Mzee FMES,
Huu wimbo ni kwamba walitunga wote yaani Franco na Sam Mangwana na kuja kuuimba wote. Ikumbukwe kuwa huyu mzee alikuwa ni KISIMA cha wasanii. Wengi walipitia kwake kama akina Mayaula, Mangwana, nk.
Mkuu vipi mbona husikii, hivi sijawahi kuesma mimi nilikuwepo huko Kinshasa, hebu ngoja nikupe darasa kijana maana sio kwenye siasa tu hata kwenye muziki nitakuumiza tu:-
1. Le Grande Franco Lwambo Lwanzo Makiadi Mandefu na Mandefu, ndio lililokuwa jina lake kamili,
2. Wapigaji wote wakubwa wa Congo Kinshasha, iliyokuja kuwa Zaire, karibu wote walitoka kwenye bendi ya Franco, yaani TP. Ok Jazz, isipokuwa tu Dr. Nico na kina John Bokeloo Isenge.
3. Sam Mangwana, ni mmoja wa waimbaji wa zamani wa Lwambo, enzi hizo alikuwa pamoja na Madilu, Simaroo, Josky Kiambukuta, Tabu Ley na kina Mayaula Mayoni, na hawa wote alikuja nao pale uwanja wa taifa in the 70s kasoro Tabu Ley ambaye tayari alikuwa na bendi yake kule Zaire.
4. Sam Mwangwana, alipotoka na hata akiwa peke yake, hakuwahi kuifikia level ya kimuziki ya Lwambo, maana Lwambo was too big kwenda chini kuimba waimbo kwa kushirikiana na Sam Mangwana, wenzetu wa-
Zaire au watu wa nchi za Francophone, huwa hwana tabia kama zetu za bongo za kujchanganya bila kujali Class, wao hujali Class, sasa kimuziki na kimaisha Sam Mnagwana, was too low of the Class kwa level za huko Zaire,
Kilichotokea ni kwamba Sam Mangwana, alikuwa ameenda Zimbabwe kwa muda mrefu, akawa amechacha sana, akarudi Kinshasa na kumuomba Verkyis Kimamangwana Wazela Mbongo Mateta, aliyekuwa then anamiliki bendi za Orch. Kamale, Orch. Lipwa Lipwa, Orch. Kiam, na Orch. Veve, kuwa amsaidie ili wapige naye album moja tu ili apate kuinuka tena, mkulu Verkyis akamkataa kabisa kuwa haweezi shusha jina lake kwa kupiga na Sam Mangwana.
Ndipo Sam Mwangwana, akatuma wapambe wakamuombeee kwa Lwambo, maana singeweza hata kwenda mwenyewe nyumbani kwa Lwambo, ndio Lwambo alipoambiwa akakubali tena kwa masharti kuwa Sam Mangwana atunge wimbo mmoja tu sio album nzima, amletee Lwambo ili auone na kumsaidia kupiga solo guitar na kuimba naye, which he did sasa njaa ya Sam Mangwana, akautengenezea album nzima na kusema kuwa ametunga na kuimba na Lwambo, lakini wimbo alioshiriki Lwambo ni mmoja tu, ambao kwa kilingala unasema hivi
"...balobaki eeeh biloba loba to lembi eee! lokuti yo kufa ye na ndokise moko moko, kusema sema walisema tumechoka, muwongo na mulosi ni watu wa kuchoma..."
Haya maneno mazito, Sam Mangwana, alkuwa anajaribu ku-get back to Verkyis aliyemkatalia kushirki naye au kumsaidia. Lakini kwamba alitunga Lwambo, hapana maana ingekuwa basi ile album ingejaa nyimbo zote akiwa Lwambo, badala yake ni huo wimbo mmoja tu!
Ahsante Mkuu