Goba, Dar: Wanne wafariki dunia, 17 wajeruhiwa baada ya jengo kuangukia nyumba za jirani

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
photo_2021-12-06_20-11-31.jpg

Watu wanne (Wanawake 2 na Wanaume 2) wameripotiwa kufariki dunia huku wengine 17 wakijeruhiwa baada ya jengo lililokuwa linajengwa eneo la Goba kwa Awadhi Jijini Dar es Salaam kuangukia nyumba za jirani

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James amesema wanaendelea kuangalia iwapo kuna wengine

Chanzo: ITV
===

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 17 kujeruhiwa baada ya jengo la ghorofa kuporomoka katika Kata ya Goba Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo (DC), Kheri James leo Jumatatu Desemba 6, 2021 amethibitishha kutokea kwa ajali hiyo, akisema baada ya jengo hilo lililokuwa linajengwa kuanguka limesababisha maafa kwenye nyumba zilizopo jirani.

“Katika ajali hii tunazo maiti nne, wanawake wawili na wanaume wawili na majeruhi wapo 17 waliopata majanga kutokana na jengo hili kuanguka” amesema DC James akiwa kwenye eneo la tukio.

Amesema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vipo katika eneo la tukio vikichukua hatua kuhakikisha kama kuna maafa mengine kwa binadamu.

“Mpaka sasa Jeshi la Zimamoto na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vipo katika eneo hili kuendelea na hatua za kuhakikisha kama waliojeruhiwa ni hao tu ama kuna ziada, lakini Serikali imechukua hatua kwa wale wote waliojeruhiwa hatua za matibabu zinaendelea” amesema DC James.

CHANZO: MWANANCHI
 
Watu wanne (Wanawake 2 na Wanaume 2) wameripotiwa kufariki dunia huku wengine 17 wakijeruhiwa baada ya jengo lililokuwa linajengwa eneo la Goba kwa Awadhi Jijini Dar es Salaam kuangukia nyumba za jirani

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James amesema wanaendelea kuangalia iwapo kuna wengine

Chanzo: ITV
Waziri wa nyumba na makazi yupo? TBS hamjambo? Nahisi majengo binafsi nao wamenza kutumia force account!
 
Back
Top Bottom