Goba, Dar: Wanne wafariki dunia, 17 wajeruhiwa baada ya jengo kuangukia nyumba za jirani

Mmiliki ni mtu toka mkoa gani?
Isije ikawa Ni wale wanaoamini kamati za ufundi ......zaidi
Mwakifulefule kabila lakohalihusiki
 
Wafuatao ndo wakulaumiwa either mmoja wao, wawili au wote kwa pamoja.

1. Msanifu jengo husika (Arch/Engineer); kwa kushindwa kuandaa na kuproduce structure analysis za hilo jengo ambazo ndio miongozo ya kipi fundi anatakiwa ajenge na kuzingatia.

2. Mmiliki wa jengo; Kama mmiliki alikuwa bahili, akataka dezo kujenga structure sensitive Kama ghorofa kwa kutumia mafundi tu bila wataalam wa usanifu Majengo, Basi matunda ya ubahili huo ndo hayo. Na hili ni tatizo kwa watanzania wengi, wanapenda Sana cheap na kurash mambo kuliko kufuata procedures zinazotakiwa.

3. Mafundi; hapa Kuna mawili,
Mosi, Yawezekana mafundi hawakuwa na uzoefu au ujuzi wa kujenga high structural building, ikiwemo kushindwa kutafsiri lugha ya kihandisi iliyopo kwenye sheets za raman, hasa structural plans ambazo huitaji akili nyingi kidogo kuzielewa specifications zake.

Pili; Wizi wa materials site, mafundi baadhi siyo waaminifu, unakuta sehemu inayotakiwa atumie ratio ya mortar 1:4 yeye anatumia 1:6 ili tu mifuko ya siment kadhaa apite nayo,
Au unakuta sehemu inayotakiwa kuwekwa zege la Grade 25 yeye anaweka 20 ili tu nondo na siment zitakazo baki ziwe faida yake. Au unakuta anatumia nondo 3 badala ya nne kwenye column au beam kama ilivyoshauriwa na mtaalam.

Ifikie mahali Sasa tuache uswahili kwenye mambo ya mhimu Kama haya ya ujenzi wa maghorofa, mambo ya kupeleka mambo kimazoea matokeo yake ndo hayo yaliyo tokea kwenye huo mpolomoko.
 
Engineer shusha technical issues acha perepeche
Back to Basics...
1638828543490.png


Ukiona hayo ni maleluweluwe basi hiki kifuata...

PPPPPPPPPPPPPPPP.gif


1638827415465.png
 
Natoa pole kwa wafiwa na wananchi wa kata ya #Goba kufuatia vifo vya watu wanne vilivyosababishwa na kuanguka kwa ghorofa lililokuwa linaendelea kujengwa katika kata hiyo.

Uchunguzi wa tukio hili zisiachiwe mamlaka za #WilayaYaUbungo bali uhusishe CRB, ERB, IET, AQRB na TISS.
 
Kwa kawaida mamlaka ziko makini Sana na ujenzi wa ghorofa yoyote. Sijui ilikuwaje wakaacha huu ujenzi wa kuungaunga ukaendelea. Makosa ya wengi hapo
1.Mmiliki
2.Mafundi
3. Mamlaka husika
 
Natanguliza poleza za dhati kwa wa hanga wa tukio hilo. MUNGU azilaze roho za marehemu mahala pema peponi. Majeruhi GET WELL SOON.

NANI ALAUMIWE KWA HILO?
....Mwenye Jengo!!!?
....Fundi/mkandarasi au
.....majirani ambao ndio wahaga zaidi.

NIKIWA KAMA MDAU WA UJENZI
Ningependa nitoe ushari huu ...

CHEAP IS EXPENSIVE



DEDICATION KWA CLIENT WOTE WAPENDA DEZO
Hamna hata picha mkuu?
 
View attachment 2035185

Watu wanne (Wanawake 2 na Wanaume 2) wameripotiwa kufariki dunia huku wengine 17 wakijeruhiwa baada ya jengo lililokuwa linajengwa eneo la Goba kwa Awadhi Jijini Dar es Salaam kuangukia nyumba za jirani

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James amesema wanaendelea kuangalia iwapo kuna wengine

Chanzo: ITV
Amejenga kwa kumtumia fundi Maiko, hata Serikali inamtumia fundi Maiko kwa Fosi Akaunti.
 
Kila siku napita hili eneo. Juzi tu nimetoka kusema hili ghorofa, mm siliamin kabisaa.

Iko hivi.
Hilo jengo lillianza kuinuliwa kuwa ghorofa wiki 2 zilizopita. Awali mchoro ulikuwa ni fremu za kawaida kama fremu nyingine barabarani. Sasa wiki 4 nyuma naona wakaweka bim, ambayo ina inchi 12 nadhan badala ya inch 30 kama ghorofa nyingne. Na kuanza kujenga kama ghorofa.
Kwahiyo ina maana msingi ule wa fremu za kawaoda haukuweza kuhimili uzito wa ghorofa iliyoongezwa , bado kuna uzito wa mbao na paa maana wameezeka hawana hata wiki.

Pia eneo lilijazwa kifusi. Nadhan na hii mvua maji yalizama chini na yakaleta joto baada jua kutoka.

Msingi amelaza tofali ila hajaweza nguzo nying, coz alijua ni fremu na sio ghorofa. kuanzia ground hajalaza tofali pia.

Kiufup kalaza tofali za msing tu. Bim nyembamba. Hakuna nguzo za kwenye kona.

Tatizo ni Eng/fund mkuu hajatoa ushaur vizur kwa tajiri.

Watu waliofariki ni zaid ya 10 nadhan.

RIP majiran zangu

Inasikitisha sana.
 
Back to Basics...
View attachment 2035336

Ukiona hayo ni maleluweluwe basi hiki kifuata...

View attachment 2035337

View attachment 2035333
Mkuu acha kuwachanganya watu.
Pale collapse imetaokana na poor or no design, naunder reinforcement .
Uzito mkubwa umewekwa kwa nguzo ambazo haziwezi kubeba mzigo wa ghorofa mbili.
Hiyo clip inayoonyesha swaying ground au hata seismic activity ni misleading, pengine ulikuwa unataka kuonyesha kitu kingine.

Hapo ni poor or no engineering design.
 
Inasikitisha, Mungu awapumzishe salama wapendwa wetu. Pole kwa familia zilizofikwa na maafa.
 
Back
Top Bottom