Nimerejea tena wakuu, nahitaji kazi

Feb 15, 2021
72
82
Habari za majukumu waungwana!
Mimi ndugu yenu mwanafamilia wa Jamii Forum nimerejea tena nikihitaji kazi. Mimi ni mhitimu wa shahada ya kwanza ya Sayansi Akua na Uvuvi (Aquatic Sciences and fisheries) katika chuo kikuu Cha Dar es salaam mwaka 2020. Umri wangu ni miaka 27, mwanaume na mkazi wa Ubungo, Dar es salaam

Nilipoteza kazi niliyokuwa nayo mwaka jana mwezi Septemba na baada ya hapo sijapata kazi ya kueleweka. Niliamua kwenda kujitolea katika taasisi moja ya kiserikali ( halmashauri) katika fani yangu ambapo nipo mpaka leo. Changamoto kubwa ni kuwa kupata pesa ya kujikimu ni ngumu sana yaani sana na nimekuwa nikilazimika kutumia akiba yangu niliyokuwa nayo na imeisha kabisa mwezi Januari mwaka huu na sina kitu kabisa.

Nimeomba sana kazi zinazoendana na zisizoendana na fani yangu niliyosomea ila sijabahatika kuitwa hata kwa usaili. Yaani maombi zaidi ya 20 sijaitwa hata moja! Imefikia hatua nimevunjika moyo sana.

Nimekuja kwenu Tena kwa mwenye koneksheni ya kazi au wazo lolote naomba anipatie, mbali na fani yangu ninaweza kufanya kazi ya sales, monitoring, marketing, educating and teaching, data collection and analysis, n.k. Pia ninafundishika kwa uharaka maana yake ninaweza kupata mafunzo katika fani yoyote na naikafanya kazi.

Namba yangu ya Whatsapp ni 0757942975 na nyingine ni 0656208659 na 0684739082

Asanteni
 
Kuna madogo wengi wa fani yako naona wamejiajiri kwenye miradi ya kuzalisha, kufuga na kuvuna samaki, sijajua nguvu ya uwekezaji wa hiyo miradi lakini naona inawalipa sana, umeshawahi kufuatilia huko mkuu??
 
Si lazima ukaanzisha mradi mpya bali unaweza kuomba kujoin na kuwekeza nguvu kazi katika miradi iliyokwisha anza inaweza kukutoa kutoka sehemu moja kwenda nyingine, sishauri uendelee kupoteza muda hapo serikalini infact mimi sio mdau wa kuajiriwa ningekushauri uangalie kwenye miradi ama taasisi nyingine tofauti na serikalini.
 
Habari za majukumu waungwana!
Mimi ndugu yenu mwanafamilia wa Jamii Forum nimerejea tena nikihitaji kazi. Mimi ni mhitimu wa shahada ya kwanza ya Sayansi Akua na Uvuvi (Aquatic Sciences and fisheries) katika chuo kikuu Cha Dar es salaam mwaka 2020. Umri wangu ni miaka 27, mwanaume na mkazi wa Ubungo, Dar es salaam

Nilipoteza kazi niliyokuwa nayo mwaka jana mwezi Septemba na baada ya hapo sijapata kazi ya kueleweka. Niliamua kwenda kujitolea katika taasisi moja ya kiserikali ( halmashauri) katika fani yangu ambapo nipo mpaka leo. Changamoto kubwa ni kuwa kupata pesa ya kujikimu ni ngumu sana yaani sana na nimekuwa nikilazimika kutumia akiba yangu niliyokuwa nayo na imeisha kabisa mwezi Januari mwaka huu na sina kitu kabisa.

Nimeomba sana kazi zinazoendana na zisizoendana na fani yangu niliyosomea ila sijabahatika kuitwa hata kwa usaili. Yaani maombi zaidi ya 20 sijaitwa hata moja! Imefikia hatua nimevunjika moyo sana.

Nimekuja kwenu Tena kwa mwenye koneksheni ya kazi au wazo lolote naomba anipatie, mbali na fani yangu ninaweza kufanya kazi ya sales, monitoring, marketing, educating and teaching, data collection and analysis, n.k. Pia ninafundishika kwa uharaka maana yake ninaweza kupata mafunzo katika fani yoyote na naikafanya kazi.

Namba yangu ya Whatsapp ni 0757942975 na nyingine ni 0656208659 na 0684739082

Asanteni
Nenda viwandani hukosi kazi
 
Kuna madogo wengi wa fani yako naona wamejiajiri kwenye miradi ya kuzalisha, kufuga na kuvuna samaki, sijajua nguvu ya uwekezaji wa hiyo miradi lakini naona inawalipa sana, umeshawahi kufuatilia huko mkuu??
Uko sahihi mkuu, ni kweli vijana wanajihusisha na hiyo miradi lakini penyewe sio rahisi sana. Kuna kampuni ambazo zinahitaji wataalamu wa hayo mambo lakini mara nyingi inakulazimu uprove experience kwao kwanza kabla hawajaanza kukulipa kama expert; Kuna wengine wanafanya kutoa elimu kwa wafugaji na ambacho inahitaji kuji-brand kwanza maana wafugaji wengine wanapata hasara! Huko kuji-brand inahitaji muda na uwekezaji kidogo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom