Kutoka Dodoma!

Kutoka Dodoma!

Huu ni mtazamo wako Mkuu, lakini kuna wengi kama shy na kibunango ambao wanaona bado CCM bado wako katika mstari. Na halafu kuhusu upinzani naona bado kabisa na kama Wtz watawakubali bas ni kwa makosa ya CCM na sio kuwa wapinzani wana dira inayojulikana ya kuiendeleza nchi hii.


Ok, hiyo dira ya CCM ya kuwashinda wapinzani ni ipi hasa?
 
Hapa kiletwe hako kapande cha kideo clipu tuone na mafundi wetu nao waingie mitamboni kukichuja hadi tupate sura,wacha yote hayo,inatosha kuona vitendo kama ni vya kusoma jina au vya kufukuza inzi ,sasa kilichompeleka mtu huyo kwenye kiti cha spika ,hivi pale ipo nafasi kwa wabunge ambao hawana cheo cha kuwafanya wawepo pale ,au ni katika kutafuta cheo chengi labda aundiwe kikamati cha kuratibu mambo ya bunge. Bado hawajatueleza ila sasa tunangojea kutibuliwa na polisi ,maana mkiupata huo mkanda wa kideo kwanza msiuweke hapa ngojeni jamaa watakavyojaribu kutibu hilo donda ndugu.
 
Mkuu Heshima mbele, according to the dataz kuna mengi yaliyojiri na yanayoendelea kujiri:-

1. Wahusika wote wa Richimonduli wameitwa tena kwenda kujibu maswali kwa Taukukuru, ikiwa ...........QUOTE]


Kaka, Naomba nikiri wewe ni kiboko kwa kuleta issues. Hiki kijiwe nakiheshimu kutokana na watu kama nyie. Jamani mambo kama haya tungeyapata wapi wajameni. Ningekuwa namjua aliyeanzisha hii kitu ningemkatia kafungu kadogo kama premium. By the way how can i contribute in monentary term for the existance of this kijiwe. Samahni bado mie mshamba mshamba hapa wakuu msije mkanielewa vibaya.
 
Mnapatia kweli ku spend muda mwingi on Chenge, Kamera, uchawi, sumu, kimeta nk katika kipindi ambacho tulitakiwa kwa nguvu zetu zote tujadili bajeti, EPA, Richmond, Meremeta ( sijui hata kama mnakumbuka) etc

Haya twendeni tutafika tu...... bring in more DATAZ!
 
Mnapatia kweli ku spend muda mwingi on Chenge, Kamera, uchawi, sumu, kimeta nk katika kipindi ambacho tulitakiwa kwa nguvu zetu zote tujadili bajeti, EPA, Richmond, Meremeta ( sijui hata kama mnakumbuka) etc

Haya twendeni tutafika tu...... bring in more DATAZ!
Wametangaza kwamba hii ni halftime huoni kwamba inapaswa kutazama na kurekebisha na kuvuta mawazo tukisikiliza namna wanavyojipanga maana kama hao marisavu wao wangekuwa ni wachezaji wazuri basi wangeliwapanga katika kipindi cha mwanzo ila tokea mechi ianze wameshabadilisha wale waliokuwa wanatisha.Na wanaowaingiza wanagombana wenyewe kwa wenyewe ,tulia kubwa lijalo.
 
Ninapata sasa hivi sms inasema Chenge ndiyo zake na ndiyo maana hata baada ya Mwanyika kukalia kiti chake baada ya yeye amekuwa kama zezeta anasoma haelewi anaambiwa hasikiii na sasa aliona anaweza kufanya zali kule jumbani .Si mimi ni vi Lunyungu @ work .

......EBoo yamezuka tena hayo.Jamani kweli kuna mambo BOngo. Sawa Wakuu leteni habari!
 
Mnapatia kweli ku spend muda mwingi on Chenge, Kamera, uchawi, sumu, kimeta nk katika kipindi ambacho tulitakiwa kwa nguvu zetu zote tujadili bajeti, EPA, Richmond, Meremeta ( sijui hata kama mnakumbuka) etc

Haya twendeni tutafika tu...... bring in more DATAZ!



Sasa mkuu wangu tutafanyaje ??ndio hali yenyewe ,kinachokuja kwenye anga zetu kwa wakati mwafaka na pia ikiwa kina maslahi ya wananchi-tunadili nacho kwanza ....then tuaangalia mbeleeee
 
Mnapatia kweli ku spend muda mwingi on Chenge, Kamera, uchawi, sumu, kimeta nk katika kipindi ambacho tulitakiwa kwa nguvu zetu zote tujadili bajeti, EPA, Richmond, Meremeta ( sijui hata kama mnakumbuka) etc

Haya twendeni tutafika tu...... bring in more DATAZ!
Masatu,
Unachokisema ni sawa na kusema eti kwa sababu ni muda wa chai, basi tuhangaike kuinywa hiyo chai ingawa kikombe ndani ni kichafu. Siye tunasema kwamba hiyo chai na iachwe hadi kikombe kiwe kisafi na maji ya kuosha yawepo na si leo tu ila kwa muda mrefu ujao. Waafrica tumekuwa na macho ya chatu. Heri ya chatu anasikia kishindo kwa mbalii. Inabidi tujiweke chini na tusafishe kila kitu na kuweka mikakati ili huko mbeleni upupu upungue. Hata ukikaa na kuijadili bajeti, unafikiri utabadilisha kitu? Peter Tosh aliimba kuwa "kila mtu ataka kwenda mbinguni ila hakuna anayetaka kufa". Kwa hiyo ili tufike mbinguni inabdi TUFE kwanza. Hapa hatujali bajeti wala Uchawi. Siye leo ni UFISADI kwanza na kila inapopatikana mwanya basi tutaingiaMO wote na kukoromboaMO humo ndaniNI hadi kieleweke. Lengo hapa ni moja MAFISADI WAANGAMIZWE ili iwe fundisho kuwa wee iba tu ila siku moja ...... Wimbo huo wa Tosh unaongezea kuwa ".... I don't want piece, i don't want freedom, I'M JUST CRYING FOR JUSTICE ..." Bila "Equal right and justice walau 40% kwa wanyonge" basi ujue siku zote Wanyonge watafungwa 666 kwa 13. Nafikiri wajua FISADI ni 666 na 13 ni gundu (Wadanganyika).
 
Huu ni mtazamo wako Mkuu, lakini kuna wengi kama shy na kibunango ambao wanaona bado CCM bado wako katika mstari. Na halafu kuhusu upinzani naona bado kabisa na kama Wtz watawakubali bas ni kwa makosa ya CCM na sio kuwa wapinzani wana dira inayojulikana ya kuiendeleza nchi hii.

Umesha sema wapinzani hawana mwelekeo na wewe unaujua mwelekeo , hawajakataa kukuokea na kukusikiliza mbona unalia lia ukiwa mbali ? watafute omba kuweka mawazo yako uone kama wataya incorporate na kuanza kujenga mwelekeo badala ya kulia lia .

Au unasemaje ?
 

Labda hii ni update


Aliyeingia bungeni usiku atajwa




na Martin Malera, Dodoma



KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kapteni John Chiligati, jana alimtaja mbele ya waandishi wa habari mbunge ambaye aliingia katika ukumbi wa Bunge jioni ya Jumatatu.

Tukio hilo linahusishwa na ushirikina kwa mujibu wa taarifa zisizo rasmi, ambazo zimekuwa zikisambaa kwa muda wa siku tatu zilizopita.

Ingawa hakumtaja kwa jina, Chiligati alisema kuwa mbunge huyo alikuwa waziri lakini sasa hana tena wadhifa huo.

Akifafanua, Chiligati alikiri kuwa mbunge huyo aliomba na kupewa ruhusa kuingia ndani ya ukumbi huo wa Bunge, ili kukagua na kuangalia nafasi atakayokuwa anaketi.
Alisema kuwa mbunge huyo alilazimika kufanya hivyo kutokana na kutokuwa na kiti maalumu cha kukalia ndani ya Bunge kutokana na kuondoka kwake kutoka katika wadhifa wa uwaziri.

Chiligati alisema kwamba, kwa kuwa Bunge lilikuwa linaanza vikao vyake siku inayofuata, mbunge huyo aliona ni busara kutafuta mahali pa kukaa jioni hiyo, ili asisumbuke asubuhi.

Alikiri kuwa ni kweli aliingia ndani ya ukumbi wa Bunge na kupita katika kila kiti, akiangalia majina kwa lengo la kutafuta kiti kilichokuwa wazi.

Alisema wakati akifanya hivyo, hakuweka uchawi wowote kama ambavyo inadaiwa na watu hivi sasa.

Kwa taratibu za Bunge, kila kundi ndani ya Bunge hilo lina mahali pake maalumu pa kukaa kwa mpangilio unaoeleweka. Makundi hayo ni pamoja na mawaziri, ambao huketi upande wa kuume kwa Spika, wapinzani, ambao huketi upande wa kushoto wa Spika na wabunge wengine ambao hukaa katika nafasi zilizosalia.

Chini ya utaratibu huo, mpangilio wa kukaa hupangwa mwanzoni mwa Bunge, ambapo kila mbunge hupangiwa kiti chake cha kukaa. Hata hivyo, wabunge wanaruhusiwa kuhama kwa muda kwenda eneo jingine na wanapomaliza dharura hiyo hurejea kwenye viti vyao.

Spika Samuel Sitta, naye alishathibitisha kuwa, zipo picha zinazomuonyesha mbunge huyo akiwa ameandamana na mtumishi mmoja wa Bunge, akipita katika viti kadhaa ndani ya ukumbi huo wakati ukiwa umefungwa.

Ingawa Sitta na Chiligati waliepuka kumtaja mbunge huyo kwa jina, lakini kiongozi ambaye alikuwa waziri na kujiuzulu katika siku za hivi karibuni ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.

Chenge alijiuzulu kutokana na kuhusishwa kwake kwenye uchunguzi unaoendeshwa na Taasisi ya Kuchunguza makosa ya rushwa ya Uingereza (SFO).

Makachero wa SFO walivutika kumchunguza Chenge katika uchunguzi wao dhidi ya Kampuni ya Bae Systems ya Uingereza iliyoiuzia Tanzania rada kwa bei ya juu.

Licha ya kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati mkataba wa mauzo hayo unafikiwa, makachero wa SFO walimkuta Chenge akiwa na akiba ya takriban dola za Marekani milioni moja kwenye akaunti iliyo katika benki moja katika visiwa vya Jersey.

Tangu ajiuzulu nafasi hiyo, Chenge hajawahi kuhudhuria vikao vya Bunge, na ni kweli hivi sasa anawajibika kutafuta nafasi ya kukaa kwa kuwa hataweza tena kukaa katika nafasi ya mawaziri aliyokuwa akikaa zamani.

Tukio hilo limewaweka wabunge roho juu, hasa baada ya Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, kuugua ghafla katikati ya wiki iliyopita na kulazimika kukimbizwa katika kliniki ya Bunge ili kupata huduma za kiafya.

Wabunge kadhaa sasa wanaonekana kuogopa kuusogelea ukumbi wa Bunge, kutokana na taarifa hizo za kuwepo kwa vitendo vya kishirikina.

“Hili tukio limetutia hofu, tunadhani kuna kila sababu ya kukamilisha uchunguzi wa tukio hili mapema. Spika ameeleza kuwa tukio hili linachunguzwa, tunaomba lichunguzwe kweli, tena kwa haraka, ili kutuondolea hofu tuliyonayo sasa,” alisema mmoja wa wabunge kutoka Mkoa wa Mwanza.

Mbunge mwingine ambaye pia hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alilieleza gazeti hili kuwa Spika anapaswa kutoa taarifa ya tukio hili bungeni na kulitolea ufafanuzi badala ya kuendelea kulizungumza kwenye vyombo vya habari.

“Hizi taarifa zipo, wabunge wengi wanazijua, lakini Spika analizungumzia kwenye vyombo vya habari. Mimi nadhani suala hili linagusa maisha yetu, ni bora akalieleza Bunge nini kilitokea,” alisema mbunge huyo.

Akizungumza na waandishi juzi, Sitta alisema kuwa, ofisi yake imekabidhi picha za video zilizomnasa mbunge huyo akiwa ameambatana na Ofisa Mwandamizi wa Bunge kwa siri, waliokuwa wakiweka vitu vinavyoaminika kuwa vya kishirikina au aina fulani ya sumu kwenye kila kiti cha mbunge.

Kwa mujibu wa Sitta, picha za mkanda huo zilizonaswa na kamera za usalama zilizomo ndani ya jengo hilo la kisasa, zimefifia kiasi cha kushindwa kubaini kwa haraka watu wanaoonekana ndani ya mkanda huo.

Kutokana na hali hiyo, Sitta alisema ofisi yake imeamua kuukabidhi mkanda wa picha hizo kwa maofisa usalama wa taifa na kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, kwa ajili ya kuzifanyia uchunguzi zaidi

Hii habari inasema kuwa Chenge alikuwa anatafuta kiti cha kukaa lakini wanazi mmeshika bango tu kuwa ni mambo ya uchawi? Sasa mlitaka Chenge akae wapi - chini au nje ya bunge?
 
mkitaka kutuzuga tuzugeni, lakini mkituzuga hakikisheni tunazugukika..

Baada ya Chenge kujiuzulu si alirudi alikokuwa anakaa mwanzoni kabla ya kuteuliwa Waziri? Kwani alipoingia Bungeni kabla ya kuwa Waziri alikuwa anakaa wapi mwanzo? si hapo aliporudi baada ya kujiuzulu? Ushahidi si huu hapa:

karamagi004.jpg


Sasa hiki kiti kingine anakitafuta kwa minajili gani wakati kiti chake alichokuwa nacho mwanzo (kabla ya kuwa Waziri) na ambacho alikirudia baada ya kuondoa bado kipo?

Nawashauri waje na kisingizio kingine. Please, jitihadini kidogo katika kuzuga
basi...



Man you got brains of several people. Big up! I neva thought of that!
 
Kama ni kitu kidogo namna hii kwa mtizamo wao ambacho just wanted clarification why took them too long hadi hivi sasa ndiyo wanasema baada ya kujipanga ? Nawakumbusha hakuna utawala wa mabavu ulidumi miaka million .CCM nyie laana kubwa inawaandama .
 
Naona sasa nilipue:

...Kuna mtu nimezungumza naye ninamuamini asilimia 100, na akisoma JF atanijua ni mimi lakini sasa naamua kumwaga mchele mazungumzo yetu na yeye kuhusu tukio hilo.

Huyo jamaa alikuwapo Dodoma kwa dharura Jumanne wiki hii na kurejea Dar Alhamisi Asubuhi, nikahisi safari yake ina uhusiano na tukio husika nikambana anieleze kilichotokea huko Dodoma na maelezo yake leo hii yalikua kama ifuatavyo:

"Nilikutana na Katibu wa Bunge, Tom Kashilila usiku wa Jumatano, muda mfupi baada ya kukutana na Kaimu Mkuu wa Usalama wa Bunge, aitwaye Magati. Magati alishituka kuona kwamba hakuwa amejulishwa na wakubwa zake kuhusu kitendo cha Chenge kudaiwa kuingia ndani ya Ukumbi wa Bunge. Akiwa Mkuu wa USalama, alipaswa kujua kila kitu. Alichanganyikiwa na kuingia kazini usiku huo. Kwa upande wake, Katibu wa Bunge alisema wanafanya uchunguzi wa kina kuhusiana na suala hilo kwani kwa uzoefu wake wa kimataifa🙂)), upo uwezekano wa kuwapo vitu hatari. Aliahidi kutoa taarifa kadiri zitakavyopatikana. Baadaye usiku wa manane akanitumia sms kusema kwamba wametoka kukagua kamera za usalama wameshindwa kuona kitu na kwamba siku itakayofuata wataendelea na kuzipitia tena. Baadaye akaja na maelezo kwamba wameshindwa kuthibitisha lolote kwa kuwa kamera zao zilikua zimezimwa. Alipoulizwa kama wamewahoji Chenge na Sagasii akasema hatuwezi kuwahoji kwa kuwa hakuna ushahidi. Ajabu mashahidi muhimu/wahusika unakataa kuwahoji wakati wao ndio wanatakiwa kuanza kuhojiwa. Baadaye Katibu akaongea na mwandishi wa habari akamwambia kwamba wao kamera zao zinakuwa wazi 24hrs lakini wamekagua hawakupata ushahidi wowote. Sagasii anaulizwa na waandishi anasema hajui lolote kwa kuwa hajaarifiwa wala kuulizwa na yeyote. Watu wa STAR TV wanashangaa wao walikuwapo juu wakati huo wakiandaa vifaa vyao kwa ajili ya Jumanne Oktoba 10 lakini hadi leo hawajaulizwa na yeyote. Huku kuna taarifa polisi na usalama wanafanyia kazi mara wamemhoji Chenge, sasa which is which?" MWISHO WA KUNUKUU NA ATANISAMEHE ALIYETAMKA MANENO HAYA MAANA NAONA NI MUHIMU WATU WAJUE NINI KINACHOENDELEA. Naamini akisoma atajua ni mimi kama hatosoma ataulizwa na wahusika ambao amezungumza ama kufanya nao kazi. ATANISAMEHE KWA MASLAHI YA TAIFA

Halafu jumlisha na hii:-

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta, jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa, ofisi yake imekabidhi picha za video zilizomnasa mbunge huyo akiwa ameambatana na Ofisa Mwandamizi wa Bunge kwa siri, waliokuwa wakiweka vitu vinavyoaminika kuwa vya kishirikina au aina fulani ya sumu kwenye kila kiti cha mbunge.

Sitta alitoa kauli hiyo baada ya kutakiwa kutoa ufafanuzi juu ya tukio hilo ambalo hivi sasa limewachanganya baadhi ya wabunge kiasi cha kuhofia kuingia na kukalia viti vyao ndani ya ukumbi wa Bunge kabla ya uchunguzi kubaini kitu kilichowekwa.

Kwa mujibu wa Sitta, picha za mkanda huo zilizonaswa na kamera za usalama zilizomo ndani ya jengo hilo la kisasa, zimefifia kiasi cha kushindwa kubaini kwa haraka watu wanaoonekana ndani ya mkanda huo.

Kutokana na hali hiyo, Sitta alisema ofisi yake imeamua kuukabidhi mkanda wa picha hizo kwa maofisa usalama wa taifa na kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, kwa ajili ya kuzifanyia uchunguzi zaidi.

WAZI Kuna yafuatayo:

(1) Dini nyingi tulizo nazo hivi sasa zimetoka nje ya nchi zetu. Kuna dini ambazo hufanya MAOMBI kukiwa na matatizo, kuna dini hufanya VISOMO na kuna nyingine HUFUNGA, etc.
Dini za kiafrika ni nyingi na inaelekea bado tuna wenzetu ambao kisirisiri bado wanaamini matambiko. Circumstances ndio tatizo, lakini kuamini matambiko ni imani na haki ya mtu.

(2)Kama kuna "substance" ilinyunyizwa, tunahitaji mkemia atupe ni chemical gani. Tuna wabunge wanaotuwakilisha na hatuhitaji "mhanga" mmoja aondoke nao (kama ilikuwa "radioactive" obviously aliyekuwa ananyunyiza nae aliadhirika).

(3) Spika kukosa busara katika ku"deal" na sakata zima. Yeye na ofisi yake wangeweza kabisa kulifikisha suala hili kwa vyombo husika ili lifanyiwe uchunguzi kabla ya kubwabwaja. Ameonyesha wazi kwamba alifurahia "kumfuma" Chenge kwenye zile video...(soma highlighted sentences to see how security was left behind by politicians and then recalled after they had finished their political assasination statements)

(4) Hili sakata haliwezi kuwa tambiko bali ushirikina kama lilifanyika, kwani lilifanyika kwa siri.
 
Masatu,
Unachokisema ni sawa na kusema eti kwa sababu ni muda wa chai, basi tuhangaike kuinywa hiyo chai ingawa kikombe ndani ni kichafu. Siye tunasema kwamba hiyo chai na iachwe hadi kikombe kiwe kisafi na maji ya kuosha yawepo na si leo tu ila kwa muda mrefu ujao. Waafrica tumekuwa na macho ya chatu. Heri ya chatu anasikia kishindo kwa mbalii. Inabidi tujiweke chini na tusafishe kila kitu na kuweka mikakati ili huko mbeleni upupu upungue. Hata ukikaa na kuijadili bajeti, unafikiri utabadilisha kitu? Peter Tosh aliimba kuwa "kila mtu ataka kwenda mbinguni ila hakuna anayetaka kufa". Kwa hiyo ili tufike mbinguni inabdi TUFE kwanza. Hapa hatujali bajeti wala Uchawi. Siye leo ni UFISADI kwanza na kila inapopatikana mwanya basi tutaingiaMO wote na kukoromboaMO humo ndaniNI hadi kieleweke. Lengo hapa ni moja MAFISADI WAANGAMIZWE ili iwe fundisho kuwa wee iba tu ila siku moja ...... Wimbo huo wa Tosh unaongezea kuwa ".... I don't want piece, i don't want freedom, I'M JUST CRYING FOR JUSTICE ..." Bila "Equal right and justice walau 40% kwa wanyonge" basi ujue siku zote Wanyonge watafungwa 666 kwa 13. Nafikiri wajua FISADI ni 666 na 13 ni gundu (Wadanganyika).

Sikonge ,

Tatizo ni kuwa by the time tunapata hicho "kikombe kisafi" breakfast time imeisha na ni lunch-time au pengine dinner-time! Sasa kwanini tusitumie kifuu kuinywa hii chai kabla time haija elapse?
 
Mkuu Heshima mbele, according to the dataz kuna mengi yaliyojiri na yanayoendelea kujiri:-

1. Wahusika wote wa Richimonduli wameitwa tena kwenda kujibu maswali kwa Taukukuru, ikiwa ...........QUOTE]


Kaka, Naomba nikiri wewe ni kiboko kwa kuleta issues. Hiki kijiwe nakiheshimu kutokana na watu kama nyie. Jamani mambo kama haya tungeyapata wapi wajameni. Ningekuwa namjua aliyeanzisha hii kitu ningemkatia kafungu kadogo kama premium. By the way how can i contribute in monentary term for the existance of this kijiwe. Samahni bado mie mshamba mshamba hapa wakuu msije mkanielewa vibaya.

Kaka,
Just give a ring to +255 71 3 444 649 he will direct you. Asante sana kwa nia njema ya kukiendeleza kijiwe!
 
Mkandara

sisi wenda hua si wagunduzi kwa sababu kitu tukikiona cha staajabisha tunakita imani.

UCHAWI si imani Ni sayansi ambayo bado tafiti zake hazijatoa majibu hii ni kutokana na Techonojia tuliyonayo hajikomaa ila theory zipo za kutosha,Ni kama vile theory za fibre optics zilikuwepo karne nyingi ila implementation ilikua ngumu kutokana na technolojia wakati huo haijakomaa.

kifupi.
electrons hua zinaishi kwenye valency band ktk maada yoyote lakini hiyo maada ukiipa energy mfano mwanga,moto,chemical(uchawi,kemia) hua electorn inaruka na kwenda kwenye condunction band,sasa basi electorn ikipoteza hiyo energy inaanguka kutoka conduction hadi valency band na nguvu iliyopotea inapaa hewani kama photons.

Na kwa vile electrons hua zinatofautiana energy vivyo hivyo photons hewani zitatofautiana energy na hii energy ndio ina characterize masafa (frequency) yake ,sasa basi hili bando la photons lililo na energy tofautitofauti huitwa spectrums,Na photon zenye energy kubwa ndizo zina frequency kubwa kumbe basi spectrum sio continuous bali discrete.

Sasa basi ktk bando hili la photons(spectrum) wanasansi ambacho wameshaona ni-
1.Radio wave 0.3-3KHz ambazo ndio masikio ya mtu yanaweza sikia,hivyo electron yoyote iliyo ktk masafa hayo masikio ya mtu yanausikia mwendo huo.

2.microwave 3-300kHz electrons iliyo ktk masafa hayo inaweza kuchemsha maji .hapa watu wengi hujiuliza kwanini ukiweka chakula kwenye microwave ni chakula tu ndio kina pata joto walakini chombo hakipati joto.kumbuka michrowave inachemsha maji tu kumbe chakula kinachemka kwa sababu kina majimaji.
3.Light 3-30GHz electrons ktk masafa hayo inatoa mwanga ambao macho ya binadamu unaweza kuyaona.
4.infrared
5.ultraviolet
6.x-ray 30-300PHz hii inaweza penyeza kwenye nyama na ndio elecrons zilizo ktk mwendo huo hua zinatumika kule hospitali kupiga x ray
7.gamma ray 30-300 EHz

Sasa basi Wataalamu wa jadi hua wanatumia chemical means (kuchanganya miti,nyama ya mtu,ubongo wa mtu)kuzirusha electrons ambazo hua zinapaa ktk spectrums with very specific frequency ambazo hazipo hapo juu Na

zinakua ktk makundi mawili 1. kuyahadaa macho na akili ya binadamu yani hizi photons zikigonga akili na macho kinafanyika modulation yani signal inahamisha frequency iliyozoa macho ama akili ndio maana badala ya mtu unaweza ona mbuzi badala ya karatasi unaweza ona fedha(mazingaombwe) mfano mtu akikupiga ngumi vizuri ktk macho unaweza ona shimo refu sehemu iliyotambalale,kumbe hii ni energy aliyo apply ktk macho ni sawasawa tu na energy ya electrons ila tofauti ziko ktk form tofauti ya energy moja ni mechanical nyingine ni electromagenet.

2.Ni hiyo ya kudhuru ambayo unaiua cell za binadamu kama ilivyo tu neuclear,x-ray ama gamma-ray.

Na kumbuka kila kitu cha moto kinatoa (emmit) microwave ndio maana upo unajotojoto na kila mwili unakua ktk resonance frequency fulani sasa mtaalamu(mchawi) anaweza kukutrace sehemu yoyote ulipo yani anachukua band yote ya microwave anaifanyia kitu kinaitwa filtering anaipeleka kwenye kitu kinaitwa matched filter anakupata.Hii matched filter kazi yake na kucompare signal inayoingia na reference aliyo nayo.

Hii reference signal anakua nayo anakua ameichukua mapema physically kutoka kwako ndio maana kuna kamsemo wanasema mlozi hawezi loga mtu asiye mjua maana anakua hana reference signal.Hii technologia nadhani hata akina bush wanatumia kuwatafuta akina Ossama.

Hizi ni theory zangu risechi sijaiweza maana wachawi hawataki kutoa ushirikiano.
Samahani kwa kuvamia maada.

Tena wala hai-qualify kuitwa THEORY kama haijafanyiwa research...bali ni HYPOTHESIS...anyways, kula tano kwa kulazimisha UCHAWI kuchukuwa mkondo wa KISAYANSI.
 
kwanini asiwawe kama wanavo uwawa vikongwe tena huko kwenye jimbo lake!!!! tena huyu kaonekana kabisa kwenye cctv na vikongwe wao ni wanashukiwa tu....
 
kwanini asiwawe kama wanavo uwawa vikongwe tena huko kwenye jimbo lake!!!! tena huyu kaonekana kabisa kwenye cctv na vikongwe wao ni wanashukiwa tu....
Wajameni,
Hivi umri wa ANDEREYA si umepitwa kidogo na wakati? Kwa nini tusimhalalishe na yeye kuwa ni KIKONGWE na hapo tumwite Ndugu Alhaji Ali Hassan Mwinyi amtembelee huko kwako na afanye kile alikifanya Shinyanga miaka ya 70 mwanzoni. Nafikiri hii kazi Mzee Ruksa ataiweza maana wengine tunasema tu. Kuuwa kikongwe ni sawa na Kumkoma Nyani. Itabidi kuagiza miwani ya kufanyia welding kibao....
 
Mkuu Wangu,

Udumu Daima.Ni kazi nzito kwa taifa hili na nakupa salute kwa kuwa pamoja always kwa ishuz za Taifa.

Madataz mengine unaibuka nayo ni kama ule mtambo uliodondoshwa Hiroshima.



Wakuu Wengine humu ndani,


Mimi bado niko na Huyu member wa Hapa anayejiita "MTU WA PWANI" ,huyu mkuu alimzushia ZITTO kwamba inasemekana ni yeye aliyeonekana ndani ya ukumbi wa BUNGE,Nilimuonya na wakulu wengine humu jamvini pia wakamuonya,still aka-insist kuwa Ni ZITTO.

Sasa ilipokuja kuthibitika kuwa si Zitto,nikamshauri huyu mkuu aje aombe radhi hapa Jamvini kwani Amedhalilisha kijiwe hiki ili tuonekane wote humu ndani ni wadaku,watoto nk. kwa kuwachafulia watu majina.Sasa bado namshauri huyu mkuu arudi hapa kuomba msamaha maanake si uungwana wala heri kumkashifu mbunge wa watu halafu members na Mods hapa tuone halafu tukae kimya kwani at last itakua ni mazoea.

Jana aliniomba ushahidi,kwa bahati mzuri MAMA akampatia maanake alinitaka nilete ushahidi la sivyo mimi nimtake radhi,sasa nilimpatia na amepotea.


Btw: Komandoo ES,bado nakusubiri kwa hamu mkuu na na hilo li-B29



Ben,

Hata mimi shahidi, nakumbuka nilichangia na nilisema "tuwe serious na tuache kuzushia watu" nilikuwa namnukuu huyo mtu wa pwani, nasikitika watu wanachangia then wanasahau walicho comment!!!
 
Wajameni,
Hivi umri wa ANDEREYA si umepitwa kidogo na wakati? Kwa nini tusimhalalishe na yeye kuwa ni KIKONGWE na hapo tumwite Ndugu Alhaji Ali Hassan Mwinyi amtembelee huko kwako na afanye kile alikifanya Shinyanga miaka ya 70 mwanzoni. Nafikiri hii kazi Mzee Ruksa ataiweza maana wengine tunasema tu. Kuuwa kikongwe ni sawa na Kumkoma Nyani. Itabidi kuagiza miwani ya kufanyia welding kibao....

Jamani mwacheni Andy!jalini mambo yenu!Mambo ya Andy mwachie yeye mwenyewe!Yaani maneno mengine kweli ni ya kusadikika!yaani conditional kibao!
yaani hilo wazo ulilotoa hapo halitakaa litokee!
Asante
Hollo
 
Back
Top Bottom