Hali ya kisiasa nchini inaendelea kuwa tete huku watu wengi zaidi wakiendelea kukosa imani na mchakato wa uchaguzi kila kukicha. Kiufupi Polepole ambaye ni kada wa ndani wa CCM emeendelea kuwafungua macho watanzania huku shauku ya kumsikiliza ikizidi kukua kila pahali.
Komredi Polepole amefungua mapya usiku wa jana na kuonesha mbinu kubwa inayotumiwa na chama tawala kushinda chaguzi zilizopita na hata zijazo. Watu wengi mtaani wameonesha kushangazwa lakini pia kuamini kuwa ni ndoto kwa CCM kuondolewa madarakani kwa tume hii ya uchaguzi na mfumo mzima wa utawala wa nchi.
Ni vyema na busara sana kama rais Samia akasoma alama za nyakati mapema na kutafuta maridhiano ya kweli na upande wa upinzani kuhusu madai ya msingi ya vyama vya upinzani kabla hajachelewa na kulazimika kufanya hivyo bila kupenda.