Mabadiliko katika mfumo wa maombi ya ajira ni kero na uonevu kwa waomba ajira

Kushdon

Member
Jan 14, 2017
15
18
kero kubwa iliyopo kwa saa ni kwamba serikali imeamua kuanzisha sera ya kutumia mfumo wa maombi ya ajira kuhusika katika maombi ya kazi za serikali kwa ngazi zote ikiwemo kazi za maafisa watendaji wa vijiji na kata zinazotangazwa na halmashauri.

Kero iliyopo katika mfumo wa maombi ya ajira wa sekretarieti ya ajira ni kwamba kwa wale waliojaza profile na kueka elimu zao zote mpaka degree mfano, mfumo unagoma kuomba kazi ya ngazi za chini kama cheti na diploma.

Mfumo huu naona ni bora ubaki kwa wale wanaoomba nafasi zinazohitaji elimu ya degree na kuendelea ila uku diploma na cheti naomba sana serikali itufikirie na kutuangalia kwa jicho la pili kwani mfumo huo hauturuhusu kuomba kazi za ngazi ya chini kwa wale tuliofika mpaka ngazi ya degree.

Zamani mfumo huu ulikua unaturuhusu kufuta baadhi ya elimu ilikueza kuomba kazi ya ngazi ya chini kama diploma na cheti ila kwa sasa haiwezekani kubadilisha na unatutenga sana wale ambao tulianzia cheti mpaka kufika degree au zaidi.

Ushauri wangu kwa serikali ni kwamba waweke mfumo huo wa maombi ya ajira ukubali kuomba kazi yeyote ata kama ni ngazi ya sekondari pekee bila kujali viwango vingine vya elimu ili kutusaidia katika kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa wahitimu wa ngazi mbalimbali, au waache mambo yalivyo kwa sasa tuendelee kuomba kazi za halmashauri kwa kutuma barua posta ili tuhusike ata na sisi tuliosoma ngazi za cheti na diploma.
 
Huo mfumo ndio mzuri sasa,kama ni kweli uko hivyo

Inakuwa kama haki sawa kwa wote...mwenye diploma hawezi kuomba kazi za degree na wa degree asiombe nafasi za diploma
 
Tamaa una degree unataka kazi ya diploma...

Mkuu umekurupuka? Soma vzr utaelewa, ameandika mfumo una identify the highest level of education only. Kama ulisoma diploma ukajiendeleza, basi dip inakuwa nullified kwa kuwa degree ndio ina-surpass other prior qualifications
 
Back
Top Bottom