BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,413
- 8,199
Leo Januari 31, 2023 Rais Samia amezungumzia suala la Plea Bargain, utaratibu wa Makubaliano ya Kumaliza Kesi kwa Kulipa Fedha kwa Serikali ambao ulitumika wakati wa Utawala wa Hayati Rais Magufuli chini ya DPP Biswalo Mganga aliyeondolewa na kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, huku akieleza kuwa Suala hilo limekuwa na utata ikiwemo baadhi ya pesa zilizolipwa kwenye akaunti zimeoneka kupelekwa Nchini China.
Ukiachana na hilo Jaji Biswalo amekuwa kwenye kashfa nyingi ikiwemo kuchukua mali za washtakiwa bila utaratibu wenye uwazi, bila uwepo wa sheria na akaunti maalumu ya Serikali inayokusanya fedha hizo.
Sasa kwa hili la leo, Jaji Biswalo anasubiri nini kuachia nafasi hiyo kuonesha Uwajibikaji? Lakini Pia, Rais Samia anasubiri nini kuunda Tume ya Majaji watatu wanaotakiwa kuchunguza suala hilo na kutoa uamuzi wa nini Rais afanye?
Anyway Taifa linasubiria ripoti ya matumizi ya fedha zaidi ya Tsh. Bilioni 50 zilizotokana na makubaliano ya washtakiwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), Rais Samia Suluhu Hassan amesema ofisi hiyo ilipitia kipindi ambacho kuna michezo ilikuwa inafanyika ambayo iliharibu taswira ya taasisi hiyo.