Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,152
Ukweli usemwe na usemwe wazi ili kila mtu aujue. Wigo wa watanzania kusoma mpaka chuo kikuu ili kupata degree umekuwa mkubwa lakini huo mfumo umekuwa ni hasara na upotevu wa rasimali (muda, pesa na nguvu) kwa 90%.
Ajira mtaani kwa 90% hakuna kwa fani nyingi, ni sawa na kucheza kamili, na elimu ya vyeti vya chuo kikuu haina mchango wowote wa mhitimu wa level ya degree kuweza kujiajiri moja kwa moja. Hapa chini ni baadhi ya fani zinazoangukia kwenye kundi hilo.
1. Public administration
2. Political science
3. Business administration
4. Procurement and supply
5. Human resource
6. Sociology
7. Environment
8. Language
9. Mass communication
10. Tourism
11. Banking
12. Accounting
13. Economy
14. Finance
15. History
16. Insurance
17. Tax
18. Cooperative
19. Marketing
20.
Kama wewe ni mhitimu wa hizo fani kwa miaka ya karibuni utaelewa hicho nilichokiandika, na kama wewe ni mwanafunzi wa hizo fani anza kujiandaa kisaikolojia, hali ni mbaya mtaani. Wahitimu ni wengi na hawana ajira yoyote, wamechoka vibaya, wameshazunguka na mabahasha mpaka soli za viatu kuchakaa, wamejitolea mpaka basi, wameshikiza mpaka wamedondoka na wengi wamekata tamaa kabisa, vyeti vyao wamesahau hata vipo wapi, havina msaada.
Bado wanakula, kulala na kutunzwa na wazazi wao, mashemeji au wajomba. Wengine wameamua kujiajiri katika fani zingine ambazo hazina uhusiano wowote wa fani walizosomea na zenye kuhitaji elimu ya darasa la nne tu.
Wajanja wengine wameamua kurudi chuo, hususani kwa ngazi ya Diploma kusoma fani za ualimu au afya ili kuingia kwenye mkondo wa kuja kupata ajira hapo baadaye.
Jamani hali ni mbaya na tete.
Ukweli usemwe!