhini, angani, majini, msituni, porini, pamoja na michakato yote ya kibayolojia inayomfungamanisha kila binadamu pamoja na vitu hivi kupitia mitandao ya vyakula vya viumbe anwai (ecological food web). Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu ikolojia ziko katika ibara ya 9B(vii). Baada ya kupitia Ilani hii, na kukagua mikakati ya kutunza mazingira iliyoko katika tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais, nimebaini kuwa, kuna mikakati 10 ya kisera inayoweza kutekelezwa ili kukuza na kuhami mfumo wa ikolojia ulio salama kwa uhai wa binadamu na viumbe baki.
 1. Kuna ahadi juu ya kuhimiza watu kuepuka kadiri inavyowezekana kutumia nishati zinazozalisha hewa ya ukaa ambayo ni chanzo kikuu cha mabadiliko ya tabia nchi; kuwekeza katika miradi ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi (climate adaptation strategies); na kuwekeza katika miradi ya kupunguza ukubwa wa vyanzo vya mabadiliko ya tabia nchi (climate mitigation strategies).
 2. Aidha kuna ahadi juu ya kuhifadhi uoto wa asili ulioko juu ya nchi, kuhifadhi uoto wa asili ulioko majini, kuhifadhi wanyama wa porini, kuhifadhi wanyama wa majini, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, na kunzisha mfuko maalum kwa ajili ya utafiti, usimamizi na tathmini juu ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi.
 3. Kadhalika kuna ahadi juu ya kuzuia uchafuzi wa mazingira unaofanyika kupitia uzalishaji wa takangumu; uzuia uchafuzi wa mazingira unaofanyika kupitia uzalishaji wa takamaji; na uzuia uchafuzi wa mazingira unaofanyika kupitia uzalishaji wa takahewa.
OFISI ZENYE UTAWALA BORA: Utawala bora ni aina ya utawala ambao unahakikisha kuwa utaratibu wa kufanya maamuzi na kutekeleza maamuzi hayo kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa jamii unazingatia misingi ya utu, uhuru, haki, ushirikishwaji, demokrasia, uwajibikaji, uhasibikaji, uwazi, tija, ufanisi, usawa mbele ya sheria, na ushiriki wa makundi yote ya jamii. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu ofisi za utawala bora ziko katika ibara ya 108-130. Baada ya kupitia ilani hii nimjiridhisha kuwa kuna jumla ya sera 16 zinazopaswa kutekelezwa kwa ajili ya kufanikisha dhana ya utawala bora.
 1. Kuna ahadi juu ya kuheshimu haki ya kujitawala katika ngazi za chini za serikali kwa kugatua madaraka, kusimamia maadili katika utumishi wa umma, kufanya mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, kuheshimu misingio ya demokrasia na haki za binadamu, kuheshimu katiba na kuzingatia utawala wa matakwa ya sheria, na sera ya kuhuisha usawa wa jinsia katika sekta ya umma na sekta binafsi.
 2. Pia, kuna ahadi juu ya kuhami uhuru wa vyombo vya habari, kuheshimu uhuru wa raia kujieleza na kuwasiliana, kuhesimu uhuru wa asasi za kiraia, kulinda uhuru wa kuabudu, kulinda haki za wafanyakazi na uhuru wa vyama vya wafanyakazi, na sera ya kukabiliana na majanga ya asili kwa kuzingatia kanuni ya utawala auni (principle of subsidiarity).
 3. Kadhalika, kuna ahadi juu ya kupambana na dawa za kulevya, menejimenti ya mahusiano ya kisiasa na kiuchumi katika ngazi ya kimataifa, menejimenti ya kidemokrasia ya vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi, na sera ya kuzuia utekaji, utesaji na uteketezaji wa uhai wa raia wasio na hatia.
 4. Vile vile kuna ahadi ya kusimamia ukuu wa nchi, yaani "state sovereignty management," kwa maana ya kusimamia ukuu wa serikali katika kutunga na kutekeleza sera za nchi, kusimamia ukuu wa mahakama katika kutafsiri sheria za nchi; kusimamia ukuu wa bunge katika kutunga sheria zinazoiongoza serikali katika kutekeleza sera zake; kusimamia ukuu wa wananchi juu ya vyombo vya dola kwa kuzingatia mgawanyo na udhibitiano wa kimadaraka kati ya serikali, mahakama na bunge; na kusimamia kazi ya kuzuia upunguzaji wa eneo la nchi kwa njia ya kumomonyoa mipaka yake au kutengeneza "viraka" vya himaya binafsi za wageni ndani yake.
UCHUMI UNAOJALI UTU: Uchumi ni mfumo unaojumuisha mambo makuu manne, yaani, michakato, kanuni za kuratibu michakato hiyo, tunu zinazowaunganisha watendaji kwa skuwaelekeza katika malengo yanayofanana, na misingi ya ustaarabu wa kugawana shida na raha za kiuchumi (processes, principles, values, and justice). Kuna michakato mitano, yaani uzalishaji, usambazaji, mauziano, utumiaji wa huduma na bidhaa, na uwekezaji (production, distribution, exchange, consumption and investment). Kuna kanuni kuu tatu zinazotumika kuratibu michakato iliyomo katika sekta ya uchumi, yaani kanuni za ushindani, ushirikiano, na uingiliaji kati kupitia mkono wa serikali ili kudhibiti madhara hasi ya ushindani na ushirikiano unaotokea sokoni (competition, cooperation, and intervention). Na kuna tunu tatu zinazohuisha malengo ya kiuchumi, yaani uhuru, mshikamano, na usawa (freedom, solidarity and equality); ambapo, tunu ya uhuru ni chimbuko la kanuni ya ushindani, tunu ya mshikamano ni chimbuko la kanuni ya ushirikiano, na tunu ya usawa ni chimbuko la kanuni ya uingiliaji kati. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu ahadi kuhusu ujenzi wa miundobinu ya kiuhumi ziko katika ibara ya 12-76. Baada ya kusoma ilani hii nimebainisha vipengele 38 vya kisera vinavyopaswa kufanyiwa kazi ili kuzalisha mfumo wa uchumi unaojali maslahi ya watu wote.
 1. Kuna ahadi juu ya ushirikishaji wa sekta binafsi katika uwekezaji, uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, na kuzalisha ajira kwa vijana, kusimamia vyama vya ushirika, kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda, biashara na mfumo wa kodi, vituo atamizi kwa ajili ya kuzalisha wajasiriamali, na kubuni sera za kifedha zinazoruhusu mzunguko wa fedha wenye kasi kubwa ya kuhakikisha kwamba fedha inapita katika mfuko wa kila raia anayejishughulisha.
 2. Pia, kuna ahadi juu ya barabara za chini, madaraja, makalvati, mizani ya kupima magari, vivuko, bandari, reli, viwanja vya ndege, na mawasiliano ya simu.
 3. Aidha, kuna ahadi juu ya ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) zifuatayo ili kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam, kwenye makutano ya barabara katika maeneo yafuatayo: Chang’ombe, Uhasibu, Kamata, Morocco, Mwenge, Magomeni, Tabata, Fire, Makutano ya Ally Hassan Mwinyi na United Nation, na Makutano ya Ally Hassan Mwinyi na Kinondoni. (Ilani ya CCM 2020-2025, ib. 55(e)(i)).
 4. Kadhalika, kuna ahadi juu ya nishati ya umeme, nishati ya mafuta, nishati ya gesi asilia, madini, utalii, maliasili, matumizi bora ya ardhi, na kuendesha sekta ya utamaduni, sanaa na michezo kibiashara.
Uchambuzi wa kisera unaohitajika unaweza kufuata mtiririko huu, japo sio lazima, maana kuna njia nyingi z kuchuna ngozi ya paka.

Lakini, vyovyote iwavyo, tunapaswa kutembea kwenye ilani kifungu baada ya kifungu. Mfano mzuri ni kufuatilia utekelezwaji wa ahadi ya kujengwa kwa barabara za angani katika mkoa wa Dar es Salaam. Kuhusu ahadi hii, kifungu cha 55(e)(i) kwenye Ilani (2020-2025) kinasema yafuatayo:

1698582696343.png

1698582633624.png

Maswali hapa ni pamoja na: Utekelezaji wa ahadi hiii umefikia hatua gani? Hatua hiyo inaendana na mpango wa ufuatiliaji uliowekwa kwenye maandiko ya CCM na serikali? Kama ni hapana kwanini, na hatua gani zichukuliwe? Waziri mwenye dhamana ya ujenzi anapaswa kuwa na majawabu kwa maswali haya.

III. Umuhumu wa kutofautisha tuhuma pasipo uthibitisho wa hatia na tuhuma zenye uthibitisho wa hatia

Kanuni mojawapo katika utawala na uongozi ni kanuni ya utoaji haki sawa kwa wote walio sawa. Msingi wa kanuni hii ni ukweli. Ndio maana katiba ya nchi inasema kwamba kila mtu anapaswa kuhesabiwa mtakatifu hadi hapo chombo halali kitakapomtia hatiani.

Kwa hiyo, tabia ya kusambaza "tuhuma zisizo na uthibitisho wa hatia," kwamba "Paul Makonda aanatuhumiwa kughihsi vyeti vya kitaaluma," ni ukiukaji wa misingi muhimu ya utawala bora.

Yaani, kusambaza "tuhuma" pasipo uthibitisho wa "hatia" ni utovu wa nidamu ya kiutawala.Na sifa moja ya mtu anayetaka kuwa kiongozi wa umma ni kutofautisha tuhuma na hatia.

Lakini, hapa suala muhimu zaidi ni kwamba, hatia inathibitishwa na ushahidi usiokanushika, kwa kutumia mizania ya uzito wa taarifa zilizopo mbele ya mtoa hukumu.

Nitaeleza. Mizania ya uzito wa taarifa zilizopo mbele ya mtoa hukumu inafanya kazi namna hii:

Katika mchakato wa uthibitisho wa maarifa (epistemic justfication), kwa kutumia kikapu cha taarifa za uthibitisho zinazounda asilimia mia moja, usahihi wa kila kauli, tuseme "Kauli P," mfano "P=Paul Makonda alighushi vyeti," huchunguzwa kwa kutumia kauli tatu kwa mpigo, ambazo ni,

 • "Kauli kwamba P ni kweli," yaani zaidi ya 50% ya ushahidi unaunga mkono kauli P (chukua upande huu).
 • "Kauli kwamba P sio kweli," yaani zaidi ya 50% ya ushahidi unapinga kauli P (chukua upoande huu).
 • "Ama kauli kwamba P ni kweli au kauli kwamba P sio kweli," yaani 50% ya ushahidi uliopo unaunga mkono kauli P na 50% ya ushahidi uliopo unapinga kauli P (hii ni njia panda, usichukue upande, jizuie kutoa hukumu).
Tukumbuke kwamba, kila mtu mwenye akili timamu analo jukumu la kiepistemolojia (epistemic duty) la kujiunga kwenye kambi ya kiimani inayoshikilia misimamo yenye kuungwa mkono na ushahidi ulio juu ya 50% na kujizui kuchagua kambi pale ambapo ushahidi alio nao hautoshelezi matakwa ya kutoa hukumu sahihi.

Basi, kwa kutumia mchakato huu tufikirie upya juu ya usahihi wa kauli zetu za kila siku dhidi ya watu baki na kama tutaona tunao ushahidi wa kutosha tuanzishe mchakato wa kuzisambaza, ama sivyo tukae kimya huku tukiendelea na utafiti/uchunguzi. Na utafiti usipozaa matunda tufunge faili la uchunguzi.

IV. Umuhimu wa siasa zinazoongozwa na itikadi ya utu badala ya itikadi ya ujenitalia

Hapo mwanzoni nimesema kuwa maoni mengi yanayotolewa dhidi ya Makondayana sura hasi, baadhi ya wasemaji wakiwa wanamtazama kwa kutumia miwani ya itikadi ya ujenitalia (genitalism), na hivyo kushindwa kuona picha kubwa iliyobebwa ba kauli zake.

Kuna watu wanaongelea ujinsia wa Makonda wakimtaja taja kama kama towashi (eunuch) na hivyo kujizuia kabisa kuchambua masuala ya kiitikadi, kisera na kiutawala anayoyaongelea.

Lakini pia, ndani ya CCM kuna viongozi wakubwa wanatumia muda mwingi kuongelea maadili ya jamii kwa kukomalia maadili ya ngono. Muda mwingi wanajifanya vinara wa kupinga uzinzi, uasherati, umalaya, ubakaji, na ulawiti.

Wakiongelea wodi za wagonjwa hospitalini wanachokumbuka haraka ni wodi za wazazi kama kwamba wodi zote na idara zote hospitalini ni wodi za wazazi.

Lakini, maadili ya jamii ni suala pana. Yanahusisha pia maadili ya uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma muhimu, maadili ya elimu, maadili ya kilimo, maadili ya ufugaji, maadili ya biashara, maadili ya siasa za kibunge, maadili ya usafirishaji wa abiria na mizigo, maadili ya ujenzi wa majengi na barabara, maadili ya utunzaji wa mazingira, na maadili ya kusanifu hoja zenye utimamu wa kimntiki, kati ya maadili mengine mengi.

Hivyo, wito wangu ni kwamba, sasa siasa za kupakana matope (gutter politics), mipasho, masimango, na kejeli zinazoanzia kwenye itikadi ya ujenitalia (genitalism) zikome.

Badala yake, itikadi ya utu (personalism) ituongoze ili kutoa nafasi ya kufanya uchambuzi wa kisera kwa kutumia kanuni za makabiliano ya hoja za kirazini zinazoongozwa na ushahidi thabiti.

Kwa ajili ya kuikubali itikadi ya utu ni muhimu kuelewa kwamba, kila kiumbehai hutambulishwa na malengo ya kibayolojia, ambayo hufanikishwa na kazi zinazofanywa na viungo 78 vilivyo mwilini mwake.

Kazi hizo ni kama vile kujongea, kutoa uchafu mwilini, kupumua, kufukuza kifo, kutambua mabadiliko ya kimazingira, kupata lishe, ukuaji, na kuzaliana. Haya ni malengo makuu mawili, yaani kujihifadhi na kuzaliana.

Hii maana yake ni kwamba, kila mtu jamii ya binadamu anaitwa kiumbehai kwa sababu viungo vyake 78 vimeunganishwa na kitu kimoja cha ziada.

Yaani angalu lengo mojawapo kati ya malengo mawili: lengo la kuhifadhi uhai wa kimwili au lengo la kuzaliana. Lengo la kwanza linahusu uhai wa kiumbehai chenyewe, na lengo la pili linahusu uhai wa ukoo wote wa kiumbehai.

Hivyo, sababu za pendekezo kuhusu ukuu wa itikadi ya utu (personalism) dhidi ya itikadi ya ujenitalia (genitalism) ni za kisayansi na kifalsafa. Nitafafanua.

Tangu kidato cha kwanza, walimu wetu wa somo la bayolojia, wametufuindisha kwamba, mwili wa kila binadamu una viungo 78. Pia wametueleza kwamba viungo hivyo vinagawanyika kwenye mifumo mikubwa kumi na moja ifuatayo:

 • (1) Mfumo wa damu (circulatory organ system),
 • (2) Mfumo wa tezi (lymphatic organ system),
 • (3) Mfumo wa hewa (respiratory organ system),
 • (4) Mfumo wa jalada la mwili lenye luhusisha ngozi, kucha, na nywele (integumentary organ system),
 • (5) Mfumo wa homoni (endocrine organ system),
 • (6) Mfumo wa chakula (digestive organ system),
 • (7) Mfumo wa kuchuja uchafu (excretory organ system),
 • (8) Mfumo wa misuli na mifupa (muscular-skeletal organ system),
 • (9) Mfumo wa ubongo na mishipa ya fahamu (nervous organ system),
 • (10) Mfumo wa kinga mwili (immune organ system), na
 • (11) Mfumo wa uzazi (genital organ system).
Mchoro ufuatao unatoa picha kubwa kuhusu mahusiano yaliyopo kwenye mifumo hii ya mwili wa kila binadamu:

1699169984369.png

Na katika falsafa ya bayolojia (philosophical biology) tunafundishwa kwamba, mifumo yote 11 iliyo kwenye mwili wa mtu inagawanyika katika makundi makuu mawili.

Kwanza kuna mifumo inayofanya kazi ya kulinda na kuendeleza maisha ya kiumbehai kimoja kimoja kwa kuzuia kifo kwa njia mbalimbali (survival organ systems).

Na pili kuna mfumo mmoja pekee unaofanya kazi ya kulinda na kuendeleza maisha ya ukoo kwa kuhamisha uhai kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto, yaani mfumo wa uzazi (genital organ system).

Mfumo wa uzazi unajumuisha jenitalia za nje ya mwili na jenitalia za ndani ya mwili. Kuna jenitalia za kiume na jenialia za kike. Katika maelezo haya, neno "jenitalia" ni unyambulisho wa neno "genitals" la Kiingereza. Kwa hiyo, viungo vinavyoitwa jenitalia ni asilimia tisa pekee katika mwili wote.

Mchanganuo huu ndiyo sababu inayowafanya baadhi ya wadadisi wa mambo kuuliza, "do organisms survive to reproduce or reproduce to survive?" Jawabu lake sio muhimu kwa sasa.

Lakini pointi kuu hapa ni kwamba kuna kazi kuu mbili zinazofanywa na viungi vya mwili. Yaani kazi ya kulinda uzima wa kiumbehai (survival/self-preservataion) na kazi ya kuendeleza uzima wa ukoo (reproduction/genitality/species-preservation).

Lakini pia, ikumbukwe kwamba, viungo vya mwili vinavyoitwa jenitali sio miongoni mwa viungo vikuu vitano vyenye jukumu la kupigana na kifo, yaani ubongo, moyo, mapafu, ini na figo. Hata ukiingia chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali yoyote hutakuta "life monitoring screen" inayoonyesha utendaji kazi wa jenitalia.

Badala yake utaona grafu za kuonyesha utendaji kazi wa ubongo, moyo, mapafu, ini, na figo. Viungo hivi vitano vikifeli unaambiwa mgonjwa wako tayari amekuwa mgeni wa Mungu. Unaanza safari ya kwenda makaburini.

Hivyo, kuna mawili hapa. Mosi, viongozi wetu wanapaswa kutumia muda mwingi kujadiliana nasi kuhusu sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa UBONGO, sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa MOYO, sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa MAPAFU, sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa INI, sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa FIGO, sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa KOO, UTUMBO MWEMBAMBA, TUMBO LA CHAKULA, UTUMBO MPANA, MIKONO, MIGUU, MACHO, MASIKIO, PUA, MIFUPA, NGOZI, na viungo kama hivyo.

Na pili,viongozi wetu wanapaswa kutumia muda muda kidogo sana kuongelea sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa JENITALIA.

Kwa hiyo, kutumia muda mwingi kuongelea sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa jenitalia na kutenga muda kidogo kuongelea sera zinazohusu utendaji kazi wa viungo vya mwili vilivyo muhimu zaidi katika kulinda maisha ya kiumbehai ni kitendocha kuinua itikafi ya ujenitalia dhidi ya itikadi ya utu pasipo uhalali.

Kwa maneno mengine, basi, kiongozi mwenye tabia ya kuinua itikafi ya ujenitalia dhidi ya itikadi ya utu anakuwa anasumbuliwa na umaskini wa kifikra na ukosefu wa vipaumbele sahihi.

Naomba ushauri huu umfikie Mary Chatanda, Mwenyekiti wa UWT CCM Taifa, pamoja na Godbless Lema, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, kati ya wanasiasa wengine wengi wenye tabia kama za watu hawa wawili.

Kauli za karibuni kutoka kwa wanasiasa hawa wawili zimenisukumu kuwataja wanasiasa hawa wawili moja kwa moja. Nimeziambatanisha hapa chini kwa njia ya picha.

Lakini, tarehe 23 Oktoba 2023 Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa CCM (UWT), Mary Chatanda, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara eneo la Darajani Mjini Magharibi Unguja alisema yafutayo kuhusu kazi za jenitalia katika siasa za Tanzania:

"Mumeo akija mpokee mwambie pole mzee na kazi, mwambie tunamtaka Samia na Mwinyi. Ukiona anakuwa mgumu msubiri saa 11 asubuhi. Ukiona anakuwa mgumu msubiri saa 7 mchana akiwa mgumu msubiri jioni."

Lakini hakuishia hapo. Baada ya kuona kwamba Rais wa Zanzibar amefanya kazi kubwa ya kujenga hospitali zilizojaa vifaa tiba katika idara mbalimbali, ikiwemo idara ya uzazi, Mary Chatanda aliwahimiza Kina baba "kuwapiga risasi wanawake bila hofu" kwa sababu kina mama wakibeba mimba watajifungulia mahali salama hospitalini. Alisahau kwamba hospitali inazo idara zaidi mbali na idara ya uzazi, ambayo kimsingi ni idara ya ujenitalia. Kwa maneno yake, Chatanda alisema:

“Rais Mwinyi amefanya kazi kubwa ya kujenga hospitali kila wilaya zenye vifaa tiva vyote. Kabla ya hapo mlikuwa mnakwenda Mnazimmoja. Kina mama tuna raha tupu. Zile hospitali zina vifaa vyote na vitanda vizuri. Kwa hiyo kina baba kazi yao ni kupiga risasi hatimaye twende kujifungulia pazuri. Chezea kina baba wewe. Nendeni tu mkafyatue risasi hospitali za wilaya zipo, hospitali ya mkoa ipo, vifaatiba vipo. CCM Oyee.”

Mary Chatanda aliyasema haya tarehe 28 Oktoba 2023 akihutubua mkutano wa hadhara eneo la Darajani Mjini Magharibi Unguja.

Kwa ujumla, katika kila hotuba yake anayoitoa jukwaani, huyu mama anafikiri kingono-ngono muda wote, utadhani wakati yuko shuleni alisoma topiki moja tu ya jenitalia, yaani topiki ya jenitolojia (genitology), kwenye somo la bayolojia.

Tena hazingatii ukweli kwamba kwa mila na destruri za Tanzania majadiliano kuhusu masuala ya ngono yanazingatia tofauti za kiumri kwa ajili ya kulinda haki za watoto.

Nimeambatanisha kitabu cha jenitolojia ili kuthibitsha kwamba lipo somo la "genitology," lakini sio somo pekee hapa duniani, kama ambavyo kina Chatanda wanataka kuwaaminisha Watanzania.

1699172576742.png

1698579141512.png

1698582765192.png

1698582818755.png

Imeandaliwa na:

Mama Amon,
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu,
Dawati ta Utafiti la Mama Amon (DUMA)
"Sumbawanga Town"
S.L.P P/Bag Sumbawanga
Tanzania.
 
Attachments

 • 1699169995719.png
  1699169995719.png
  34.2 KB · Views: 8
 • Genitology-reading-the-genitals-Book.pdf
  4.3 MB · Views: 3

Siku ya Alhamisi 26 Oktoba 2023 Saa 03:00 asubuhi, Katibu mwenezi wa Taifa wa CCM Ndugu Paul C. Makonda alipokelewa Rasmi katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu Lumumba, Mkoani Dar es Salaam. Makonda aliongea mengi, lakini kuna kauli nne zenye mtazamo chanya zinazopaswa kufanyiwa kazi na wajasiriadola makini ndani na nje ya CCM. Kauli hizo ni hizi hapa:

1. Kazi ya chama cha siasa ni kuisimamia serikali kwa kuwa sikio na ulimi wa kuwasemea wananchi. Kuhusu jambo hili Makonda alisema:

"Kazi ya chama ni kuwa sikio na kuwasemea wananchi... Tutachukua hatua bila kusubiri, kwa kiongozi yeyote atayerudisha nyuma jitihada za chama kuendelea kuaminiwa na wananchi."

2. Kupinga taarifa zilizofiniwa kimakusudi (disinformation) na kukataa taarifa zilizofitinika kwa bahati mbaya (malinformation). Kuhusu jambo hili Makonda alisema:

“Duniani kote watu wanaishi kwa taarifa na taarifa zinafanya uamuzi, ukiwa na chanzo kibovu utafanya uamuzi mbovu, lakini ukiwa na chanzo kizuri utafanya uamuzi sahihi wakati wote.”

3. Kujitenga na tabia ya kusema uwongo kama mbinu ya kuwabeba watendaji wazembe serikalini. Kuhusu jambo hili Makonda alisema:

“Sitakuwa tayari kuwa msemaji wa chama ambacho kimepewa dhamana na wananchi, na wanaomsaidia mheshimiwa mwenyekiti wanashindwa kutekeleza nisimame hadharani kusema uongo, hapana. Kila kiongozi wa serikali atabeba msalaba wake mwenyewe.”

4. Utayari wa kuachana na siasa za jino kwa jino, kisasi kwa kisasi. Kuhusu jambo hili Makonda alisema:

“Wengi wanahamaki, wana bashasha na wengi wao wanawaza kwamba Makonda ataenda kulipa kisasi, wanawaza makonda atakwenda kufanya nini, wengine wanasema Usiyemtaka kaja na alikuwa haonekani alienda kujificha wapi? Nasema mbele ya watanzania na Mbele ya Mwenyenzi Mungu mimi sina kisasi kwa mtu yeyote."

5. Utayari wa Makunda kujumuika kwenye mashindano ya hoja zinazosimama au kuanguka kutokana na ushahidi uliowekwa mezani. Kuhusu jambo hili Makonda alisema:

"Mbowe akiruka [kwa hoja za] angani tutamfuata, akienda [kwa hoja za] nchi kavu tutamfuata, akiingia kwenye [hoja za] boti tutamfuata, atapigwa [kwa hoja] kila kona kwa sababu moja tu. Hoja, na uwezo na utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi hauna shaka. Kwa hiyo kama kuna mtu yeyote amemcheleweshea Mbowe na chama chake cha watoa taarifa kibali cha kutumia helikopta, kwa niaba ya chama cha mapinduzi, nikiwa msemaji chini ya Mwenyekiti Dkt. Samia, Mbowe apewe kibali. Na kama kaka yangu Mbowe huna mafuta nimeshakuombea tayari."

Kwa maoni yangu, kauli tano za Makonda nilizonukuu hapo juu ni chachu katika ujenzi wa mwavuli wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini Tanzania.

Sasa Chadema, ACT na wengine, wamepewa nafasi ya kumjibu Makonda kwa hoja kwa kuibua "taarifa" zitakazomnyima usingizi Makonda.

Kwa njia hiyo mwavuli wa siasa za vyama vingi utaomarika na kuzuia jua kali ya utapiamaendeleo kuwachoma wananchi utosini.

Katika hatua ya sasa, ambapo Ilani ya CCM (2020-2025) imekuwa inatekelezwa kwa mwaka wa tatu, kuna maswali mengi kuhusu utekelezaji yanayohitaji majibu kutoka kwa Makonda.

Mfano mzuri ni utekelezwaji wa ahadi ya kujengwa kwa barabara za angani katika mkoa wa Dar es Salaam. Kuhusu ahadi hii, kifungu cha 55(e) kwenye Ilani (2020-2025) kinasema yafuatayo:
View attachment 2796856
View attachment 2796850

Hivyo, wito wangu ni kwamba, sasa siasa za mipasho, masimango, na kejeli zinazoongozwa na itikadi ya ujenitalia (genitalism) badala ya itikadi ya uperisona (personalism) viwekwe pembeni kidogo ili kupata nafasi ya kufanya siasa chanya kwa kutumia kanuni za makabiliano ya hoja za kirazini.

Naomba wito huu umfikie Mary Chatanda na Godbless Lema, kati ya wanasiasa wengine wengi. Kauli zinazonisukumu kuwataja wanasiasa hawa nimeziambatanisha hapa chini.

View attachment 2796801

View attachment 2796860

View attachment 2796862

Safi sana
 
Hoja kwa hoja Ili tufikie maendeleo ya kweli.
Vyama vya upinzani badala ya kufanya tathimini ya utekelezaji wa ilani ya CCM na kuibana wao wanaendekeza gutter politics!
 
Asante Mama Amon kwa kuzimulika Hoja zolizotolewa na Bwana Makonda.

Binafsi nimependezwa na uwasilishaji wako hasa jinsi ulivyotumia vokali kuwasilisha herufi za kwanza za sera za chama chetu: afya, elimu, ikolojia, uongozi na uchumi.

Hiyo ilikuwa njia nzuri ya kukumbuka na kujumlisha sera za CCM.

Hata hivyo, nadhani CHADEMA watatumia mkakati tofauti kuwasilisha sera zake. Kama tunavyoona tayari

 • Wanashambulia(Attack) mfano huyo Godbless Lema
 • Wananyonya(Exploit) rejea uzi wa Lukasi mwashambwa kuhusu Join the train
 • Wanapuuzia Sera(Ignore) Sijawahi kusikia wakiuza Sera
 • Wanakutenga(Ostracize) manake ukipishana nao kihoja unapachikwa ukabila na kupewa genge la Usukuma!
 • Na kukudoofisha(Undermine) mfano rahisi ni hawa ndugu zetu wa Sauti ya Wananchi
Attack, Exploit, Ignore,Ostracize, Undermine! Hizo ni vokali zao.

Pamoja na kuwa CCM bado inahitaji maboresho...kushughulikia makelele ya maskini, janga la ukosefu wa ajira, ukosefu wa haki wa ufisadi,(washugulikiwe) ukandamizaji wa Wamasai na maendeleo duni Vijijini, Ugawiaji wa Bandari bado nina kavitumaini vichache na CCM, ila basi, Vyama vyote vya Siasa Vibadilike, including CCM

Makonda ana hoja na zijibiwe.
 
Tangu Paul Makonda alipoanza kazi baada ya kuteuliwa kuwa Katibu mwenezi wa Taifa wa CCM mitandao ya kijamii imesema mengi juu yake na ofisi aliyoteuliwa kuitumikia.

Maoni mengi yana sura hasi, baadhi wakiwa wanamtazama kwa kutumia miwani ya itikadi ya ujenitalia (genitalism), na hivyo kushindwa kuona picha kubwa iliyobebwa ba kauli zake. Kwa mfano kuna watu wanaongelea habari ya utowashi wa Makonda na kupiga kisogo kabisa masuala ya kiitikadi, kisera na kiutawala anayoyaongeleai.

Lakini, kwenye kauli zake kuna masuala yanayohusu misingi ya utu (personalism) ambayo hayapaswi kufunikwa na kejeli zinazia kwenye itikadi ya ujenitalia na ambayo nimeamua kuyaweka bayana hapa kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa.

Hivyo, katika aya ziafuatazo nitajadili mambo yafuatayo: (1) Hoja tano za Paul Makonda, (2) Umuhimu wa siasa zinazoongozwa na uchambuzi makini wa kisera, (3) Umuhumu wa kutofautisha tuhuma pasipo hatia na tuhuma zenye uthibitisho wa hatia, na (4) Umuhimu wa siasa zinazoongozwa na itikadi ya utu (personalism) badala ya itikadi ya ujenitalia (genitalism).

I. Hoja tano za Paul Makonda

Saa 03:00 asubuhi ya Alhamisi 26 Oktoba 2023 , Katibu mwenezi wa Taifa wa CCM Ndugu Paul C. Makonda alipokelewa Rasmi katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu Lumumba, Mkoani Dar es Salaam.

Siku hiyo, Makonda aliongea mengi, lakini kuna kauli tano zenye mtazamo chanya na zinazopaswa kufanyiwa kazi na wajasiriadola makini ndani na nje ya CCM. Kauli hizo nazifupisha hapa chini:

1. Utayari wa Makonda kukubaliana na kanuni kwamba kazi ya chama cha siasa ni kuisimamia serikali kwa kuwa sikio na ulimi wa kuwasemea wananchi. Kuhusu jambo hili Makonda alisema:

"Kazi ya chama ni kuwa sikio na kuwasemea wananchi... Tutachukua hatua bila kusubiri, kwa kiongozi yeyote atayerudisha nyuma jitihada za chama kuendelea kuaminiwa na wananchi."

2. Utayari wa Makonda kupinga taarifa zilizofitiniwa kimakusudi (disinformation), kukataa taarifa zilizofitinika kwa bahati mbaya (malinformation), na kupiga kisogo taarifa zilizomegwa kwa makusudi ili kupotosha hadhira (censorship). Kuhusu jambo hili Makonda alisema:

“Duniani kote watu wanaishi kwa taarifa na taarifa zinafanya uamuzi, ukiwa na chanzo kibovu utafanya uamuzi mbovu, lakini ukiwa na chanzo kizuri utafanya uamuzi sahihi wakati wote.”

3. Utayari wa Makonda kujitenga na tabia ya kusema uwongo kama mbinu ya kuwabeba watendaji wazembe serikalini. Kuhusu jambo hili Makonda alisema:

“Sitakuwa tayari kuwa msemaji wa chama ambacho kimepewa dhamana na wananchi, na wanaomsaidia mheshimiwa mwenyekiti wanashindwa kutekeleza nisimame hadharani kusema uongo, hapana. Kila kiongozi wa serikali atabeba msalaba wake mwenyewe.”

4. Utayari wa Makonda kuachana na siasa za jino kwa jino, kisasi kwa kisasi. Kuhusu jambo hili Makonda alisema:

“Wengi wanahamaki, wana bashasha na wengi wao wanawaza kwamba Makonda ataenda kulipa kisasi, wanawaza makonda atakwenda kufanya nini, wengine wanasema Usiyemtaka kaja na alikuwa haonekani alienda kujificha wapi? Nasema mbele ya watanzania na Mbele ya Mwenyenzi Mungu mimi sina kisasi kwa mtu yeyote."

5. Utayari wa Makonda kujumuika kwenye mashindano ya hoja zinazosimama au kuanguka kutokana na ushahidi uliowekwa mezani. Kuhusu jambo hili Makonda alisema:

"Mbowe akiruka [kwa hoja za] angani tutamfuata, akienda [kwa hoja za] nchi kavu tutamfuata, akiingia kwenye [hoja za] boti tutamfuata, atapigwa [kwa hoja] kila kona kwa sababu moja tu. Hoja, na uwezo na utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi hauna shaka."

Kwa maoni yangu, kauli tano za Makonda nilizonukuu hapo juu ni chachu katika ujenzi wa mwavuli wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini Tanzania.

Sasa Chadema, ACT na vyama vingine, ambavyo Makonda amevitaja kuwa ni "vyama vya watoa taarifa" wamepewa nafasi ya kumjibu Makonda kwa hoja kwa kufanya kazi ya "watoa taarifa" za kweli, hasa zile "taarifa" zitakazomnyima usingizi Makonda.

Kwa njia hiyo spoku za mwavuli wa siasa za vyama vingi zitaimarika na na kuuwezesha mwavuli kuzuia jua kali la utapiamaendeleo kuwachoma wananchi utosini.

II. Umuhimu wa siasa zinazoongozwa na uchambuzi makini wa kisera

Demokrasia ya vyama vingi ni kamamwavuli wenye spoku nyingi, kila spoku ikiwakilisha chama kimajawapo, wakati ile nguo ya juu ya mwavuli inawakilisha maslahi ya pamoja katika Taifa bila kujali tofauti za umri, dini, jinsia, itikadi, rangi wala ukanda.

Kusudi mwavuli huu uweze kuzalisha kivuli kinacholinda maslahi ya pamoja ni lazima spoku zote zifanye kazi kwa "mtindo wa vuta nikuvute."

Katika mtindo huu vyama vya upinzani hutafiti, kufanya uchambuzi wa kisera na kutoa taarifa za ukosoaji kwa umma kuhusu mapungufu ya serikali na chama tawala. Nachi chama tawala kikijibu mapiga ama kwa kukanusha au kuchukua hatua za marekebisho stahili.

Hivyo, katika hatua ya sasa, ambapo Ilani ya CCM (2020-2025) imekuwa inatekelezwa kwa mwaka wa tatu, kuna maswali mengi kuhusu utekelezwaji wake yanayopaswa kuibuliwa na vyama vya upinzania na yanayohitaji majibu kutoka kwa Makonda.

Kwa ujumla, napendekeza kwamba, sera zote zilizo katika ilani za vyama vyote vya siasa, zinaweza kugawanywa, bila kubaki, katika makundi matano. Makundi hayo ni: Afya tele, Elimu bora, Ikolojia rafiki, Ofisi zenye utawala bora, na Uchumi unaojali utu. Nakumbuka maeneo haya matano kwa msaada wa vokali tano za Kiswahili, yaani “A, E, I, O, U.”

Kwa kuzingatia maeneo haya matano, katika aya zifuatazo napendekeza kufupisha ahadi 90 nilizoziona kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ili kuweka rejea murua itakayotusaidia kufanya ufuatiliaji na tathmini ya kazi za serikali kuanzia 01 Januari 2021.

AFYA TELE: Afya ni hali ya binadamu kuwa na mwili na akili vyenye kutenda kazi zake barabara. Hali hii ni matokeo ya kuwa na kinga dhidi maradhi yanayoambukiza na yasiyoambukiza, mkamilishano thabiti kati ya nafsi na mwili, na masikilizano kati ya mwili na mazingira yake, ambapo mazingira yanahusisha makazi, malazi, chakula na jamii ya watu wanaomzunguka mhusika. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu afya ziko katika ibara za 81-100. Baada ya kuipitia Ilani hii, nimejiridhisha kwamba, kuna sera 16 ambazo zinapaswa kutekelezwa na serikali yake ili kukuza na kuhami afya ya kila raia.

 1. Kuna ahadi kuhusu ujenzi na ukarabati wa vituo vya huduma za afya, ushirikishwaji wa sekta binafsi katika huduma za afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, upatikanaji wa watumishi na mabingwa wa kada ya afya, na sera ya mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
 2. Pia, kuna ahadi kuhusu mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza, mapambano dhidi ya magonjwa yanayotokana na virusi kama vile VVU, upatikanaji wa mlo kamili na bora, na sera ya uduma za ustawi wa wazee.
 3. Aidha, kuna ahadi kuhusu huduma za ustawi wa watoto na familia, huduma za watu wenye ulemavu, kusimamia upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira, kusimamia mipango miji na mipango vijiji, sera ya ujenzi wa nyumba na makazi bora, sera ya bima ya afya kwa wote, na sera ya afya ya mama na mtoto. Lakini, katika ilani hii, haikutajwa ahadi ya “bima ya afya kwa watu wote.” Hii ni ahadi ya jukwaani.
ELIMU BORA: Elimu ni mchakato wa kupata taarifa, maarifa na ufundi wa kufanya utafiti na kubuni tekinolojia za kumsaidia mwanafunzi aliyefuzu kuyamudu mazingira yake ya kimaumbile, kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiutamaduni. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu elimu ziko katika ibara za 78-80, na ahadi kuhusu sayansi na tekinolojia ziko katika ibara za 101-103. Baada ya kupitia ilani hii, nimeona kuwa sekta hii itaboreshwa kwa kupitia utekelezaji wa mikakati ya kisera 10.
 1. Kuna ahadi kuhusu elimu ya msingi, elimu ya sekondari , elimu ya ufundi stadi, na sera ya elimu ya Juu.
 2. Pia kuna sera za kuanzisha makampuni ya katika sekta mbalimbali ili kuendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu; kujenga mfumo wa Taifa wa ubunifu (national innovation system); na sera ya kuendeleza vituo atamizi kwa ajili ya kukuza na kuendeleza ubunifu wa kisayansi na kitejinolojia.
 3. Kadhalika, kuna ahadi kuhusu kuhamasisha matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika uzalishaji, usambazaji, na utawala kwa kutumia tekinolojia ya kidijitali; kuanzisha vituo vya umahiri wa sayansi na teknolojia (centres of excellence) katika taasisi za elimu ya juu; na sera ya kuimarisha mafunzo ya walimu wa sayansi, teknolojia na ufundi katika ngazi za shule za msingi, shule za sekondari, vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi na vyuo vikuu.
IKOLOJIA RAFIKI: Neno "ikolojia" linamaanisha mazingira. Mazingira ya binadamu yanajumuisha wanyama, mimea, wadudu, hewa, maji na vitu vyote vilivyo baki vilivyoko ardhini, angani, majini, msituni, porini, pamoja na michakato yote ya kibayolojia inayomfungamanisha kila binadamu pamoja na vitu hivi kupitia mitandao ya vyakula vya viumbe anwai (ecological food web). Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu ikolojia ziko katika ibara ya 9B(vii). Baada ya kupitia Ilani hii, na kukagua mikakati ya kutunza mazingira iliyoko katika tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais, nimebaini kuwa, kuna mikakati 10 ya kisera inayoweza kutekelezwa ili kukuza na kuhami mfumo wa ikolojia ulio salama kwa uhai wa binadamu na viumbe baki.
 1. Kuna ahadi juu ya kuhimiza watu kuepuka kadiri inavyowezekana kutumia nishati zinazozalisha hewa ya ukaa ambayo ni chanzo kikuu cha mabadiliko ya tabia nchi; kuwekeza katika miradi ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi (climate adaptation strategies); na kuwekeza katika miradi ya kupunguza ukubwa wa vyanzo vya mabadiliko ya tabia nchi (climate mitigation strategies).
 2. Aidha kuna ahadi juu ya kuhifadhi uoto wa asili ulioko juu ya nchi, kuhifadhi uoto wa asili ulioko majini, kuhifadhi wanyama wa porini, kuhifadhi wanyama wa majini, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, na kunzisha mfuko maalum kwa ajili ya utafiti, usimamizi na tathmini juu ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi.
 3. Kadhalika kuna ahadi juu ya kuzuia uchafuzi wa mazingira unaofanyika kupitia uzalishaji wa takangumu; uzuia uchafuzi wa mazingira unaofanyika kupitia uzalishaji wa takamaji; na uzuia uchafuzi wa mazingira unaofanyika kupitia uzalishaji wa takahewa.
OFISI ZENYE UTAWALA BORA: Utawala bora ni aina ya utawala ambao unahakikisha kuwa utaratibu wa kufanya maamuzi na kutekeleza maamuzi hayo kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa jamii unazingatia misingi ya utu, uhuru, haki, ushirikishwaji, demokrasia, uwajibikaji, uhasibikaji, uwazi, tija, ufanisi, usawa mbele ya sheria, na ushiriki wa makundi yote ya jamii. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu ofisi za utawala bora ziko katika ibara ya 108-130. Baada ya kupitia ilani hii nimjiridhisha kuwa kuna jumla ya sera 16 zinazopaswa kutekelezwa kwa ajili ya kufanikisha dhana ya utawala bora.
 1. Kuna ahadi juu ya kuheshimu haki ya kujitawala katika ngazi za chini za serikali kwa kugatua madaraka, kusimamia maadili katika utumishi wa umma, kufanya mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, kuheshimu misingio ya demokrasia na haki za binadamu, kuheshimu katiba na kuzingatia utawala wa matakwa ya sheria, na sera ya kuhuisha usawa wa jinsia katika sekta ya umma na sekta binafsi.
 2. Pia, kuna ahadi juu ya kuhami uhuru wa vyombo vya habari, kuheshimu uhuru wa raia kujieleza na kuwasiliana, kuhesimu uhuru wa asasi za kiraia, kulinda uhuru wa kuabudu, kulinda haki za wafanyakazi na uhuru wa vyama vya wafanyakazi, na sera ya kukabiliana na majanga ya asili kwa kuzingatia kanuni ya utawala auni (principle of subsidiarity).
 3. Kadhalika, kuna ahadi juu ya kupambana na dawa za kulevya, menejimenti ya mahusiano ya kisiasa na kiuchumi katika ngazi ya kimataifa, menejimenti ya kidemokrasia ya vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi, na sera ya kuzuia utekaji, utesaji na uteketezaji wa uhai wa raia wasio na hatia.
 4. Vile vile kuna ahadi ya kusimamia ukuu wa nchi, yaani "state sovereignty management," kwa maana ya kusimamia ukuu wa serikali katika kutunga na kutekeleza sera za nchi, kusimamia ukuu wa mahakama katika kutafsiri sheria za nchi; kusimamia ukuu wa bunge katika kutunga sheria zinazoiongoza serikali katika kutekeleza sera zake; kusimamia ukuu wa wananchi juu ya vyombo vya dola kwa kuzingatia mgawanyo na udhibitiano wa kimadaraka kati ya serikali, mahakama na bunge; na kusimamia kazi ya kuzuia upunguzaji wa eneo la nchi kwa njia ya kumomonyoa mipaka yake au kutengeneza "viraka" vya himaya binafsi za wageni ndani yake.
UCHUMI UNAOJALI UTU: Uchumi ni mfumo unaojumuisha mambo makuu manne, yaani, michakato, kanuni za kuratibu michakato hiyo, tunu zinazowaunganisha watendaji kwa skuwaelekeza katika malengo yanayofanana, na misingi ya ustaarabu wa kugawana shida na raha za kiuchumi (processes, principles, values, and justice). Kuna michakato mitano, yaani uzalishaji, usambazaji, mauziano, utumiaji wa huduma na bidhaa, na uwekezaji (production, distribution, exchange, consumption and investment). Kuna kanuni kuu tatu zinazotumika kuratibu michakato iliyomo katika sekta ya uchumi, yaani kanuni za ushindani, ushirikiano, na uingiliaji kati kupitia mkono wa serikali ili kudhibiti madhara hasi ya ushindani na ushirikiano unaotokea sokoni (competition, cooperation, and intervention). Na kuna tunu tatu zinazohuisha malengo ya kiuchumi, yaani uhuru, mshikamano, na usawa (freedom, solidarity and equality); ambapo, tunu ya uhuru ni chimbuko la kanuni ya ushindani, tunu ya mshikamano ni chimbuko la kanuni ya ushirikiano, na tunu ya usawa ni chimbuko la kanuni ya uingiliaji kati. Katika Ilani ya CCM (2020-2025), ahadi kuhusu ahadi kuhusu ujenzi wa miundobinu ya kiuhumi ziko katika ibara ya 12-76. Baada ya kusoma ilani hii nimebainisha vipengele 38 vya kisera vinavyopaswa kufanyiwa kazi ili kuzalisha mfumo wa uchumi unaojali maslahi ya watu wote.
 1. Kuna ahadi juu ya ushirikishaji wa sekta binafsi katika uwekezaji, uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, na kuzalisha ajira kwa vijana, kusimamia vyama vya ushirika, kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda, biashara na mfumo wa kodi, vituo atamizi kwa ajili ya kuzalisha wajasiriamali, na kubuni sera za kifedha zinazoruhusu mzunguko wa fedha wenye kasi kubwa ya kuhakikisha kwamba fedha inapita katika mfuko wa kila raia anayejishughulisha.
 2. Pia, kuna ahadi juu ya barabara za chini, madaraja, makalvati, mizani ya kupima magari, vivuko, bandari, reli, viwanja vya ndege, na mawasiliano ya simu.
 3. Aidha, kuna ahadi juu ya ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) zifuatayo ili kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam, kwenye makutano ya barabara katika maeneo yafuatayo: Chang’ombe, Uhasibu, Kamata, Morocco, Mwenge, Magomeni, Tabata, Fire, Makutano ya Ally Hassan Mwinyi na United Nation, na Makutano ya Ally Hassan Mwinyi na Kinondoni. (Ilani ya CCM 2020-2025, ib. 55(e)(i)).
 4. Kadhalika, kuna ahadi juu ya nishati ya umeme, nishati ya mafuta, nishati ya gesi asilia, madini, utalii, maliasili, matumizi bora ya ardhi, na kuendesha sekta ya utamaduni, sanaa na michezo kibiashara.
Uchambuzi wa kisera unaohitajika unaweza kufuata mtiririko huu, japo sio lazima, maana kuna njia nyingi z kuchuna ngozi ya paka.

Lakini, vyovyote iwavyo, tunapaswa kutembea kwenye ilani kifungu baada ya kifungu. Mfano mzuri ni kufuatilia utekelezwaji wa ahadi ya kujengwa kwa barabara za angani katika mkoa wa Dar es Salaam. Kuhusu ahadi hii, kifungu cha 55(e)(i) kwenye Ilani (2020-2025) kinasema yafuatayo:

View attachment 2796856
View attachment 2796850

Maswali hapa ni pamoja na: Utekelezaji wa ahadi hiii umefikia hatua gani? Hatua hiyo inaendana na mpango wa ufuatiliaji uliowekwa kwenye maandiko ya CCM na serikali? Kama ni hapana kwanini, na hatua gani zichukuliwe? Waziri mwenye dhamana ya ujenzi anapaswa kuwa na majawabu kwa maswali haya.

III. Umuhumu wa kutofautisha tuhuma pasipo uthibitisho wa hatia na tuhuma zenye uthibitisho wa hatia

Kanuni mojawapo katika utawala na uongozi ni kanuni ya utoaji haki sawa kwa wote walio sawa. Msingi wa kanuni hii ni ukweli. Ndio maana katiba ya nchi inasema kwamba kila mtu anapaswa kuhesabiwa mtakatifu hadi hapo chombo halali kitakapomtia hatiani.

Kwa hiyo, tabia ya kusambaza "tuhuma zisizo na uthibitisho wa hatia," kwamba "Paul Makonda aanatuhumiwa kughihsi vyeti vya kitaaluma," ni ukiukaji wa misingi muhimu ya utawala bora.

Yaani, kusambaza "tuhuma" pasipo uthibitisho wa "hatia" ni utovu wa nidamu ya kiutawala.Na sifa moja ya mtu anayetaka kuwa kiongozi wa umma ni kutofautisha tuhuma na hatia.

Lakini, hapa suala muhimu zaidi ni kwamba, hatia inathibitishwa na ushahidi usiokanushika, kwa kutumia mizania ya uzito wa taarifa zilizopo mbele ya mtoa hukumu.

Nitaeleza. Mizania ya uzito wa taarifa zilizopo mbele ya mtoa hukumu inafanya kazi namna hii:

Katika mchakato wa uthibitisho wa maarifa (epistemic justfication), kwa kutumia kikapu cha taarifa za uthibitisho zinazounda asilimia mia moja, usahihi wa kila kauli, tuseme "Kauli P," mfano "P=Paul Makonda alighushi vyeti," huchunguzwa kwa kutumia kauli tatu kwa mpigo, ambazo ni,

 • "Kauli kwamba P ni kweli," yaani zaidi ya 50% ya ushahidi unaunga mkono kauli P (chukua upande huu).
 • "Kauli kwamba P sio kweli," yaani zaidi ya 50% ya ushahidi unapinga kauli P (chukua upoande huu).
 • "Ama kauli kwamba P ni kweli au kauli kwamba P sio kweli," yaani 50% ya ushahidi uliopo unaunga mkono kauli P na 50% ya ushahidi uliopo unapinga kauli P (hii ni njia panda, usichukue upande, jizuie kutoa hukumu).
Tukumbuke kwamba, kila mtu mwenye akili timamu analo jukumu la kiepistemolojia (epistemic duty) la kujiunga kwenye kambi ya kiimani inayoshikilia misimamo yenye kuungwa mkono na ushahidi ulio juu ya 50% na kujizui kuchagua kambi pale ambapo ushahidi alio nao hautoshelezi matakwa ya kutoa hukumu sahihi.

Basi, kwa kutumia mchakato huu tufikirie upya juu ya usahihi wa kauli zetu za kila siku dhidi ya watu baki na kama tutaona tunao ushahidi wa kutosha tuanzishe mchakato wa kuzisambaza, ama sivyo tukae kimya huku tukiendelea na utafiti/uchunguzi. Na utafiti usipozaa matunda tufunge faili la uchunguzi.

IV. Umuhimu wa siasa zinazoongozwa na itikadi ya utu badala ya itikadi ya ujenitalia

Hapo mwanzoni nimesema kuwa maoni mengi yanayotolewa dhidi ya Makondayana sura hasi, baadhi ya wasemaji wakiwa wanamtazama kwa kutumia miwani ya itikadi ya ujenitalia (genitalism), na hivyo kushindwa kuona picha kubwa iliyobebwa ba kauli zake.

Kuna watu wanaongelea ujinsia wa Makonda wakimtaja taja kama kama towashi (eunuch) na hivyo kujizuia kabisa kuchambua masuala ya kiitikadi, kisera na kiutawala anayoyaongelea.

Lakini pia, ndani ya CCM kuna viongozi wakubwa wanatumia muda mwingi kuongelea maadili ya jamii kwa kukomalia maadili ya ngono. Muda mwingi wanajifanya vinara wa kupinga uzinzi, uasherati, umalaya, ubakaji, na ulawiti.

Wakiongelea wodi za wagonjwa hospitalini wanachokumbuka haraka ni wodi za wazazi kama kwamba wodi zote na idara zote hospitalini ni wodi za wazazi.

Lakini, maadili ya jamii ni suala pana. Yanahusisha pia maadili ya uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma muhimu, maadili ya elimu, maadili ya kilimo, maadili ya ufugaji, maadili ya biashara, maadili ya siasa za kibunge, maadili ya usafirishaji wa abiria na mizigo, maadili ya ujenzi wa majengi na barabara, maadili ya utunzaji wa mazingira, na maadili ya kusanifu hoja zenye utimamu wa kimntiki, kati ya maadili mengine mengi.

Hivyo, wito wangu ni kwamba, sasa siasa za kupakana matope (gutter politics), mipasho, masimango, na kejeli zinazoanzia kwenye itikadi ya ujenitalia (genitalism) zikome.

Badala yake, itikadi ya utu (personalism) ituongoze ili kutoa nafasi ya kufanya uchambuzi wa kisera kwa kutumia kanuni za makabiliano ya hoja za kirazini zinazoongozwa na ushahidi thabiti.

Kwa ajili ya kuikubali itikadi ya utu ni muhimu kuelewa kwamba, kila kiumbehai hutambulishwa na malengo ya kibayolojia, ambayo hufanikishwa na kazi zinazofanywa na viungo 78 vilivyo mwilini mwake.

Kazi hizo ni kama vile kujongea, kutoa uchafu mwilini, kupumua, kufukuza kifo, kutambua mabadiliko ya kimazingira, kupata lishe, ukuaji, na kuzaliana. Haya ni malengo makuu mawili, yaani kujihifadhi na kuzaliana.

Hii maana yake ni kwamba, kila mtu jamii ya binadamu anaitwa kiumbehai kwa sababu viungo vyake 78 vimeunganishwa na kitu kimoja cha ziada.

Yaani angalu lengo mojawapo kati ya malengo mawili: lengo la kuhifadhi uhai wa kimwili au lengo la kuzaliana. Lengo la kwanza linahusu uhai wa kiumbehai chenyewe, na lengo la pili linahusu uhai wa ukoo wote wa kiumbehai.

Hivyo, sababu za pendekezo kuhusu ukuu wa itikadi ya utu (personalism) dhidi ya itikadi ya ujenitalia (genitalism) ni za kisayansi na kifalsafa. Nitafafanua.

Tangu kidato cha kwanza, walimu wetu wa somo la bayolojia, wametufuindisha kwamba, mwili wa kila binadamu una viungo 78. Pia wametueleza kwamba viungo hivyo vinagawanyika kwenye mifumo mikubwa kumi na moja ifuatayo:

 • (1) Mfumo wa damu (circulatory organ system),
 • (2) Mfumo wa tezi (lymphatic organ system),
 • (3) Mfumo wa hewa (respiratory organ system),
 • (4) Mfumo wa jalada la mwili lenye luhusisha ngozi, kucha, na nywele (integumentary organ system),
 • (5) Mfumo wa homoni (endocrine organ system),
 • (6) Mfumo wa chakula (digestive organ system),
 • (7) Mfumo wa kuchuja uchafu (excretory organ system),
 • (8) Mfumo wa misuli na mifupa (muscular-skeletal organ system),
 • (9) Mfumo wa ubongo na mishipa ya fahamu (nervous organ system),
 • (10) Mfumo wa kinga mwili (immune organ system), na
 • (11) Mfumo wa uzazi (genital organ system).
Mchoro ufuatao unatoa picha kubwa kuhusu mahusiano yaliyopo kwenye mifumo hii ya mwili wa kila binadamu:

View attachment 2804408

Na katika falsafa ya bayolojia (philosophical biology) tunafundishwa kwamba, mifumo yote 11 iliyo kwenye mwili wa mtu inagawanyika katika makundi makuu mawili.

Kwanza kuna mifumo inayofanya kazi ya kulinda na kuendeleza maisha ya kiumbehai kimoja kimoja kwa kuzuia kifo kwa njia mbalimbali (survival organ systems).

Na pili kuna mfumo mmoja pekee unaofanya kazi ya kulinda na kuendeleza maisha ya ukoo kwa kuhamisha uhai kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto, yaani mfumo wa uzazi (genital organ system).

Mfumo wa uzazi unajumuisha jenitalia za nje ya mwili na jenitalia za ndani ya mwili. Kuna jenitalia za kiume na jenialia za kike. Katika maelezo haya, neno "jenitalia" ni unyambulisho wa neno "genitals" la Kiingereza. Kwa hiyo, viungo vinavyoitwa jenitalia ni asilimia tisa pekee katika mwili wote.

Mchanganuo huu ndiyo sababu inayowafanya baadhi ya wadadisi wa mambo kuuliza, "do organisms survive to reproduce or reproduce to survive?" Jawabu lake sio muhimu kwa sasa.

Lakini pointi kuu hapa ni kwamba kuna kazi kuu mbili zinazofanywa na viungi vya mwili. Yaani kazi ya kulinda uzima wa kiumbehai (survival/self-preservataion) na kazi ya kuendeleza uzima wa ukoo (reproduction/genitality/species-preservation).

Lakini pia, ikumbukwe kwamba, viungo vya mwili vinavyoitwa jenitali sio miongoni mwa viungo vikuu vitano vyenye jukumu la kupigana na kifo, yaani ubongo, moyo, mapafu, ini na figo. Hata ukiingia chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali yoyote hutakuta "life monitoring screen" inayoonyesha utendaji kazi wa jenitalia.

Badala yake utaona grafu za kuonyesha utendaji kazi wa ubongo, moyo, mapafu, ini, na figo. Viungo hivi vitano vikifeli unaambiwa mgonjwa wako tayari amekuwa mgeni wa Mungu. Unaanza safari ya kwenda makaburini.

Hivyo, kuna mawili hapa. Mosi, viongozi wetu wanapaswa kutumia muda mwingi kujadiliana nasi kuhusu sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa UBONGO, sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa MOYO, sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa MAPAFU, sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa INI, sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa FIGO, sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa KOO, UTUMBO MWEMBAMBA, TUMBO LA CHAKULA, UTUMBO MPANA, MIKONO, MIGUU, MACHO, MASIKIO, PUA, MIFUPA, NGOZI, na viungo kama hivyo.

Na pili,viongozi wetu wanapaswa kutumia muda muda kidogo sana kuongelea sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa JENITALIA.

Kwa hiyo, kutumia muda mwingi kuongelea sera zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa jenitalia na kutenga muda kidogo kuongelea sera zinazohusu utendaji kazi wa viungo vya mwili vilivyo muhimu zaidi katika kulinda maisha ya kiumbehai ni kitendocha kuinua itikafi ya ujenitalia dhidi ya itikadi ya utu pasipo uhalali.

Kwa maneno mengine, basi, kiongozi mwenye tabia ya kuinua itikafi ya ujenitalia dhidi ya itikadi ya utu anakuwa anasumbuliwa na umaskini wa kifikra na ukosefu wa vipaumbele sahihi.

Naomba ushauri huu umfikie Mary Chatanda, Mwenyekiti wa UWT CCM Taifa, pamoja na Godbless Lema, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, kati ya wanasiasa wengine wengi wenye tabia kama za watu hawa wawili.

Kauli za karibuni kutoka kwa wanasiasa hawa wawili zimenisukumu kuwataja wanasiasa hawa wawili moja kwa moja. Nimeziambatanisha hapa chini kwa njia ya picha.

Lakini, tarehe 23 Oktoba 2023 Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa CCM (UWT), Mary Chatanda, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara eneo la Darajani Mjini Magharibi Unguja alisema yafutayo kuhusu kazi za jenitalia katika siasa za Tanzania:

"Mumeo akija mpokee mwambie pole mzee na kazi, mwambie tunamtaka Samia na Mwinyi. Ukiona anakuwa mgumu msubiri saa 11 asubuhi. Ukiona anakuwa mgumu msubiri saa 7 mchana akiwa mgumu msubiri jioni."

Lakini hakuishia hapo. Baada ya kuona kwamba Rais wa Zanzibar amefanya kazi kubwa ya kujenga hospitali zilizojaa vifaa tiba katika idara mbalimbali, ikiwemo idara ya uzazi, Mary Chatanda aliwahimiza Kina baba "kuwapiga risasi wanawake bila hofu" kwa sababu kina mama wakibeba mimba watajifungulia mahali salama hospitalini. Alisahau kwamba hospitali inazo idara zaidi mbali na idara ya uzazi, ambayo kimsingi ni idara ya ujenitalia. Kwa maneno yake, Chatanda alisema:

“Rais Mwinyi amefanya kazi kubwa ya kujenga hospitali kila wilaya zenye vifaa tiva vyote. Kabla ya hapo mlikuwa mnakwenda Mnazimmoja. Kina mama tuna raha tupu. Zile hospitali zina vifaa vyote na vitanda vizuri. Kwa hiyo kina baba kazi yao ni kupiga risasi hatimaye twende kujifungulia pazuri. Chezea kina baba wewe. Nendeni tu mkafyatue risasi hospitali za wilaya zipo, hospitali ya mkoa ipo, vifaatiba vipo. CCM Oyee.”

Mary Chatanda aliyasema haya tarehe 28 Oktoba 2023 akihutubua mkutano wa hadhara eneo la Darajani Mjini Magharibi Unguja.

Kwa ujumla, katika kila hotuba yake anayoitoa jukwaani, huyu mama anafikiri kingono-ngono muda wote, utadhani wakati yuko shuleni alisoma topiki moja tu ya jenitalia, yaani topiki ya jenitolojia (genitology), kwenye somo la bayolojia.

Tena hazingatii ukweli kwamba kwa mila na destruri za Tanzania majadiliano kuhusu masuala ya ngono yanazingatia tofauti za kiumri kwa ajili ya kulinda haki za watoto.

Nimeambatanisha kitabu cha jenitolojia ili kuthibitsha kwamba lipo somo la "genitology," lakini sio somo pekee hapa duniani, kama ambavyo kina Chatanda wanataka kuwaaminisha Watanzania.

View attachment 2804479

View attachment 2796801

View attachment 2796860

View attachment 2796862

Imeandaliwa na:

Mama Amon,
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu,
Dawati ta Utafiti la Mama Amon (DUMA)
"Sumbawanga Town"
S.L.P P/Bag Sumbawanga
Tanzania.

Hivi sasa alipotolewa ukatibu mwenezi wa Itikadi na kuwa Mkuu wa Mkoa, bado hizi pumba ulizoandika hapa unaona zinastahili?
 
Back
Top Bottom