Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,788
- 218,415
Bado twaendelea na nyuzi za mwezi 3 ambao ni Mwezi wa Mungu
Kama tulivyoandika awali kuhusu lundo la watu kukamatwa na kupewa kesi nzito za Uhujumu uchumi , Baadaye watu hao wakapewa option ya kurudi uraiani ambayo ni kukiri makosa na kulipa kiasi kizito cha fedha ili kufidia uchumi waliouhujumu .
Wengi kutokana na uoga na kuchoshwa kukaa jela wakaamua kukubali jambo hilo bila kujali kama lipo kisheria au ni matakwa ya Wakamataji , wale ambao walikuwa na mzigo mkubwa kwenye akaunti zao ukapigwa chakachua juu kwa juu , wale wenzangu na miye , ikalazimika ndugu zao kujikamua na kuchangishana kwa kuuza hiki na kile , zikiwemo nyumba , mazao na mashamba ili kuwaokoa ndugu zao , wamo hata wauza bia waliokamatwa kwa makosa ya kodi tu lakini wakapewa Uhujumu uchumi (soma ripoti ya CAG hii hapa)
Pamoja na DPP kuwa Mwanasheria lakini bado alivunja Sheria na wala hakuguswa
Kwenye kampeni hii haramu Biswalo Mganga alishirikiana na wafuatao kwa karibu sana , japo kuna mnyororo mrefu
Hata hivyo lundo la hela walizokusanya hazikujulikana ziliwekwa kwenye akaunti gani , hii ni kwa mujibu wa serikali mpya iliyoingia madarakani baada ya Magufuli
Sasa ikiwa kama Nchi inaweza kuwa na kikundi cha watu wakaamua kupanga mambo yao kwa kutumia Mahakama zetu na wakavunja sheria , hata kama walikuwa wanazuia uhalifu jambo lao linakosa Uhalali .
Cha kushangaza ni hiki , Pamoja na makosa yote haya , ilikuwaje Rais wa sasa ameendelea kumteua Biswalo kwenye nafasi zingine ? siri hii anaijua mwenyewe .
Swali letu ni hili PLEA BARGAIN ilianzishwa kwa faida ya nani na pesa zilizokabidhiwa ziko wapi ?
NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO